Milioni Hamsini (50,000,000) zimeingia kimakosa kwenye Account yangu

Kaka huo mpunga daah! embu jaribu kuongea na bank iliyokaribu nawe uliza kwanza imetoka kwny account gani uckute ni michezo yao ya kusafisha counterfeit money kama ndivyo mpige pasu kwa pasu na mwenye huo mpunga.
 
Bado hujachukua? Chukua na peleka kwenye uwekezaji wakikuuliza waambie ni kweli halafu utaanza kuwalipa tena tawanya ili wasije kuchukua zote maramoja
 
hilo n kosa la jinai kutoa hyo pesa,na kuitoa mara moja pesa kama hiyo lazma ushikwe coz lazma confirmation zfnyike na branch uliyowekwa kama n miss post itaonekana tuu,
 
mkuu sijui nikushauri nini ila ngoja nikupe mfano kidogo. Kuna rafiki yangu aliwahi kukuta mil 12 kwenye account yake. Naye bila kuchelewa akaitoa na kuitumia then akaachana na hiyo akaunti.
Kumbe ile ela iliingia kwake kimakosa baadae akawa hunted na kukamatwa kwa kosa la cyber crime. Japo mwisho alikuja kuachiwa lakini alikuwa kawekwa ndani kwa week mbili na aliachiwa kwa kurudisha nusu ya ile ela na kuhonga honga sana.
So akili kumkichwa linaweza kuwa ni zali au inawezekana ni shari pia.



Hapo kwa cyber crime charges either umetudanganya au jamaa yako nae alikuwa nunda kukubali hiyo charge......ask me why
 
Hii inanikumbusha Mwaka juzi nikiwa udsm niliwekewa hela ya field mara mbili kwa wakati tofaut,
nikahisi kuwa nikiichukua watanikata kwenye instlement itakayofuata,
nashukuru Mungu nilizitafuna na sikufatiliwa,
 
kwani wao wanajua chanzo cha mapato yako, hadi wawe na uhalali wa kuamini kuwa wewe ulitambua hizo hela si zakwako na ukaamua kuzichukua kwa nia mbaya? WOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO.
 
Hii inanikumbusha Mwaka juzi nikiwa udsm niliwekewa hela ya field mara mbili kwa wakati tofaut,
nikahisi kuwa nikiichukua watanikata kwenye instlement itakayofuata,
nashukuru Mungu nilizitafuna na sikufatiliwa,
 
we kuchua tu hiyo hela....hao bank wenyewe wezi na hiyo usikute wanatumia account yako kupiga michongo yao...sasa hiyo ndiyo mshahara wako kwa wao kutumia account yako.
 
Mimi wakati banki ya posta walikuwa wanatumia vitabu jamaa alikosea kuniandikia salio pale kwenye balance si akaongeza mimi nikaenda kuchukua kwa mara ya kwanza nikasema ngoja nichukue kidogo nione upepo utakavyoenda mara nikafanikiwa na jamaa akaniandikia salio sawa si nikasema sasa naenda kupiga yote kufika pale nikaona jamaa amechukua kitabu akaanza kukipekua kuanzia mwanzo akawa anafwatilia kwa makini niliingiza mkono pale kaunta nikakinyakua kitabu nikatoka aro hadi leo sijawahi kuisogelea tena hiyo banki na hiyo akaunti nakumbuka ilikuwa kama mwaka 1994 hivi.

hivi majuzi nimeenda kwenye akaunti yangu ya NMB nikauliza salio nikaona kuna hela imeongezeka nikasema naiacha kwanza kwa muda nikaenda mara ya pili nikakuta tena salio limeongezeka zaidi nikasema nitaenda nikapoa kukaa kama baada ya wiki nikaenda kuulizia salio nikakuta ile hela haiko ikabidi nichukue statement chaajabu kenye statement haikuoneka.

Hapo kwenye nyekundu usifanye hivyo siku nyingine walinzi wanaweza wakakupiga risasi
 
sdhani kama dr nditi angeweza kukupa jibu kama hili
he was my banking law lecturer
lazima ujue duties za customer kwa bank
mojwapo ni kureport fedha au salio liloingizwa ktk account yake ambalo sio lake
atakuwa hana hatia kama customer hajawithdraw amount that exceeds his normal savings au hajawahi kujua kama kuna ongezeko kama hilo
failure to do that akiwithdraw na kutimka ni kosa la jinai
unadhani ni wote wanaofahamu akaunti zao zina kiasi gani?and how will they prove hilo?
 
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)

Ninamfahamu mkandarasi mmoja aliyeingiziwa 200 million akazitumia immediately kuagiza building, bank walivyogundua ikabidi wakae chini wamweombe wasainiane mkataba wa kukopeshana. Hivyo kama wewe una mradi wenye faida inazidi 30% kwa mwaka; wekeza huko kichwani ukichukulia kama ni mkopo GAZETI
 
Last edited by a moderator:
simple unapocheki salio lako risiti itakuambia una kiasi gani
unapojaribu kudraw kiasi kinachozidi salio lako uliloweka bank
ni wizi tayari hapo intetion inakuwa proved
once umecheki salio computer za bank zitaonyesha muda na siku uliocheki salio
ndio maana sheria imeweka duties za customer kwa bank

unadhani ni wote wanaofahamu akaunti zao zina kiasi gani?and how will they prove hilo?
 
NDUGU zangu ni ajabu kweli, yaani huwezi kuamini, Ile kufika tu NMB si
nikaamua kutest kwnza kwa kwenda Kaunta na kutaka kutoa salio langu lote,
Niliomba 2,350,000. Yaani yule dada alipoiona tu Kadi yangu ya ATM akamwita
mwenzake. Wakaalikana kama watatu hivi, nilimsikia mmoja kwa mbali tena kwa
Kunong'ona akisema ndiyo mwenyewe GAZETI, kumbe gazeti ni****** Kisha
niliambiwa nikaonane na Meneja.

Meneja alinipokea kwa ukarimu sana na kunisifu kwa kitendo changu cha kuelezea
jambo hili kwenye mtandao, Inasemekana matawi mengi ya NMB yalikuwa busy kutafuta
makosa hayo, akaniambia si vizuri sana kufuata baadhi ya ushauri uliotolewa humu
kwani ungenisababishia matatizo, hata hivyo nimeongezewa 500,000 kama ahsante
kwa kutozitoa fedha zile mapema.

Nashukuru kwa ushauri mwingi nilioupata hapa na nimejifunza mengi kupitia Comment
zenu, pia meneja kanishauri mambo mengi sana linapotokea jambo la namna hiyo kubwa
ikiwa ni kutoa taarifa mapema kwani anasema kuna wakati unaweza kujikuta ukitumbukia
kwenye kesi kubwa ambayo umetegeshewa na kukufanya uonekane ni mwizi. Mengi kanieleza
nashindwa kufafanua yote isipokuwa nawashauri watu wa Benki kutoa vipeperushi vya ushauri
kwa wateja linapotokea tatizo kama hili wafanyeje?
 
GAZETI uwiiiiiiiii si nilikuambia watakujua? pole ila nahisi roho ilikuuma as umeshukua masiku kurudi humu kutupa update.

Usingesema hiyo balance yako na bei labda ungesha nunua viwanja, gari etc

Sasa wote walikusubiria I guess wahudumu wote waisumuliana asubuhi wakusubiri ktk branch zao zote nchini.

Sasa ungekuwa unasubiri kwenda mahakamani na kulipa kidogo kidogo, huku matunda unajivunia. mkopo wa bure bila interest.

Enjoy zawadi ila duh hata 1 million walikuwa wabahiri kutoa duh, halafu umewatetea kama vile marafiki zako au ndo na mkopo umepewa labda.

Angalia wasikutoe kwenye gazeti la udaku, wafanyakazi hao kupata pesa...:wink2:
 
Last edited by a moderator:
GAZETI uwiiiiiiiii si nilikuambia watakujua? pole ila nahisi roho ilikuuma as umeshukua masiku kurudi humu kutupa update.

Usingesema hiyo balance yako na bei labda ungesha nunua viwanja, gari etc

Sasa wote walikusubiria I guess wahudumu wote waisumuliana asubuhi wakusubiri ktk branch zao zote nchini.

Sasa ungekuwa unasubiri kwenda mahakamani na kulipa kidogo kidogo, huku matunda unajivunia. mkopo wa bure bila interest.

Enjoy zawadi ila duh hata 1 million walikuwa wabahiri kutoa duh, halafu umewatetea kama vile marafiki zako au ndo na mkopo umepewa labda.

Angalia wasikutoe kwenye gazeti la udaku, wafanyakazi hao kupata pesa...:wink2:
Dah, hii JF ni balaa yaani utafikiri kila Mtanzania anapita huku,
Lakini inabaki kuwa tunajifunza kutokana na MAKOSA. Ushauri
ulionisisimua zaidi humu ndani ni ule wa MKOPO BILA RIBA.
 
Back
Top Bottom