Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

Mimi ni Mlokole nataka kuoa Mroma

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,439
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?
 
Inategemeana, je unamwonaje msimamo wake kwenye wokovu? wewe umeokoka maana yake unajitambua na unajitahidi kutotenda dhambi, mfano uzinzi! umejitunza? Yeye je ni kama wewe? amejitunza? au ana mahusiano ambayo hajakueleza kwa kuwa anajua kuwa akikueleza unaweza usimuelewe!!!?
Umeshawahi kuongea naye kwa habari ya ndoa? au wewe unafikiri kumuoa wakati yeye hajui? Ongea naye kwa kuwa wewe ndio unamjua vizuri kuliko sisi, kama hataki kuokoka itakusumbua uko mbele.
 
AMOSI 3:3 je watu 2 waweza kutembea pamoja wasipokuwa wamepatana? mkioana mtakuwa mnasali wapi? romani au efatha?
 
Oa tu...maadam mpatane kwanza juu ya tofauti za imani zenu.
 
Inategemeana, je unamwonaje msimamo wake kwenye wokovu? wewe umeokoka maana yake unajitambua na unajitahidi kutotenda dhambi, mfano uzinzi! umejitunza? Yeye je ni kama wewe? amejitunza? au ana mahusiano ambayo hajakueleza kwa kuwa anajua kuwa akikueleza unaweza usimuelewe!!!?
Umeshawahi kuongea naye kwa habari ya ndoa? au wewe unafikiri kumuoa wakati yeye hajui? Ongea naye kwa kuwa wewe ndio unamjua vizuri kuliko sisi, kama hataki kuokoka itakusumbua uko mbele.

kuhusu kumwoa tumeongea sana na yupo tayari,mahusiano alikuwa nayo kwa sababu ana mtoto mmoja na hawajawahi kuishi pamoja,kuhusu usumbufu mbele ya safari nahisi ndugu inaweza kuwa hivyo lakini namwona ni mwanamke mnyenyekevu sana kuliko wengi niliokutana nao makanisani
 
...wewe uko tayari kubadili dini na kusali ROMA ama wataka yeye awe kondoo wa Mwingira?
 
This is y i hate religion but ilove jesus..calling others blind doest mean tht u got a clear vision..nyinyi walokole hvi kuokoka ndo kusalia uko kwenye hayo makanisa yenu??alokwambia waroma awajaokoka ninani?unauahakika baaada ya kuokoka kwako utendi dhambi?ama ndo painting a grave wakati ndani kumeoza?mwenye mamlako ya kuhukumu ni mungu tu..acheni hizo ..
 
Ni vizuri lakini hautapata majibu halisi hapa.
Cha muhimu ni nyinyi kwa nyinyi kuheshimiana maana mkristo yoyote haachi maneno ya busara na yenye hekima,
Neno la Mungu ni Roho hivyo haliitaji uwe mlokole au Rc ndipo ukombolewe, Imani yako inakutosha.
 
kuhusu kumwoa tumeongea sana na yupo tayari,mahusiano alikuwa nayo kwa sababu ana mtoto mmoja na hawajawahi kuishi pamoja,kuhusu usumbufu mbele ya safari nahisi ndugu inaweza kuwa hivyo lakini namwona ni mwanamke mnyenyekevu sana kuliko wengi niliokutana nao makanisani

Angalia mambo yafuatayo,
1.Mtoto wake : una-muadapt? au anaenda kwa baba yake?
2.Imani yake: Anakuja kwako? au unaenda kwake.
3.Ndugu: huyo mke ni wa kwako sio wa ndugu, hivyo patana na moyo wako.
4.Ex-wake: pata uhakika kuwa wamemalizana kabisa na hasa hatima ya mtoto.
Kwa kuwa wewe umechagua fungu lililo jema hakikisha na yeye anafata fungu ulilochagua.

Kama ni mnyenyekevu hawezi kukataa.
 
Ndugu mlokole unaoa mwanamke au uroma? Oa mwanamke anayefaa. Inaonekana wewe unataka kuoa dhehebu. Kasome Mithali 31:10-31 uone aina ya mwanamke wa kuoa. Usioe dhehebu hutapata mwanamke anayefaa kwani si wote hapo kwenu (kwenye ulokole) wana tabia inayofaa. Yesu alisema imani iendane na matendo. Kusema tu mimi ni mlokole wakati matendo ni tofauti si sawa. Angalia matendo zaidi kuliko ulokole au uroma. Namjua mtu mmoja alioa mwanamke akidhani ni mlokole kumbe balaa. Hiyo ndoa ilisambaratika na huyo bwana kaoa tena baada ya kuvumilia muda mrefu. Yule mwanamke alitoroshea watoto kenya. Alihangaika sana na sikumbuki kama aliwapata wote. Mtu anaweza akajifanya mlokole ili tu aolewe au aoe akibaini kuwa ulokole ni muhimu katika mada ya ndoa. So take your time and choose a good and intelligent wife not otherwise. By the way I am also a believer!! Read James 2:14-26.
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?
 
Angalia mambo yafuatayo,
1.Mtoto wake : una-muadapt? au anaenda kwa baba yake?
2.Imani yake: Anakuja kwako? au unaenda kwake.
3.Ndugu: huyo mke ni wa kwako sio wa ndugu, hivyo patana na moyo wako.
4.Ex-wake: pata uhakika kuwa wamemalizana kabisa na hasa hatima ya mtoto.
Kwa kuwa wewe umechagua fungu lililo jema hakikisha na yeye anafata fungu ulilochagua.

Kama ni mnyenyekevu hawezi kukataa.

Mkuu nahisi unaelewa sana kinachonitatiza
kuhusu baba wa mtoto walishamalizana kwani alishaoa mwanamke mwingine,lakini ana uhusiano wa karibu na yule bibi wa mtoto wake yaani mama wa x wake
kuhusu mtoto atabakia na uhusiano na baba yake kwani hata sasa hivi wana uhusiano mzuri
kuhusu imani yupo tayari kunifata kwa ,Mwingira
 
Kwa kuwa mnapendana ni lazima mtatembea pamoja;
Haijalishi ni kwa efata au ni kwa polikapu;

Kabla ya pingu za maisha mkubaliane kuwa mtasali wapi?
Ili wote muwe wamoja kwa kuwa mtakuwa ni mwili mmoja.

Usione aibu kuongea naye, ukiruhusu ya kila mtu kusali kwake
mwisho wa siku itakugharimu sana.
 
wapendwa katika bwana
nimetatizwa na kitu hapa,mimi ni mlokole nasali Efatha bible,nimejaribu kuomba na ku connect na baadhi ya wapendwa wenzangu lakini nahisi sikufanikiwa
ila imekuja kutokea nikaonana na mwanamke ambaye anasali roman catholic na tumependana sana japo sikutarajia wala sikua na plan yoyote ya kumwoa
naomba ushauri kwa yafuatayo:
kama nikioa mtu ambaye hajaokoka je nitaathirika kiroho?
je naweza kumuudhi mungu kwa hilo?
je maisha yetu huko mbele ya safari yatafika mbali?
je anaweza kuathiri wokovu wangu?
je naweza kwenda mbinguni?
je unafikiri naweza kumshawishi huko mbele ya safari akaokoka?

Kwahiyo ujui kuwa roma ndiyo kanisa kristu aliloacha? Ujui kuwa roma ndiyo ukristu wa kweli? Achana na conspiracy theories , tena fanya research juu ya catholic church...nenda catholic.com, whyimcatholic.com utapata majibu juu ya imani ya kikatoliki na siyo mataptap ya wasabato na wapteotestanti aka waasi...
 
Angalia mambo yafuatayo,
1.Mtoto wake : una-muadapt? au anaenda kwa baba yake?
2.Imani yake: Anakuja kwako? au unaenda kwake.
3.Ndugu: huyo mke ni wa kwako sio wa ndugu, hivyo patana na moyo wako.
4.Ex-wake: pata uhakika kuwa wamemalizana kabisa na hasa hatima ya mtoto.
Kwa kuwa wewe umechagua fungu lililo jema hakikisha na yeye anafata fungu ulilochagua.

Kama ni mnyenyekevu hawezi kukataa.
Wewe. na watu8 mmeonge point sn.
Kama ni matter ya dini, naamini kwa huo umri uliokuwa nao wewe hukuzaliwa ndani ya Efatha, maana haya ni madhehebu ya 90`s.
Kama wewe uliweza kubadilika, yeye atashindwa nini, wakati unatuambia ni mnyenyekevu?

Mjomba, kama mmependana na huyo dada kwa dhati, na lugha zenu zinaendana ni bora umuoe, ishu ya kuokoka ni function ya ushawishi wako na jinsi atakavyoona mwelekeo wa matendo yako.
 
Last edited by a moderator:
na ndio maana nikasema 'kupatana' kama mwanamke anakutii,anakubali kile unachosema OA. but usiache kuomba Mungu zaidi.
 
This is y i hate religion but ilove jesus..calling others blind doest mean tht u got a clear vision..nyinyi walokole hvi kuokoka ndo kusalia uko kwenye hayo makanisa yenu??alokwambia waroma awajaokoka ninani?unauahakika baaada ya kuokoka kwako utendi dhambi?ama ndo painting a grave wakati ndani kumeoza?mwenye mamlako ya kuhukumu ni mungu tu..acheni hizo ..

