Mimi ni Polisi: Kisa cha mke wa Waziri

Mimi ni Polisi: Kisa cha mke wa Waziri

Mimi ni Polisi: Kisa cha Mke wa Waziri

“Yanyukwe....Yakobolewe” (hii iliashiria kupiga makofi)

“Ipo siku moja nitarudi nyumbani, kwa baba na mama nikiwa kamanda… (repeat)”

Weka changer…

“Mama nipokee, nimechoka zangu na safari, nimetoka zangu Msumbiji na bunduki yangu mkononi mama..(rudia kiitikio)”

“Malela! Malela! Malela (Malela)…Malela! Malela wangu namtafuta! Nimesikia Malela yupo Tabata, Malela! Malela! Malela wangu namtafuta”

Badilisha CD hiyo hatujafiwa hapa…

“Isamawela, isamawela..Isamawela Isamawela (isamawelaaa);
Tutamaliza, tutamaliza..tutamaliza, tutamaliza… (huu wimbo una-emotion jamani)”

“Ugonile ndaga (ugonile ndaga fijo) ugonile ndaga (ugonile ndaga fijo)
Ugonile ndaga fijo (ugonile ndaga fijo)

Wanyakyusa wosa (ugonile ndaga fijo)..ugondile ndaga fijo (ugonile ndaga fijo)
NA wapare/wachaga/wakurya/wajita/wasukuma/insert tribe (ugonile ndaga fijo)…ugonile ndaga fijo (ugonile ndaga fijo)”

“Mama Jeniii mamaa (mama Jeni), Mama Jeni (mama Jeni) ouoo (Mama Jeni)…;

Mama Jeni nitarudi (Mama Jeni), Mama Jeni (mama Jeni) ouoo (Mama Jeni)…”

“Mama bonge (eeh), hebu sikia (eeh) mwanao bonge (eeh) anavyolia;
Alizoea (eeh) chipsi mayai (eeh) soda bagia (eeh) na mishikaki;
Akaja depo (eeh) kuamka sa nane (eeh) ugali harage (eeh) bila kuungwa;
Na sasa boongeee..;
Bonge analia bonge (jamani bonge) bonge analia bonge…”

Ilikuwa tarehe 31/12/2011 usiku tukiupokea mwaka mpya wa 2012 tukiwa porini huku kuruta wakiendelea mafunzo yao ya kujiunga na Jeshi la Polisi (recruit course) mimi nikiwa kama Mkufunzi. Ulikuwa ni mkesha bila kupenda. Hapo kuruta walipiga disko kuanzia saa moja jioni hadi mwaka ulipoingia.

Nakumbuka mchana wa siku hiyo kuruta walipikiwa pilau ambayo kila mtu alitamani wangekula tu ugali kwani liligombaniwa na wala hawakushiba. Sisi tu waalimu kuwasimamia ilikuwa kama fatiki, hawazuiliki.

Mida ya kama saa nne niligundua wameanza kuchoka na sauti zinafifia nikawaambia wanyamaze nikawahadithia kisa kilichonikuta miaka ya mwanzo wa ajira yangu.

07[SUP]th[/SUP] August 2001, Dar es salaam

Baada ya kumaliza depo nilipangiwa kufanya kazi mkoa wa Dar es salaam. Nilikuwa kikosi cha FFU na hivyo kazi yangu kubwa ilikuwa malindo na kuzuia fujo, ingawa kwa kipindi kile nikiwa Dar sikupata kushiriki sana kwenye kazi hiyo ya kuzia fujo. Moyoni nilikuwa natamani sana ningebahatika kwenda maana nilikuwa natamani niwapige virungu wale waliokuwa wakituita sisi ‘darasa la saba’.

Mimi nilijiunga na Jeshi la Polisi kwani ndiyo ilikuwa ndoto yangu. Tangu nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana sare zao na magwaride yao na kwa kuwa nilikulia maeneo ya Moshi nilihakikisha nahudhuria sherehe zote za kipolisi ambazo zilifanyika pale CCP.

Nilifanikiwa kujiunga na Jeshi hili mara baada ya kumaliza kidato cha Sita. Nilipata daraja la pili katika masomo yangu ya ECA hivyo nikakosa fursa ya kusomeshwa kwa mkopo wa serikali. Kwa bahati mbaya wazazi wangu pia hawakuwa na uwezo wa kunilipia ada ukizingatia nilikuwa nikipenda sana kusoma masomo ya biashara.

Kwa ufupi ilinibidi nijiunge na Jeshi la Polisi ila moyoni sikukata tamaa nikajiambia ipo siku nitakuja kusoma masomo hayo ya biashara.

Maisha yaliendelea hadi siku hii ya tarehe 07/08/2001. Nilipangwa lindo kwa Waziri mmoja ambaye kwa minajili ya maadili ningeomba nisimtaje jina wala wadhifa.

Itaendelea kesho...

Sasa si ungemuuzia shingongo km umeshindwa. Kuimalizia
 
Mentor unatimiza ahadi yako ileeeeee au?
 
Last edited by a moderator:
Kumbe polisi mnawapenda enhee? Maana nnavyofuatilia utadhani sio wale mnaowaita polisi wetu policcm
 
Kumbe polisi mnawapenda enhee? Maana nnavyofuatilia utadhani sio wale mnaowaita polisi wetu policcm

mimi najipambanua hapa kila siku siwapend,na kila janga wanalolipata kwangu naona dogo,nawachukia sana tangu nikiwa mdogo
 
not makerere, ni chuo flani kikubwa sana USA, jina limenitoka kdg, nilibatika kuisoma kdg thesis yake inahusu masuala ya ugaidi

PhD holder unafanya nini jeshi la polisi,tena la Tanzania waratibu wa ujambaz na unyang'anyi pamoja na kubaka,,,,,kwanza utashindwa kuifanyia kazi maana mostly wanaokuzunguka either hawatathamini ua PhD au hawajafika walau kidati cha 6
 
mimi najipambanua hapa kila siku siwapend,na kila janga wanalolipata kwangu naona dogo,nawachukia sana tangu nikiwa mdogo

Inawezekana bado hujakua, bado mdogo. Huduma za kipolisi haziepukiki, kama ni mtu.mzima lazma ushahudumiwa na polisi.

Kama bado ipo siku utahitaji huduma yao, na utaenda kuitafta kituoni mikono nyuma!

Ilikuwaje uichukie polisi tangu utoto? Maana wengine tumeichukia hivi karibuni lkn tukiwa watoto ukiulizwa kazi gani unasema nataka kuwa polisi!

Mimi niliichukia mwaka 2006 kwa sababu ya askari wa wazo hill baada ya kunifanyia hujuma lkn tangu hapo nawakubali na nimeshuhudia wakisaidia uokozi wa maisha na mali kwa watu wanaozihitaji huduma zao.

Mfano nikiwa mwanza 2012, waliwakamata majizi ya kuiba pesa za watu kwa njia ya mtandao. Walimu wengi ni wahanga wa hili lkn ni utendaji wa polisi unaowachukia sasa makosa haya yameadimika.

Ipo siku utawahitaji
 
mimi najipambanua hapa kila siku siwapend,na kila janga wanalolipata kwangu naona dogo,nawachukia sana tangu nikiwa mdogo

hata kama huwapendi lakini fahamu kuwa there mere presence is your security, assume kama wasingekuepo au walale nyumbani kwa siku moja tuu impact yake itakuaje
 
PhD holder unafanya nini jeshi la polisi,tena la Tanzania waratibu wa ujambaz na unyang'anyi pamoja na kubaka,,,,,kwanza utashindwa kuifanyia kazi maana mostly wanaokuzunguka either hawatathamini ua PhD au hawajafika walau kidati cha 6

hivyo ndivyo wewe unavyodhani, bila hawa wasomi nani atatengeneza sera za kisasa kwa jeshi la kisasa?
 
Inawezekana bado hujakua, bado mdogo. Huduma za kipolisi haziepukiki, kama ni mtu.mzima lazma ushahudumiwa na polisi.

Kama bado ipo siku utahitaji huduma yao, na utaenda kuitafta kituoni mikono nyuma!

Ilikuwaje uichukie polisi tangu utoto? Maana wengine tumeichukia hivi karibuni lkn tukiwa watoto ukiulizwa kazi gani unasema nataka kuwa polisi!

Mimi niliichukia mwaka 2006 kwa sababu ya askari wa wazo hill baada ya kunifanyia hujuma lkn tangu hapo nawakubali na nimeshuhudia wakisaidia uokozi wa maisha na mali kwa watu wanaozihitaji huduma zao.

Mfano nikiwa mwanza 2012, waliwakamata majizi ya kuiba pesa za watu kwa njia ya mtandao. Walimu wengi ni wahanga wa hili lkn ni utendaji wa polisi unaowachukia sasa makosa haya yameadimika.

Ipo siku utawahitaji

ntamaholo mimi si mtoto na wazo la kuwachukia polisi halitanitoka na hata wanifanyie jema gani,,,,na nshawai kuwaambia,na nshawai kula ban hapa kisa polisi,,,nawachukia polis as taasisi na namchukia polis mmojammoja,mtu akishakua polis akil zake zinahama kwenye utu,na hata kama ndugu yangu atakua polis basi hapo ndo tutakua sepatae,kumbe na wewe umekiri kwamba washawai kukuzingua,sasa nikuulize polis wapo kwajili ya kuzingua watu au kuwalinda wao na mali zao????polisi na kibaka wote sawa tu,ofkoz siwapend na bora nimeweka wazi
 
Last edited by a moderator:
hivyo ndivyo wewe unavyodhani, bila hawa wasomi nani atatengeneza sera za kisasa kwa jeshi la kisasa?

we naweee,hili jesh lina sera za kisasa???unaemdanganya hapa nani???nenda kaunta ya kituo chochote cha polis halaf niambie umekuta kuna desktop ngap?????uje tuambie hapa hata december mwaka huu uje useme umekuta walau desktop ngap???,na uingie ofis za wakuu wa vituo uniambie umekuta wakuu wangap wa vituo desktop zao zinafanya kaz na zipo connected na internet,,,,
 
hata kama huwapendi lakini fahamu kuwa there mere presence is your security, assume kama wasingekuepo au walale nyumbani kwa siku moja tuu impact yake itakuaje

Daniel M polisi wapo na kila mwaka wanatengewa bajet ndo wala rushwa,ndo wanaolinda mtandao wa uhalifu,,,,unadhan polis hawawajui wauza unga wa kinondoni????yaan kuna scenareo nyingi naweza kukupa hapa ili kuonesha kuwa polisi ni majambaz wanaovaa sare,,,,hata uwe msafi mfumo wa jesh la polis utakubadilisha,,,,
 
Last edited by a moderator:
ntamaholo mimi si mtoto na wazo la kuwachukia polisi halitanitoka na hata wanifanyie jema gani,,,,na nshawai kuwaambia,na nshawai kula ban hapa kisa polisi,,,nawachukia polis as taasisi na namchukia polis mmojammoja,mtu akishakua polis akil zake zinahama kwenye utu,na hata kama ndugu yangu atakua polis basi hapo ndo tutakua sepatae,kumbe na wewe umekiri kwamba washawai kukuzingua,sasa nikuulize polis wapo kwajili ya kuzingua watu au kuwalinda wao na mali zao????polisi na kibaka wote sawa tu,ofkoz siwapend na bora nimeweka wazi

Nilikuja kujifunza kuwa udhaifu wa mtu mmoja siyo udhaifu wa taasisi. Wakati wapo wengi wasiofuata maadili ya kazi zao, wapo wengine akikuhudumia utafurahi hadi basi.

Wewe utakuwa na matatizo yako maana haiwezekan uwachukie bila sababu ya msingi. Hata viongozi wa vyama vya siasa, leo huwachukia kesho huwasifia. Hivyo ndivyo ilivyo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom