Milioni tano naweza pata wazo gani la kufungua biashara

clearmind

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
424
724
Habari za Leo ndugu zangu, vijana wenzangu? Natumaini Mungu anaendelea kutupigania katika mapito yetu ya kila siku.

Nimekaa natafakari sana Hili wazo: Kwamba Kwa umoja wetu, kupitia mikakati sahihi, tunaweza kabisa kuondokana na Hali ya UMASIKINI, utegemezi na janga la ukosefu wa ajira.

Mawazo yangu ni kutaka tuungane vijana mia Moja then tuwe na kikao Cha pamoja ambacho kitatoa wazo la kibiashara lenye uhitaji wa milioni mia Tano.

Tuweke strategies thabiti za kuweza kufanya hiyo biashara na tukishamaliza, tukubaliane kuchanga(kupitia akaunti ya pamoja Benki) Kwa mwaka mmoja ili kuweza kufikisha hicho kiasi Cha pesa.

Milioni mia Tano Kwa watu mia Moja ni sawa na milioni Tano kwa kila mmoja kwa mwaka. Naombeni kuwasiliana.

Mawazo yenu ni muhimu sana.
 
kikao Cha pamoja ambacho kitatoa wazo la kibiashara lenye uhitaji wa milioni mia Tano.
JF inapatikane nchini na nje ya nchi.

Yawezekana mwenye(wenye) nia kama yako wako nchini na wengine nje ya nchi.

Je umelifikiria hilo? Nini mawazo yako? au umelenga watu wa wapi zaidi?
 
Mkiweza kukusanya milioni 500 .....
Basi Haina haja ya kutafuta wazo..
Mmachangishana Tema mara ya pili mnapata bilioni...

Hivyo hivyo...Hadi bilioni 10....mngawana
Hoja ni kwamba tuwe na wazo la biashara Kisha tuanze kuchanga. Tukianzisha biashara Kwa pamoja, kuna faida nyingi kuliko kugawana fadha.
 
Imagine hio ni intro la bonge ya series, afu mweka hazina ambaye nifounder pia anafake kifo ili auhujumu huo mradi nakupiga hela,
Bonge la idea
 
JF inapatikane nchini na nje ya nchi.

Yawezekana mwenye(wenye) nia kama yako wako nchini na wengine nje ya nchi.

Je umelifikiria hilo? Nini mawazo yako? au umelenga watu wa wapi zaidi?
Ni swali zuri, Nina Imani teknolojia inaweza kutusaidia kujadiliana Kwa pamoja bila shida. Kwa mfano, nimewahi kufanya kikao Cha namna hii na vijana wenzangu watano online, na jambo letu likafanikiwa bila shida.
 
Imagine hio ni intro la bonge ya series, afu mweka hazina ambaye nifounder pia anafake kifo ili auhujumu huo mradi nakupiga hela,
Bonge la idea
Pesa zinakusanywa Benki boss. Na makusanyo yatatokana na makubaliano ya members wote.
 
Katika hiyo pesa nikopeshe milioni Moja tu nitalipa Kwa libs ya 20%
 
Imagine hio ni intro la bonge ya series, afu mweka hazina ambaye nifounder pia anafake kifo ili auhujumu huo mradi nakupiga hela,
Bonge la idea
Sidhani kama mawazo hasi yanajenga.

Kama kila mtu angekuwa na mawazo hasi, si dhani kama Tanzania (watanzania) wangekuwa namafanikio waliyo nayo.

Daima jambo kubwa huanza kwa wazo, kimasihara kama hivi, be positive itakusaidia hata katika mipango yako binafsi.
 
Mpaka kufikia kuchanga na kuwa na wazo la biashara, Ina maana tutakuwa na kanuni na taratibu ambazo zitatuongoza Kwa kila hatua. Tutakutana katika vikao na kujadili mambo mbalimbali pia na kufanya tathmini ya mikakati yetu.
 
Sitaki kuonekana pessimistic lakini kwa Wabongo hawa wanaowaza upigaji 24/7 hawa sijui kama hamtazungukwa na signatories wa hiyo akaunti na pesa kupigwa!
Ni muhimu kama watu wanapatikana, mambo yote haya yakajadilika. Na mipango ikawekwa kisheria pia. Fikra zangu ni kwamba tunaweza kuwa watu wa kada tofauti tofauti na wengine wenye uelewa mzuri wa kutusaidia namna ya kusonga na kufikia malengo.
 
Mkiweza kukusanya milioni 500 .....
Basi Haina haja ya kutafuta wazo..
Mmachangishana Tema mara ya pili mnapata bilioni...

Hivyo hivyo...Hadi bilioni 10....mngawana
nikecheka km Mwarabu wa DP World
 
Modes naomba title ya mwanzo irudishwe tafadhali. Hapa siombi wazo la biashara. Mmeandika milioni Tano badala ya milioni mia tano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom