Mimi kabla sijany'ongwa nakunyonga wewe - Balozi Kagasheki

Huyu mpe tu miezi miwili atakuwa kimyaa, Kama hayupo vile. Twiga na faru bado wanahitajika nje huko, ni miradi ya watu hiyo.
Mimi nilijua mama Tibaijuka alirudi Nairobi, kumbe bado yupo. Ni yapi yaliyomsibu tena jamani mpaka anakosa makali.

''Mama vua gamba njoo huku tukuvishe gwanda, litakupendeza sana na litakupa uhuru wa kutenda".
 
Tatizo hapa kama nilivyosema hapo mwanzo,mfumo huu unahitaji chama kingine kwani imetafuna mpaka mapafu ya chama(kansa).Ndio maana leo utasikia mjumbe wa kamati ya bunge kupitia cha mapinduzi amekamatwa kwa kula rushwa.Kesho utasikia mwenyekiti wa kamati ya bunge amepewa offer ya safari ya Japan na Uchina ili kupindisha maamuzi ya kamati husika ili mradi kila kukicha kulindana na deal kwa kwenda mbele
 
Quote me on this: "Mwanasiasa yeyote anayekurupuka kufanya maamuzi kabla ya kusoma wizara, idara au wakala aliyopangiwa lazima atakuwa ana mapungufu ambayo yataonekana baadaye", kiongozi makini take time to study the fully system in all angles before.... making any decision wait and see".
 
Alishatuhabarisha kuwa wizara hiyo ina utajiri wa kutisha. kama huna moyo wa uvumilivu kam EM, basi utakwenda na maji. Tusubiri tuone, ni mapema mno kutabiri kama ufuatiliaji wake ni endelevu au ndo mambo ya kutumia media zaidi kufunika watu macho huku anakidhi appetite yake ya kuhodhi mali. tulishaona kwa mwenzake.
 
...hakuna kitu ni blah blah zile zile. Huyu ana marafiki wengi sana ambao pia ni wawindaji (jamaa zake mama Sitti) na hii sasa ni yy kutengeneza himaya yake, kama walivyofnya wengine ! Utasikia wamesimamishwa, then rudishwa na kulipwa mafweza kibao....
 
ndio, watanzania wengi tuna utamaduni wa uzembe na uvivu! Bila kuletewa mishemishe ufanisi zero! Rejea Maslow's theory x
 
kagasheki hana jipya kitumbua cha maliasili ni cha wakubwa...watu wanamiliki vitalu vya wanyama pori, mahoteli makubwa hifadhini na biashara za kusafirisha magogo na ndio mabosi wake...atawafanya nini changa la macho tu hapa hamna lolote
 
Kagasheki ni moja ya majembe mapya ya Jk yaliyoanza kulima vizuri ...... subira itatupa majibu...... tumuunge mkono wakati tunampa muda wa kutathmini ukali wa jembe hili.
 
[h=2][/h] Jumatano, Agosti 29, 2012 06:40 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

*Asema ataendelea kupambana na wanaohujumu Maliasili
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, amesema ataendelea kupambana na mitandao ambayo imekuwa ikihujumu sekta ya utalii nchini kwa sababu haogopi kufa.

Kagasheki aliitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua namna anavyopambana na mitandao ya watu wanaohujumu Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Katu siogopi kufa kwani kifo ameumbiwa mwanadamu na hakuna anayejua lini mwenzake atakufa, katika hili nitaendelea kulinda na kusimamia haki na sheria za nchi pamoja na kupambana na wale wanaohujumu wizara yangu.

“Nitapambana na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo ili kuweza kulinda heshima ya taifa langu kwa ujumla.

Kauli hiyo ya Waziri Kagasheki, imekuja baada ya kutokea kuwa mmoja wa mawaziri wanaopambana na vitendo vya kifisadi ndani ya wizara wanazoziongoza.

Hivi karibuni Waziri Kagasheki, aliwasimamisha kazi baadhi ya maofisa wa Idara ya Wanyamapori kwa kile alichosema kuwa walishindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha wanyama zaidi ya 100 wakiwamo twiga wanne, kutoroshwa na kupelekwa nchini Qatar.

Mbali na waliosimamishwa, pia aliwafukuza kazi maofisa kadhaa wa idara hiyo akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Obeid Mbagwa.

Awali, akifungua mkutano wa Umoja wa Mashirika yanayohusika na masuala ya utalii nchini, Waziri Kagasheki alisema, idadi ndogo ya watalii wanaoingia nchini inatia aibu kwa kuwa kuna vivutio vingi tofauti na nchi zingine barani Afrika.

Kutokana na hali hiyo, alisema umefika wakati wa kufanya tathmini ya kina ili kujua mbinu za kuwavutia watalii wengi.

Wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Waziri alisema, ipo haja ya kuongeza nguvu katika sekta hiyo ili iweze kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kila mwaka.

“Idadi ya watalii kwa hapa nchini inatia aibu ukilinganisha na nchi zingine za Afrika, jambo ambalo naona kuna haja ya kuongeza nguvu ya ziada katika kukabiliana na hali hii.

“Baadhi ya nchi zilinishangaza kwa kuwa na idadi kubwa kuliko ya Tanzania ambayo ni pamoja na nchi ya Kenya ambayo huingiza watalii milioni 1.4, Zimbabwe milioni 2.4 kwa mwaka.

“Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona kuna haja ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kisera na sheria ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta hii muhimu na nyeti.

“Kama kutakuwa na usimamizi mzuri katika sekta hii, pato la taifa litaongezeka kuliko ilivyo sasa na hili lazima tuliangalie kwa masilahi ya taifa.

“Sekta hii ya utalii huchangia asilimia 26 ya fedha za kigeni na katika pato la taifa ni sekta ya pili ikitanguliwa na sekta ya madini.

“Sasa kuna haja ya kuisimamia vyema sekta hii kwa kutangaza utalii wa ndani nje ya nchi ili iweze kurudi kuwa namba moja kama ilivyokuwa hapo awali,”alisema Kagasheki.

Alisema ni vema viongozi katika Sekta hiyo wakajijengea hali ya kufanyakazi kwa vitendo na si kwa maneno ili kuweza kupata mafanikio .

Balozi Kagasheki, alionya mitandao ambayo haiitakii mema Tanzania huku akiutaja mtando wa kompyuta wa Avaaz unaowataka watu wajiorodheshe kupinga kuhamishwa kwa Wamasai 48,000 kutoka Serengeti.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja ya vyombo vya habari vya nchini kuisaidia Serikali katika kuitangaza sekta hiyo kama vyombo vya habari vya Kenya vinavyofanya.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
...hamna lolote magamba hawa huyu anatafuta misifa tuu. YY shemegi zake mbona ni wadau wakubwa wa ufisadi ktk sekta hiyo hiyo ya maliasili ! Hapo kawekwa kwa kupigiwa chapuo na hao hao ili kulinda maslahi yao.

Eti idadi ya watalii inatia aibu ! Kwani nini isitie aibu wakati wanajua huko magetini kuna vitabu feki kibao na familia za hao hao akina Nagu ect ndiyo zimejaa huko na kutajirika kila kukicha. Mnaona kenya wana idadi kubwa na wananufaika lkn wengi wa hao watalii wanafaidi vivutio vyetu kwa njia za panya. Wahusika wanajulikana lkn hawaguswi sababu ni ndg wa vigogo wa chama na sirikali !! Kama ilivyokuwa serena lodges miaka ilee kulazimishwa kujengwa kila mahali, na sasa zote zimedoda huo uwanja Dhaifu aliomgawia Turdo utadoda na sana sana watakuwa wanatua wao na wale wezi wa wanyama !

Jumatano, Agosti 29, 2012 06:40 Na Bakari Kimwanga, Dar es Salaam

*Asema ataendelea kupambana na wanaohujumu Maliasili
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki, amesema ataendelea kupambana na mitandao ambayo imekuwa ikihujumu sekta ya utalii nchini kwa sababu haogopi kufa.

Kagasheki aliitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua namna anavyopambana na mitandao ya watu wanaohujumu Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Katu siogopi kufa kwani kifo ameumbiwa mwanadamu na hakuna anayejua lini mwenzake atakufa, katika hili nitaendelea kulinda na kusimamia haki na sheria za nchi pamoja na kupambana na wale wanaohujumu wizara yangu.

“Nitapambana na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo ili kuweza kulinda heshima ya taifa langu kwa ujumla.

Kauli hiyo ya Waziri Kagasheki, imekuja baada ya kutokea kuwa mmoja wa mawaziri wanaopambana na vitendo vya kifisadi ndani ya wizara wanazoziongoza.

Hivi karibuni Waziri Kagasheki, aliwasimamisha kazi baadhi ya maofisa wa Idara ya Wanyamapori kwa kile alichosema kuwa walishindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha wanyama zaidi ya 100 wakiwamo twiga wanne, kutoroshwa na kupelekwa nchini Qatar.

Mbali na waliosimamishwa, pia aliwafukuza kazi maofisa kadhaa wa idara hiyo akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Obeid Mbagwa.

Awali, akifungua mkutano wa Umoja wa Mashirika yanayohusika na masuala ya utalii nchini, Waziri Kagasheki alisema, idadi ndogo ya watalii wanaoingia nchini inatia aibu kwa kuwa kuna vivutio vingi tofauti na nchi zingine barani Afrika.

Kutokana na hali hiyo, alisema umefika wakati wa kufanya tathmini ya kina ili kujua mbinu za kuwavutia watalii wengi.

Wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Waziri alisema, ipo haja ya kuongeza nguvu katika sekta hiyo ili iweze kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kila mwaka.

“Idadi ya watalii kwa hapa nchini inatia aibu ukilinganisha na nchi zingine za Afrika, jambo ambalo naona kuna haja ya kuongeza nguvu ya ziada katika kukabiliana na hali hii.

“Baadhi ya nchi zilinishangaza kwa kuwa na idadi kubwa kuliko ya Tanzania ambayo ni pamoja na nchi ya Kenya ambayo huingiza watalii milioni 1.4, Zimbabwe milioni 2.4 kwa mwaka.

“Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona kuna haja ya kufanya marekebisho mbalimbali ya kisera na sheria ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta hii muhimu na nyeti.

“Kama kutakuwa na usimamizi mzuri katika sekta hii, pato la taifa litaongezeka kuliko ilivyo sasa na hili lazima tuliangalie kwa masilahi ya taifa.

“Sekta hii ya utalii huchangia asilimia 26 ya fedha za kigeni na katika pato la taifa ni sekta ya pili ikitanguliwa na sekta ya madini.

“Sasa kuna haja ya kuisimamia vyema sekta hii kwa kutangaza utalii wa ndani nje ya nchi ili iweze kurudi kuwa namba moja kama ilivyokuwa hapo awali,”alisema Kagasheki.

Alisema ni vema viongozi katika Sekta hiyo wakajijengea hali ya kufanyakazi kwa vitendo na si kwa maneno ili kuweza kupata mafanikio .

Balozi Kagasheki, alionya mitandao ambayo haiitakii mema Tanzania huku akiutaja mtando wa kompyuta wa Avaaz unaowataka watu wajiorodheshe kupinga kuhamishwa kwa Wamasai 48,000 kutoka Serengeti.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja ya vyombo vya habari vya nchini kuisaidia Serikali katika kuitangaza sekta hiyo kama vyombo vya habari vya Kenya vinavyofanya.

Toa Maoni yako kwa habari hii
 
Siku hizi kila waziri anasema haogopi kufa hamna kitu wanajidai tuu na yeye ataanza kupata michongo atatuibia tuu
 
Nini mawaziri,

Hata majambazi wanapoenda kazini hawaogopi kufa.

Kwa matendo yao utawajua, na ukiona longolongo zinazidi, saundi nyingi, ujue kazi zero hapo.

Watu wana cover.
 
hao walio fukuzwa muda si mrefu utasikia ni wakurugenzi au mabalozi nje ya nchi walipo weka pesa zao
 
kumbe huwa wanauana huko eenh...kauli ya "siogopi kufa",ni kubwa sana inashahabiana na ile ya "liwalo na lile"...
 
Atupe ukweli wa Serengeti wanayotaka kuuzia falme za kiarabu......Kama anataka kuifanyia haki Tanzania akomeshe uwindaji wa kijinga katika mbuga zetu.
 
Akiwa anakabidhiwa ofis ndani ya wizara ya mali asil na utalii,kagashek amewaambia watendaj wa wizara hiyo kuwa atawanyonga wale watakaoiteteresha wizara,,,,,
nadhan anamaanisha atawawajibisha.
Sos,clouds habar

Kagasheki kweli anamaanisha? Mbona hatuoni hatua zinazochukuliwa au anakosa support?
 
Back
Top Bottom