Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

mm ni nduguye wa damu
ni sisi ni matwins
hvyo usishangae sana rafiki,
bora umejisemea ili nikwambie tukoje, una lingine la kusema?
Kwa avatar nilifikiri EMT nilivyosoma post ilibidi nihakikishe kuwa huyu kweli ni EMT ninaye mfahamu ndipo nilipogundua sio. Thank God
 
Kwani unaoa dini/dhehebu au unaoa binadamu? UPENDO WA KWELI HAUZUIWI NA VITU VIDOGO KAMA HICHO NA UKIKISHINDA HICHO KIKWAZO HIYO NDIO DINI SAFI,FUNGUKA.
 
waroma pia wana charismatic kama walokole vile haina tatizo biblia si ile japo ni maamuzi ya kila mmoja sehemu atakapo penda kuasali..
 

Mshirikishe mchungaji wako. Ila mwenye maamuzi ni wewe mwenyewe kutokana ni imani yako.

Kwa upande wangu naona si sawa kwani tofuti za kiimani zitawaletea matatizo hapo baadaye.
 
Mkuu hapo nilipobold ni typing error au huo ndio ukweli wenyewe
 
Kazi kweli kweli , mtoa mada kazi kwako umeomba ushauri naona wengi wamekupa ushauri sasa ni wajibu wako kusoma na kuchuja yepi yanakufaa na kuyaweka kwenye matendo. Sitii neno naweza nikawa biased sababu mi ni mkatoliki na sioni sababu ya kuongeza kwani mengi waliotangulia wameshakwambia na ni mambo mazito na mazuri kama lengo lako lilikua kutafuta ushauri basi ufuate..
 
Mambo ya rohoni hutambulika kwa njia ya roho. Unaweza kuwa profesa lakini kwa mambo ya rihoni ukazidiwa na ambaye hana elimu dunia.

Maajabu ya dunia haya...Yani wewe kunyooshea kidole mwenzako na kumuita mdhambi ni mambo ya rohoni...Seriously...!!!!! Kama mkuu wangu unakipimo cha kupimia dhambi za watu huku kikuhakikishia wewe hutendi dhambi nakiomba maana nitakinunua kwa npesa yoyote.....Wacha kujkidanganya mkuu hakuna aliye mkamilifu hapa duniani ila Baba aliye mbinguni...Wote tu wasafiri katika hii dunia yenye kila aina ya uozo ndanio ytake....Tafadhali hebu usijidanganye eti kwasababu wewe ni mtu wa rohoni..
 
Kumuoa mtu wa nje ya imani yako ni upungufu mkubwa wa kushindwa kuhimili mikiki ya shetani na maanisha shetani anakuwa amekutawala hadi kumfikilia huyo mtu!
Kama si kanisa unalo amini wewe akibadili dini na kuja kwako kwa akili yako unafikiri amefuata dini au wewe? na kama kakuona wewe ni zaidi ya Mungu wake aliyekuwa anamwabudu unafikiri wewe anashindwa kukusaliti? au unadhani huyo Mungu wako anashindwa kumsaliti? Usiishi kwa kumtegemea mwanadamu bali bwana aliye juu mbinguni, katika jina la Yesu naomba huyo pepo mchafu aliyeyatawala mawazo yako aondoke sema Ameni!!!!!!!!!
Usimuoe shinda tamaa zako za kimwili mrejee mwokozi wako na tubu kwa kuweka hisia nje ya maandiko unayo yaamini usijilinganishe na Muumba wako yaani dunia nzima umetafuta wa imani yako umekosa?
 

Wewe hujaokoka, ila unamajivuno ya kubatizwa kwa kile kinachoitwa eti 'maji mengi"

Sasa nikuuliza maji yana wingi? maji ya kwenye kijiko sisimizi anaona ni bahari.

Au nijibu haya yafuatayo.
-Maji ya kwenye kisoda na ya kwenye chupa yenyewe yapi mengi?
-Maji ya kwenye chupa na ya kwenye simtank yapi mengi?
-Maji ya kwenye simtank na ya kwenye bwawa yapi meni?
-maji ya kwenye bwawa na ya kwenye bahari yapi mengi?

hao wachungaji huwa wanawadanganya ndo mana huwa mnakiburi cha kujiona hamna dhambi, wakati huenda hata huyo binti ushamchakachua kabla ya ndoa.
 
Umempenda yeye au dini yake?.....acha uzinifu kijana hapo najua tayari umeshamaliza...
 
waroma pia wana charismatic kama walokole vile haina tatizo biblia si ile japo ni maamuzi ya kila mmoja sehemu atakapo penda kuasali..

Watu wengi wakiwemo wakatoliki wanakosea sana..Wanadhani ukarismatic ni aina fulani ya upentekoste au ulokole ndani ya kanisa..na wamefikia kuact kama vichaa wa kilokole na kipentekoste..charismatic siyo na wala haifanani hata kidogo na heresy kama za kilokole na waprotestanti
 
hatujaongea hilo kwa undani,ila yupo tayari kwenda na mimi efatha

hilo sio suala la kukurupuka.
Inabidi mkubaliane strongly sana ili msije kuwekeana nira huko mbele.
Suala la imani ni la msingi sana. Asikudanganye mtu kabisa.
 

mmmmmmmmm haya maswali yako kiboko, majibu sasa:
1) kuathirika kiroho kivipi?
2) sidhani kama ukiwa mlokole au mpagani ndio guarantee ya kuishi miaka mingi: Mfano, marehemu bi kidude, mugabe, kingunge ngombalemwiru.
3)wokovu wako utauharibu mwenyewe kwa matendo yako.
4) mbinguni unajipeleka mwenyewe au umeambiwa waliooana wote kwa efatha wataenda mbinguni?
5)wakati unamshawishi uwe makini unaweza ukampoteza kimoja.
 

Tumsifu Yesu Kristu, umempa jibu la kumtosheleza. Ulokole ni njia ya kuwatenganisha mtu na ndugu zake, wazazi wake hata watoto wake kwa kisingizio eti.....nimempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wangu.......kwani wakristu wengine tunamwabudu nani kama si Yesu Kristu alifia msalabani kwa ajili yetu?
 
mh! hapa sasa tukushauri nini, kutamani kwenyewe dhambi tayari..., kama unataka ushaur nenda kwa padr wako sio um JF
 
mimi niongelee juu ya swali Zima la imani. Ninavyofaham mimi wokovu una misingi yake miiko yake. kwani wewe una miaka mingapi katika wokovu? kitu kilicho mfanya Mfalme Suleimani kukosana na Mungu ni pale alipooa wanawake wa mataifa mengine hao walikuwa wakiamini miungu mingine( imani tofauti na suleimani). Maandiko pia yanasema usifungiwe nira pamoja na wasioamini! wewe waamini wokovu yeye je? vipi siku moja akikwambia unanipigia makele ya kuomba mimi nimelala utajisikiaje? siku akija na bia home utasemaje? maana wakatoliki wanakunywa! uamzi ndugu unabaki kwako wewe mwenyewe maana yeye hatakuwa na shida hata kidogo ila wewe! hata hivyo wahenga walisema ndege wa rangi moja huruka pamoja! nawakilisha!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…