Walau amethubutu, is it sustainable?
Kagasheki afanye zaidi yahapo tumumini zaidi.
a) Tukamatie waliobeba twiga wetu. Lakini hasa mapapa ilitujue ilikuwaje ndege ya jeshi la inchi nyingine ingie na kubeba wanyama wetu kama vile inteligensia ya Mkuu wako haipo au ipo kuvidhibiti vyama vya upinzani tuu??
b) Na hao walio uwa Faru wetu sheria ichukuwe mkondo bila mizwengwe na kwa kipindi kifupi waende kifungon.
Tunashindwa kuwaamini viongozi wetu, siku zote mnafanya mambo ya nguvu ya soda na kutuaminsha hewa pasi na utendaji wa haki na kizalendo.
Mh Kagasheki mi mi ni muumini m zuri wa utendaji wako uliotukuka.Tena naamini una utashishi na dhamira ya kweli katika kuwatumikia wananchi,lakini hofu yangu kubwa ni kuingiliwa na kupata mashinikizo kama ya mama Tibaijuka. Mama huyu alianza vizuri sana na kujenga imani kwa wananchi hususani kwa staili yake ya kukagua viwanja na kutoa amri kali kuvunja uzio ambalo ulikuwa ni maeneo ya wazi,lakini kasi yake haieleweki imefikia wapi ilihali kesi nyingi ambazo zinatishia amani ya nchi hii zitasababishwa na migogoro ya ardhi ndani ya Tanzania yetu tunayoipenda kwa moyo wetu wote. Umeanza vizuri bila kuwafumbia macho wala kumung'unya maneno lakini je kasi hii itakuwa ni ya kudumu au ndio nguvu ya soda?Historia inatukumbusha kuwa viongozi wengi wa serikali walio beba dhamira ya dhati kuwatumikia wananchi wengi wameanguka kutokana na kushindwa kusimamia wananchi na kulinda rasilimali za taifa ama kwa kupata mashinikizo toka kwa wakubwa wao waliowateuwa wakisahau kuwa ameapa kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzani. Wakati fulani ilinipa wakati mgumu kutokana na uamuzi wa rais kushindw kukupa uwaziri kamili wakati utendaji wako ni wa viwango vya juu,kwa hili aliloliona mh rais kukuteua waziri kamili ametutendea haki wananchi ila cha msingi zingatia heshima yako kama mwanadiplomasia isidondoke kwa kusababishwa na mashinikizo ya wakubwa zako,kilicho muhimu tenda kwa uaminifu bila kuvunja sheria wala kumuonea mtu.Mungu akusaidie katika mjukumu yako ya kila siku.
Watanzania ni watu tunaodanganyika kiurahisi sana!
Huyu Kagasheki si alikuwaga wizara ya mambo ya ndani wakati Polisi wetu
(japo hatuwapendi kwa kutumiwa kwao) walikuwa wanapunjwa zile posho zao mpaka Lema akakisanua kwenye hotuba yake ya kambi ya upinzani??
Mbele ya siasa dhaifu hakuna kiongozi wa kujitangaza jembe!
- Mheshimiwa Kagasheki, hajawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ila alikuwa Waziri Mdogo, na kisheria mwenye mamlaka ya mwisho kwenye Wizara ni Waziri sio Waziri Mdogo!!
William.
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.
Mkuu W. J. Malecela hata baba yako alikuwa na mkwara huo lakini unaona alikotufikisha Mama yako mpaka povu huwa linamtoka lakini ilipokuja kusigne petition ya zito akaingia mitini
Precise,
Baba na mama yake wanahusika nini na mawazo yake au na mada hii? Kama umefirisika kupinga hoja kwa hoja kaa kimya.
Waziri Tibaijuka a.k.a.Mama matamko
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.
Kwani baba yake hajawahi kushika uwaziri mkuu? Alifanya nini cha maana zaidi ya kufisadi hii nchi na alikuwa na mikwara kama ya Kagasheki. wewe ndio uliyefilisika kihoja unatetea wezi na watoto zao humu jamvini
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.
- Mheshimiwa Kagasheki, hajawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ila alikuwa Waziri Mdogo, na kisheria mwenye mamlaka ya mwisho kwenye Wizara ni Waziri sio Waziri Mdogo!!
William.
Marazote ninapo post hapa nipo makini sana, sababu najua kuna watu kama nyie mnatafutiza upenyo wa kuhalalisha yale mnayoona yanaridhisha hoja zenu.....
Vipi mkuu, hoja ya kuwajibika kwa pamoja huwa inaishia na kuanzia wapi???
Wewe nachelea kusema unaropoka au una ujinga wa kutofahamu unachokiongelea.nakuomba nikufahamishe kama ifuatavyo mjinga wewe.
Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) ni miongoni mwa mashirika yanayowajibika moja kwa moja kwa wizara ya maliasili na utalii.moja kati ya majukumu yake makuu ikiwa ni kuhifadhi na kulinda maliasili zote zilizoko ndani ya mipaka ya hifadhi za taifa,ikiwa ni pamoja na viumbe hai wote pamoja na mimea hai na mfu kama kuni.
Ni kosa kwa mtu yeyote ambaye si muajiliwa ndani ya hifadhi kuingia ndani ya hifadhi bila kibali maalumu, au malipo halali na kwa kupitia katika milango rasmi ya kuingilia na kutoka hifadhini.ikiwa ni kwa muda maalumu na atatoka kulingana na kibali au malipo yake kukaa ndani ya hifadhi kuisha,
FARU KUUAWA.
Tukio hili lilitokea kwa mara ya pili,huko katika eneo la kusini magharibi pakijulikana kama MORU AREA,eneo hili lina ulinzi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na vifaa vizuri vya kisasa vya ulinzi wa wanyama pori ikiwemo magari mazuri ya kisasa,askari wenye mafunzo maalumu ya ulinzi wa wanyama pori pamoja na silaha nzuri za kisasa.achilia mbali makazi mazuri ya kuishi askari hao na vifaa vya mawasiliano na viona mbali vikubwa na vya kisasa kabisa.
Pamoja na hayo yote lakini faru aliuawa na majangili bila hawa walinzi kuwa na taarifa lakini pia siku kadhaa baada ya faru kuuawa,mkuu wa kituo husika aliendelea kutoa taarifa ya makabidhiano ya faru makao makuu ya hifadhi ya serengeti kwamba faru wale wako hai na salama.
Mpaka pale wasamaria wema walipotoa taarifa ya kuuona mizoga miwili ya FARU walioonekana wakiwa wameishauawa.jambo ambalo lilimlazimu mkuu wa hifadhi kufuatilia na kubaini ukweli katika eneo la tukio.wakati huo askari wale wakiwa bado wakitoa taarifa ya faru kuwa hai.
Sasa pamoja na yule mkuu kubaini tukio hilo bado aliishia kumuweka yule mkuu wa kituo chini ya ulinzi kwa muda mfupi katika kituo cha polisi pale seronera na kisha kudhaminiwa.lakini pia kuna tetersi kuwa mkuu yule wa kituo alikuwa na tuhuma kadhaa za kukutwa na ama masalia ya nyama za wanyama pori au mnyama kamili(si faru)
Na pia utawala wa TANAPA makao makuu hawakuweza kuchukuwa hatua zozote za msingi kutokana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwashikilia wahusika mpaka upelelezi kamili ambapo ungekamilika.
Mimi binafsi nilikuwepo siku faru hao wakipokelewa na kukabidhiewa kwa Mh Rais kikwete wakitokea afrika kusini.na nilimshuhudia rais akitoa kauli yake kwamba faru wale wapewe ulinzi kuliko anaopewa yeye.
Pia niliona na kutathmini zoezi zima lilivyokuwa na thamani kubwa kupita maelezo na likikutanisha watu mbnalimbqli maarufu duniani viongozi na wafadhili pia.
KAGASHEKI,amechukuwa hatua stahiki tena kwa wakati muafaka tukizingatia viongozi wetu wengi ni waoga kwa kuchukua maamuzi magumu kama haya ya Kagasheki.na tulipaswa kumpongeza na si kumponda.
ALLUTTA CONTINUA........
Watanzania tuanze kuwa na tabia ya kuwapongeza viongozi wetu pale ambapo wanachukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi au jambo lolote ambalo ni la kidhalimu.hii itawapa morali na pia kujiamini katika nafasi zao kiutendaji.
.
Commonmwananchi. kwa navyotambua Hifadhi ya Serengeti ina miradi mitatu ya Faru ambayo ni Mradi wa Moru, Mradi wa Ndasiata maarufu kama Faru wa JK na mradi wa Nyamarubwa. Faru waliyouwawa mwaka huu ni wa Moru ambako haukuwepo wakati wa kuwapokea kama ulivyojieleza. Faru wa JK wamebakia watatu baada ya mmoja kuuwawa kwa ujangili mwaka 2010 na mmoja kufa kwa ugonjwa mwaka jana.
Muhimu ni watanzania kutambua kuwa ujangili ni tatizo kubwa hapa nchini na nchi nyingine barani africa. Kwa mawazo yangu siamini kama ukiwasimamisha kazi watumishi utazuia ujangili. Ni vizuri watumishi kuchukuliwa hatua hususani kufukuzwa kazi kwa wale wasiowaadilifu baada ya kubaini makosa yao. Kiulinzi ni vizuri kuwasimamisha kazi walinzi pasipo kutangaza kwani si salama kwa wanyama wetu.
Haya ndiyo maoni yangu.