Mimi ni Polisi: Kisa cha mke wa Waziri

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Mimi ni Polisi: Kisa cha Mke wa Waziri


"Yanyukwe....Yakobolewe" (hii iliashiria kupiga makofi)

"Ipo siku moja nitarudi nyumbani, kwa baba na mama nikiwa kamanda… (repeat)"

Weka changer…

"Mama nipokee, nimechoka zangu na safari, nimetoka zangu Msumbiji na bunduki yangu mkononi mama..(rudia kiitikio)"

"Malela! Malela! Malela (Malela)…Malela! Malela wangu namtafuta! Nimesikia Malela yupo Tabata, Malela! Malela! Malela wangu namtafuta"

Badilisha CD hiyo hatujafiwa hapa…

"Isamawela, isamawela..Isamawela Isamawela (isamawelaaa);
Tutamaliza, tutamaliza..tutamaliza, tutamaliza… (huu wimbo una-emotion jamani)"

"Ugonile ndaga (ugonile ndaga fijo) ugonile ndaga (ugonile ndaga fijo)
Ugonile ndaga fijo (ugonile ndaga fijo)

Wanyakyusa wosa (ugonile ndaga fijo)..ugondile ndaga fijo (ugonile ndaga fijo)
NA wapare/wachaga/wakurya/wajita/wasukuma/insert tribe (ugonile ndaga fijo)…ugonile ndaga fijo (ugonile ndaga fijo)"

"Mama Jeniii mamaa (mama Jeni), Mama Jeni (mama Jeni) ouoo (Mama Jeni)…;

Mama Jeni nitarudi (Mama Jeni), Mama Jeni (mama Jeni) ouoo (Mama Jeni)…"


"Mama bonge (eeh), hebu sikia (eeh) mwanao bonge (eeh) anavyolia;
Alizoea (eeh) chipsi mayai (eeh) soda bagia (eeh) na mishikaki;
Akaja depo (eeh) kuamka sa nane (eeh) ugali harage (eeh) bila kuungwa;
Na sasa boongeee..;
Bonge analia bonge (jamani bonge) bonge analia bonge…"


Ilikuwa tarehe 31/12/2011 usiku tukiupokea mwaka mpya wa 2012 tukiwa porini huku kuruta wakiendelea mafunzo yao ya kujiunga na Jeshi la Polisi (recruit course) mimi nikiwa kama Mkufunzi. Ulikuwa ni mkesha bila kupenda. Hapo kuruta walipiga disko kuanzia saa moja jioni hadi mwaka ulipoingia.

Nakumbuka mchana wa siku hiyo kuruta walipikiwa pilau ambayo kila mtu alitamani wangekula tu ugali kwani liligombaniwa na wala hawakushiba. Sisi tu waalimu kuwasimamia ilikuwa kama fatiki, hawazuiliki.

Mida ya kama saa nne niligundua wameanza kuchoka na sauti zinafifia nikawaambia wanyamaze nikawahadithia kisa kilichonikuta miaka ya mwanzo wa ajira yangu.

07[SUP]th[/SUP] August 2001, Dar es salaam

Baada ya kumaliza depo nilipangiwa kufanya kazi mkoa wa Dar es salaam. Nilikuwa kikosi cha FFU na hivyo kazi yangu kubwa ilikuwa malindo na kuzuia fujo, ingawa kwa kipindi kile nikiwa Dar sikupata kushiriki sana kwenye kazi hiyo ya kuzia fujo. Moyoni nilikuwa natamani sana ningebahatika kwenda maana nilikuwa natamani niwapige virungu wale waliokuwa wakituita sisi ‘darasa la saba'.

Mimi nilijiunga na Jeshi la Polisi kwani ndiyo ilikuwa ndoto yangu. Tangu nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana sare zao na magwaride yao na kwa kuwa nilikulia maeneo ya Moshi nilihakikisha nahudhuria sherehe zote za kipolisi ambazo zilifanyika pale CCP.

