Milioni Hamsini (50,000,000) zimeingia kimakosa kwenye Account yangu

uwoga wenu ndiyo unawapa shida.....toa hela hizo katika ac yako....si wamukuingizia wenyewe
 
Kwa mujibu wa sheria za kibenki,makosa yafanywayo na benki hayambani mteja. Hayo ni makosa ya benki. Hupaswi kuogopa. Toa hizo pesa na uzitumie. Utajuta kuziachaacha pesa za bure

Unajua banking wewe au unasema tu... usimtafutie mwenzio matatizo bure, ka hujui piga kimya
 
Hiyo pesa tumia mkuu mafisadi wanazitakatisha sema wamejichanganya wangeleta kwangu waone hakuna sheria ya kukutia hatiani ni kosa la bank na watakao kulipia hiyo pesa ni watumishi wa bank husika
 
Mkuu ucjal we kua na subira... hakuna bank inayoweza ku-withdraw ela kwenye a/c ya mtu lazima wawasiliane na A/c holder.
Pili, nenda kaombe bank statement iwenayo kama reference incase ela ikatolewa bila kukutaarifu unaweza uliza kwa branch manager
 
chukua hizo pesa kisheria huna hatia..negligence inahamia kwa upande wa benki wenyewe...wanachoweza kufanya benki ni ku recovery hiyo pesa kwa njia ya kukukata kila unapoweka pesa mpaka warudishe pesa zao but there is no way waka kuincriminated trust me.niliwahi kumuuliza one of the Prof N. N. NDITI ambaye ni taalam wa mambo ya sheria za benki na hilo ndo lilikuwa jibu lake...even banks make mistake,and Loss!so ni burden kwao.

Kumbe profesa nae hajui anakariri tu....
 
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)
nimekutumia mimi hizo ni zakwako chukua. nitakutafuta tuzungumze
 
mkuu sijui nikushauri nini ila ngoja nikupe mfano kidogo. Kuna rafiki yangu aliwahi kukuta mil 12 kwenye account yake. Naye bila kuchelewa akaitoa na kuitumia then akaachana na hiyo akaunti.
Kumbe ile ela iliingia kwake kimakosa baadae akawa hunted na kukamatwa kwa kosa la cyber crime. Japo mwisho alikuja kuachiwa lakini alikuwa kawekwa ndani kwa week mbili na aliachiwa kwa kurudisha nusu ya ile ela na kuhonga honga sana.
So akili kumkichwa linaweza kuwa ni zali au inawezekana ni shari pia.

Sina nia ya kumshauri jambo lolote kwa sasa, lakini hiyo haiwezi Ku amount cyber crime mkuu. Kuna reasons za kusema hivyo.
 
Habari zenu ndugu zangu, nimeacha pesa kidogo sana kwenye
Account yangu ya NMB. (2,356,700) Nimeenda kuangalia salio
nimekuta 52,356,700.

Je naweza kuchukua hizi pesa na nisishitakiwe?
kama nitashitakiwa kuna uwezekano wa kushinda kesi?

Tafadhali naombeni maelezo haraka iwezekanavyo.

NB kwenye heading ni (50,000,000)

Angalia bwana...unaweza kukuta mtu anakuuliza baadaye kama mahali aliyokutolea uliipata? Angalia bwana, wanaume wa Uingereza huko wana michezo mibaya, oohoo!

Ushauri wangu ni kwamba, fungua account nyingine ya savings, na iweke hiyo hela yote 50Ml ili upate interest ambayo si haba kwa kiasi hicho cha fedha. Siku wakikudai warudishie hiyo 50M yao wewe baki na interest ya bure!
 
But in that case rightfull owner hakuwa identified.

Kama benki ikiweka pesa kwenye account yako under a mistake of fact or law, benki hiyo iko entitled to recover it from you.

You will not be allowed to unjustly enriched yourself at the expense of another aka the bank b'se kama sh 50,000 ilitakiwa ije kwenye account yangu lakini ikawekwa kwenye account yako kimakosa, benki itabidi itafute 50,000 na kuziweka kwenye account yangu.

In doing so benki itakuwa ime-suffer loss ya 50,000 na kama wakishtukia kuwa hiyo 50,000 waliweka kwenye account yako kimakosa, then they would be entitled to recover it from you.

Na je kama hakuna ambaye anapata hasara ya hio kitu je utakua na uhalali wa hio hela? Mfano nimechukua hela iliyoko insured na huyo mtu akarudishiwa hela na insurance company na maisha yakaendelea nini tatizo hapo?

Hapo insurance company ndo itakuwa imepata hasara, and it would be entitled to bring a restitutionary claim against you to recover the money they paid to you kimakosa unless you can show that you have changed position in good faith tokea ulipopewa hizo fedha.
 
daaaah kweli mwaka mgumu huu watu wana ugwadu na pesa hadi wameibua opost ya zamani :A S-eek:

mie nashangaa sana post ina miaka 2..jamaa anakaribia kurud uraian.

coz mashart ya benki yanakataza wizi.
we una mil 2 na acc yako haina historia ya kupokea pesa nyingi...kama we sio mwizi ukikuta zaidi ya haki yako unapaswa uende kwa branch meneja kuulizia vinginevyo uprove beyond reasonable dought kwamba hukuwa na nia mbaya ya kuchukua kisiko halali yako..(mie sio mwanasheria wa maswala ya banking)
 
Back
Top Bottom