Mimba za utotoni: Nani wa kulaumiwa?

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
71
110
81539D47-95AA-4336-BAAB-ACC0BE9BC0C6.jpeg


Mlipuko wa virusi vya Corona unaoshuhudiwaduniani kote umeleta athari kubwa katikauchumi na maisha ya watu, kwani biasharazimefungwa, shule zimefungwa, na waajiriwawengi wanafanya kazi majumbani, huku wale ambao kwa bahati mbaya iliwalazimu kutoka ilikupata pesa za kulisha familia wakiwa katikahali ngumu kimaisha.

Ni katika mazingira kama haya ndipolinapojitokeza suala ambalo limekuwa likipigiwakelele sana na mashirika mbalimbali ya kijamii, nalo ni mimba za utotoni.

Kutokana na shule kufungwa, wanafunziwamebaki majumbani wakitakiwa kujisomea, nawaalimu wao wamejitahidi kutoa mafundishokupitia mitandao ya kijamii na hata kwatelevisheni. Lakini jambo la kusikitisha nikwamba, idadi kubwa ya watoto wa kike wamepata ujauzito katika kipindi hiki ambachoshule zimefungwa ili kudhibiti maambukizi yavirusi vya Corona.

Kwa mfano, nchini Tanzania, mikoa ya Ruvuma, Mara, Arusha na Mtwara imeongoza kwawanafunzi kupata mimba wakiwa majumbanikatika kipindi hiki cha likizo kutokana na jangala virusi vya Corona, huku Mtwara, idadi hiyoikifikia wanafunzi 100! Katika mazingira hayamtu unajiuliza, inakuwaje binti yuko nyumbani, anajisomea, lakini anapata ujauzito? Ina maanawazazi hatuko makini kufuatilia mienendo yawatoto wetu?

Ni wazi kwamba jukumu kubwa la mzazi amamlezi ni kuhakikisha kuwa mtoto wake anafanyavizuri katika masomo, ikiwa ni hatua yakumsaidia kujenga mazingira mazuri kwa ajili yamaisha yake ya baadaye, lakini mzazi anapokosamuda wa kufanya hivyo, madhara yake ni hayo. Hapo inapaswa kukumbukwa kwamba, tarehe 30 Juni 2017, rais wa Tanzania John Magufulialitangaza kuwa mtoto wa kike akipata mimbahataruhusiwa kurejea tena shule. Sasa haomabinti waliopata ujauzito, hawatawezakuendelea na masomo, na kwa sababu hiyo, tayari matarajio yao katika maishayamevurugika.

Lakini pia, kuna wazazi ambao wanawatumiawatoto wao wa kike kama vitega uchumi, yaaniwanawauza kwa wanaume ili waweze kupatamahitaji yao.

Kuna habari ya kusikitishaimetokea kule nchini Kenya ambapo wanaumewatu wazima wanawalipa kina mama miraa, helaama sukari ili waweze kujamiiana na mabintizao. Kisa cha hivi karibuni zaidi, kilitokea kijijicha Mswakini, tarafa ya Hindi, ambapomsichana mmoja mwenye miaka 16 anayesomadarasa la sita alipewa mimba na mzee wa umriwa miaka 59 baada ya mama wa msichana huyokulipwa miraa, muguka na kilo kadhaa za sukari.

Inasikitisha sana pale ambapo mzazi badala yakumlea mtoto katika mazingira mazuriyatakayomsaidia katika maisha yake ya baadaye, unakuwa ndio chimbuko la kuharibu maishayake.

Kwa upande mwingine, kama muhusika waudhalilishaji wa kingono ni ndugu wa karibu, wazazi ama walezi huwa wanaona hayakupeleka mashtaka sehemu husika, na badalayake huamua kumaliza tatizo hilo kimya kimya. Lakini waswahili husema, kimya kingi kina mshindo mkuu. Kwani kwa kufanya hivyo, unakuwa unakandamiza haki ya mtoto wako yakujiendeleza kielimu na hata kumuathirikisaikolojia, pale ambapo alitazamia mzazi amamlezi kumtetea, lakini unakubali kukaa kimyakwa malipo kidogo ili tu kuficha aibu ya familia.

Umefika wakati wa vyombo vya usalamakuchukua nafasi yake kuhakikisha wale wanaotenda vitendo vya udhallishaji wa watotowanaadhibiwa, na wazazi, walezi ama waalimuwanaojihusisha na tabia mbaya ya kuwa nauhusiano wa kimapenzi na wanafunziwanachukuliwa hatua kali.

Wazazi na walezi pia ni muda wa kusimamakidete kutetea haki za watoto wetu, wa kike nawa kiume, wanaofanyiwa vitendo vyakudhalilishwa. Tujipangie muda wa kuongeakwa uwazi na watoto wetu, kuwaonyeshakwamba tunawajali kwa vitendo halisi na siomaneno matupu, na pia kuhakikisha tunalinda nakutetea haki zao.
 
Maadili ni swala la jamii nzima, wazazI na watu wote.
Watoto wengi hupewa mimba na wtoto wwnzao
Watu wazima pia wanabadua toto aise.

Upo ushaidi kabaisa njemba iko na miaka 45± kafumwa anakula uroda katoto miaka 11 kako drs la nne.

Alikamatwa kapelekwa polisi cha achabu kaa lock up siku moja jemba iko uraini kesi hakuna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom