Mimi kabla sijany'ongwa nakunyonga wewe - Balozi Kagasheki

Kauli kama hizo tumezisikia mara nyingi sana, na hazina maana..ukweli ni kuwa kauli ni jambo moja na kuchukua hatua thabiti kuwakabili wezi wa hii nchi ni hatua nyingine ngumu sana kuchukuliwa hasa na watawala wa CHAMA CHA MAJAMBAZI aka CCM.

Ni kweli mkuu, hizo kauli huwa ni nguvu ya soda au moto wa mabua tu na tumezizoea. Hata Kikwete wakati anaingia madarakani mwaka 2005 alisema "hakuna tena kusaini mkataba wa uchimbaji wa madini wa kinyonyaji". Lakini haukupita muda mrefu Karamagi akaenda kusaini mkataba wa kinyonyajo huko London, Uiingereza.
Suala la kusafirisha wanyama hai, lilifanywa kwa ndege ya jeshi na ndege ya jeshi haingii nchi nyingine bila kibali cha jeshi la nchi hiyo. Kwa maana hiyo kuna mikono ya wakubwa kabisa wa nchi katika suala hilo. Lembeli alilalamika bungeni kuwa huko wizara ya mali asili na utalii watu wana kiburi mno, hicho kiburi si bure wanakula la wakubwa wa nchi. Kwahiyo Kagasheki anayo kazi huko si kidogo.
 
Filipo. Huo ni mkwara wa Kagasheki kuvuta pesa. CCM ingekua makini huyu jamaa hasingepitishwa kugombea ubunge,hafai kabisa. Anayebisha atafute aliondoka WIPO kule Geneva Uswizi kwa skandali gani! Ni aibu eti leo ni waziri mwandamizi ktk nchi yetu. Hiki chama ni chaka la wezi!

Naona hutaki kumalizia. Kagasheki aliondolewa kule Uswizi kwa kutuhumiwa kutafuna U$250,000 za WIPO.

Hapa ni mwizi kuwatisha wezi wenzake, na kwa kuwa wanamjua ni mwizi mwenzao sidhanim kama itakuwa ni kazi ngumu kumshirikisha mwenzao.
 
Naona hutaki kumalizia. Kagasheki aliondolewa kule Uswizi kwa kutuhumiwa kutafuna U$250,000 za WIPO.

Hapa ni mwizi kuwatisha wezi wenzake, na kwa kuwa wanamjua ni mwizi mwenzao sidhanim kama itakuwa ni kazi ngumu kumshirikisha mwenzao.

dah, hivi unao ushahidi wa haya madai yako? yaani hao waswisi wakuachie tu baada ya kuvuta
usd250,000! labda uwe na ushahidi na madai yako vinginevyo ulilofanya ni jitihada za kumchafua tu.
 
Filipo. Huo ni mkwara wa Kagasheki kuvuta pesa. CCM ingekua makini huyu jamaa hasingepitishwa kugombea ubunge,hafai kabisa. Anayebisha atafute aliondoka WIPO kule Geneva Uswizi kwa skandali gani! Ni aibu eti leo ni waziri mwandamizi ktk nchi yetu. Hiki chama ni chaka la wezi!

naamini hili lilishazungumzwa hapa ukumbini na watu walipoombwa walete data zaidi wakaumwaga.
labda wewe umepata ushahidi wa haya madai, hebu tuwekee basi hapa ukumbini. vinginevyo hizi ni jitihada
za kumchafua tu.
 
- Maneno mazito sana hayo, yanaonyesha the man is serious, ndio tunachotaka sio kwenda huko kwenye wizara kuuuza meno na kucheka cheka, lazima wafanyakazi wajue sasa kazi, saafi sana mleta mada UBARIKIWE TU!

William.

Huyu Mh. tunamjua utendajiwake, hakuingia leo kwenye baraza. Amekuwa naibu waziri wa Home affairs muda mrefu, lakini kule kwao kutoka wilaya moja haadi nyingine mpaka kusindikizwa na polisi Bml-Muleba, Chato-Bukombe, Ngara-Karagwe, Bukombe-Bml, nk. Leo amebadilika?? Haya ni maneno tu kapewa zawadi hiyo!!
 
Waziri wa maliasili utalii amewasimamisha askari 28,waden na mkuu wa intelijensia wa hifadhi ya serengeti kwa kushindwa kutoa taarifa wizarani kuhusu kuuwawa kwa faru ktk hifadhi hiyo.Faru huyo ni miongo mwa faru 5 ambao Jk aliwatoa kwa Zuma,mpaka sasa waliouwawa ni watatu.
Source ;Wapo fm
 
Hiyo sio dawa ya kufanya faru wasiuwawe... anatakiwa achunguze huyo mlinzi wa faru analipwa tshs ngapi na faru anauzwa tshs ngapi.. ! Nadhani hata wafanyakazi wa BOT na NMB hawafanani mishahara... lazma yule wa BOT alipwe zaidi coz BOT ni nyeti zaidi ya NMB..
 
sasa anayefukuza kazi mlinzi ni waziri? Kwani wakuu wa vitengo na taasisi kama TANAPA wako wapi wasichukue hatua stahiki?

Mi nilitegemea angemfukuza kazi mkurugenzi wa wanyama pori au TANAPA kwa kushindwa kusimamia au kutekeleza majukumu yake vizuri yeye anadeal na wengine kabisa

Huyu anatafuta umaarufu, tena cheap hakuna lolote
 
Waziri wa maliasili utalii amewasimamisha askari 28,waden na mkuu wa intelijensia wa hifadhi ya serengeti kwa kushindwa kutoa taarifa wizarani kuhusu kuuwawa kwa faru ktk hifadhi hiyo.Faru huyo ni miongo mwa faru 5 ambao Jk aliwatoa kwa Zuma,mpaka sasa waliouwawa ni watatu.
Source ;Wapo fm

hawa watu Mauige hakuwaona?????nimejiuliza hili swali kimyakimya
 
Labda amegundua mengi zaidi juu yao ambayo hatuyajui. Mie nahisi lazima ameuliza maswali na kujibiwa na hakuridhika hadi akachukua hatua hiyo. Sidhani kama muhaya huyo anaweza fukuza tuuuu. Ila si amemfukuza bosi wa hicho huko labda bila yeye habari hazitoki hapo serengeti.
 
Waziri amechemsha katika uamuzi wake pamoja na waliomshauri ni vilaza.
Kusimamisha askari 28 maana yake nguvu kazi yote ilokuwa inasimamia faru hao haitakuwa kazini kwa kudhani ametatua ndo ameongeza tatizo kwa sababu askari walio katika faru walifundishwa namna ya kufuatilia wanyama hao.Sitashangaa majangili wakiingia kuwawinda tena.
Pia faru hana immunity ya kutowindwa,anawindwa kama wanyama wengine kama alivyo tembo.
Waziri atafute vigogo wenzie ambao wanafanya biashara ya hizo pembe za faru na tembo kuliko kuwashukia watendaji wa chini.
Pia mbona hasemi neno kuhusu OCD na Afisa Usalama ambao walikamatwa wakichimba dhahabu huko Serengeti,na ni kipindi hicho hicho faru walipigwa je OCD na Afisa Usalama siyo kwamba wanajua hilo?
Nawasalimu sana JF.
 
Mh Kagasheki mimi ni muumini mzuri wa utendaji wako uliotukuka.Tena naamini una utashishi na dhamira ya kweli katika kuwatumikia wananchi, lakini hofu yangu kubwa ni kuingiliwa na kupata mashinikizo kama ya mama Tibaijuka.

Mama huyu alianza vizuri sana na kujenga imani kwa wananchi hususani kwa staili yake ya kukagua viwanja na kutoa amri kali kuvunja uzio ambalo ulikuwa ni maeneo ya wazi,lakini kasi yake haieleweki imefikia wapi ilihali kesi nyingi ambazo zinatishia amani ya nchi hii zitasababishwa na migogoro ya ardhi ndani ya Tanzania yetu tunayoipenda kwa moyo wetu wote.

Umeanza vizuri bila kuwafumbia macho wala kumung'unya maneno lakini je kasi hii itakuwa ni ya kudumu au ndio nguvu ya soda? Historia inatukumbusha kuwa viongozi wengi wa serikali walio beba dhamira ya dhati kuwatumikia wananchi wengi wameanguka kutokana na kushindwa kusimamia wananchi na kulinda rasilimali za taifa ama kwa kupata mashinikizo toka kwa wakubwa wao waliowateuwa wakisahau kuwa ameapa kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzani.

Wakati fulani ilinipa wakati mgumu kutokana na uamuzi wa rais kushindw kukupa uwaziri kamili wakati utendaji wako ni wa viwango vya juu,kwa hili aliloliona mh rais kukuteua waziri kamili ametutendea haki wananchi ila cha msingi zingatia heshima yako kama mwanadiplomasia isidondoke kwa kusababishwa na mashinikizo ya wakubwa zako,kilicho muhimu tenda kwa uaminifu bila kuvunja sheria wala kumuonea mtu.

Mungu akusaidie katika mjukumu yako ya kila siku.
 
Kagasheki hana lolote kachemka vibaya namshangaa waziri mzima anaingilia mamlaka asiyohusika nayo.Waziri anawasimamisha kazi walinzi TANAPA ?.Walinzi hawawajiki hata kwenye bodi ya TANAPA hawa ni wafanyakazi wadogo sana meneja mwajiri au mhifadhi mkuu Serengeti anatosha kuwasimamisha kazi au kuwafukuza kazi.

 
Hizo sifa zitathibitishwa tu pale watakaposhughulikiwa hawa wezi na kama serikali itaendelea kuwakumbatia ajiuzulu ndo ntakubaliana na wewe!
 
Watanzania ni watu tunaodanganyika kiurahisi sana!

Huyu Kagasheki si alikuwaga wizara ya mambo ya ndani wakati Polisi wetu
(japo hatuwapendi kwa kutumiwa kwao) walikuwa wanapunjwa zile posho zao mpaka Lema akakisanua kwenye hotuba yake ya kambi ya upinzani??
Mbele ya siasa dhaifu hakuna kiongozi wa kujitangaza jembe!
 
Back
Top Bottom