Mimi kabla sijany'ongwa nakunyonga wewe - Balozi Kagasheki

nimeipenda hii kauli ya waziri wa mali asili na utalii wakati akikabiziwa ofisi na waziri mstaafu Maige. Hii inaonesha kwamba huenda huyu jamaa amejipanga kukabiliana na viwavi.
source tbc1

Watanzania mbona tunapenda kuwapa watu heshima za kijinga...huu ustaafu uko wapi? waziri hastaafu wala kustaafishwa anaondoka kwa kujiuzulu, kushindwa ubunge, au kufukuzwa kazi huyu maige amefutwa kazi yaani alikosa imani ya Boss wake akaondolewa.
 
Angeongea wa cdm angekuwa ameshahojiwa na polisi siku mbili, ccm wangekuwa wameshaandamana, vyombo vyao ya habari vingeirudiarudia na kukemea mara mia! Lakini kwa kuwa ni mwenzao, wanampongeza sana! Upuuzi mtupu!!!!!

acha ushabiki upofu wa siasa wewe..kauli ya Nassari ilikua ya kipuuzi, kijinga, kipumbavu na inayonyesha kukosekana kwa umakini kwa huyu jamaa na ubunge wake utakua wa miaka 2.5 tu. CDM kama chama makini kingebidi kitoe statement kurekebisha ile kauli.
 
Kuna bwana mmoja anamiliki kitalu cha kuwinda alikuwa ananielezea jinsi wanavyotoa rushwa kupata hivyo vitalu yaani ni balaa! Hao wanaoidhinisha hivyo vitalu ni mabilionea maana hawa mabwana wanaushawishi mkubwa mno wa pesa!

Namtakia kila la kheri balozi, tafadhali sana ziba mianya yote na hawa wa vitalu naomba utaratibu ufuatwe. Kumpa mtu kitalu hata hajaomba kitalu chenyewe ni aibu kubwa!
 
nimeipenda hii kauli ya waziri wa mali asili na utalii wakati akikabiziwa ofisi na waziri mstaafu Maige. Hii inaonesha kwamba huenda huyu jamaa amejipanga kukabiliana na viwavi.

Kauli hizi tulishazizoea siku nyingi sana ni kama miaka 50 iliyopita hivi.Huu ni muendelezo tu wa kauli za viongozi wetu mara wanapochaguliwa/kuteuliwa huwa ni wakali sana.Tatizo la Watanzania wengi ni wasahaulifu sana nnaomba msizisahau ahadi za Jk ni ngapi zilishatekelezwa mpaka sasa hivi?Viongozi wanapoingia madarakani wanawapa wananchi matumaini sana na baada ya hapo hawaonekani wakiyasimamia maneno yao(ahadi)kwa vitendo na inawezekana kabisa viongozi wetu hawa wanatudharau kwa kuujua udhaifu wa wananchi wao.
 
nimeipenda hii kauli ya waziri wa mali asili na utalii wakati akikabiziwa ofisi na waziri mstaafu Maige. Hii inaonesha kwamba huenda huyu jamaa amejipanga kukabiliana na viwavi.

Ha ha ha we acha kujifurahisha.hapo kwenye blue ni kweli huyo ni mstaafu au amestaafishwa na kufukuzwa kazini?Kapenda kuachia ngazi?Ameachishwa.Yale yale ya Edward Lowassa mstaafu au kajiuzulu?Acha ujinga kidogo.
 
- Maneno mazito sana hayo, yanaonyesha the man is serious, ndio tunachotaka sio kwenda huko kwenye wizara kuuuza meno na kucheka cheka, lazima wafanyakazi wajue sasa kazi, saafi sana mleta mada UBARIKIWE TU!

William.
Mkuu Malecela, uzoefu katika nchi yetu unaonesha kauri za viongozi wetu na matendo yao hutofautiana sana!
 
tunachohitaji hapa ni vitendo na wala sio maneno.tukihitaji maneno tutanunua kanga au tutamtafuta makamba retired.
 
Alikwina- sia alikua waziri mdogo wa mambo ya ndani, alikua na uwezo wa kuwakamata hao waliosafirisha twiga wetu nje na wanyama wengine, alifanya effort gani hata kufuatilia au kutuma taarifa za kiitelejensia hazikumfikia, na Polisi walivyokuwa wanatumia nguvu nyingi kudhibiti wapinzani na kuwaachia majambazi alikua wapi, hamna kitu hapa kama mnabisha muulizeni Sitta
 
Kagasheki time to walk the talk, taifa limekusikia; linakuangalia! usije ukaanza visingizio eti unapigwa majungu!! pale kuna mchwa waliokubuhu, angalia sana leseni, uvunaji wa maliasili, vitalo vya uwindaji, huko ndio ulaji uliko na hao watu wamezoea, kwao it is business as usual.
 
Nikisikia Kamran kaondolewa nchini na TANAPA kumesafishwa na pia kusitisha mtindo wa kugongea visa 'wageni wa wakubwa wangali bado kwenye ndege basi nitaamini maneno yake!
 
Kagasheki waterere hao wezi wa mifugo ya nchi. sasa na yeye asiwe mwanasiasa kwenye nyaraka za serikali aka Twiga
 
hakuna kitu hizo ndo zenu magamba na kauli za kisanii mfano kilimo kwanza etc, twahitaji vitendo sio nahau

Kama ni kweli awanyonge kwanza wale waliosafirisha twiga hai ndipo tutakuwa na imani naye.
 
hana ubavu nchi hii haitaji maneno inahitaji utendaji huku ni kutishia nyau mtu mzima ndio corruption itaongezeka zaidi maana hii idara usiseme, mengi ya mejificha hataweza ni kelele za chura kumzuia ng'ombe kunywa maji
 
Balozi Kagasheki said:
Mimi nataka kufanya kazi kwa kushirikiana na sio kwa ugomvi: waziri haelewani na naibu wake; vurugu tupu. Hii inaondoa ufanisi katika kazi na kama naibu waziri na waziri wanashindwa kuelewana itasababisha hata watendaji wa ngazi ya chini kushindwa kuelewana pia.

Katika Bunge lililopita mbunge mmoja alitaka mawaziri wabadhirifu wanyongwe au wapigwe risasi mimi sitaki kufikia huko nitawanyonga wafanyakazi wabadhirifu kabla ya kunyongwa mimi; nasema hili kwa nia njema kabisa na sio kutisha watu.

Kwa usanii hakuna kama viongozi wa CCM na baya zaidi ni kuwa hawajifunzi, sijui ni unafiki wao, ulimbukeni wao, ukilaza wao au ni ulafi tu. Ukweli ni kuwa aidha wizara yake haitafikia huko na hivyo haitakuwapo na haja ya kunyongana au itafika huko ikiwa na maana kuwa yeye mwenyewe ameshiriki kikamilifu kulifikisha hapo.

Hilo moja, lakini la pili, kwa kuwa yeye ni mteuliwa tu, itakuwaje kama wizara itafika huko kwa maelekezo ya bosi wake? Je atakuwa tayari kumnyonga bosi wake kabla ya yeye kukubali kunyongwa? Mbona huyu Balozi ana kumbukumbu fupi sana, amesahau yaliyomkuta Nyamongo akiwa Waziri mdogo wa Mambo ya Ndani kuhusu Barrick gold?

Je Balozi amesahau yaliyowakuta wale wote waliothubutu angalau kufurukuta baada tu ya kuteuliwa kama dadake Profesa Tibaijuka na wengineo. Huo moto anaodai yuko tayari kuanza nao mbona kama wa kifuu tu na je utazidi moto ule wa bosi wake 2005? Balozi Kagasheki acha unafiki, tulia ule kama nguruwe wenzako huko CCM...siku zenu zahesabika!
 
Mbona huyu waziri ana hatarisha hali ya amani lkn sijasikia akitafutwa kuhojiwa? Kuna sheria tz inaruhusu mtu kumnyonga mwenzake?
 
Ishomire anasema tu hajaijua vizuri wizara ile ina backward and forward linkages kibao..ni ngumu kama nini...alikwenda Diallo pale wakasema hana njaa ataiweza akajaribu kumng'oa Severe Mkurugenzi wa Wanyamapori, akaambulia kung'olewa yeye, akaja Maghembe akajaribu kupandisha royalty rates za miti na vitalu, wenye vitalu wakalalamika akaambulia kung'olewa yeye, akaja Mwangunga akajaribu kutikisa yakamshinda (alilia na kupiga magoti bungeni kule ili asijiuzulu na ndio ilikuwa salama yake) huruma ya kike ilimwokoa, akaamua kuungana nao. Maige amejaribu kutikisa pale ameambulia kuitwa fisadi.....Hv kuna mkubwa gani anayeogopwa pale maliasili asiye hata na jina anayeweza kusafirisha twiga wakubwa kwenye ndege kupelekwa nje halafu iwe inachukuliwa kirahisi tu kama ilivyo sasa???nani anaweza kugawa tu vitalu pale maliasili hata kwa mtu asiyeomba halafu iwe rahisi tu??? Nani anayejua orodha ya wamiliki wa vitalu...hebu fikiria mw/kiti wa bodi ya Ngorongoro ni Msekwa, kabla marehemu mzee kawawa hajafa alikuwa ana vitalu kadhaa, hatujui alimwachia nani.kuna akina Kinana wana biashara za mambo hayo hayo...hawa watu wote wapo karibu sana na Ikulu za awamu zote tatu.....na hii ya nne....mie siamini kama watumishi wa maliasili ni wezi au mafisadi kuliko wa wizara nyingine..kuna akina Dr. Prof. Iddi alirudi zake SUA vimemo vilimshinda...Dr. Kilahama alikuwa vibrant kabla ya kuwa mkurugenzi wa misitu sasa kanyamazishwa ili astaafu kwa amani....kuna Tarimo mlokole wa watu alishinikizwa kusaini madude yakamtokea puani akastaafishwa kabla ya muda wake na waadilifu wengine wengi tu. Infact ukiwa maliasili kama ni mtu safi unaogopa kwa sababu hutadumu..ukitaka kudumu uwe mtu wa ndiyo mzee watakushinikiza kuharibu yakilipuka utatolewa kafara lakini watakulinda kiaina....ndivyo ilivyo hata sasa...subirini muone kama Maige hatapewa cheo cha kuteuliwa hivi karibuni.....angalieni wote wanaoshutumiwa wangapi wapo jela achilia mbali walioshitakiwa au kufukuzwa??? Mie wala siamini kuwa mawaziri wote wanaowenda maliasili hushindwa kwa sababu ni wezi au wana njaa...Waziri aliyewahi kudumu kwa muda mrefu pale ni Meghji tu ambaye naye ameshutumiwa sana lakini hakuna kesi wala uchunguzi wowote ulifanyika juu yake...so mie nadhani tunawaonea tu raia wenzetu wa maliasili....Kagasheki hana lolote hajaijua tu ile wizara..baada ya siku chache tu mtasikia tayari kashaharibu...tatizo la malisili haliko pale na ni kubwa zaidi kuliko tunavyofikiria....naishia hapa
 
Back
Top Bottom