Miradi mingi ya Magufuli haina tija? Ni white elephant?

Moja ya miradi mikubwa ambayo baadhi ilifaulu sana ni kuwateka Watanzania wanamageuzi na kuwapoteza wengine kabisa.

Kuna iliyofeli japoa inawauma hadi kesho kama kumpiga risasi Lisu alafu asife.

Kuna ya kawaida ambayo hata haisemwi tena kama kuwapa Trafiki elfu tano tano wakapige viatu rangi.

Miradi ni mingi sana kwa kweli ila kwa sasa naomba kuta hoja.

Mkuu haya ni majungu una ushahidi?
 
Kwa hiyo basi unakubali kwamba Dar - Morogoro ni pesa za ndani. Sasa sisi tunaposema pesa za ndani kuna ubaya gani? Nani atasema kama sio sisi? Haijalishi kama ni robo au asilimia 40 etc ni lazima tujipongeze.

OK hiyo ''white elephant nafikiri ni kichwa cha hii thread.

Kwa hiyo hospitali za 1.5b tusiseme ati kwa sababu tu bei yake sio kubwa? Je, mbona awamu zote walishindwa kufanya hayo? Give credit where is due.

Mradi wa bwawa la Mwl Nyerere haukuweza kufanyika wakati wa awamu zote, Je, kwa nini sasa. Nafahamu huwezi kutoa credit kwa sababu ya chuki, chuki hazitakuletea Amani. JPM anafanya kazi kubwa katika uongozi wake na hiyo imekuwa game changer kubwa sana sio kwa Tanzania tu bali ulimwenguni kote hivi sasa nchi za magharibi wanatukodolea mimacho tu na wana wasi wasi kwamba Afrika inaamka na hawawezi tena kutuburuza. Angalia hata Franco phone countries wameamua kuondoa pesa zao ambazo wafaransa walikuwa wananeemeka.

Deni unalouliza liko linakuwa constantly kwa kiwango kile kile kwa muda mrefu na madeni mengine yanalipwa. Ukiangalia ukuaji wa deni la taifa lipo constant ukiachilia mwaka 2008-9 (recession).

Nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe Watanzania. Hakuna mjomba wala shangazi atakayekuja kutusaidia na maendeleo hayana chama. Wahenga walisema mjenga nchi ni mwananchi.

Ninasema sina tatizo la kukopa bali nina tatizo la hadaa ya kuwa ni pesa za ndani. Deni la taifa ni karibu sasa 60t. 1/3 ni deni la hii miaka minne ya awamu ya tano ambayo ina miaka minne tu kulinganisha na awamu nne kwa pamoja zilizopita. Nimetaja hivyo vituo vya afya na figure yake ili kukuonyesha hivyo vituo sio sehemu ya hilo deni kwani ulivitaja ili kuhalalisha hilo deni.

Miradi mikubwa na iliyochukua zaidi ya 1t ni mitatu tu, nayo ni hilo bwawa la 6.5t, reli 7.5t na ndege ambazo ni 1.8t. hiyo miradi miwili mikubwa ukiachia ndege za cash, iko kwenye hatua za ujenzi tena wa awali kabisa, hakuna mradi hata mmoja kati ya hiyo miwili uliofikia robo. Sasa hilo deni linatoka wapi wakati hadithi ni kuwa miradi ni ya pesa za ndani. Uje na majibu ya kueleweka maana hapa sio kwenye mkutano wa hadhara, ambapo watu wanahubiriwa bila kuhoji lolote na kuishia kupiga makofi tu.
 
1. Sawa, mosi unaweza kuleta takwimu za deni la taifa nje na ndani wakati JPM anachukua mikoba.
2. Weka figures hapa Serikali ya awamu ya 5 wametumia kiasi gani kwenye madeni waliyoyakuta na madeni mapya waliyoyaleta.
3. Weka hapa figures za madeni yaliyopo ambayo unalalamikia.
4. Marejesho deni letu hivi sasa la ndani na nje?
 
Kwanza mimi sio mtunza taarifa za deni la taifa bali ninajua wakati JK anatoka deni lilikuwa 39t kwa pamoja. Na hadi kufikia hivi sasa ni karibu kabisa na 60t kwa pamoja. Ww mtetezi ndio unapaswa kuweka hapa la ndani ni kiasi gani na la nje ni kiasi gani lakini jumla ndio hiyo. Sikatai serekali kuwa kuna madeni inalipa, lakini uwiano wa kulipa na kukopa hauwiani, ndio maana deni linakuwa kwa kasi halafu inaletwa hadithi kuwa ni miradi ya fedha za ndani.

Silalamikii deni, bali nasema kiongozi yoyote ambaye angekopa kama huyu na asitoe ajira wala kupandisha mishahara, angeweza kufanya haya yanayofanyika sasa hata na zaidi, na bado angeheshimu demokrasia. Iwapo umeamua kusifia sifia lakini usitake kuonyesha kuwa kuna maajabu kwenye haya, kwani deni la taifa nalo linapanda kwa nguvu na wala sio pesa za ndani kama inavyohubiriwa.
 
Wanandugu.

Serikali ya awamu ya 5 imejipambanua kama ya wanyonge na imekuja na miradi lukuki inayotafuna mabilioni ya pesa za walalahoi, lakini miradi hii haina na wala haionyeshi dalili ya kuwa na tija yoyote huko mbeleni. miaka mitano hiyo inakatika tunapigwa porojo lakini mabilioni yanateketea.

Daraja la Mfugale
Huu ni mradi wa hovyo niliowahi kuuona na unareflect hisia kwamba utawala huu umejaa ubinafsi.

Daraja limejengwa kimkakati kuwapa upendeleo wanasiasa wanaowahi ndege airport.

Wanyonge wanaotoka na kwenda Tandika na maeneo mengine ya Temeke inawachukua wastani wa dakika 45 kuvuka Tazara, ni kero kuliko ilivyokuwa kabla halijajengwa.

Rais ajae alibomoe ndani ya siku 100 lijengwe upya watu wote walifaidi.

SGR
Huu mradi miaka minne sasa inaenda mitano hakuna cha maana zaidi ya kuona minguzo na minondo tu inasimikwa kila siku.

Nguzo zenyewe zinaonekana kujengwa sehemu zinazopitwa na watu wengi ionekane kuna kitu kinajengwa kumbe ni uzugaji.

Ndege
Kila nikilitizama anga naona ndege za biashara ni zilezile tu: SwisAir, Turkish, Emirates.

Hizi za Rubondo island mbona hatuzioni zinabeba nini kwenda wapi?

Dar es salaam
Huu ni mji lakini ni mradi tosha. Toto pendwa hajatatua hata kero moja; foleni, maji, mafuriko na hata usafi siku za jumamosi umemshinda.

Miaka mitano inakatika bado miradi inayowapa unafuu watanzania inabaki kuwa ile ile iliyobuniwa awamu zilizopita; daraja la Kigamboni, mwendokasi, shule za kata, barabara za lami kila kona, treni za Mwakyembe, watu wengi wameajiriwa sekta binafsi awamu zilizopita.

Sasa huu utawala kuna mradi gani wa maana umefanya ukafanikisha? Muda unaenda miaka mitano hiyo inakatika jamani.
Kila kukicha ni kuongelea miradi isiyo kuwa na Tija kwa wanyonge. Tumejenga SGR, tumejenga fly over ,tumenunua ndege so what! Kwani ukifanya hayo yanakuzuiaje kufuata misingi ya haki na demokrasia? ,inakuzuiaje kuajiri watoto wa wakulima walio someshwa kwa kuuza mashamba,ng'ombe mpka kuku? Kusema kweli sisi watoto wa wanyonge tunaumia sana kwa ubaguzi ulio halalishwa ni hii awamu . remember tomorrow is here.
 
Miradi yote hata wawakilishi wa nchi za nje walipopelekwa wakashangaa kuona mambo ya ulaya yanawekwa hapa Tanzania

Kwa mujibu wa kituo cha dunia cha uwekezaji wanakubali kuwa katika bara zima la Africa Tanzania ndio inatumia pesa zake kwenye miradi yenye tija

Mungu mpemaisha marefu jpm

State agent
Huyo ni mjinga sana aanzishe miradi yake yenye tija tuione,naona huyo alikurupuka usingizini ndio akaandika hii threads,akalale naona uso una matongotongo
 
Mbona deni linakuwa au mnapiga huku mnakopa kuzuga
Mungu atazidi kumbariki Magufuli Miradi yenye Tija nimingi sana ikiisha kutakuwa Ulaya hapa,hata akikopa tunafahamu kazi ya hizo fedha,kazi zinaonekana dhahiri hata kipofu anaona
 
Kila kukicha ni kuongelea miradi isiyo kuwa na Tija kwa wanyonge. Tumejenga SGR, tumejenga fly over ,tumenunua ndege so what! Kwani ukifanya hayo yanakuzuiaje kufuata misingi ya haki na demokrasia? ,inakuzuiaje kuajiri watoto wa wakulima walio someshwa kwa kuuza mashamba,ng'ombe mpka kuku? Kusema kweli sisi watoto wa wanyonge tunaumia sana kwa ubaguzi ulio halalishwa ni hii awamu . remember tomorrow is here.
Hivi wewe umekimbia umande?Nitajie mradi usiokuwa na Tija,Mfano Kiwanja cha ndege cha Mpanda kitakapokamilika nani wataajiriwa kama sio hao watoto?Barabara zitarahisisha usafiri,nahizo barabara hazijengwi leo na kuisha leo,mzee umesomea wapi wewe jinga kabisa
 
Mungu atazidi kumbariki Magufuli Miradi yenye Tija nimingi sana ikiisha kutakuwa Ulaya hapa,hata akikopa tunafahamu kazi ya hizo fedha,kazi zinaonekana dhahiri hata kipofu anaona
True uwazi tu juu ya kodi zetu ndo muhimu
 
Kwanza mimi sio mtunza taarifa za deni la taifa bali ninajua wakati JK anatoka deni lilikuwa 39t kwa pamoja. Na hadi kufikia hivi sasa ni karibu kabisa na 60t kwa pamoja. Ww mtetezi ndio unapaswa kuweka hapa la ndani ni kiasi gani na la nje ni kiasi gani lakini jumla ndio hiyo. Sikatai serekali kuwa kuna madeni inalipa, lakini uwiano wa kulipa na kukopa hauwiani, ndio maana deni linakuwa kwa kasi halafu inaletwa hadithi kuwa ni miradi ya fedha za ndani.

Silalamikii deni, bali nasema kiongozi yoyote ambaye angekopa kama huyu na asitoe ajira wala kupandisha mishahara, angeweza kufanya haya yanayofanyika sasa hata na zaidi, na bado angeheshimu demokrasia. Iwapo umeamua kusifia sifia lakini usitake kuonyesha kuwa kuna maajabu kwenye haya, kwani deni la taifa nalo linapanda kwa nguvu na wala sio pesa za ndani kama inavyohubiriwa.

Mkuu wewe umesema deni la taifa linapaa kwa hiyo ni jukumu lako kuleta huo ushahidi sio mimi. Mimi ninachofahamu ni kwamba kwenye miradi hii yote kuna pesa za ndani ie makusanyo yanayotokana na shughuli mbali mbali za Serikali kupata mapato (ie utalii, kodi mbali mbali, mauzo ya madini, mauzo ya bidhaa nk). Sasa haiwezekani tupate hizo pesa halafu tusitumie tutegemee pesa za mikopo tu kwenye shughuli za maendeleo ya Taifa nk.)

Kwa hiyo basi yale maneno yako kwamba miradi yote tunayofanya ni ya madeni ie mikopo sio kweli. Kuna percentage ambayo wewe/mimi hatuifahamu. Vile vile hata ingekuwa hivyo maana yake ni nini? Ina maana kwamba pesa zinazopatikana kwenye mapato kuna mahali zinakwenda. Je, ni wapi huko? Pengine hilo ndio lingefuatia.

Nafahamu kuna changamoto mbali mbali lakini hizi zisituzuie kufanya mambo kwa uwazi zaidi na ufanisi kutokana na kwamba kila unapofanya jambo fulani kuna cha kujifunza. Deni letu linapanda constant kwa muda mrefu ukiondoa tu 2008/9 wakati wa recession.
 
Miradi yote hata wawakilishi wa nchi za nje walipopelekwa wakashangaa kuona mambo ya ulaya yanawekwa hapa Tanzania

Kwa mujibu wa kituo cha dunia cha uwekezaji wanakubali kuwa katika bara zima la Africa Tanzania ndio inatumia pesa zake kwenye miradi yenye tija

Mungu mpemaisha marefu jpm

State agent
Wewe na wenzetu wanaopenda kusifia njoo tumsifu mhe rais jmt jpm kwa kazi nzuri.
 
Mkuu wewe umesema deni la taifa linapaa kwa hiyo ni jukumu lako kuleta huo ushahidi sio mimi. Mimi ninachofahamu ni kwamba kwenye miradi hii yote kuna pesa za ndani ie makusanyo yanayotokana na shughuli mbali mbali za Serikali kupata mapato (ie utalii, kodi mbali mbali, mauzo ya madini, mauzo ya bidhaa nk). Sasa haiwezekani tupate hizo pesa halafu tusitumie tutegemee pesa za mikopo tu kwenye shughuli za maendeleo ya Taifa nk.)

Kwa hiyo basi yale maneno yako kwamba miradi yote tunayofanya ni ya madeni ie mikopo sio kweli. Kuna percentage ambayo wewe/mimi hatuifahamu. Vile vile hata ingekuwa hivyo maana yake ni nini? Ina maana kwamba pesa zinazopatikana kwenye mapato kuna mahali zinakwenda. Je, ni wapi huko? Pengine hilo ndio lingefuatia.

Nafahamu kuna changamoto mbali mbali lakini hizi zisituzuie kufanya mambo kwa uwazi zaidi na ufanisi kutokana na kwamba kila unapofanya jambo fulani kuna cha kujifunza. Deni letu linapanda constant kwa muda mrefu ukiondoa tu 2008/9 wakati wa recession.

Sio mimi ninasema deni la taifa linapaa, bali linapaa na hilo halina mjadala. Sikatai kwamba kuna miradi baadhi inajengwa kwa fedha za ndani, ila ni miradi midogo midogo sana ambayo huwezi kujisifia kama inavyofanyika, na hata ukijisifia basi ni kidogo lakini sio kufikia kiwango cha kuharibu demokrasia eti kwa kisingizio cha kuleta maendeleo.

Ni kweli kuna pesa zinapatikana kwenye mapato ya ndani, ila kwa mwenendo wa serikali yetu huwezi kuamini sana kiwango kinachotajwa, kwa sababu uwongo ni mwingi. Mfano kila mara serikali na rais huwa wanasema toka awamu hii ianze kumejengwa viwanda 4,000, je hilo ni kweli?

Hizo changamoto ndio huwa tunazisema mara kibao ambapo nyie hutumia msemo wa kuwa tunapinga kila kitu. Hapa hatuongelei deni la taifa nje ya awamu hii, tunazungumzia la awamu hii, na lenyewe lingekuwa 1/3 ya deni lote la taifa mpaka leo. Sasa kama awamu hii pekee yenye miaka minne tayari ina theluthi moja ya deni lote huoni kama ni hatari kidogo? Toka nje ya box ili uone vizuri.
 
Kwa hiyo kwenye deni hupo sahihi? Kwa sababu 1) Hujui deni alilolikuta 2) Hiyo 1/3 unaiongelea ndiyo imekutisha ingawaje huna specifics? Sasa kama huna specifics unawezaje kujadili na ku-judge? Then unasema ni miradi modogo midogo sana midogo sana kwa judgement yako au sio? Unapoongelea demokrasia iliyoharibika ni ipi hiyo?

Then unasema huwezi kuamini kinachopatikana ie mapato etc kwa nini huamini? Kuhusu viwanda 4,000 unasema sio kweli, Je, unaweza kuweka definition ya kiwanda/viwanda wanavyosema? Vile vile unaweza kuweka definition yako ya kiwanda/viwanda? Isije ikawa mawazo yako na ya serikali hayakubaliani wakisema kiwanda wana maana gani na wewe una maana gani. Tuanzie hapo then tupate ufafanuzi wao, huwezi kupinga tu bila kuwa na hivyo vingezo kwa sababu kila linalosemwa wewe unaonekana unapiga tu.

Kuhusu hilo deni kama unakumbuka nilikuuliza mwanzoni wakati JK anaondoka deni la ndani na la nje lilikuwa kiasi gani hukujibu. Kwa hiyo basi utaona tunajadili na kuhukumu kwa sababu za hisia tu au majungu hatuna facts. Lets put some facts then tujadili. Kwa hiyo basi tukubaliane sisi wote hapa tunapata habari nusu nusu kutoka kwenye sources mbali mbali na hizi tunazozipata sio conclusive facts, hivyo tunaweza kabisa kusema ni majungu. Hivyo basi hatuna moral authority ya kukashifu au kusifia kwa sababu hatuna tools zote zinazotuwezesha ku-judge fairly.
 
Mkuu haya ni majungu una ushahidi?
Mkuu bana swali lako si swali. labda ni mwendelezo tu wa mada na mzozo, ina maana we si mfuatiliaji mzuri wa vyombo vya habari ee!!! kwan nani asiyejua yanayoendelea ??? shida ni hii hali iilyopo yaan ukisema tu wakakujua yako ngumu, ukiponea chupuchupu bas ujue kucha huna.
 
Back
Top Bottom