Mambo 6 ya kufanya pale mtu unayempenda anapokupuuza

Akidu

Member
Sep 19, 2022
47
76
Kama utakuwa miongoni mwa watu ambao hujisikia upweke kupita kiasi katika mahusiano yao basi ujumbe huu unaweza kukusaidia.

Leo tuangalie namna ya kukabiliana na mtu ambaye unampenda sana lakini anaonyesha kukupuuza sana kila wakati ukionyesha kumhitaji.

Kabla ya kujua njia hizo tuangalie sifa za mtu ambaye unampenda sana lakini anafanya ujione mpweke muda wote.

SIFA ZA MWANAUME AU MWANAMKE AMBAYE UKIMPENDA SANA ANAKUPUUZA KUPITA KIASI

Sifa za mwanamme au mwanamke ambaye ukimpenda sana anakupuuza kupita kiasi ni;

1. ANAONYESHA TABIA MCHANGANYIKO
Mwanzoni kabisa wa mahusiano yenu ataonekana mcheshi sana, anajiamini kupita kiasi,anaonyesha kukupenda sana, kukusifia, anaonyesha kujali sana mahitaji yako, kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo kuuliza hatima ya mahusiano yenu lakini ukionyesha kumpenda sana tu anakuwa tofauti ghafla anakuwa mkali kupita kiasi, anakuwa mkosoaji kupita kiasi wa muonekano wako, atakupangia namna ya kuvaa, kuongea, atakosoa mawazo yako, atakuwa na dharura za mara kwa mara ukitaka kuzungumza nae.

2. ANATAKA UHURU MUDA WOTE
Mara kwa mara atadai umekuwa msumbufu na king'ang'anizi sana, atakuwa anatafuta dharura ya kukata simu ukipiga, atakuwa anachelewa kujibu sms mpaka utakuwa unapata hasira kupita kiasi juu yake. Na endapo utauliza kuhusu ukimya wake anakufokea, kukutukana, kukujibu vibaya, kujibu kwa mkato, au anakaa kimya sana kuliko mwanzo.

3. ANAJISIFIKIA KUPITA KIASI NA ANAKUKOSOA KUPITA KIASI
Mara kwa mara utaanza kujiona hauna hadhi ya kuishi naye au kuzungumza nae, atafanya ujione upo na bahati yeye kukupenda na atafanya uamini kama atakuacha huwezi kupendwa na mtu yeyote.

Ataanza kukufokea, kukutukana, kukujibu vibaya, kukosoa kupita kiasi muonekano wako mbele ya marafiki zake, atakosoa mawazo yako, atakosoa uvaaji wako, atakosoa uongeaji wako, atakosoa historia yako, atakosoa wazazi wako, atakosoa kipato chako, atakosoa vipaumbele vyako.

Kisha atajisifia kupita kiasi kuhusu maisha ya nyumbani kwao, atajisifia kupita kiasi kuhusu muonekano wake na mafanikio yake, atafanya ujichukie na kujidharau na kumuona yeye hana dosari yoyote.

4. ANASISITIZA SANA MIPAKA BAINA YENU
Mara kwa mara atakuwa na kisingizio cha kuondoka ukilalamika tabia zake, akiona ukaribu baina yenu unazidi kuongezeka anatafuta sababu ya kuibua ugomvi ili kuepuka ukaribu baina yenu.

Atafanya makosa kisha anageuza kibao kwako, mara kwa mara atafanya ujione upo na tatizo juu ya migogoro katika mahusiano yenu lakini yeye atakuwa anataka aonekane mkamilifu muda wote.

5. ANAKUWA NA MATARAJIO AMBAYO SIO HALISI
Anakuwa na masharti magumu sana kuhusu mtu ambaye anaweza kuwa mwenza wake lakini yeye ataonekana kujisifia kupita kiasi kuwa yeye ni bora kuliko wewe na watu wengine wote.

Kwa sababu anajiona hana dosari yoyote huku anakosoa kupita kiasi watu wengine ataonekana kubadilisha wanaume au wanawake mfululizo ili ampate mtu mkamilifu lakini yeye haonekani kujali mapungufu yake na ukitaja dosari zake anakugeuzia kibao na kukufanya adui.