Unajua mkuu katika watu ambao huwa nawadharau kwa kiasi kikubwa ni Walokole...Hawa watu ni waajabu sana....Lakini nilichogundua ni kuwa hawa viumbe wa ajabu kichwani ni watupu mno..Wangekuwa na elimu ingewakomboa angalau...
 
mi naamini ungeweza kupeleka hizo hoja kwa wasimamizi wako wa kiroho ingekuwa vema zaidi, kuliko kuzileta hapa, mahala ambapo shetani anapatawala kwa zaidi ya asilimia 90...(taking into consideration mitusi inayomwagwa hapa daily),.....pia, kwa jibu la swali kuwa endapo utaenda mbinguni..i guarantee you, even mwingira cant tell u that, and if he does, atakuwa ametenda dhambi ya uongo...kama unaijua biblia, utakuwa umepitia maneno ya Mungu ambayo watu kwa namna nyingi wamekuwa wakiifafanua tofauti kwa mitazamo tofauti yenye mlengo wa kupotosha, kukataza ama kutawala watu...wapo waliotafsiri baadhi ya maneno ya Bible kuwa yanatutaka tusifungamane na watu wasioamini...ila jiulize, Yesu alipokuja, alifungamana na watu wa aina gani?, je alihangaika na watu gani....Maria magdalene alikuwa mwanamke wa aina gani??, Lazaro alikuwa mtu yupi??.....Pia jiulize, wakati wa NUHU, ni yeye pekee ndiye alikuwa mwaminifu kwa Mungu, hatukuelezwa habari ya wanawe wala wakwe zake...lakini wakwe za Nuhu waliokolewa kwa imani ya Nuhu na uaminifu wa Nuhu kwa Mungu......kiufupi, Imani yako kwa Mungu, inaweza kuwa chachu ya wokovu kwa mtu utayefungamana naye.....Wakristo wote, ilimradi tunamkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu, na kuwa alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, akafufuka, akapaa mbinguni, na atarudi tena kuhukumu.....basi wote tu sawa, tunatofautiana mitazamo ambayo imewekwa na binadamu kwa milengo tofauti tofauti......
 
Mkuu nahisi unaelewa sana kinachonitatiza
kuhusu baba wa mtoto walishamalizana kwani alishaoa mwanamke mwingine,lakini ana uhusiano wa karibu na yule bibi wa mtoto wake yaani mama wa x wake
kuhusu mtoto atabakia na uhusiano na baba yake kwani hata sasa hivi wana uhusiano mzuri
kuhusu imani yupo tayari kunifata kwa ,Mwingira

Ok, kama mmekubaliana kuhusu imani sioni tatizo kwa upande huo.

Kwa upande wangu ningepata shida sana na hayo mahusiano ya mama wa Ex na mchumba wako, lakini pia ukaribu wa baba na mtoto, manake kuna ukaribu na Ex wake, Mimi kama Renegade sipendi kuoa mwanamke aliyezaa na mtu mwingine, kwa kuwa najua kuwa kutakuwa na connection ya kudumu na ex wake, wakati wote kwenye tatizo la mtoto lazima watakuwa pamoja, hivyo ni kama kuwa na mke mwenye waume wawili, that is how i feel,Nakumbuka hata wazee waliwahi kuniambia juu ya jambo hili.
 
Ninatatizwa kidogo ukisema kunifuata kwa Mwingira. Mwingira ana imani? Au kukufuata kumwamini Kristo Yesu???? Mwingira ni imani gani? Mimi naijua imani moja tu ya kumwamini Yesu Kristo!!! Nijuavyo mimi Mwingira ni mtumishi wa Mungu na sifa na utukufu ni kwa MUNGU. Yote anayofanya Mtumishi Mwingira ni Yesu Kristo aliyeko ndani yake hivyo tumtukuze Kristo sio mtumishi wake. Mungu alichukizwa na kosa moja tu la Musa alilojitwalia utukufu na akamwambia hataiona nchi ya ahadi!!! Tumpe utukufu Mungu sio mwanadamu!
Mkuu nahisi unaelewa sana kinachonitatiza
kuhusu baba wa mtoto walishamalizana kwani alishaoa mwanamke mwingine,lakini ana uhusiano wa karibu na yule bibi wa mtoto wake yaani mama wa x wake
kuhusu mtoto atabakia na uhusiano na baba yake kwani hata sasa hivi wana uhusiano mzuri
kuhusu imani yupo tayari kunifata kwa ,Mwingira
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom