Miluzi mingi

monakule

Member
Sep 29, 2012
86
22
MILUZI MINGI
Nawaza nianze lipi, Kesho niwe wa maana.
Nimekazwa kwa mshipi, Na kaburi naliona.
Thamani yangu ni ngapi, Nihungame Maulana.
Miluzi sasa ni mingi, Napotea mawindoni.

Nawaza hadi magumu, Kuyasema nachelea.
Liwe moja baragumu, Ramani nitakosea.
Najua mwisho mgumu, Naweza pia potea.
Miluzi sasa ni mingi, Mawindoni napotea.

Huku ni ajira kwanza, Na kule kilimo kwanza.
Pale ni viwanda kwanza,Na hapa elimu kwanza.
Yule eti kasi kwanza, Huyu NI KAZI TU kwanza.
Miluzi sasa ni mingi, Mawindoni napotea.

Elimu sasa ni bure, Tatizo bado kuisha.
Kufunga Paka kengere, Macho yake yanatisha.
Kumeza unga wa ndere, Roho yangu yakanusha
Miluzi sasa ni mingi, Mawindoni napotea.

By Mtemi KALOGI II
 
Back
Top Bottom