Miradi iliyoachwa na Wakoloni kabla ya uhuru

Miradi iliyoachwa na Wakoloni kabla ya uhuru

Magufuli anajenga stiglers gorge ambayo ilimshinda mkoloni

Mzungu alijenga miradi iliyotesheleza uhitaji wa wakati huo. Isitoshe bado alitoa elimu bora kuliko hii watu wana PhD na wanachafua lugha ya PhD.
 
Watu weusi wengi wanajua tu kuzaliana, kufuata Imani za kijinga na kujisifia upumbavu.
 
S
Ifuatayo ni miradi mikubwa iliyojengwa na wakoloni:-

1. Ujenzi wa Bandari ya DSM
2. Ujenzi wa Bandari ya Tanga
3. Ujenzi wa Bandari ya Mtwara
4. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa DSM
5. Ujenzi wa uwanja wa Bandari ya Pemba
6. Ujenzi wa Ikulu ya DSM
7. Ujenzi wa Dsm College (Baadae ikaboreshwa na kuwa UDSM baada ya uhuru)
8. Ujenzi wa Bandari ya Zanzibar
9. Ujenzi wa reli ya kati, Dar-Tabora-Mwanza, Tabora -Kigoma
10. Ujenzi wa mji wa Tanga + Master Plan
11. Ujenzi wa Jiji la DSM + master plan yake
12. Ujenzi wa Bandari ya Mwanza
13. Ujenzi wa bandari ya Bukoba na Musoma
14. Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay
15. Ujenzi wa Bandari ya Ujiji Kigoma
16. Uundaji wa meli ya MV. Liemba (Ziwa Tanganyika)
17. Uunzi wa meli ya MV. Victoria (Ziwa Victoria)

18. Ujenzi wa shule za Sekondari za kale, mfano Mzumbe, Ilboru, Tanga Tech, Moshi Tech, Mazengo, Mtwara Tech, Tabora Boys+Girls, Pugu, Kibaha, Minaki, Bwiru boys & Girls, Msalato, Ifunda, Iyunga, Mkwawa, Nganza, Tosamaganga, Kilakara, nk

19. Ujenzi wa Ikulu ya Z'bar
20. Ujenzi wa majengo mengi ya Wizara za serikali, vituo vya polisi, magereza na Mahakama.
21. Ujenzi wa shule za msingi za serikali na za Seminari
22. Ujenzi wa makanisa, mf. St. Joseph na Azania Front (Posta Dar) na Misikiti kwa upande wa Z'bar
23. Ujenzi wa hospitali kubwa, mf. Muhimbili
24. Ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme mf. Hale + Nyumba ya Mungu.
25. Ujenzi wa vyuo vikuu vya kati, mfano Dar Tech, Arusha Tech, vyuo vya Ualimu, Kilimo, nk
26. Ujenzi wa reli ya Tanga
27. Ujenzi wa gridi ya kwanza ya Taifa ya umeme
28. Uanzishaji wa mashirika ya umma mfano Posta na simu pamoja na Benki yake
29. Ujenzi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar (Leo Shamba la Bibi)
30. Ujenzi wa vivuko, mfano Kigamboni na Posta jijini Dar
31. Na kadhalika na kadhalika.

Lakini pamoja na yoooote hayo, miradi hiyo yooote, Bado wazee wetu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, walisimama mbele ya kadamnasi na kuwaambia wananchi kuwa hao watu (wakoloni) hawafai, waondoke watupishe. Na kweli wakapisha rasmi Desemba mwaka 1961.

Sasa mwaka huu 2020, mimi ni nani hata nisimpinge ccm kwenye uchaguzi huu, pale anapotumia miradi ya maendeleo kadhaa iliyojengwa na serikali anayoiongoza, kama kigezo cha yeye kutaka kuchaguliwa tena na kubakia madarakani?

Tafakari...!!!.

Wakuu, mbona mwahangaika sana na hao wakoloni kunani khasa?
 
Ni madarasa makubwa mawili tu ndio yaliyojengwa na Wakoloni katika shule ya Ilboru, kanisa la KKKT na majengo mengine yalijengwa na wanawake wa kiarusha/kimasai walioitwa ''Ndoye o' matofali'' mwaka 1904.
Tanga School
Taboes Boys and Girls
Machame Girls
Old Moshi
Ndanda
Ndala Girls
 
Hapana.

Zipo hoja za msingi sana kumkataa Magufuli kuliko kutumia upotoshaji wa namna hii.

Hii inakosa ukomavu wa mawazo kabisa.

Nina hakika 100% huyu sio mkuu 'Sky...'; sijui kwa nini anakubali kuuza jina kwa hoja dhaifu kama hizi.

Ujumbe wa sky uko wazi, kuwa kama miradi ya maendeleo ndio kigezo cha kukaa madarakani, basi hata wakoloni walipaswa wakae madarakani, maana tayari walikuwa na miradi ya maendeleo. Lakini pamoja na miradi hiyo, bado haikuwa kigezo cha wazee wetu kukubali kutawaliwa bila ridhaa yao, kwa kisingizio cha miradi ya maendeleo.
 
S

Wakuu, mbona mwahangaika sana na hao wakoloni kunani khasa?

Watu wanajaribu kuonyesha kuwa miradi ya maendeleo si kitu kigeni nchi hii, kwani hata wakoloni walifanya miradi, na bado wazee wetu waliwakataa.
 
Watu wanajaribu kuonyesha kuwa miradi ya maendeleo si kitu kigeni nchi hii, kwani hata wakoloni walifanya miradi, na bado wazee wetu waliwakataa.

Ukisema hivyo unasigina historia ya ukoloni Tanzania.

Sasa hiyo miradi walojenga ilimfaidia nani?

Wataka turudi tena kwenye historia kama ile ya reli ya kati na kusudio la wakoloni wa kijerumani kutaka kusafirisha malighafi nje ya Germany East Africa?
 
Ujumbe wa sky uko wazi, kuwa kama miradi ya maendeleo ndio kigezo cha kukaa madarakani, basi hata wakoloni walipaswa wakae madarakani,
Hapo hakuna 'rocket science' ya kumsumbua mtu kuielewa!
Ninachokataa ni upotoshaji, hata bila kuangalia 'merit' ya mjadala kama huo.
 
ni kwel wakoloni walijenga miundombinu mingi sana nchini lakini ilikuwa na manufaa yao binafsi na si kwamba walitujengea sisi wabongo.. sisi bado tulikuwa vichakani tukitwanga mahindi kwa kinu
 
Ukisema hivyo unasigina historia ya ukoloni Tanzania.

Sasa hiyo miradi walojenga ilimfaidia nani?

Wataka turudi tena kwenye historia kama ile ya reli ya kati na kusudio la wakoloni wa kijerumani kutaka kusafirisha malighafi nje ya Germany East Africa?

Hiyo miradi ya mkoloni mpaka sasa sisi ndio tunaofaidi. Hata sasa malighafi zetu bado tunasafirisha kwenda nje tena kwa bei watakayo hao hao wazungu. Hapa lengo la mleta mada ni kuwa, miradi ya maendeleo isitumike kama sehemu ya kuharibu demokrasia yetu.
 
Hapo hakuna 'rocket science' ya kumsumbua mtu kuielewa!
Ninachokataa ni upotoshaji, hata bila kuangalia 'merit' ya mjadala kama huo.

Uko sahihi, ila ni vyema ww ungeweka hizo hoja zako nzuri za kumpinga Magufuli. Mleta mada kaona hizo zinafaa kwa mtazamo wake. Kama wewe uliona hizo ni nyepesi au upotoshaji, ww ungemkosoa na kuweka za kwako nzuri zaidi. Unakwama wapi kalamu1?
 
Hiyo miradi ya mkoloni mpaka sasa sisi ndio tunaofaidi. Hata sasa malighafi zetu bado tunasafirisha kwenda nje tena kwa bei watakayo hao hao wazungu. Hapa lengo la mleta mada ni kuwa, miradi ya maendeleo isitumike kama sehemu ya kuharibu demokrasia yetu.

Miradi ya maendeleo ni lazma itumike ili kuweza kuboresha zaidi demokrasia kwani yule ambae anatekeleza ahadi ya kukamilisha miradi hiyo ana haki kabisa ua kujivunia matunda yake.

Anakuwa hastahiki haki hiyo endapo ameshindwa kutekeleza na kukamisha miradi hiyo kwa miaka zaidi ya 40 na zaidi.

Kwa sasa raisi alieko madarakani JPM ana haki zote za kujivunia kwa kutekeleza na kukamilisha miradi hiyo.

Kwa kuwa sasa hata mimi sasa Tanga Line naitumia kwa uzuri basi, naona wazi nadeserve haki hiyo.
 
Uko sahihi, ila ni vyema ww ungeweka hizo hoja zako nzuri za kumpinga Magufuli. Mleta mada kaona hizo zinafaa kwa mtazamo wake. Kama wewe uliona hizo ni nyepesi au upotoshaji, ww ungemkosoa na kuweka za kwako nzuri zaidi. Unakwama wapi kalamu1?
Sijakwama popote, ila kama wewe unataka ionekane hivyo., Ninakuelewa vizuri sana kutokana na historia ya majibishano kati yetu humu JF.
 
Mwaga Pombe 2020 kataa CCM ya Magufuli. imekua GENGE la KIGAIDI linalo ratibu MATESO na MAUJI kwa Watanzania.
Miaka5 ya Magufuli Hakuna ajira mpya sijawahi ona popote. Hafai.
 
Back
Top Bottom