Milipuko Mikubwa yarindima Kibamba...

Mimi na ndugu zangu tumepatwa na hofu kubwa milio ilisikika karibu kabisa na nyumbani, ila watu niliowasiliana nao wanasema ni wanajeshi wapo mazoezini..

Mimi nipo maeneo ya Luguruni sikusikia kitu ila jamaa kanipigia simu juu ya mabomu haya nimeamka hakuna kinachoendele narudi kuvuta shuka, kwani ni maeneo gani hasa ama ni Transforma??!!
 
[h=1]Usain Bolt aandikisha historia London[/h]
9 Agosti, 2012 - Saa 23:08 GMT

120809222551_usain_bolt_304x171_reuters_nocredit.jpg
Bolt aliwaongoza wanariadha wenzake wa Jamaica katika kutwaa medali zote tatu za mbio za mita 200

Usain Bolt usiku wa Alhamisi alifanikiwa kuwa mwanariadha wa kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki, kuweza kuutetea ubingwa wake kikamilifu katika mbio zote fupi, mita 100 na vile mia 200.
Bolt aliwaongoza wanariadha wenzake kutoka Jamaica katika kunyakuwa medali zote tatu katika mashindano hayo ya mita 200.
Muda wa Bolt katika mashindano hayo ulikuwa ni sawa na ule wa Michael Johnson katika mashindano ya Atlanta, na uliokuwa muda bora zaidi wa dunia wakati huo, wa sekunde 19.32.
Mwanariadha ambaye hufanya mazoezi na Bolt, Yohan Blake, alipata medali ya fedha, huku Warren Weir akichukua ya shaba.
Blake alikuwa amemshinda Bolt katika mashindano ya Jamaica ya kufuzu kushirikishwa katika mbio za London, lakini Blake hakuwezana na kasi ya Bolt wakati huu.
"Hili ndilo jambo ambalo nililitaka, na nimefanikiwa kulipata. Ni fahari kuu kwangu," mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 aliielezea BBC.
"Baada ya msimu mgumu, nilifika hapa na kufanikiwa. Nilidhani kuvunja rekodi iliwezekana. Nafikiri nilikuwa kasi, lakini sikuwa katika hali nzuri ya kuridhisha."
"Nilihisi mgongo wangu ulilemewa kidogo, kwa hiyo kile nilichofanya kujaribu kuendelea kwa kadri. Mimi ninazingatia kazi yangu sana, na michezo ya London ilikuwa ni muhimu sana kwangu."
 
kibamba iko dar es salaam ndugu,maeneo hayo kuna kambi za jwtz na jkt na ndiko yaliko makao makuu ya majeshi hayo,kwa taarifa tu mchana wa leo mida ya saa saba,kulikua na pilikapilika za wanajeshi wakiwa wanatembea maeneo ya nje ya kambi sikuelewa kulikuwa na nini bali walikuwa kama wanaelekezana kitu.
 
[h=1]Usain Bolt aandikisha historia London[/h]
9 Agosti, 2012 - Saa 23:08 GMT

120809222551_usain_bolt_304x171_reuters_nocredit.jpg
Bolt aliwaongoza wanariadha wenzake wa Jamaica katika kutwaa medali zote tatu za mbio za mita 200

Usain Bolt usiku wa Alhamisi alifanikiwa kuwa mwanariadha wa kwanza katika historia ya michezo ya Olimpiki, kuweza kuutetea ubingwa wake kikamilifu katika mbio zote fupi, mita 100 na vile mia 200.
Bolt aliwaongoza wanariadha wenzake kutoka Jamaica katika kunyakuwa medali zote tatu katika mashindano hayo ya mita 200.
Muda wa Bolt katika mashindano hayo ulikuwa ni sawa na ule wa Michael Johnson katika mashindano ya Atlanta, na uliokuwa muda bora zaidi wa dunia wakati huo, wa sekunde 19.32.
Mwanariadha ambaye hufanya mazoezi na Bolt, Yohan Blake, alipata medali ya fedha, huku Warren Weir akichukua ya shaba.
Blake alikuwa amemshinda Bolt katika mashindano ya Jamaica ya kufuzu kushirikishwa katika mbio za London, lakini Blake hakuwezana na kasi ya Bolt wakati huu.
"Hili ndilo jambo ambalo nililitaka, na nimefanikiwa kulipata. Ni fahari kuu kwangu," mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25 aliielezea BBC.
"Baada ya msimu mgumu, nilifika hapa na kufanikiwa. Nilidhani kuvunja rekodi iliwezekana. Nafikiri
nilikuwa kasi, lakini sikuwa katika hali nzuri ya kuridhisha."
"Nilihisi mgongo wangu ulilemewa kidogo, kwa hiyo kile nilichofanya kujaribu kuendelea kwa kadri. Mimi ninazingatia kazi yangu sana, na michezo ya London ilikuwa ni muhimu sana kwangu."
Mara mabomu mara riadha, wapi na wapi!!!!?
 
Vipi wakuu mambo yanaendeleaje? Hali imetulia? Maana kuna watu tuna safari ya mkoa alfajiri na mapema.......
 
Hebu Laleni Acheni woga Transformer zimezidiwa zimebutuka moja baada nyingine ....somalia mtakaa kweli nyinyi ?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Uhai wa bomu la kijeshi ni zaidi ya miaka 25; iwapo mabomu hayo yame-expire kiasi cha kulipuka yenyewe basi huenda kuna sababu mbili: ama ni yale yaliyoachwa na utawala wa Nyerere aliyekuwa ameimarisha sana jeshi lake kupambana na uvamizi kutokea popote kwa vile akikuwa kazungukwa na maadui wengi wakati huo. Ama yemenunuliwa na serikali zetu miaka ya hivi karibuni lakini yakiwa yemashazeeka - mitumba.

Tanzania kaa chonjo; hayo maneno ya Lowassa kuwa jeshi liko tayari inawezekana siyo kweli, kwani tunajua kuwa serikali ilishakiri zaidi ya mara tatu kuwa hina pesa: kwa waalimu, kwa madakatari na kwa wafanyakazi wote. Tuna uhakika kuwa kuna kipindi wafanyakazi wa serikali wanacheleweshewa mishahara yao kwa vile serikali haina pesa. Pesa zote za serikali zinatumiwa na viongozi kujineemesha wao na familia zao tu; hakuna la maana wanalofanyia nchi hii. Ninasubiri swala linalohitaji matumzi halisi ya kijeshi lifike nione itakuwaje. Tuliokuwapo mwaka 1979 tunajua hali ilikuwaje, na sioni kama leo tuko tayari tena.
 
Ndo maana movie za kibongo hazilipi. zinatolewa nyingi kwa mpigo. hebu check hapa na nadhani nyingine ntakuwa nimezisahau.
.Babu Ambi wa Loliondo
.TRL kufukuzwa
.MV Spice Islander
.Mafuriko na Mabwepande
.Baraza la mawaziri kuchakachuliwa na dhaifu
.Watalii kuuawa serengeti
.Dr. Ulimboka
.Drs. kufukuzwa
.Mwakyembe na Chizi
.MV Skagit
.Muhongo ft. Maswi na Tanesco
.Mgomo wa Walimu
.Leo mabomu Kibamba
.Lake Nyasa ndo bado iko studio, soon itakuwa released
.
.
Wapenzi wa movie za kibongo wataongezea nyingine.
Kwa style hii wasanii wetu hawawezi wakina TISS hawawezi kupata hela maana movie zimezidi na uchumi wetu wapenzi wa movie sio mzuri. hatuwezi kununua zote, tutaishia ku-burn tu.
 
Tuombe ya Mbagala yasijirudie au mama wa Kimalawi ameamua kufanya kweli wakati rais wenu yuko akitanua Ghana. Mie simo shauri yenu mnamchokoza mama mwenye misuli kuliko wanaume laini wa kibongo. Tupeni update basi. Kama ni mibomu ya jeshi sijui Hussein Mwinyi atanusirikaje. Maana itajengeka dhana kuwa wizara yake ya ulinzi sasa kazi yake ni kuua wabongo wasio na hatia. Akiambiwa ajiuzulu analeta za kuleta.
 
Back
Top Bottom