Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 374,279
- 866,735
Nawaheshimu sana manabii na mitume wenye karama ya kweli na wanaotumia karama hiyo katika roho na kweli na bila manufaa binafsi.. Karama haiuzwi ni huduma ya bure ni kipawa cha kiroho na kimungu... Kuitumia karama kwa manufaa binafsi yoyote yale ni kwenda kinyume na dhima yake.... Ni laana...!!!!
Kuna akina mama ndani ya ndoa kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kupata watoto na wamehangaika kila mahali kuanzia hospitalini mpaka kwa waganga wa kienyeji na hata mitishamba... Na mwishowe kuangukia huku kwa manabii na mitume kama sehemu ya mwisho
Wote tunafahamu raha ya ndoa ni watoto na mwanamke akikosa kuzaa hata kama tatizo ni la baba... Wanandugu hasa mawifi na mamamkwe hawaishi kuchonga... Kuna ndoa zimevunjika kwa sababu hii... Kwahiyo inafika mahali wanawake hujilipua na kufanya lolote ili mradi tu apate mtoto.....
Manabii na mitume hawa wana njia mbalimbali za kusaidia hili tatizo... Lakini nyingi ni haramu
1. Kuna wenye karama ya kweli ya kuombea na kutatua tatizo na kweli mama akabeba mimba na kujifungua salama... Lakini hutakiwa kulipa pesa nyingi... Hapa si tatizo sana kama mtoto atapatikana japo laana ya kuuza huduma itamwangukia mtumishi husika
2. Matapeli kwa kutumia jina la Mungu huku wakimtumia mhitaji kingono na wakati huohuo akimpa dawa za kawaida za mitishamba na hata za hospital.... Hapa kuna wakati watoto wanaozaliwa si wa baba halisi wa ndoa bali wa watumishi waombeaji
3. Mimba tasa na mimba za kuzimu... Hapa ni mazingaombwe uchawi na usanii... Hizi mimba huishia kuharibika ama kuzidisha muda wa kujifungua na kujifungua watoto wasio kamili... Nyakati nyingine watoto wenye maumbo ya ajabu... Ama kama wakiwa wazima basi wanakuwa na tabia na mienendo ya ajabu
4. Mimba za kuzugia na kubahatisha... Hapa mwombeaji ni wale wazee wa try n error... Anavuta muda huku akitumia mbinu za kawaida kabisa za kuwezesha mtu kupata mtoto.. Hapa maombi huwa mengi na ya muda mrefu... Hatimaye kwa rehema za Mungu muda huwadia na kujaliwa kupata mimba na kujifungua mtoto asiye na kasoro yoyote... Sifa anapata mwingine mjanja wa mjini tu wakati aliyekata kiuno ni mumeo....
Katika yote hayo jina la Yesu na Mungu hutumika sana.. Huku kukiwa na shuhuda mia kidogo mbele ya cameras za walioombewa na kufanikiwa kubeba mimba ama kupata watoto... Yote haya yanafanyika kumnufaisha nabii ama mtume kifedha na wakati mwingine kingono... Eti wengine huambiwa manii zao zina upako wa kufungua njia na kusafisha kizazi hivyo ni muhimu na ni lazima akulale.... Mungu anawaona
Dada mama ndugu na rafiki kama una tatizo kama hili tumia njia za kawaida za kitaalam na hata za kiasili huku ukimwomba Mola wako akujaalie... Huku ukiwa umepima na mwenzako kujua shida iko wapi... Kuna baadhi walishachezea vizazi vyao. Hawa wameshakuwa wagumba... Ni tasa wasioweza kuzaa asilani na ndio ambao hujiongeza kwa kujifunga matambara na hatimaye kuiba watoto....
Ogopeni sana mimba za kuombewa