Nilifanikiwa kujiunga na Jeshi hili mara baada ya kumaliza kidato cha Sita. Nilipata daraja la pili katika masomo yangu ya ECA hivyo nikakosa fursa ya kusomeshwa kwa mkopo wa serikali. Kwa bahati mbaya wazazi wangu pia hawakuwa na uwezo wa kunilipia ada ukizingatia nilikuwa nikipenda sana kusoma masomo ya biashara.

Kwa ufupi ilinibidi nijiunge na Jeshi la Polisi ila moyoni sikukata tamaa nikajiambia ipo siku nitakuja kusoma masomo hayo ya biashara.

Maisha yaliendelea hadi siku hii ya tarehe 07/08/2001. Nilipangwa lindo kwa Waziri mmoja ambaye kwa minajili ya maadili ningeomba nisimtaje jina wala wadhifa.

Kupangwa lindo kwa viongozi kulikuwa na faida na hasara zake. Kulikuwa na viongozi waliokuwa na utu sana. Kama mmepangwa jioni mtaandaliwa maji ya kuoga, chakula cha jioni na mnakuta chumba chenu cha ulinzi (centry box) kimepulizwa dawa ya mbu na kufanyiwa usafi na asubuhi mnapewa chai kabla hamjaondoka.

Sitaongelea kwa waziri mmoja hivi ambaye ukifika kwake hata salamu haji kuwapa, hakuna huduma yeyote ila sasa uchelewe kufika dakika moja tu kesi yake utaisimulia.

07/08/2001…Jumanne

Siku hii nilipangwa lindo kwa mheshimiwa waziri huyu. Ilikuwa lindo la asubuhi. Kama kawaida na sheria, inatubidi tufike eneo la lindo robo saa kabla ya muda wa lindo. Na kawaida yangu nilikuwa napenda sana kutunza muda. Hata askari wenzangu walikuwa wakijua na wengi walikuwa wakifurahi ukipangwa lindo ambalo Mentor ndiyo anakuja kuku-leave unafurahi kwani una uhakika wa kuondoka kazini kwa muda.

Tulifika nyumbani kwa waziri saa 05:45 asubuhi na kukabidhiana lindo na kisha kuanza kuzunguka kuhakikisha kote ni salama.

Ni hadi ilipofika saa kumi na mbili na nusu asubuhi niliposikia kelele za mtoto akilia. Alikuwa ni mtoto Tina. Tina alikuwa darasa la sita na asubuhi hiyo kama asubuhi nyingi ambazo nimewahi kuwa lindo kwa waziri huyo alikuwa akilia kwa kutokutaka kwenda shule. Mama yake alisikika akimkaripia kuwa avae haraka asijeachwa na basi la shule.

Kalikuwa na akili lakini kalidekezwa sana. Ni wale watoto waliorushwa madarasa kwani pamoja na kuwa darasa la sita alikuwa ameruka darasa la kwanza na la tatu hivyo kihalisia alikuwa mdogo.

Tinna alitoka nje huku akilia; hajavaa tai, viatu, hajabeba begi wala kuchukua ‘lunch box' yake. Nilimuangalia anavyolazimishwa kwenda shule nikakumbuka wakati nipo kijijini. Nilimuonea wivu kwa bahati anayoipata ya kuweza kwenda shule kwa starehe vile. Nilitamani bahati ile ingeniangukia mimi. Nilishindwa kuendelea na shule kwa kuwa mama yangu mjane alishindwa kunilipia ada ya chuo baada ya kushindwa kupata daraja la kwanza hivo kuwa vigumu kupata mkopo wa kusoma chuo.

Mama Tinna alimwita Tinna nje na huku amebeba viatu vyake. Tinna alikuwa akikataa kuvaa viatu akisema hataki kwenda shule.

Ndipo mama yake Tinna alipotamka maneno ambayo hadi kesho hayatokaa yafutike akilini mwangu. Mama Tinna alimshika Tinna kwa nguvu na kisha akamwambia (huku akininyoshea kidole), "Ukikataa kwenda shule utakuja kuwa kama Yule pale."

.
.
.
.
.
.
2008, November

Kwa ufupi tu: Nilibahatika kupata ruhusa ya kwenda masomoni mwaka 2006. Nilikuwa nimeomba kwenda kusoma masomo ya Uhasibu na kukubaliwa kujiunga na chuo cha uhasibu cha Arusha (IAA). Niliomba ruhusa kazini na kukubaliwa kuhamia mkoani arusha.

"Hallo mentor" Nilipokea simu kutoka kwa lecturer wangu wa Business Mathematics. Kipindi hiki nilikuwa mwaka wa tatu wa masomo yangu na kwa kuwa nilikuwa na masomo machache muhula huo mwalimu huyu alikuwa akipenda sana kuniomba nimsaidie kusahihisha mitihani/tests za wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Kwa kweli nilipenda hesabu na kufundisha hivyo sikuona shida, nikawa namsaidia.

Aliendelea, "Aisee, nimeamka sijisikii vyema kidogo naomba uende darasa langu la first year ukawasaidie kufanya masahihisho ya test ya juzi."

"Ok sir!" Niliitikia na kwenda kwanza kuangalia ratiba nijue kipindi chake ni saa ngapi na kinafanyikia darasa gani.

Ile kuingia tu darasani, hamadi! Macho yangu yakagongana ana kwa ana na sura ambayo kwa wakati ule sikukumbuka ni wapi niliwahi kuiona. Kalikuwa kabinti karembo na kamekaa dawati la mbele kabisa mwa darasa. Hadi leo nakumbuka kalikuwa kamevalia jeans shirt ya blue na jeans nyekundu. Kichwani alikuwa na weave ila ya kwake ilimpendeza. Nililipotezea lile wazo ovu la kumtamani mwanafunzi wa mwaka wa kwanza na kuendelea na kilichonipeleka darasani pale. Baada ya kufanya masahihisho niliwaambia kama kuna atakayekuwa na shida atanitafuta na kuwaachia namba yangu ya simu ubaoni.

Ama hakika msema kweli mpenzi wa Mungu, namba ile niliiandika makusudi kwa kuwa akili yangu ya kibazazi ilikuwa bado ikimuwaza binti Yule. Sikuwa na njia nyingine ila kuamini kuwa labda ataichukua na kunitafuta.

<Na hapa sijisifii> Ila hazikupita siku mbili nilipokea simu kutoka kwa namba ngeni. Alisema anaomba nimfundishe statistics kwani hakuwa akielewa vyema. Tulikubaliana tukutane jioni darasani na ndivyo ilivyokuwa.

Alikuwa ndiye, yule yule binti mrembo aliyekuwa amekaa siti ya mbele darasani. Na wakati namfundisha ndipo nilipogundua kuwa hakuwa mwingine bali Tinna, binti wa mke wa waziri. Moyoni nilifurahi kuona Tinna yule aliyekuwa akiambiwa asiposoma atakuja kuwa kama mimi ndiye huyu ninamfundisha 'Statistics'. Ila pia nilijiambia lazima nimlipizie mama yake kwa kupitia yeye.

Ilikuwa kazi rahisi sana kumfanya Tinna aangukie katika mtego wangu. Kwa muda wa miezi kama sita hivi nilimfanya Tinna aamini kuwa kwangu amempata mwanaume. Ila sasa alianza kuniganda na kunizuia mimi kufurahia maisha yangu na watoto wa Arusha. Rafiki yangu alipenda kuwaelezea kwa kusema, "They are very beautiful, until they smile (if you know what I mean)".

Nilipanga kumpotezea Tinna (ambaye hadi wakati huu hakuwa akijua kuwa mimi ni askari wala kuwa namfahamu ni binti yule wa waziri aliyekuwa akilia kwa kutokutaka kwenda shule). Nilianza kwa kumpotezea taratibu na kutokujibu sms zake wala kupokea simu. Akaanza kulalamika na kutuma meseji ambazo nilikuwa nishazizoea kama, "Mentor, kama kuna kitu nimekukosea, nisamehe tafadhali"

Baada ya wiki mbili niliona haachi kunisumbua ikabidi nihamie plan B. Nilianza kwa kumweleza kuwa mimi ndiye niliyemkosea na ndiye niliyetakiwa kumuomba msamaha. Hakunielewa hadi siku nilipoamua liwalo na liwe, nikamuomba tukutane kwa maongezi.

09 &#8211; 15 July, 2006, Nairobi

Ilikuwa wiki ya kawaida sana ukiachia kuwa nilikuwa nje ya kituo changu cha kazi. Nilikuwa nimechaguliwa kwenda seminaya &#8216;Post Traumatic Stress Disorder' na jinsi ya kuwasaidia watu kama hao. Ilikuwa semina nzuri yenye mafundisho mazuri hasa kwa wataalamu wa usalama na matukio yanayotokea duniani. Semina hii ilifanyika chuo cha Catholic University of Eastern Africa huko eneo la Rongai katika viunga vya jiji la Nairobi.

Siku ya kwanza ya kujiandikisha nilikutana na binti mmoja ambaye naye alikuwa mwanafunzi wa chuoni hapo. Aliitwa Catherine. Alikuwa akipenda sana kunitania kwa kuniongelesha Kiswahili ambacho kwa kweli sijui nani aliwaambia sisi huongea hivyo. "Habari yako ndugu!" "Naomba nikuombe twende tukanywe chai" "Naomba nikusalimu!" etc etc Well, kwa ajili ya kumfurahisha nami nilikuwa nikimjibu kama atakavyo.

Jumamosi, 15 July

Siku ya Jumamosi ya tarehe 15 tulitoka kwenda kutembea walau tulijue jiji la Nairobi kiasi kabla hatujarudi makwetu kesho yake. Alinionesha vyema maeneo ya katikati ya jiji hilo ambako kuna msongamano wa watu na magari mengi hadi unashangaa. Tulianzia huku chini railway, tukapanda kwa miguu kuelekea club maarufu ya F2, kisha tukaingia Kimathi street, tukaenda mpaka Odeon na kuchepuka kuelekea river road. Tulipata mahali tukakaa na kupata mlo wa mchana ambapo kwa mbele yetu kulikuwa na kiji hotel kama sikosei kaliitwa EXPATRIATES & DIASPORA HOTEL.

Nilimtania kuwa itabidi niingie pale walau kwa nusu saa tu maana na mimi ni expatriate. Kimzaha mzaha tukajikuta tumo ndani ya hoteli ile na haikuwa hadi mida ya saa kumi na mbili jioni ndipo tulipotoka kurudi chuoni. Tuliamua kutokuliongelea kabisa lililotokea mule ndani kwani hakuna aliyekuwa amepanga litokee wala kujua madhara yake muda huo.

12 April 2009, 2335hrs &#8230;Arusha

"Baby I know that you like me, you my future wifey
Soulja Boy Tell 'Em, yeah
You can be my Bonnie, I can be your Clyde
You could be my wife, text me, call me
"

Ilikuwa ni ringtone ya simu yangu. Ndiyo kwanza nilikuwa nimepanda kitandani ili nilale. Nilinyanyuka na kuchukua simu lakini kabla sijaipokea nikaangalia na kukuta ni namba nisiyoifahamu. Kuangalia vyema zaidi haikuwa hata ya Tanzania. Ilianza na +254.

Kwa wasiwasi niliipokea, "Hello!"

"Hi! Mentor" Iliitikia sauti ya pili.
Alikuwa Catherine.
Mh! Kwani bado alikuwa na namba yangu? Miaka yote hiyo? Mbona hakuwahi kunitafuta? Kwa kiasi moyo ulifurahi kusikia sauti yake na kujua kuwa bado kumbe ananikumbuka. Ila yalioendelea baada ya hapo yalinifanya nikachanganyikiwa kabisa, sikuelewa, sikuamini sikujua nifanyeje, nikatamani nisingeipokea simu ile.

Kate alinikumbushia siku ile pale EXPATRIATES & DIASPORA HOTEL na kwamba tendo lile ambalo tulilifanya mule ndani bila vizuizi vyovyote lilipelekea yeye kushika mimba na tarehe 17/04/2007 alijifungua mtoto wa kiume, Nelson.

Aliendelea kuniambia eti, hakutaka kuniambia kabisa na hata hivyo ameniambia tu kwa sababu wazazi wake wamemlazimisha. Alijua sikuwa na nia ya kumpa mimba hivyo pia sikuwa tayari kulea. Ndiyo maana aliamua kukata mawasiliano kabisa ili nisifahamu chochote kuhusu yeye.

Sikujua nifurahie habari zile au nisikitike au nifanyeje, kifupi nilichanganyikiwa. Nilishindwa cha kumwambia ila ilinibidi na mimi kuwaeleza wazazi wangu ambao (hasa mama yangu) walisikitika na kukasirika sana. Walisema jambo hilo kamwe haliwezi kuongelewa kwenye simu. Itanibidi kupanga safari mimi na Tina wote twende Moshi tukalizungumzie hilo swala akiwepo na mtoto, Nelson.

"We Mentor! Acha uongo! We unaaminije kuwa ni wa kwako! Huo ni uongo! Yani miaka yote hiyo mtu ana mtoto wako asikuambie! Mentor unanidanganya! Miaka mitatu ni mingi sana kutokumwambia mtu! " alidakia Tinna kwa maswali mengi.
Na kabla sijamjibu akaendelea, "Ulikuwa unampenda huyo dada? Kwa hiyo ukikuta ni wako utaamuaje? Utabaki na huyo dada? Kwahiyo ndo unamaanisha nini? Mentor mi siamini hata kidogo, haiwezekani. Kwa nini asikuambie miaka yote hiyo&#8230;"

Tina alikuwa na kila sababu ya kulalamika na kutokuamini hadithi ile kwani kwa upande mmoja ni kweli haikuwa na mashiko. Ila nilidhamiria kuisimamia kama vile ni ya kweli. Nilimwambia tu kuwa nilichanganyikiwa sana kupata habari zile ndiyo maana akawa ameona mabadiliko yale kwenye mawasiliano yetu.

"Hapana Mentor! Mi siamini!" Alilalamika Tina.

Maneno haya yalinifanya nihamie Plan C kwani nilihisi uongo wangu haujajitosheleza kumfanya Tina aniamini na aniache kwa amani. Kwa kuwa tulikuwa peke yetu chumbani kwangu nilianza kutoa machozi huku nikimweleza jinsi ambavyo mimi mwenyewe nilikuwa nimechanganyikiwa kwa habari ile. Hadi leo siamini kama ni mimi niliweza kulia vile. Nilionesha wazi kuwa nimechanganywa sana na habari ile na nilichomuomba Tina ni kuniacha tu peke yangu niwaze na pia niende Moshi nitakapofika na kujua hali halisi ndipo nitakapoweza kufanya maamuzi. Ilimbidi sasa Tinna aanze kunibembeleza mimi kwani aliona jinsi nilivyoumizwa na kuathiriwa na hali ile.

Nilimuomba Tinna tuwe tu tunawasiliana kama marafiki kwa kipindi kile hadi nitakapojua mustakabali wangu na Kate, mama Nelson. Hofu yangu kubwa ilikuwa kuleta drama/scene kubwa kiasi cha kuharibu cover yangu maana hakuna mwanafunzi aliyekuwa akijua kuwa mimi ni askari na pia kwa kufahamu yeye alikuwa binti wa waziri, ingeweza kuniletea shida si tu shuleni, bali hata kazini.

Nilifanikiwa kumaliza chuo salama salimini huku tukiachana na Tinna kwa amani. Nilirudi kituoni kwangu mkoani Arusha ambapo nilihamishwa kikosi kutoka FFU kwenda kazi za kawaida ambapo nilikuwa nikifanya ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD) kama mhasibu wa wilaya.

2010, July

Bahati nyingine iliniangukia miezi michache baada ya kumaliza masomo yangu. Kutokana na elimu yangu na utendaji wangu wa kazi (tangu kuajiriwa sijawahi kupatwa na shitaka lolote la kiutendaji/nidhamu), nilichaguliwa kwenda kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi almaarufu kama 'makirikiri' na baada ya kozi nilibaki kuwa mhasibu wa Polisi wilaya ya Arusha. Mara mojamoja nilikuwa nikienda vituoni ili na mimi nijifunze kazi za Polisi kwani ukweli ni kwamba huwezi kukaa tu ofisini kila siku mwishowe utakuwa kiongozi na hujui chochote.

03/06/2011, Kituo kidogo cha Polisi Sekei

"Afande!" aliita askari aliyekuwepo nje ya kituo.

Nilitoka nje na kumuona dereva wa bodaboda akiwa ameshikilia mkono huku akionesha kuugulia maumivu makali. Pembeni kulikuwa na pikipiki yake ambayo kwa hali iliyokuwa nayo nilishangaa kama ni mkono wake tu ndio umepata tatizo.

"Afande, bodaboda huyu kagongwa amekujua kuchukua PF.3" Aliniambia askari yule.

"Duh! Alifanikiwa kushika hata namba za aliyemgonga kweli?" Niliuliza huku nikichukulia kuwa aliyemgonga alikimbia kwani katika wale watu waliokuwa wamemzunguka hakuna hata mmoja aliyeonekana kuwa na uwezo wa kumiliki gari.

Askari aliyekuwa naye aligeuka na kunionesha kwa kidole gari ambalo lilikuwa ndiyo linawekwa vizuri sehemu ya kuegesha magari huku sehemu ya mbele kushoto ya gari hilo ikiwa imeharibiwa kutokana na ajali hiyo.

Ilinibidi kumwagiza askari kumwandikia PF 3 haraka aende kutibiwa mapema na kuwaomba wale waliokuwepo eneo la tukio kama wataweza kubaki wachache niendelee kuchukua maelezo. Waliokuwepo eneo la tukio walianza kuniambia kuwa isingekuwa ustaarabu wa mwendesha gari, wangeshampiga tayari. Tukio lenyewe lilitokea katika makutano ya barabara za Arusha-Moshi na Waterfall. Mwendesha gari alikuwa akitokea kwenye barabara hiyo ya Waterfall akitaka kuingia kwenye barabara kuu ya Arusha-Moshi ambayo mwendesha pikipiki huyo alikuwa akiitumia.

Kabla hawajamalizia kunielezea mkasa mzima ....

Itaendelea tena kesho, Alhamisi...
 
Mentor nawe umeamua kufata nyayo za waendeleza kesho?
Haya bwana
 
Last edited by a moderator:
Aaaagrrrrhh. Mentor unaanza kuleta mambo ya kesho kama zile story za Mzizi Mbichi sorry! I mean Mzizi Mkavu.
 
mwaka jana uliahidi hiki kisasi cha


: itaendelea

can't biliv ndo kinaanza rasmi
 
Mentor.......malizia leo ili tujifunze. Lkn nikependa ulivyoingia jeshini ukiwa form six leavers! Wapo watu hadi leo huamini ualim na jeshini hupokelewa waliokata tamaa ya maisha, walioshindwa! Kumbe kuna watu wenye cv babu kubwa wamo majeshini.

Siku moja niliona picha ya kumwaga kamanda barlow, maofisa waliokuwa wamebeba jeneza, yupo bonge mmoja kipindi hicho alikuwa ocd kwimba. Jamaa ni phd holder wa social justice toka makerere university
 
Acha nami niimbe kidogo , Apigwe ee Amini apigwee*2
na ule wa kumalizia kufunga kambi wa Salama salama salama salama tumekuja salama na tutarudi salama au ule wa sifa ya afande Na Mentor ni komandoo lelelee ni komandoo na mentor ni komandoo lelelee ni komandoo*2
kweli nikikumbuka natamani turudi enzi za 70's acha tu jeshi kutam sana
 
Yaani mentor miaka hiyo ukapata DIV 2 ukashindwa kwenda chuo, na ilikuwa under Government Sponsorship (sio loan), ulicheza sheree! ....
 
Mentor mambo ya ntaendelea kesho ndo yananifanyaga nikimbie jukwaa haya.............

je usipofika kesho itakuwaje??
ama utatuitumia ujumbe toka kuzimu??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom