Mimi kabla sijany'ongwa nakunyonga wewe - Balozi Kagasheki

Walau amethubutu, is it sustainable?

Kagasheki afanye zaidi yahapo tumumini zaidi.

a) Tukamatie waliobeba twiga wetu. Lakini hasa mapapa ilitujue ilikuwaje ndege ya jeshi la inchi nyingine ingie na kubeba wanyama wetu kama vile inteligensia ya Mkuu wako haipo au ipo kuvidhibiti vyama vya upinzani tuu??

b) Na hao walio uwa Faru wetu sheria ichukuwe mkondo bila mizwengwe na kwa kipindi kifupi waende kifungon.

Tunashindwa kuwaamini viongozi wetu, siku zote mnafanya mambo ya nguvu ya soda na kutuaminsha hewa pasi na utendaji wa haki na kizalendo.
 
Kweli inabidi tupongeze japokuwa safari ni ndefu,tatizo la viongozi wetu hata viapo vyao vinakwamisha kuepuka au kukata kupokea atayoamriwa na rais. Wanapoapa wanasema nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na naahidi kuilinda na kuhifadhi katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ee Mungu nisaidie.Kiapo hiki tayari kina mapungufu kwani hakijafafanua kwa mambo yenye maslahi ya nchi na wananchi,labda uwe kama Magufuli haambiliki na mwenye mtazamo chanya
 
Mh Kagasheki mi mi ni muumini m zuri wa utendaji wako uliotukuka.Tena naamini una utashishi na dhamira ya kweli katika kuwatumikia wananchi,lakini hofu yangu kubwa ni kuingiliwa na kupata mashinikizo kama ya mama Tibaijuka. Mama huyu alianza vizuri sana na kujenga imani kwa wananchi hususani kwa staili yake ya kukagua viwanja na kutoa amri kali kuvunja uzio ambalo ulikuwa ni maeneo ya wazi,lakini kasi yake haieleweki imefikia wapi ilihali kesi nyingi ambazo zinatishia amani ya nchi hii zitasababishwa na migogoro ya ardhi ndani ya Tanzania yetu tunayoipenda kwa moyo wetu wote. Umeanza vizuri bila kuwafumbia macho wala kumung'unya maneno lakini je kasi hii itakuwa ni ya kudumu au ndio nguvu ya soda?Historia inatukumbusha kuwa viongozi wengi wa serikali walio beba dhamira ya dhati kuwatumikia wananchi wengi wameanguka kutokana na kushindwa kusimamia wananchi na kulinda rasilimali za taifa ama kwa kupata mashinikizo toka kwa wakubwa wao waliowateuwa wakisahau kuwa ameapa kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzani. Wakati fulani ilinipa wakati mgumu kutokana na uamuzi wa rais kushindw kukupa uwaziri kamili wakati utendaji wako ni wa viwango vya juu,kwa hili aliloliona mh rais kukuteua waziri kamili ametutendea haki wananchi ila cha msingi zingatia heshima yako kama mwanadiplomasia isidondoke kwa kusababishwa na mashinikizo ya wakubwa zako,kilicho muhimu tenda kwa uaminifu bila kuvunja sheria wala kumuonea mtu.Mungu akusaidie katika mjukumu yako ya kila siku.

- Apewe nafasi afanye vitu vyake, ameingia huko amekuta madudu ya kutisha sana, mengine wala hayatakuja kusemwa to the public maana ni aibu sana kwa aliyepita, aachwe kama alivyoanza afanye vitu vyake, akiharibu ndio tumshike shati, lakini ameanza vizuri kumbe tunao viongozi wanaoweza bila kuoneana aibu, saafi sana mehshimiwa, BRAVO SANA!!

William.
 
Watanzania ni watu tunaodanganyika kiurahisi sana!

Huyu Kagasheki si alikuwaga wizara ya mambo ya ndani wakati Polisi wetu
(japo hatuwapendi kwa kutumiwa kwao) walikuwa wanapunjwa zile posho zao mpaka Lema akakisanua kwenye hotuba yake ya kambi ya upinzani??
Mbele ya siasa dhaifu hakuna kiongozi wa kujitangaza jembe!

- Mheshimiwa Kagasheki, hajawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ila alikuwa Waziri Mdogo, na kisheria mwenye mamlaka ya mwisho kwenye Wizara ni Waziri sio Waziri Mdogo!!

Mkuu W. J. Malecela hata baba yako alikuwa na mkwara huo lakini unaona alikotufikisha Mama yako mpaka povu huwa linamtoka lakini ilipokuja kusigne petition ya zito akaingia mitini
 
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.

Ukivunja taratibu si mbaya cha muhimu kama kuna utaratibu unaolinda wezi ni muhimu ukaanza kuangaliwa ili watu wasitumie loophall
 
ukitaka kujua kuwa atachemka, fuatilia jinsi yule mpakistan wa wänyama haina pale KIA, alivyochikichia, ndo utajua jinsi RA alivyona nguvu kubwa mbugani.
Katika hali halisi,serikali hii kamwe haitaweza kusafisha maovu yaliyopo ila inaweza kuyaimarisha tu ili kuipa wakati mgumu serikali ijayo ya wazalendo nahisi.
 
Mkuu W. J. Malecela hata baba yako alikuwa na mkwara huo lakini unaona alikotufikisha Mama yako mpaka povu huwa linamtoka lakini ilipokuja kusigne petition ya zito akaingia mitini

Precise,

Baba na mama yake wanahusika nini na mawazo yake au na mada hii? Kama umefirisika kupinga hoja kwa hoja kaa kimya.
 
Kwani baba yake hajawahi kushika uwaziri mkuu? Alifanya nini cha maana zaidi ya kufisadi hii nchi na alikuwa na mikwara kama ya Kagasheki. wewe ndio uliyefilisika kihoja unatetea wezi na watoto zao humu jamvini
 
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.

Hapa huyu Mh. KG amekwenda kasi sana!
 
Kwani baba yake hajawahi kushika uwaziri mkuu? Alifanya nini cha maana zaidi ya kufisadi hii nchi na alikuwa na mikwara kama ya Kagasheki. wewe ndio uliyefilisika kihoja unatetea wezi na watoto zao humu jamvini

Ndio baba yake alishika uwaziri. Lakini cheo cha baba yake kinahusiana vipi na hoja za hapa? Kama wewe unaamini dini: Uislamu au Ukristo. Huyu jamaa atasimama pekee yake kujibu yale aliyofanya duniani kwa Mwenyezi Mungu. Sasa kwanini wewe unataka kumuhukumu kwa kumuhusisha na yale aliyofanya baba yake?
 
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.

Wewe nachelea kusema unaropoka au una ujinga wa kutofahamu unachokiongelea.nakuomba nikufahamishe kama ifuatavyo mjinga wewe.

Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) ni miongoni mwa mashirika yanayowajibika moja kwa moja kwa wizara ya maliasili na utalii.moja kati ya majukumu yake makuu ikiwa ni kuhifadhi na kulinda maliasili zote zilizoko ndani ya mipaka ya hifadhi za taifa,ikiwa ni pamoja na viumbe hai wote pamoja na mimea hai na mfu kama kuni.

Ni kosa kwa mtu yeyote ambaye si muajiliwa ndani ya hifadhi kuingia ndani ya hifadhi bila kibali maalumu, au malipo halali na kwa kupitia katika milango rasmi ya kuingilia na kutoka hifadhini.ikiwa ni kwa muda maalumu na atatoka kulingana na kibali au malipo yake kukaa ndani ya hifadhi kuisha,

FARU KUUAWA.
Tukio hili lilitokea kwa mara ya pili,huko katika eneo la kusini magharibi pakijulikana kama MORU AREA,eneo hili lina ulinzi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na vifaa vizuri vya kisasa vya ulinzi wa wanyama pori ikiwemo magari mazuri ya kisasa,askari wenye mafunzo maalumu ya ulinzi wa wanyama pori pamoja na silaha nzuri za kisasa.achilia mbali makazi mazuri ya kuishi askari hao na vifaa vya mawasiliano na viona mbali vikubwa na vya kisasa kabisa.

Pamoja na hayo yote lakini faru aliuawa na majangili bila hawa walinzi kuwa na taarifa lakini pia siku kadhaa baada ya faru kuuawa,mkuu wa kituo husika aliendelea kutoa taarifa ya makabidhiano ya faru makao makuu ya hifadhi ya serengeti kwamba faru wale wako hai na salama.

Mpaka pale wasamaria wema walipotoa taarifa ya kuuona mizoga miwili ya FARU walioonekana wakiwa wameishauawa.jambo ambalo lilimlazimu mkuu wa hifadhi kufuatilia na kubaini ukweli katika eneo la tukio.wakati huo askari wale wakiwa bado wakitoa taarifa ya faru kuwa hai.

Sasa pamoja na yule mkuu kubaini tukio hilo bado aliishia kumuweka yule mkuu wa kituo chini ya ulinzi kwa muda mfupi katika kituo cha polisi pale seronera na kisha kudhaminiwa.lakini pia kuna tetersi kuwa mkuu yule wa kituo alikuwa na tuhuma kadhaa za kukutwa na ama masalia ya nyama za wanyama pori au mnyama kamili(si faru)

Na pia utawala wa TANAPA makao makuu hawakuweza kuchukuwa hatua zozote za msingi kutokana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwashikilia wahusika mpaka upelelezi kamili ambapo ungekamilika.

Mimi binafsi nilikuwepo siku faru hao wakipokelewa na kukabidhiewa kwa Mh Rais kikwete wakitokea afrika kusini.na nilimshuhudia rais akitoa kauli yake kwamba faru wale wapewe ulinzi kuliko anaopewa yeye.

Pia niliona na kutathmini zoezi zima lilivyokuwa na thamani kubwa kupita maelezo na likikutanisha watu mbnalimbqli maarufu duniani viongozi na wafadhili pia.

KAGASHEKI,amechukuwa hatua stahiki tena kwa wakati muafaka tukizingatia viongozi wetu wengi ni waoga kwa kuchukua maamuzi magumu kama haya ya Kagasheki.na tulipaswa kumpongeza na si kumponda.

ALLUTTA CONTINUA........

Watanzania tuanze kuwa na tabia ya kuwapongeza viongozi wetu pale ambapo wanachukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi au jambo lolote ambalo ni la kidhalimu.hii itawapa morali na pia kujiamini katika nafasi zao kiutendaji.

.
 
- Mheshimiwa Kagasheki, hajawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ila alikuwa Waziri Mdogo, na kisheria mwenye mamlaka ya mwisho kwenye Wizara ni Waziri sio Waziri Mdogo!!

William.

Marazote ninapo post hapa nipo makini sana, sababu najua kuna watu kama nyie mnatafutiza upenyo wa kuhalalisha yale mnayoona yanaridhisha hoja zenu.....

Vipi mkuu, hoja ya kuwajibika kwa pamoja huwa inaishia na kuanzia wapi???
 
Uwajibikaji wa pamoja ni ule wa kushiriki pamoja katika maamuzi na utekelezaji wa shughuli zote za umma. Ukija tazama kwa mfumo wa baraza letu la mawaziri wenye mamlaka ya mwisho kiwizara ni waziri na si naibu waziri.ndiyo maana utasikia waziri husika atasimamia suala fulani kisheria,tofauti na naibu waziri.Kwa suala la Kagasheki,yeye alikuwa naibu waziri toka enzi ya Masha na Nahodha.Ndiye aliyejaribu kwa nafasi aliyo nayo kufuatilia maslahi ya polisi kwa nafasi yake hadi alipoteuliwa kuwa waziri kamili.Sasa basi tumhukumu kwa nafasi aliyopewa lwa kuwa sasa ni full mandate.
 
Wewe nachelea kusema unaropoka au una ujinga wa kutofahamu unachokiongelea.nakuomba nikufahamishe kama ifuatavyo mjinga wewe.

Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) ni miongoni mwa mashirika yanayowajibika moja kwa moja kwa wizara ya maliasili na utalii.moja kati ya majukumu yake makuu ikiwa ni kuhifadhi na kulinda maliasili zote zilizoko ndani ya mipaka ya hifadhi za taifa,ikiwa ni pamoja na viumbe hai wote pamoja na mimea hai na mfu kama kuni.

Ni kosa kwa mtu yeyote ambaye si muajiliwa ndani ya hifadhi kuingia ndani ya hifadhi bila kibali maalumu, au malipo halali na kwa kupitia katika milango rasmi ya kuingilia na kutoka hifadhini.ikiwa ni kwa muda maalumu na atatoka kulingana na kibali au malipo yake kukaa ndani ya hifadhi kuisha,

FARU KUUAWA.
Tukio hili lilitokea kwa mara ya pili,huko katika eneo la kusini magharibi pakijulikana kama MORU AREA,eneo hili lina ulinzi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na vifaa vizuri vya kisasa vya ulinzi wa wanyama pori ikiwemo magari mazuri ya kisasa,askari wenye mafunzo maalumu ya ulinzi wa wanyama pori pamoja na silaha nzuri za kisasa.achilia mbali makazi mazuri ya kuishi askari hao na vifaa vya mawasiliano na viona mbali vikubwa na vya kisasa kabisa.

Pamoja na hayo yote lakini faru aliuawa na majangili bila hawa walinzi kuwa na taarifa lakini pia siku kadhaa baada ya faru kuuawa,mkuu wa kituo husika aliendelea kutoa taarifa ya makabidhiano ya faru makao makuu ya hifadhi ya serengeti kwamba faru wale wako hai na salama.

Mpaka pale wasamaria wema walipotoa taarifa ya kuuona mizoga miwili ya FARU walioonekana wakiwa wameishauawa.jambo ambalo lilimlazimu mkuu wa hifadhi kufuatilia na kubaini ukweli katika eneo la tukio.wakati huo askari wale wakiwa bado wakitoa taarifa ya faru kuwa hai.

Sasa pamoja na yule mkuu kubaini tukio hilo bado aliishia kumuweka yule mkuu wa kituo chini ya ulinzi kwa muda mfupi katika kituo cha polisi pale seronera na kisha kudhaminiwa.lakini pia kuna tetersi kuwa mkuu yule wa kituo alikuwa na tuhuma kadhaa za kukutwa na ama masalia ya nyama za wanyama pori au mnyama kamili(si faru)

Na pia utawala wa TANAPA makao makuu hawakuweza kuchukuwa hatua zozote za msingi kutokana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwashikilia wahusika mpaka upelelezi kamili ambapo ungekamilika.

Mimi binafsi nilikuwepo siku faru hao wakipokelewa na kukabidhiewa kwa Mh Rais kikwete wakitokea afrika kusini.na nilimshuhudia rais akitoa kauli yake kwamba faru wale wapewe ulinzi kuliko anaopewa yeye.

Pia niliona na kutathmini zoezi zima lilivyokuwa na thamani kubwa kupita maelezo na likikutanisha watu mbnalimbqli maarufu duniani viongozi na wafadhili pia.

KAGASHEKI,amechukuwa hatua stahiki tena kwa wakati muafaka tukizingatia viongozi wetu wengi ni waoga kwa kuchukua maamuzi magumu kama haya ya Kagasheki.na tulipaswa kumpongeza na si kumponda.

ALLUTTA CONTINUA........

Watanzania tuanze kuwa na tabia ya kuwapongeza viongozi wetu pale ambapo wanachukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi au jambo lolote ambalo ni la kidhalimu.hii itawapa morali na pia kujiamini katika nafasi zao kiutendaji.

.

Commonmwananchi. kwa navyotambua Hifadhi ya Serengeti ina miradi mitatu ya Faru ambayo ni Mradi wa Moru, Mradi wa Ndasiata maarufu kama Faru wa JK na mradi wa Nyamarubwa. Faru waliyouwawa mwaka huu ni wa Moru ambako haukuwepo wakati wa kuwapokea kama ulivyojieleza. Faru wa JK wamebakia watatu baada ya mmoja kuuwawa kwa ujangili mwaka 2010 na mmoja kufa kwa ugonjwa mwaka jana.

Muhimu ni watanzania kutambua kuwa ujangili ni tatizo kubwa hapa nchini na nchi nyingine barani africa. Kwa mawazo yangu siamini kama ukiwasimamisha kazi watumishi utazuia ujangili. Ni vizuri watumishi kuchukuliwa hatua hususani kufukuzwa kazi kwa wale wasiowaadilifu baada ya kubaini makosa yao. Kiulinzi ni vizuri kuwasimamisha kazi walinzi pasipo kutangaza kwani si salama kwa wanyama wetu.

Haya ndiyo maoni yangu.
 
Waziri Tibaijuka ni feki kweli kweli, makazi na viwanja yako wapi au mpaka wahisani??? viwanja bei juu ardhi imegeuzwa biashara kwa afisa ardhi uko wapi???
 
Uwajibikaji wa pamoja ni kutekeleza maamuzi na kusimamia utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa kwa pamoja. Kwa mfumo wa baraza letu la mawaziri,waziri atawajibika moja kwa moja kwa wizara husika na kutekeleza yale yote yanayohusu wizara hiyo.Tena ukitazama utaona hata mikataba yote ya wizara anaye husika kuisaini ni waziri na naibu waziri.Kazi ya naibu waziri ni kumsaidi waziri kusimamia utekelezaji wa majukum ya wizara na kumshauri pale inapobidi. Hali ndiyo iliyopelekea kuhoji kuna haja gani ya kuwa na naibu wakati wizara ina makatibu wakuu na wakurugenzi ambao kazi zao zimeainishwa kisheria. Kwa suala la Kagasheki,utaona kwamba yeye muda wake wote amekuwa chini ya mamalaka ya waziri mwenye dhamana hiyo,kumhukumu kwasasa ni kutokumtendea haki japokuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa kiutendaji alipokuwa naibu waziri wa mambo ya ndani.
 
Commonmwananchi. kwa navyotambua Hifadhi ya Serengeti ina miradi mitatu ya Faru ambayo ni Mradi wa Moru, Mradi wa Ndasiata maarufu kama Faru wa JK na mradi wa Nyamarubwa. Faru waliyouwawa mwaka huu ni wa Moru ambako haukuwepo wakati wa kuwapokea kama ulivyojieleza. Faru wa JK wamebakia watatu baada ya mmoja kuuwawa kwa ujangili mwaka 2010 na mmoja kufa kwa ugonjwa mwaka jana.

Muhimu ni watanzania kutambua kuwa ujangili ni tatizo kubwa hapa nchini na nchi nyingine barani africa. Kwa mawazo yangu siamini kama ukiwasimamisha kazi watumishi utazuia ujangili. Ni vizuri watumishi kuchukuliwa hatua hususani kufukuzwa kazi kwa wale wasiowaadilifu baada ya kubaini makosa yao. Kiulinzi ni vizuri kuwasimamisha kazi walinzi pasipo kutangaza kwani si salama kwa wanyama wetu.

Haya ndiyo maoni yangu.

Kihorohonjo
Nakushukuru kwa kuchangia kwa jinsi unavyoelewa wewe.ukweli ni kwamba kuna faru katika makundi tajwa lakini ni mawili,Moru kopjes na hao wa JK kule ndasiata hills.na pia nakufahamisha kuwa kuna uhamisho uliofanyika wa ndani kwa ndani ambao huenda ni kwa sababu za kiusalama pia.hii ni kutokana na habari nilizoelezwa na mmoja wa watumishni ndani ya hifadhi wakati nilipoulizia ili kujua undani wa suala hilo.

Suala la kusimamishwa kazi maaskari husika ni pamoja na kupisha uchunguzi huru ufanyike bila kuingiliwa au kuvurugwa.

Na pia sioni tishio lolote ambalo linaweza tokea kutokana na habari hizi kutangazwa na pia askari walioajiliwa katika hifadhi ni wengi wa kutosha kuziba pengo la hao waliosimamishwa. na pia wengine wanaweza toka katika hifadhi zingine na kuja kuimarisha ulinzi na hata ikibidi waajiliwe wapya kwani ni jana tu kulikuwa na mahafali ya wahitimu katika chuo cha pasiansi
Kule mwanza.

Ujangili unachipukia kwa kasi sana sasa hivi na hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa kwea wahusika pale inapobainika uzembe au ufisadi fulani kwa maliasili zetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom