Usiku ulioacha alama kwenye maisha yangu katika medani za utafutaji

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
380
883
Familia yangu ya hapa jf hi for everybody!!!

Baada ya kumaliza chuo na kujikusanya vijisenti vya bumu, niliamua kuchangamkia fulsa ya kilimo cha WhatsApp kilichokuwa kinavuma kwa kipindi hicho. Nilijiunga kwenye group moja la WhatsApp la jamaa mmoja aliyekuwa anavuma huko insta kama bikira wa kisukuma ( r.i.p). Ama kweli utajiri ulikuwa kama wote kwa jinsi nondo zilivyokuwa zinashushwa. Niliingiza pesa nyingi sana kwenye kilimo na yote ilifia huko yaani zaidi ya milion nane yaani ukumbuke wakati nikiwa chuo nilikuwa nakopesha hivyo niliweza kutengeneza capital nzuri tu ya kuja kuanzia maisha uraiani.

Baada ya kilimo kunifanya hamna, niliishiwa hadi mia mbovu. Ikanibidi nianze upya kuzichanga sarafu ndogondogo, nilifanya kazi zote za halali, nilijifunza ukuli nikawa napakia na kupakua mizigo kwenye magari, nilibeba sana mizigo sokoni pale mgandini tanga. Baada ya kama mwaka mzima nikiwa nafanya hizo kazi bila kubadilisha upepo wa maisha, niliamua kujiingiza kwenye uchimbaji madini.

Huko kwenye madini nilijitoa mhanga, hata familia yangu sikuwajulisha kuwa nachimba, it is very risk! Unashuka zaidi ya mita mia na hamsini chini ya ardhi, hata iwe mchana huko ni giza totoro. Nilifanya kazi hiyo ngumu na ya risk kwa malengo mnoo. Ilipofika January 2019 nilibadilisha upepo, kulingana na juhudi niliyokuwa nayo katika kazi nikapewa usimamizi pale mgodini, pia nikawa nakopesha kwa riba kwa wachimbaji ambao walikuwa wanakatwa kwenye mgao siku ya mwisho. Nilitengeneza pesa, afya yangu ya enzi namaliza chuo ikaanza kurejea!!

Ng'ombe wa maskini hazai!! Ni kauli ya kipuuzi kwelikweli lakini ni kama ina ukweli fulani. