Mimba za kuzimu

Mkuu jichawi, post yako inaonesha kabisa unawahurumia wanaoziendea nguvu za giza kama suluhisho la matatizo yao, kumbe si kweli! Swali... je wewe binafsi unaitazamaje hatima yako, baada ya maisha ya hapa duniani, roho yako itakuwa wapi? Nakukaribisha umwamini Yesu usitumikishwe na dunia maana inapita na mambo yake,
 

Moaka juzi tu hapa nime rudia hiyo offer. Sijapata effect yoyote.

Hawa ndugu zetu wengine wanaendekeza ushirikina sana.

Kuna mama mmoja mzungu ana miaka 61. Alishika mimba akiwa na miaka 61. Naturally, bika kutumia fertility treatment.

Angekuwa bongo watu wangesema hii ni mimba ya mzimu na kusema uchawi.

Kumbe kuna a perfectly sound scientific explanation. Huyu mama alipata ajali katika miaka yake ya ujana, menstruation ika stop. Mme wake akawa ana matatizo ya kupandisha jongoo. Baadaye mmewe akafariki, akapata mwanamme mwingine. Mwanamme mwingine ndiye aliyempa mimba. Madaktari wakashangaaa sana lakini wakasema huyo mama biological clock yake ilikuwa ni sawa na ya mwanamke wa kwenye miaka ya 30s.

Kibongobongo ungeambuwa habari zote za uchawi kabla hata ya uchunguzi.
 
kbla ya yote naomba nijue wewe ni dini gani na unaamini kuwa mungu yupo
 
Bishana kwenye simba na yanga, Ccm na Ukawa, kuku na bata na vitu vingine.....achana na hii maneno, hizi mambo wanajua waliopitia na waliokuwa "jikoni"
 
Bishana kwenye simba na yanga, Ccm na Ukawa, kuku na bata na vitu vingine.....achana na hii maneno, hizi mambo wanajua waliopitia na waliokuwa "jikoni"
Unajuaje mimi sijapitia na sijakuwa jikoni?
 
Jamii forum ni zaidi ya uijuavyo aise,ila ndugu zangu naomba kujua ,kuna vifo vingi sana vinatokea sasa hivi vya watu kudondoka bafuni na kufariki katk kupita pita kuna stori kuwa hivyo ni vifo vya kishirikina@ naombeni mtujuze wadau
 
Inaelekea usingesoma shule pia ungebisha kama mwafrika anaweza kuandika kimombo.....usichokijua haimaanishi hakipo
Usichokijua haimaanishi hakipo.

Lakini haimaanishi kwamba kipo.

Ukisema kipo bila utafiti zaidi utakubali kwamba pembetatu duara ipo.

Toa uthibitisho kwamba mauzauza hayo yapo kiuhalisia, nje ya hadithi.
 

Mkuu! Mfano tumeenda hospital ikaonekana mwanamke ndiye mwenye tatizo. Suluhisho ni nini?
 
Usichokijua haimaanishi hakipo.

Lakini haimaanishi kwamba kipo.

Ukisema kipo bila utafiti zaidi utakubali kwamba pembetatu duara ipo.

Toa uthibitisho kwamba mauzauza hayo yapo kiuhalisia, nje ya hadithi.
Dini zote zinazoeleza kuhusu uchawi ni za uongo, dunia nzima wanapofanya mambo haya hawana akili.....ila mwenye akili ni wewe peke yako.
 
Dini zote zinazoeleza kuhusu uchawi ni za uongo, dunia nzima wanapofanya mambo haya hawana akili.....ila mwenye akili ni wewe peke yako.
Dini ngapi unazijua wewe?

Umesoma vitabu vingapi vya dini tulinganishe mimi na wewe nani anajua dini zaidi?

Kama dunia nzima watu waliamini dunia iko bapa, wachache wakaamini dunia ni duara, hilo lilifanya dunia iwe bapa?

Unataka kusema kwamba wengi wakisema jua halipo litaacha kuwepo?

The truth is not democratic.

Hujajibu swali.

Unaweza kuthibitisha uchawi upo?
 
Duh! Hebu kabla ya kuujua uchawi mjue Mungu kwanza.....au nae ni mpaka umuone kwa macho?
 
Duh! Hebu kabla ya kuujua uchawi mjue Mungu kwanza.....au nae ni mpaka umuone kwa macho?
Mungu ni nani?

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo na si hadithi tu?
 
Nimemaliza, ikitokea ukamjua Mungu ndio utajua na haya yote......kumbe tatizo ni kubwa zaidi kuliko nilivyofikiria.
Hujamaliza, hata hujaanza bado.

Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaamini katika hadithi isiyothibitishika.

Kati yako unayeamini katika kitu ambacho huwezi kuthibitisha na mimi ninayekuuliza maswali ambayo umeshindwa kuyajibu, nani ana matatizo hapa?
 
Kama umeshindwa kufunzwa dini na kumjua Mungu katika makanisa yote na misikiti kila kona, siwezi kukufundisha hapa Jf ukamjua.
 
Kama umeshindwa kufunzwa dini na kumjua Mungu katika makanisa yote na misikiti kila kona, siwezi kukufundisha hapa Jf ukamjua.
Unachojua wewe ni makanisa na misikiti tu.

Tatizo linaanzia hapo.

A little knowledge is dangerous indeed. Utashi wako unaanzia na kuishia katika makanisa na misikiti.

I have been to Dharamsala.

Hujathibitisha kwamba mungu wako huyo yupo. Huwezi.

Kwa sababu hayupo.

Na dunia yako yote imejengeka katika uongo huo.

Ndiyo maana unaamini katika ujinga kama uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…