Mimi baba, sipendi mambo ya Housegirl

basi mnahela
anzeni kununua vitu vya supamarket ambavyo ni rahisi kupika
mtajenga mkipata pensheni zenu

Mimi ni mhasibu mama ni mchumi! muda wa kurudi home ni saa 4:30pm kwa wote. Huwa nipo tayari kumasaidia ila sema anapokuwepo housegirl nashindwa kumsaidia. ila napenda kumsaidia
 
NN, hutaki hausi gelo sababu ya lifestyle ya huko

Hapana. Sitaki hausigeli kwa sababu ninajua niko resourceful. I can do it by myself.

chakula cha supamarket almost kimetayarishwa vizuri wewe ni kwenda kumalizia tu

This is a canard! Kuna vyakula vingi tu ambavyo havijatayarishwa na ambavyo ukivinunua unatengeneza mlo wako from scratch. Ushaishi majuu wewe au unafuata tu kile usimuliwacho?

hapa siku nakula kuku nina kazi ya kumkimbiza, nimchinje, nimnyonyoe na kumpika

Not entirely true. Mimi mbona nikiendaga magengeni wananichinjia na kuninyonyolea? Acha ku paint picha isiyo entirely true.

huko mna maharage ya kopo, mie nina masaa 3 ya kusubiri maharage yaive kwenye mkaa

Ndiyo maana nimeuliza kama ushawahi kuishi majuu. Hata maharage ambayo hayajapikwa yapo na yapo mengi tu. Ni uamuzi wa mnunuzi na mlaji.

huko mna dishwasher hapa nika kazi ya kusugua sufuria kwa mchanga wa bahari

Kuwa na dishwasher hakukuzii kuosha vyombo kwa mikono. Na tena kama hujui, kuosha kwa mikono ni economical zaidi. Naanza kushawishika hujawahi kuishi majuu wewe.

mna washing mashine, nina kazi ya kufua, na kuanika nisubiri zikauke

Kwa hiyo?

maji na umeme 24/7 hapa maji yakitoka hatulali tunajaza hadi vijiko.
Siku nyingine zote ni ya kuchota kisimani au bomba la kijiji

Heheheheee poleni. Lakini sioni cha kushindwa kufanya mwenyewe hapo. Ukishindwa we mvivu au unajiona matawi ya juu.

umeme ungekuwepo ningechemsha maharage ya wiki nzima lakini siwezi andaa vitu na kutegemea kutunza kwenye friji sababu umeme sio wa uhakika

Hapo ndo resourcefulness inapokuja. Kama kweli shida huleta maarifa basi utaumiza kichwa chako na kubuni njia na mbinu za kukabiliana na hiyo adha. Lakini kama ukitaka mteremeko basi utaajiri hausigeli. I feel very sorry for them.

hata hivyo familia ngapi zinauwezo wa kumiliki friji?

Sijafanya sensa!

Huko unasafisha nyumba labda mara moja kwa wiki, hakuna vumbi lakini huku kudeki ndani kila siku is a must, kufuta madirisha na vitu vyote ndani vinginevyo utakuwa kama unakaa chini kwa vumbi

Hapa umeongeza chumvi, binzari, hoho, na nazi!

haya una watoto wadogo, huko mnapeleka day care centre, kwanza day care ni chache, ni gharama kubwa mtanzania wa kawaida hawezi kuaford hata kama inawezekana kuaford bado hazina usalama kwa watoto wadogo sana

Nami ni Mtanzania. Nimezaliwa na kukulia Tanzania. Nakumbuka kabisa kazini kwa wazazi wangu wote wawili kulikuwa na daycare centers. Ukikuna kichwa hakuna linaloshindikana. Kama enzi hizo kulikuwa na daycare centers huko makazini kwa nini sasa ishindikane? Ni ugoigoi wa kufikiri tu huo.

bado uende kazini na trafiki jam kama uko dar, sure you need someont to help you somewhere

Majuu hakuna traffic jams?

lifestyle ni tofauti na mazingira ni tofauti.

I'm still not convinced. Try again.
 
umemaliza yote mpendwa mpaka mtima wange umeshemelelwa
 
Tangu nifunge ndoa na mke wangu, yeye amekuwa akisisitiza kuwa na house girl, kila anayekuja anakuwa na vituko vya jabu, na wa mwisho ambaye tumemfukuza jana alikuwa eti ana majini tukisali na kulitaja jina la yesu anasumbuka, eti akawa anaomba tusisali na tukienda church tumuache. Sasa mimi nimemueleza wife tutafute mtu wa kuja kwa kutwa ila yeye eti anasisitiza mpaka mtu wa kuishi naye, unajua namshangaa, na ndiyo utamaduni wa wanawake woote sijui, mambo eti housgirl, housegirl, wanawake mtakoma lini?
maelezo yako mkuu ninaona hayajakamilika , umuhimu wa house girl unategemea na familia yako ilivyo. kama mkeo anafanya kazi basi ni muhimu kuwa na msaidizi, kama hafanyi kazi-yaani anashinda hme tu na hakuna watoto wadogo sana zaidi ya mmoja unaweza kusemna hahitajiki.
house girl nyumbani anasaidia
1. kazi za ndani
2. back up ya shughuli nyingine wakati wa dharula ndani ya family- kwamfano waweza mtuma mbali na nyumbani , mkoa mwingine kukuwakilisha ktk jambo lolote
3. ni walinzi pia, kwani unauhakika nyumbani kuna mtu- hili hasa kama wote hamshindi nyumbani na ni watu wa kusafiri

sasa housegirl wa kuja na kuondoka jioni faida zake ni kuwa
hahitaji kuwa mtu wa utamaduni au imani inayofanana na familia yako, kwakuwa anakuwa kazini muda mfupi tu.

hasara yake , ni kuwa
1. kwa kuja na kuondoka manake ni lazima umlipe mshahara wa mtu unaotosha kulipa nyumba na bills za umeme, maji nk
2. kwakuwa anatakiwa kujitegemea kila jambo huko anakokaa, wengi hushawishika kuwa wadokozi hapo ndani kwako au hata kuleta wezi wakubwa- kumbuka anahitaji kujilipia gharama za maisha.

ushauri wangu ni huu;
1. kama unaweza kumlipa kati ya 150,000-200,000 waweza chukua wa kuja na kurudi jioni, otherwise utajiingiza kwenye hasara kubwa
2. kwa kutumia sala na maombi utapata house girl mzuri, omba Mungu, uwe mvumilivu utampata siku moja. usimlaumu tu mkeo

kwaheri
 
Mimi ni mhasibu mama ni mchumi! muda wa kurudi home ni saa 4:30pm kwa wote. Huwa nipo tayari kumasaidia ila sema anapokuwepo housegirl nashindwa kumsaidia. ila napenda kumsaidia

bolded and red: Najaribu kuhusisha hiyo na 'theme' ya 'topic' hii sipati jawabu. Pengine sasa tunahitaji kila mtu atambulishe fani yake hapa!
 
2. kwa kutumia sala na maombi utapata house girl mzuri, omba Mungu, uwe mvumilivu utampata siku moja. usimlaumu tu mkeo

kwaheri

Maisha ni vita..........ili umpate mke bora yakupasa uombe.........kazi nzuri uombe............jirani mwem uombe..............yaani kila kitu ni maombi kwa kwenda mbele.............Sasa tunatakiwa hata beki tatu tuombe pia....Tatizo ni pale unapoomba na kuamini ulompata ndo jibu la ombi lako, halafu anakufanyizia vilevile..........!
 
Hapana. Sitaki hausigeli kwa sababu ninajua niko resourceful. I can do it by myself.

This is a canard! Kuna vyakula vingi tu ambavyo havijatayarishwa na ambavyo ukivinunua unatengeneza mlo wako from scratch. Ushaishi majuu wewe au unafuata tu kile usimuliwacho?

Not entirely true. Mimi mbona nikiendaga magengeni wananichinjia na kuninyonyolea? Acha ku paint picha isiyo entirely true.

Ndiyo maana nimeuliza kama ushawahi kuishi majuu. Hata maharage ambayo hayajapikwa yapo na yapo mengi tu. Ni uamuzi wa mnunuzi na mlaji.

Kuwa na dishwasher hakukuzii kuosha vyombo kwa mikono. Na tena kama hujui, kuosha kwa mikono ni economical zaidi. Naanza kushawishika hujawahi kuishi majuu wewe.

Kwa hiyo?

Heheheheee poleni. Lakini sioni cha kushindwa kufanya mwenyewe hapo. Ukishindwa we mvivu au unajiona matawi ya juu.

Hapo ndo resourcefulness inapokuja. Kama kweli shida huleta maarifa basi utaumiza kichwa chako na kubuni njia na mbinu za kukabiliana na hiyo adha. Lakini kama ukitaka mteremeko basi utaajiri hausigeli. I feel very sorry for them.

Sijafanya sensa!

Hapa umeongeza chumvi, binzari, hoho, na nazi!

Nami ni Mtanzania. Nimezaliwa na kukulia Tanzania. Nakumbuka kabisa kazini kwa wazazi wangu wote wawili kulikuwa na daycare centers. Ukikuna kichwa hakuna linaloshindikana. Kama enzi hizo kulikuwa na daycare centers huko makazini kwa nini sasa ishindikane? Ni ugoigoi wa kufikiri tu huo.

Majuu hakuna traffic jams?

I'm still not convinced. Try again.

Salutation for you kaka!
 
Kama hamna watoto mnaweza ishi bila.Yani hata huyo wa kuja anakua sio wa kila siku bali mara chache ndani ya wiki kuwasaidia kufanya usafi labda na kufua.Chakula na vyombo vyenu mnashughulikia wenyewe.

Lizy, hii inategemea mnafanya kazi wapi na mtoka.kurudi nyumbani saa ngapi. All in all, haya yote yanawez akumrudia mwanamke, maana mkirudi mwanaume ataa kwenye coach, hafanyi lolote, na jioni anataka huduma za kitandani.
 
..Wengine humu wanajibu kutokana na personal experiences zao kwamba wanahitaji au hawahitaji..ili ku-reflect cha kumjibu muanzisha thread. Ila tukiangalia reality makazini kuna stress sana jamani,mdada utoke kazini saa 10.30 jioni unaparamia daladala au una-drive unaganda kwenye foleni weee-..then ufike home uanze shughuli za mapishi..mume nae atake haki yake usiku...inachosha kwakweli..! Mume akiwa ni mwepesi wa kusaidia..atlist but ni wanaume wachache sana wenye moyo kama huo. Na nyumba haitakiwi kuwa empty kila siku, sio vizuri...ikifika weekend mtu unakuwa na kazi moja tu kusafisha nyumba na usafi mwingine kwa ujumla,hata weekend yenyewe unaiona chungu..na kwa wale wanaokwenda makazini mpaka saturday ndio wanatia huruma kabisaa...

#M-convince mkeo huyo housegirl awe anakuja na kuondoka...ili na nyie mpate muda wa ku-enjoy matunda ya kazi zenu. Huyo mdada wa kazi sio kwamba mnatumikisha,ila anawasaidia baadhi ya kazi.. Sio majumba yote yanawa-mistreat housegirlz jamani!!
 
Kusema kweli ingekua wanawake hatuendi makazini na kuchelewa kurudi house girl hata hahiyajiki. Lkn km wake wanaoshinda nyumbani house girl si lazima. Lkn pia waume wawe tayari kusaidia kazi wake zao.
 
Back
Top Bottom