6. HAWEZI KUMUAMINI MTU YEYOTE
Mara kwa mara atasema na kusisitizia kwamba wanawake au wanaume sio watu wa kuwaamini na huo utakuwa ujumbe wake kwa kila mtu na atakupa ushahidi wa watu kibao ambao maisha yao yameharibiwa na watu wa jinsia tofauti.

Anaweza kukusaliti lakini anaogopa kusalitiwa muda wote anakuwa na hofu, anakuwa na hofu ya kuibiwa fedha lakini yeye anaweza kutumia fedha zako nyingi bila ridhaa yako, anafanya mipango yake kwa siri, anakuwa mkali kupita kiasi na anakuwa na hasira za karibu kwa vitu vidogo vidogo sana, anabeba chuki moyoni muda mrefu na kuweka kinyongo muda mrefu sana.

7. PAKITOKEA UGOMVI ANAONDOKA BILA KUSULUHISHA
Siku zote atafanya ujione mkosaji tu lakini yeye ataonekana hana kosa hata moja.
Ukisema kuhusu tabia zake anakuwa na hasira kupita kiasi, anakuwa mkali kupita kiasi, anafoka, kutukana, kutoa vitisho, anabamiza mlango na kuondoka zake.

Ukitaka maelezo kuhusu ushahidi wa makosa yake anageuza kibao kwako na kutoa maelezo hayana uhalisia wowote na tukio, anakuwa muongo sana na haonyeshi kujuta kwa makosa yake.

8. UKIWA NA MAUMIVU AU HUZUNI ANAONDOKA BILA KUJALI HALI YAKO
Hata kama unaumwa sana haonekani kujali maumivu yako anaweza kuondoka zake hajali kabisa hali yako.

Kwa sababu hataki kabisa ukaribu na wewe ukiwa na maumivu au matatizo anatafuta sababu ya kuondoka na kukuacha ukiwa na matatizo lakini siku akiwa na matatizo anakuja kwako kutaka faraja na msaada.

Muda mwingi anatumia kufanya kazi, michezo, kukaa na marafiki,simu hapokei, sms hajibu lakini ukiwa nae karibu simu yake ipo busy kufanya mawasiliano na watu wengine.

JE, MWENZA ASIEPENDEKA HUWA ANAFIKIRIA NINI JUU YAKO
Kwa sababu hujui anafikiria nini juu yako unaweza kuumia sana hivyo leo tuangalie nini huwa anafikiria juu yako.

Kujua anafikiria nini juu yako andika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako katika mahusiano yako na mwenza wako.

1. Huwa nikipata kile ambacho ninataka kwa Mwenza wangu huwa sijui ninataka nini tena kwake?

2. Kama mtu ambaye ninampenda akiacha kuonyesha ushirikiano huwa sionyeshi hisia zozote, ninaweza kujisikia vizuri sana?

3. Sipendi kuona watu wengine wananitegemea kwa chochote?

4. Huwa nikiwa mbali na mwenza wangu huwa ninaMiss uwepo wake lakini nikiwa nae pamoja huwa ninajisikia vibaya sana na kutamani kumkimbia?

5. Mwenza wangu huwa anataka niwe Romantic sana kuliko ambavyo mimi ninaweza kuwa Romantic?

6. Ninajisikia vibaya sana nikiwa karibu na mwenza wangu?

7. Ninapenda zaidi kuwa na mwenza wa kulala naye mara moja na kumuacha kuliko mwenza wa kudumu naye?

8. Huwa ninamchukia Mwenza wangu bila sababu yoyote?

9. Ninapata wakati mgumu sana kumtegemea Mwenza wangu?

10. Sipendi kumueleza mwenza wangu kama ninampenda?

11. Uhuru wangu ni bora zaidi kuliko mahusiano yangu na mwenza wangu?

12. Ninapata wakati mgumu sana kumfariji na kumliwaza Mwenza wangu akiwa na maumivu au huzuni huwa sijui cha kufanya kumsaidia?

13. Huwa ninapata furaha ya haraka sana kama mahusiano yangu yakivunjika huwa ninashangaa namna ambavyo ninamtoa kichwani mtu yeyote haraka sana?

Kama umejibu NDIYO maswali mengi maana yake upo na AVOIDANCE ATTACHMENT STYLE kwa maana malezi ya utotoni mwako yalikuwa hayana ukaribu wowote wa kihisia na wazazi wako hivyo tangu utotoni mwako umeishi huku hujui kupewa faraja au kufariji watu wengine badala yake umezoea kujenga mahusiano ya juu juu na watu wengi na hauna rafiki wa kweli.

Vilevile umekuwa hauna upendo wowote wa dhati kwa mwenza wako au watu wengine wa karibu.

VYANZO VYA MWENZA WAKO KUONYESHA KUKUPUUZA SANA UKIMUHITAJI
1. Amevunja mahusiano ya kimapenzi baina yake na mwenza wake ambapo bado anampenda sana Mwenza wake huyo na anapata ugumu kumtoa kichwani.

2. Anaogopa kuumizwa sana kama atajenga mahusiano ya kimapenzi ya karibu sana (hataki umjue sana).

3. Anaogopa kuonekana dhaifu mbele yako. Hasa watu wenye hasira kupita kiasi muda wote huwa hawataki ukaribu na mtu yeyote kwa sababu wanaogopa kuonekana dhaifu wakiwa na hisia kali sana za mapenzi hivyo huamua kuibua ugomvi kuzuia ukaribu na mtu yeyote.

4. Anakuwa anataka kuwa na wanawake au wanaume wengi sana katika mahusiano kwa wakati mmoja. (Anakuwa katika mahusiano na wanaume au wanawake wengi sana kwa wakati mmoja).

5. Anaweza kuwa na mwenza wake ambaye wanapendana sana lakini anataka iwe siri usigundue.

6. Anaweza kuwa anakupima kama unaweza kujitesa sana ili uonekane unampenda sana kuliko mtu yeyote.

SABABU ZA UTOTONI
Kama unaona mwenza wako anakupuuza kupita kiasi utotoni mwake atakuwa na historia ifuatavyo;

1. UPENDELEO KUPITA KIASI
Mwanaume au mwanamke anaweza kujiona special sana katika mahusiano yake na watu wengine kwa sababu wazazi wake wamepa upendeleo kupita kiasi tangu akiwa mdogo amezoea kunyenyekewa tu, kuombwa msamaha, kubembelezwa tu lakini yeye hana msaada wowote kwa watu wengine.

Kwa sababu amezoea kunyenyekewa tu anataka kwake ujione hauna akili timamu, ujione mnyonge sana, ujione mtumwa tu kwake na muda wote uishi vile anataka yeye bila kuhoji chochote

2. ADHABU KUPITA KIASI
Mwanaume au mwanamke anaweza kukufanya ujione mnyonge, ujione mpweke, ujione hauna maana yoyote kwa sababu ya matukio ya utotoni kama kupigwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupuuzwa, kukaripiwa kudhalilishwa hadharani, kugombezwa sana, kuishi katika hali ya taharuki muda wote hivyo hawezi kuishi kwa amani na mtu yeyote kwa sababu hajazoea.

3. UPWEKE KUPITA KIASI
Mtu mwengine akiwa mkubwa anafanya ujione mpweke sana kwa sababu tangu utotoni ameishi maisha ya upweke sana labda kwa sababu ya kifo cha mzazi katika umri mdogo, kutelekezwa bila kumjua baba au mama mzazi tangu utotoni, mzazi kusafiri safiri mara kwa mara, mzazi kufanya kazi ngumu muda wote hivyo hana mazoea na mtu yeyote tangu utotoni, kulelewa na watu wengi sana mfululizo labda housegirls wengi sana, kuishi mara kwa baba mara kwa mama mara kwa ndugu n.k bila kujenga ukaribu na mtu yeyote hivyo hawezi kujenga ukaribu na mtu yeyote ukubwani hata ufanye kitu gani.

4. UGOMVI WA WAZAZI, TALAKA NA MALEZI YA MZAZI MMOJA
Mtu mwengine anaweza kukufanya ujione mnyonge sana ujione mpweke sana kwa sababu ya kumbukumbu za ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi, talaka au kutengana kwa wazazi pamoja na malezi ya mzazi mmoja hivyo tangu utotoni hajui kujenga ukaribu na mtu yeyote na anaogopa kujenga mazoea na mtu yeyote kwa hofu ya kuumizwa.

UFUMBUZI WAKE
Njia za kukabiliana na mwanaume au mwanamke ambaye anafanya ujione mpweke sana fanya yafuatayo;

1. PATA UTULIVU WA AKILI
Mwenza wako pale anakupuuza kupita kiasi utaona mabadiliko yafuatayo mwilini mwako;

a. Moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kichefuchefu, miguu kuishiwa nguvu, tumbo kuvurugika, kuumia kooni, kutetemeka sana, kutokwa jasho viganjani, kutamani kumdhuru, kumuombea mabaya kimyakimya.

b. Kumchukia kisirisiri,hasira kupita kiasi, kupoteza hamu ya kula au kula vyakula bila mpangilio, kulala popote, kuweweseka, kuumwa kichwa na mgongo, kuchanganyikiwa, upweke kupita kiasi, hofu ya kitu kibaya kutokea ghafla, kupata uchungu mkali sana moyoni, kifua kubana sana, kushindwa kuvuta pumzi vizuri.

Fanya yafuatayo vuta pumzi ndefu kupitia puani zuia pumzi kifuani, kisha hesabu sekunde tano kisha ruhusu pumzi itoke polepole huku unahesabu sekunde tano, fanya zoezi hilo kwa dakika mbili au zaidi kutuliza akili.

Pia piga miayo mfululizo (Yawning), toa pumzi kutoka tumboni kuja nje kupitia mdomoni pumua haraka haraka sana kama (Bata belly breathing).

2. EPUKA KUPIGA SIMU MFULULIZO
Acha kupiga simu mfululizo, na kutuma sms mfululizo, epuka kumfuata kimyakimya kisirisiri utamfanya azidi kuwa na kiburi na majivuno, ataona huwezi kuishi bila yeye.

Kama anakata simu, atafanya kisingizio cha kukata simu ukipiga epuka kupiga simu kwake mpaka apige yeye, kama anatumia muda mwingi sana kujibu sms acha kutuma sms kwake hata kwa dharura acha.

Mtu yeyote akiona unataka ukaribu naye muda wote anakuona huna pa kwenda na atapoteza hisia za mapenzi moja kwa moja.

3. JALI SANA MUONEKANO WAKO NA CHAKULA CHAKO
Kula chakula bora kiafya, kunywa maji mengi, pata matunda, pata vinywaji bora kiafya, pumzika, vaa nguo nzuri zenye kupendeza sio kwa ajili yake bali kwa ajili yako mwenyewe.

Zingatia yeye sio binadamu muhimu sana kuliko watu wote duniani. Anatakiwa ajue wapo wanaume au wanawake wazuri zaidi yake ambao wanataka kujenga mahusiano na wewe.

Epuka kumpa umuhimu mkubwa sana kuliko watu wote duniani wakati yey hawezi kufanya hivyo kwako.

Mtu yeyote ambaye anajali maisha yake muache huru na wewe jali maisha yako.
Anaejitenga na wewe jitenge naye ajue yeye sio binadamu special sana katika huu ulimwengu.

4. ONYESHA UNAMPENDA LAKINI UNAWEZA KUISHI BILA YEYE
Mwambie kwamba unampenda sana lakini huwezi kuvumilia tabia kama kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupuuzwa, kupelekeshwa, kufanywa kichekesho na ikiwa hawezi kukuheshimu wala kujirekebisha tabia upo tayari muachane na kila mtu aendelee na maisha yake.

5. KUWA MVUMILIVU
Kama anafanya kazi ngumu, au masomo, au safari n.k vumilia lakini ikiwa ni tabia yake ya muda mrefu onyesha unaweza kupendwa na watu wengine na maisha yakaendelea kama kawaida. Anatakiwa ajue yeye ni binadamu tu kama walivyo wengine na endapo atakuacha pengo lake utaziba kwa kumpenda mtu mwingine.

6. KAMA ANAONYESHA KUKUVUNJIA HESHIMA ONDOKA
Epuka kujishusha sana, kunyenyekea sana, kujiona takataka, kuvumilia udhalilishaji kutoka kwa mtu yeyote kwa sababu amekuzidi kitu fulani badala yake onyesha unaweza kupendwa na watu wengine na lengo lake unaweza kuziba muda.

Itaendelea...
 
MAMBO 6 YA KUFANYA PALE AMBAPO MTU AMBAYE UNAMPENDA UONAPO ANAKUPUUZA SANA
Kama utakuwa miongoni mwa watu ambao hujisikia upweke kupita kiasi katika mahusiano yao basi ujumbe huu unaweza kukusaidia.

Leo tuangalie namna ya kukabiliana na mtu ambaye unampenda sana lakini anaonyesha kukupuuza sana kila wakati ukionyesha kumhitaji.

Kabla ya kujua njia hizo tuangalie sifa za mtu ambaye unampenda sana lakini anafanya ujione mpweke muda wote.

SIFA ZA MWANAUME AU MWANAMKE AMBAYE UKIMPENDA SANA ANAKUPUUZA KUPITA KIASI
Sifa za mwanamme au mwanamke ambaye ukimpenda sana anakupuuza kupita kiasi ni
1.ANAONYESHA TABIA MCHANGANYIKO
Mwanzoni kabisa wa mahusiano yenu ataonekana mcheshi sana, anajiamini kupita kiasi,anaonyesha kukupenda sana,kukusifia, anaonyesha kujali sana mahitaji yako,kupiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo kuuliza hatima ya mahusiano yenu lakini ukionyesha kumpenda sana tu anakuwa tofauti ghafla anakuwa mkali kupita kiasi,anakuwa mkosoaji kupita kiasi wa muonekano wako,atakupangia namna ya kuvaa, kuongea,atakosoa mawazo yako,atakuwa na dharura za mara kwa mara ukitaka kuzungumza nae.

2.ANATAKA UHURU MUDA WOTE
Mara kwa mara atadai umekuwa msumbufu na king'ang'anizi sana, atakuwa anatafuta dharura ya kukata simu ukipiga,atakuwa anachelewa kujibu sms mpaka utakuwa unapata hasira kupita kiasi juu yake.Na endapo utauliza kuhusu ukimya wake anakufokea, kukutukana, kukujibu vibaya,kujibu kwa mkato,au anakaa kimya sana kuliko mwanzo.

3.ANAJISIFIKIA KUPITA KIASI NA ANAKUKOSOA KUPITA KIASI
Mara kwa mara utaanza kujiona hauna hadhi ya kuishi naye au kuzungumza nae,atafanya ujione upo na bahati yeye kukupenda na atafanya uamini kama atakuacha huwezi kupendwa na mtu yeyote.

Ataanza kukufokea, kukutukana, kukujibu vibaya, kukosoa kupita kiasi muonekano wako mbele ya marafiki zake,atakosoa mawazo yako,atakosoa uvaaji wako,atakosoa uongeaji wako,atakosoa historia yako,atakosoa wazazi wako,atakosoa kipato chako,atakosoa vipaumbele vyako.

Kisha atajisifia kupita kiasi kuhusu maisha ya nyumbani kwao, atajisifia kupita kiasi kuhusu muonekano wake na mafanikio yake,atafanya ujichukie na kujidharau na kumuona yeye hana dosari yoyote.

4.ANASISITIZA SANA MIPAKA BAINA YENU
Mara kwa mara atakuwa na kisingizio cha kuondoka ukilalamika tabia zake,akiona ukaribu baina yenu unazidi kuongezeka anatafuta sababu ya kuibua ugomvi ili kuepuka ukaribu baina yenu.

Atafanya makosa kisha anageuza kibao kwako ,mara kwa mara atafanya ujione upo na tatizo juu ya migogoro katika mahusiano yenu lakini yeye atakuwa anataka aonekane mkamilifu muda wote.

5.ANAKUWA NA MATARAJIO AMBAYO SIO HALISI
Anakuwa na masharti magumu sana kuhusu mtu ambaye anaweza kuwa mwenza wake lakini yeye ataonekana kujisifia kupita kiasi kuwa yeye ni bora kuliko wewe na watu wengine wote.

Kwa sababu anajiona hana dosari yoyote huku anakosoa kupita kiasi watu wengine ataonekana kubadilisha wanaume au wanawake mfululizo ili ampate mtu mkamilifu lakini yeye haonekani kujali mapungufu yake na ukitaja dosari zake anakugeuzia kibao na kukufanya adui.

6.HAWEZI KUMUAMINI MTU YEYOTE
Mara kwa mara atasema na kusisitizia kwamba wanawake au wanaume sio watu wa kuwaamini na huo utakuwa ujumbe wake kwa kila mtu na atakupa ushahidi wa watu kibao ambao maisha yao yameharibiwa na watu wa jinsia tofauti.

Anaweza kukusaliti lakini anaogopa kusalitiwa muda wote anakuwa na hofu,anakuwa na hofu ya kuibiwa fedha lakini yeye anaweza kutumia fedha zako nyingi bila ridhaa yako,anafanya mipango yake kwa siri ,anakuwa mkali kupita kiasi na anakuwa na hasira za karibu kwa vitu vidogo vidogo sana,anabeba chuki moyoni muda mrefu na kuweka kinyongo muda mrefu sana.

7.PAKITOKEA UGOMVI ANAONDOKA BILA KUSULUHISHA
Siku zote atafanya ujione mkosaji tu lakini yeye ataonekana hana kosa hata moja.
Ukisema kuhusu tabia zake anakuwa na hasira kupita kiasi,anakuwa mkali kupita kiasi,anafoka, kutukana, kutoa vitisho,anabamiza mlango na kuondoka zake.

Ukitaka maelezo kuhusu ushahidi wa makosa yake anageuza kibao kwako na kutoa maelezo hayana uhalisia wowote na tukio,anakuwa muongo sana na haonyeshi kujuta kwa makosa yake.

8.UKIWA NA MAUMIVU AU HUZUNI ANAONDOKA BILA KUJALI HALI YAKO
Hata kama unaumwa sana haonekani kujali maumivu yako anaweza kuondoka zake hajali kabisa hali yako.
Kwa sababu hataki kabisa ukaribu na wewe ukiwa na maumivu au matatizo anatafuta sababu ya kuondoka na kukuacha ukiwa na matatizo lakini siku akiwa na matatizo anakuja kwako kutaka faraja na msaada .

Muda mwingi anatumia kufanya kazi, michezo,kukaa na marafiki,simu hapokei , sms hajibu lakini ukiwa nae karibu simu yake ipo busy kufanya mawasiliano na watu wengine.

JE MWENZA ASIEPENDEKA HUWA ANAFIKIRIA NINI JUU YAKO
Kwa sababu hujui anafikiria nini juu yako unaweza kuumia sana hivyo leo tuangalie nini huwa anafikiria juu yako

Kujua anafikiria nini juu yako andika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako katika mahusiano yako na mwenza wako.

1.Huwa nikipata kile ambacho ninataka kwa Mwenza wangu huwa sijui ninataka nini tena kwake?
2.Kama mtu ambaye ninampenda akiacha kuonyesha ushirikiano huwa sionyeshi hisia zozote, ninaweza kujisikia vizuri sana?
3.Sipendi kuona watu wengine wananitegemea kwa chochote?
4.Huwa nikiwa mbali na mwenza wangu huwa ninaMiss uwepo wake lakini nikiwa nae pamoja huwa ninajisikia vibaya sana na kutamani kumkimbia?
5.Mwenza wangu huwa anataka niwe Romantic sana kuliko ambavyo mimi ninaweza kuwa Romantic?

6.Ninajisikia vibaya sana nikiwa karibu na mwenza wangu?
7.Ninapenda zaidi kuwa na mwenza wa kulala naye mara moja na kumuacha kuliko mwenza wa kudumu naye?
8.Huwa ninamchukia Mwenza wangu bila sababu yoyote?
9.Ninapata wakati mgumu sana kumtegemea Mwenza wangu?
10.Sipendi kumueleza mwenza wangu kama ninampenda?

11.Uhuru wangu ni bora zaidi kuliko mahusiano yangu na mwenza wangu?
12.Ninapata wakati mgumu sana kumfariji na kumliwaza Mwenza wangu akiwa na maumivu au huzuni huwa sijui cha kufanya kumsaidia?
13.Huwa ninapata furaha ya haraka sana kama mahusiano yangu yakivunjika huwa ninashangaa namna ambavyo ninamtoa kichwani mtu yeyote haraka sana?

Kama umejibu NDIYO maswali mengi maana yake upo na AVOIDANCE ATTACHMENT STYLE kwa maana malezi ya utotoni mwako yalikuwa hayana ukaribu wowote wa kihisia na wazazi wako hivyo tangu utotoni mwako umeishi huku hujui kupewa faraja au kufariji watu wengine badala yake umezoea kujenga mahusiano ya juu juu na watu wengi na hauna rafiki wa kweli.

Vilevile umekuwa hauna upendo wowote wa dhati kwa mwenza wako au watu wengine wa karibu.

VYANZO VYA MWENZA WAKO KUONYESHA KUKUPUUZA SANA UKIMUHITAJI
1.Amevunja mahusiano ya kimapenzi baina yake na mwenza wake ambapo bado anampenda sana Mwenza wake huyo na anapata ugumu kumtoa kichwani

2.Anaogopa kuumizwa sana kama atajenga mahusiano ya kimapenzi ya karibu sana (hataki umjue sana)
3.Anaogopa kuonekana dhaifu mbele yako.Hasa watu wenye hasira kupita kiasi muda wote huwa hawataki ukaribu na mtu yeyote kwa sababu wanaogopa kuonekana dhaifu wakiwa na hisia kali sana za mapenzi hivyo huamua kuibua ugomvi kuzuia ukaribu na mtu yeyote

4.Anakuwa anataka kuwa na wanawake au wanaume wengi sana katika mahusiano kwa wakati mmoja.(Anakuwa katika mahusiano na wanaume au wanawake wengi sana kwa wakati mmoja)

5.Anaweza kuwa na mwenza wake ambaye wanapendana sana lakini anataka iwe siri usigundue
6.Anaweza kuwa anakupima kama unaweza kujitesa sana ili uonekane unampenda sana kuliko mtu yeyote

SABABU ZA UTOTONI
Kama unaona mwenza wako anakupuuza kupita kiasi utotoni mwake atakuwa na historia ifuatavyo
1.UPENDELEO KUPITA KIASI
Mwanaume au mwanamke anaweza kujiona special sana katika mahusiano yake na watu wengine kwa sababu wazazi wake wamepa upendeleo kupita kiasi tangu akiwa mdogo amezoea kunyenyekewa tu, kuombwa msamaha, kubembelezwa tu lakini yeye hana msaada wowote kwa watu wengine

Kwa sababu amezoea kunyenyekewa tu anataka kwake ujione hauna akili timamu,ujione mnyonge sana,ujione mtumwa tu kwake na muda wote uishi vile anataka yeye bila kuhoji chochote

2.ADHABU KUPITA KIASI
Mwanaume au mwanamke anaweza kukufanya ujione mnyonge,ujione mpweke, ujione hauna maana yoyote kwa sababu ya matukio ya utotoni kama kupigwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupuuzwa, kukaripiwa kudhalilishwa hadharani, kugombezwa sana,kuishi katika hali ya taharuki muda wote hivyo hawezi kuishi kwa amani na mtu yeyote kwa sababu hajazoea.

3.UPWEKE KUPITA KIASI
Mtu mwengine akiwa mkubwa anafanya ujione mpweke sana kwa sababu tangu utotoni ameishi maisha ya upweke sana labda kwa sababu ya kifo cha mzazi katika umri mdogo, kutelekezwa bila kumjua baba au mama mzazi tangu utotoni,mzazi kusafiri safiri mara kwa mara,mzazi kufanya kazi ngumu muda wote hivyo hana mazoea na mtu yeyote tangu utotoni, kulelewa na watu wengi sana mfululizo labda housegirls wengi sana,kuishi mara kwa baba mara kwa mama mara kwa ndugu n.k bila kujenga ukaribu na mtu yeyote hivyo hawezi kujenga ukaribu na mtu yeyote ukubwani hata ufanye kitu gani.

4.UGOMVI WA WAZAZI, TALAKA NA MALEZI YA MZAZI MMOJA
Mtu mwengine anaweza kukufanya ujione mnyonge sana ujione mpweke sana kwa sababu ya kumbukumbu za ugomvi wa mara kwa mara wa wazazi,talaka au kutengana kwa wazazi pamoja na malezi ya mzazi mmoja hivyo tangu utotoni hajui kujenga ukaribu na mtu yeyote na anaogopa kujenga mazoea na mtu yeyote kwa hofu ya kuumizwa.

UFUMBUZI WAKE
Njia za kukabiliana na mwanaume au mwanamke ambaye anafanya ujione mpweke sana fanya yafuatayo

1.PATA UTULIVU WA AKILI
Mwenza wako pale anakupuuza kupita kiasi utaona mabadiliko yafuatayo mwilini mwako
a.Moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kichefuchefu, miguu kuishiwa nguvu, tumbo kuvurugika, kuumia kooni, kutetemeka sana, kutokwa jasho viganjani, kutamani kumdhuru, kumuombea mabaya kimyakimya,

b. kumchukia kisirisiri,hasira kupita kiasi, kupoteza hamu ya kula au kula vyakula bila mpangilio, kulala popote, kuweweseka, kuumwa kichwa na mgongo, kuchanganyikiwa, upweke kupita kiasi,hofu ya kitu kibaya kutokea ghafla,kupata uchungu mkali sana moyoni,kifua kubana sana,kushindwa kuvuta pumzi vizuri .

Fanya yafuatayo vuta pumzi ndefu kupitia puani zuia pumzi kifuani, kisha hesabu sekunde tano kisha ruhusu pumzi itoke polepole huku unahesabu sekunde tano,fanya zoezi hilo kwa dakika mbili au zaidi kutuliza akili.

Pia piga miayo mfululizo (Yawning),toa pumzi kutoka tumboni kuja nje kupitia mdomoni pumua haraka haraka sana kama (Bata belly breathing)

2.EPUKA KUPIGA SIMU MFULULIZO
Acha kupiga simu mfululizo, na kutuma sms mfululizo,epuka kumfuata kimyakimya kisirisiri utamfanya azidi kuwa na kiburi na majivuno,ataona huwezi kuishi bila yeye.

Kama anakata simu,atafanya kisingizio cha kukata simu ukipiga epuka kupiga simu kwake mpaka apige yeye,kama anatumia muda mwingi sana kujibu sms acha kutuma sms kwake hata kwa dharura acha.

Mtu yeyote akiona unataka ukaribu naye muda wote anakuona huna pa kwenda na atapoteza hisia za mapenzi moja kwa moja.

3.JALI SANA MUONEKANO WAKO NA CHAKULA CHAKO
Kula chakula bora kiafya,kunywa maji mengi,pata matunda,pata vinywaji bora kiafya, pumzika,vaa nguo nzuri zenye kupendeza sio kwa ajili yake bali kwa ajili yako mwenyewe.

Zingatia yeye sio binadamu muhimu sana kuliko watu wote duniani.Anatakiwa ajue wapo wanaume au wanawake wazuri zaidi yake ambao wanataka kujenga mahusiano na wewe.

Epuka kumpa umuhimu mkubwa sana kuliko watu wote duniani wakati yey hawezi kufanya hivyo kwako.
Mtu yeyote ambaye anajali maisha yake muache huru na wewe jali maisha yako.
Anaejitenga na wewe jitenge naye ajue yeye sio binadamu special sana katika huu ulimwengu.

4.ONYESHA UNAMPENDA LAKINI UNAWEZA KUISHI BILA YEYE
Mwambie kwamba unampenda sana lakini huwezi kuvumilia tabia kama kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupuuzwa, kupelekeshwa, kufanywa kichekesho na ikiwa hawezi kukuheshimu wala kujirekebisha tabia upo tayari muachane na kila mtu aendelee na maisha yake.

5.KUWA MVUMILIVU
Kama anafanya kazi ngumu,au masomo,au safari n.k vumilia lakini ikiwa ni tabia yake ya muda mrefu onyesha unaweza kupendwa na watu wengine na maisha yakaendelea kama kawaida.Anatakiwa ajue yeye ni binadamu tu kama walivyo wengine na endapo atakuacha pengo lake utaziba kwa kumpenda mtu mwingine.

6.KAMA ANAONYESHA KUKUVUNJIA HESHIMA ONDOKA
Epuka kujishusha sana, kunyenyekea sana,kujiona takataka, kuvumilia udhalilishaji kutoka kwa mtu yeyote kwa sababu amekuzidi kitu fulani badala yake onyesha unaweza kupendwa na watu wengine na lengo lake unaweza kuziba muda itaendelea..........
thank you sir!!
 
4.ONYESHA UNAMPENDA LAKINI UNAWEZA KUISHI BILA YEYE
Mwambie kwamba unampenda sana lakini huwezi kuvumilia tabia kama kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kupuuzwa, kupelekeshwa, kufanywa kichekesho na ikiwa hawezi kukuheshimu wala kujirekebisha tabia upo tayari muachane na kila mtu aendelee na maisha yake.
Naona waalimu wa mahusiano mnatofautiana sana.

Wanasema ni kosa kubwa sana kumtakia mpenzi wako kuwa mtakuja "kuachana" utakuja "kumuwacha" iwe ni kwa sababu mambo/tabia zake fulani fulani nk au lah Japo binafsi sijawahi kukoma kutoa hiyo tahadhari ya kuacha mtu.
 
Back
Top Bottom