Mimi ni Polisi: Fastjet

Mimi ni Polisi: Fastjet

Mdogo wangu Mentor kajifunze uwe romantic na wewe
ticket miaezi mitatu bado unasubiria tuu aise hapo kweli kaona hapa kauzu
Ila nae huyo hafikirii mpaka ashauriwe na mashosti wakati mapenzi ni ya kwake

Hahaha ila kwa Mentor huyo kutoa nauli ya ndege sio jambo dogo. Ye mwenyewe hata hajawahi hata kuwaza kama ipo siku atajilipia kusafiri na ndege
 
Last edited by a moderator:
kifupi ni kwamba umekutana na malaya ndugu yangu chapa lapa! mwanamke ambaye ana consultants kama mia hivi tena mashankupe huyo hakufai ndugu, mtu anayejielewa hana muda huo, tena ndiyo anatakiwa awe wa kwanza kukushauri matumizi sahihi ya pesa, ili hata anapokuja kukubomua pakubwa wala usiwe na shaka!

Thanks mkuu CYBERTEQ.

Dunia ya Leo hakuna mapenzi, zamani sawa saiv ni urefu wa mkono wako ndio unakupa penzi zuri na mwanamke mzuri, huo ni ukweli,yale mambo nampenda jinsi alivyo hayapo, na kingne wanawake wa leo hawaulizi tena kabira gani wewe anaanza kazi gani unafanya??!!!

Cc: Wadada wote...

Hahahahahhahaha pole sana afande Mentor. Msalimie huyo Winnie au kama vipi nipatie namba yake niwasiliane naye ili niongee naye biashara muhimu

Ahaha katibu mwenezi #teamB umeibukia wapi leo!?? Labda nikupe ya Vaileth Shirima...Winnie bado nna biashara na yeye!!!

Mdogo wangu Mentor kajifunze uwe romantic na wewe
ticket miaezi mitatu bado unasubiria tuu aise hapo kweli kaona hapa kauzu
Ila nae huyo hafikirii mpaka ashauriwe na mashosti wakati mapenzi ni ya kwake

Ha! Kaka Mr Rocky yani hapo unaona sikuwa romantic!???
 
Last edited by a moderator:
binamu umesahau kitu hapa ungemwambia apae kwa kifaa hichi
AA.jpg
Mdogo wangu Mentor kajifunze uwe romantic na wewe
ticket miaezi mitatu bado unasubiria tuu aise hapo kweli kaona hapa kauzu
Ila nae huyo hafikirii mpaka ashauriwe na mashosti wakati mapenzi ni ya kwake
 
Hujawahi kufanikiwa mkuu, wakuonee huruma bhana hata siku 1 na wewe utusue Mentor aka Mr Sikati Tamaa
 
Last edited by a moderator:
Inaumiza sana, inapasua sana kichwa!!!!

Winnie will pay the price, very sorry my brother Mentor!!
 
Hahaha ila kwa Mentor huyo kutoa nauli ya ndege sio jambo dogo. Ye mwenyewe hata hajawahi hata kuwaza kama ipo siku atajilipia kusafiri na ndege

Mkuu Nicas Mtei ni sawa ila kwa hawa dada zetu hawa hawajui namna tunavyotoil kuyaweka maisha yao sehem nzuri
Tunajinyima ili wapate pesa za salon, wapate usafiri mzuri wapate pesa za club na ukikosea tuu ndo unaambiwa hayo ya Mentor


Ha! Kaka Mr Rocky yani hapo unaona sikuwa romantic!???


Kwake hapo anaona hukuwa romantic Mentor maana kitendo cha kuambiwa ( akisukumwa na mashosti wake) ticket ina miezi mitatu kwake yeye sio kabisa
Alitegemea anaambiwa hayo aliyotaka
Ila nafikiri mashosti wana nguvu katika maisha yake kuliko yeye na ni mbaya sana kutokuwa na maamuzi haswa katika suala zima la matumizi
 
Last edited by a moderator:
Hahahah....naomba tu hasira za kutoswa zisihamie kwa raia lol
 
Hahahah....naomba tu hasira za kutoswa zisihamie kwa raia lol

Nimejitolea mhanga aniamishie mm
Bint wa kike hawezi kumchomesh mahindi kiivi
Pata picha kamshahara kotee kakata tiket ya ndege ...daaa kweli mapenzi upofu
 
Inaumiza sana, inapasua sana kichwa!!!!

Winnie will pay the price, very sorry my brother Mentor!!
 
Mimi ni Polisi: Fastjet

30 June 2014


Ama kweli wahenga hawakukosea waliposema, Ngombe wa masikini hazai. Akizaa hufaa. Asipokufa basi dume. Kama jike, tasa! Leo nimeugundua ukweli wa huu usemo.

Jumamosi, 07 July 2012 Mitaa ya Mwenge Mwenge

Kwa askari Polisi, suala la kutokuwa na siku ya sikukuu ni jambo la kawaida kabisa. Siku hii nilipangwa zamu ya ukaguzi mida ya mchana maeneo ya Mwenge.Baada ya kumaliza kukagua malindo yote ya mchana kama inipasavyo kuwajibika. Nilikuwa katikati ya kutoa ripoti ya malindo hayo kwa mkuu wangu wa kituo. Ghafla

Nilimsimamisha askari aliyekuwa akiendesha gari na nikazima radi call kwa muda (nitajibu hii kesi baadaye..ndivyo nilivyowaza kichwani). Nilishuka haraka kwenye gari na kuelekea kule nilipoona kile kilichonivutia.

Samahani dada naomba kukusemesha kidogo Nilijikuta nimeshamtamkia maneno hayo binti niliyemsimamisha. Kwanza alishtuka maana kusimamishwa randomly na Polisi kibongobongo sio ishara nzuri. Aliniangalia juu mpaka chini kasha kushusha pumzi baada ya kujihakikishia sina nia ovu kwake.
Naitwa Afande Mentor (huku nikimuonesha jina langu lililoandikwa upande wa kulia mwa shati langu E. E. Mentor)

Naitwa Winnie! Bado alionekana kuwa na wasiwasi.

Kikweli sikumbuki yaliyoendelea pale ila nakumbuka kumweleza maneno ambayo kwa kawaida mtu angetumia robo saa ila mimi nilitumia dakika si zaidi ya nne. Mwisho wa siku tulibadilishana namba za simu na kuondoka. Nilimpigia tena mkuu wa kituo na kuomba radhi kuwa tuliona tukio ikabidi tukalishughulikie kwa haraka, ila ni minor na hakuna dhara lolote lililotokea. Askari dereva tuliyekuwa naye (mtu mzima kidogo kuliko mimi) aliishia kutingisha kichwa asiamini kilichotokea.

Winnie alinivutia sana nilipomuona. Katoto kazuri kabisa. Sikutaka kumuonesha hilo mapema ila tuliendelea kuwasiliana kwa kipindi kile na hata kuja kuwa marafiki wazuri tu. Kwa wakati ule ndio alikuwa ameanza kazi kampuni moja ya vinywaji hapa Dar. Haikupita muda mrefu sana na mimi na Winnie tukawa wapenzi. Ahaha aliniambia alivutiwa sana na jinsi nguo zangu zilivyokuwa zimenipendeza tofauti na mapolisi wengine anaowaonaga barabarani. Nilikuwa nimetupia shati langu la maboresho, nadhifu kabisa lililonoshika vizuri na viatu vyangu vimengarishwa mpaka unaweza kujiona.

Maisha yalikuwa mazuri.

Mwaka 2013 Septemba Winnie alipata kazi mkoani Mwanza na ilimbidi kuhamia huko. Ilikuwa ngumu kwetu kwani ilikuwa mwanzo sana wa penzi letu. Ila tulijiapiza kujaribu na kujitahidi kufanya penzi letu lidumu na kuendelea. Mawasiliano yalikuwa ndiyo kitu ambacho kilituweka pamoja. Na kwa hilo liliwezekana ingawa marafiki zake (ok, na zangu pia) walikuwa wakitukatisha sana tamaa.

Kwa upande wangu sikuwasikiliza kabisa wote walioniambia kuwa huko aliko anachepuka, au ana mtu mwingine kwa hiyo na mimi nitafute wa kupoozea wakati tunaendelea kuwasiliana. Alikuwa pia akiniambia hayo yalikuwa yakimtokea pia kwa upande wake na nilimtia moyo kuvumilia.

March, 2014

Mentor: Good morning sunshine
Winnie: Good morning darling, how are you
Mentor: Am good and not so good
Winnie: Why, whats wrong dear?
Mentor: I miss you badly
Winnie: ooooowh! Thanks d...I miss you too, you know!
Mentor: I do! I do! I just cant help it though
Winnie: Haya banaila tumeonana juzi tu over your birthday
Mentor: Yeahbut that was way back in January!
Winnie: By the way, I could come over during sabasaba, si kutakuwa na long weekend!

Yes! Yes! Yes! Nilifurahi kusikia vile na mara moja nilimweleza kuwa nitalishughulikia hilo. Tulikubaliana nifanye booking ya Fastjet kwa ajili ya yeye kuja Ijumaa asubuhi ya tarehe 04/07 na kuondoka tarehe 07/07 jioni. Gharama zake kwa fastjet zilikuwa considerably low. Kwa kamshahara kangu ka upolisi ningeweza kabisa kulifanikisha hilo na baada ya kufanya booking nilimweleza kuwa kila kitu kipo tayari. Aliniahidi kuongea na supervisor wake ili aruhusiwe kutokwenda ofisini hiyo Ijumaa na alikubaliwa.


Fast forward, 29[SUP]th[/SUP] June 2014Jumapili, 1835hrs

Kutokana na mechi ziendeleazo za mashindano ya kombe la dunia ratiba yangu ya kuongea na bebi Winnie ilibidi ibadilike. Nilikuwa nikmpigia kabla ya mechi za saa moja na tena kabla ya mechi za saa tano. Jana, nilimpigia jioni saa kumi na mbili hivi. Kwanza hakupkea simu hivyo nikasema ntampigia tena simu mechi itakapoisha. Na ndivyo nilivyofanya.

Mentor: Hey D tsup!
Winnie: Hey
Mentor: (nikaguna maana niliitikiwa flatly) Howv u been? Umeshindaje?
Winnie: Mentor, I have something to tell youI cant make it to Dar hiyo tarehe 04

Dah nilijihisi kuchoka. Ka laki mbili kangu nilijibana nikakata tiketi za fastjet  NON REFUNDABLE  mbona kanayeyuka hivi hivi? Ratiba zangu nilizozifuta kwa minajili ya kuspend wikiendi yangu na mpenzi wangu Winnie! Lakini kwa nini?

Nilimbembeleza sana Winnie aniambie nini hasa sababu ya yeye kushindwa kuja ila kila kisingizio alichokuwa akikitoa hakikuwa na mashiko. Baada ya kuongea kwa muda mrefu na dakika zangu za YATOSHA kwisha nilikata tamaa na kuamua kukata simu nijiandae kuangalia mechi ya saa tano usiku. Hata hivyo sikuwa nikiiangalia kwani suala la Winnie kuahirisha safari bila kuwa na sababu maalum ilinipa wasiwasi.

Huwezi nilaumu kwani niliwaza labda umbali umekuwa tatizo, hivyo uvumilivu umemshinda. Lakini kwa nini wakati huu ambapo ndio alikuwa karibu kuja kuonana nami? Niliwaza labda amekutana na mtu mwingine na tayari keshaangukia katika mtego wake. Niliwaza na kuwazua lakini sikupata jibu.

30[SUP]th[/SUP] June 2014facebook status ya rafiki yake Winnie

Vaileth Shirima (20[SUP]TH[/SUP] June 2014): Wanaume wengine sijui wapoje! Kama huna hela kaa na masikini wenzako wasio na sura na shepu! Mwanaume huna hela unakazana kutaka kumhudumia Miss Tanzaniautaweza wapi!?? Unajifanya upo romantic unanibukia ndege za wanuka shombo mwaka kabla. Kama upo romantic nipigie simu leo niambie babe nimekukatia ticket ya saa moja jioni jiandae uje Dar nina hamu na wewe!#Kantangazeeee

Nilikuwa napitia pitia facebook ndipo nilipokutana na ujumbe huu ulioandikwa na rafiki wa mpenzi wangu. Mwanzo sikuuelewa lakini baada ya kuendelea kumbana Winnie anieleze ukweli ndipo aliponifungukia kuwa, marafiki zake wamemshawishi akatae kuja kwani sijawa romantic kisa nimembukia ndege miezi mitatu kabla badala ya kukata tiketi Alhamisi yeye asafiri Ijumaa

Kwa kweli nimekosa cha kumjibu. Hadi sasa sielewi. Pesa yangu imepotea hivi hivi na Winnie ndo kaamua kuniacha kisa ushauri wa mashosti. Sikatai ni mzuri, lakini nilifanya vile kutokana na upendo wangu kwake na kuendana na uwezo wangu

Wasalaam wapendwa,
Mentor.
Hahahahaha pole afande , ila tatizo nikwamba ulivutiwa sana na Winnie hukutazama makunyanzi namba hizo zinawenyewe we afande utaweza wapi na shukuru umemjua mapema ungevuta ndani hakika ungetafuta ajira mbadala kama si ujambazi .
 
Hivi mwallu anajua kama ulikua na mchepuko Winnie?ha ha ha
Vijana wa teamB utawajua kwa vitendo tu mishe zao
 
Last edited by a moderator:
Afande Mentor achana na mademu sio professional yako,kama unataka mega kisha run...kama Mr Rocky
Ha ha ha


Mkuu mwekundu mbona unanisingizia aise Mentor yanamkumba kwa kupenda saaana mpaka anajisahau na akitoswa anaumia sana
Sijui kama hapa alilifaidi tunda au ndo alikuwa anategemea kuja kufaidi tunda lake na ticket yake ya ndege miezi mitatu kabla
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom