Milipuko Mikubwa yarindima Kibamba...

CONFIRMED NEWS.
Usiku wa kuamkia leo nilikuwa msibani maeneo ya Kiluvya.
Ilipojiri mida ya saa 6 usiku hali ya wasiwasi ilianza kutanda kutokana na mlipuko wa kwanza kusikika kwa kishindo ukilipuka.
Muda mchache baadae ukaripuka mlipuko mwingine mkubwa zaidi ya ule wa mwanzo kiasi kufanya watu kuwa na wasiwasi zaidi.
Haikuwa radi wala hakikuwa ni kishindo cha transformer kulipuka bali kilikuwa ni kishindo mithiri ileile ya vishindo vilivyotokea Gongo la mboto kwani milipuko ile naikumbuka vizuri kwani nilikuwapo kule.

Baada ya kupita nusu saa ama dakika ishirini ukalipuka mlipuko mwingine, kitu kilichopelekea watu watoke nje na kuwa tayari kwa kuokoa nafsi zao.
kisha mlipuko wa mwisho uliosikika ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba kuta za nyumba na ardhi ziliachwa zinatetemeka.

kama kawaida yangu nilichukua simu yangu na kuingia JF ambapo nilikuta mtoa mada ameweka tayari habari hii na kama kawaida ya wachangiaji wa siku hizi wa JF wengi wamekuwa na mzaha kitu ambacho si kizuri.

Mtoa mada alieleza habari ilivyo kisha kwa kuamini kutojuwa kilichomsibu akapotea ghafla na hakuendelea na updates.
Ila kuna baadhi ya wana JF waliisikia milipuko hiyo na wakathibitisha hilo, na kuna mmoja amesomeka kuwa milipuko hiyo imesikika karibu na maeneo anayoishi kitu kilichomfanya awe na wasiwasi.
Lakini inashangaza watu wanashindwa kupata more updates toka kwa wana JF waliopo ambao wameisikia milipuko hiyo na kuiripoti hapa bali wamekaa wakimsubiri mtoa mada aje athibitishe ili waamini...shame

Inasikitisha hata kuona uongozi wa JF wanashindwa pata habari kamili za kilichotokea usiku wa kuamkia leo ni kipi haswa kutokana na kinachodaiwa kuwa ni milipuko.
JF ni mtandao mkubwa na sidhani kama unakosa mtu toka kambi ya jeshi hapo Kibamba ambaye angeweza towa details juu ya milipuko hiyo...lakini inatia kichefuchefu mpaka saa hizi kuona habari imeandikwa UNCONFIRMED.

JF ulikuwa ni mtandao wa kuthibitisha na wa uhakika wa haraka sana.
Wengi tuliukimbilia kwa habari zenye kuthibitishwa.
Lakini kwa hichi kioja cha leo ambapo milipuko imetokea saa 6 usiku lakini mpaka sasa saa 4 asubuhi na hakuna juhudi zozote toka kwa uongozi kueleza milipuko ile ilikuwa ni ya nini nashindwa kutofautisha mtandao wa JF na blog ya Le Mutuz
 
Mwanadamu anapojitolea kutoa habari hata kama ni ya Kizushi sisi wasomaji kazi yetu ni kuzifanyia kazi sio kumtukana mtoa habari endapo zimekosewa wewe msomaji kazi yako ni kumelimisha mtoa habari unapotukana hujaisadia jamii inayosoma habari hiyo mfano huyo kasikia milipuko anaijulisha jamii wenye ndugu karibu tufanye utafiti juu ya hilo mwenzetu kasikia mlio alafu akae kukujulisha unaelekea wapi wewe unayetukana unaweza ukastamili????????????? binafsi nakupongeza hata kama ni habari za uongo tuzifanyie kazi.
 
Wakuu kiukweli ni mlipuko mmoja tu umetokea na ni wa transfoma ndio maana umeme nao umekatika......lakini kwa sababu hili ni jukwaa la siasa tunaweza kusema ni milipuko 5 au 6 ili tupate sababu ya kuwalaumu . ....


NO Data NO right to speak.
Mitikisiko imesikika ni minee acha kupapatika ili uonekane na wewe ni Great thinker.
Na kwa taarifa yako habari hiyo imerushwa mpaka redioni.
 
Kwahiyo mpaka sasa haijulikani kama ni Mabomu, transformer (hujuma ya wazee wa kutengeneza mgao) au radi??

Strange...!!!
 
na hii ni tatizo kubwa sana......watoaji wa mada hu-mislead watu......na watu nao hukurupuka kama kuku waangaliavyo mwewe...."kwa jicho moja" na kuanza kuchangia UPOTOFU lwa mapovu ya kutosha
Habari sahihi ikija kinyume chake ni aibu kwa JF


Sasa habari sahihi imerushwa redioni je utamlaumu mtoa mada au utawalaumu waliolipua mabomu hayo bila kutoa taarifa?
Na hapo kuna baadhi ya wachangiaji wamekuthibitishia kuwa wameisikia milipuko hiyo, kisha wewe unakaa kulalama tu
 
kama mvua ilikuwa inanyesha jibu lake hizo ni radi zimepiga na tanesco wamezima umeme kwa sababu wana vifaa chakavu so wanaohofia vinaweza kuungua sababu ya radi. mia
Sio radi mzee ni transformer zililipuka tena zaidi ya tatu mimi nipo mbezi nilipata kusikia moja na umeme ukakatika ghafla ndugu yangu yupo kibamba nae akanipigia kuniambia kuna milipuko kadhaa na umeme umekatika nilipomwambia itakuwa ni transformer juu ya mvua zinaziendelea akanigomes eti milipuko ni mikubwa sana, bila shaka ilimwamsha toka usingizini.
 
MODS nao wanabeba sehemu ya lawama maana zinawekwa habari za kupotosha kwa makusudi wanakaa kimya wapotoshaji wangekuwa wanalimwa ban bila mzaha mtu angejishauri mara mbili kabla ya kupost kitu, mods acheni mzaha!


Haya sasa kwa hili wa kupigwa ban ni mtoa mada au wewe uliekurupuka na kupapatika?
Tuliza uno chini hilo uwe unasoma wanachoandika wenzio, sio lazima uchangie.
 
Yalikuwa ni mambomu kweli kwani kwa ndani kuna kambi na wenyewe wanadai walikuwa wanayategua ila najiuliza kama walikuwa wanayategua ama kuyalipua kwanini hawakutoa taarifa kwa wananchi wanategua kimya kimya??

Kibamba jana watu wamelala kimashaka sana sababu ya hiyo milipuko na wanadai wataendelea kuyategua kwaniinasemekana yameisha muda wake wa matumizi kwa hiyo tusubiri kuona mengi.

Asante mzaliwa wa mjini.
 
Haya sasa kwa hili wa kupigwa ban ni mtoa mada au wewe uliekurupuka na kupapatika?
Tuliza uno chini hilo uwe unasoma wanachoandika wenzio, sio lazima uchangie.

niondolee uharisho wako usiniharibie week end mie huwa sibishani na goigoi wa kufikiria!!
 
wewe ni nani hadi uanze kunipangia thread ya kuchangia na ipi ya kuacha? sibishani na vichwa panzi mimi!


Mimi ni Shifta, zee la kisomali.
Ninaishi kwa Mirungi na Maji.
Napatikana Baidoa, Kismay na Mogadishu, Islii na Garitha pale Kenya, na nikiwa Dar napatikana Maeneo mbali mbali ya Kariakoo.

Huwa nachukia sana wakurupukaji wanaojishaua kuandika ushuzi hapa jamvini na wewe ukiwa ni moja wao wa hawa washambenga.

So siwezi kufumbia macho wapuuzi muugeuze mtandao huu kuwa ni kambi yenu ya kuandika ushuzi.

Nakusubiri uje tena.
 
Mimi na ndugu zangu tumepatwa na hofu kubwa milio ilisikika karibu kabisa na nyumbani, ila watu niliowasiliana nao wanasema ni wanajeshi wapo mazoezini..

kama mtoa mada ameisha kufa basi story imeisha lete new story
 
Hayo mabomu yanawafaa Malawi wakayadondoshe ziwa Nyasa ili explorers wakimbie...si unajua tena kijana mdogo akikutukana muonyeshe kazi
 
Back
Top Bottom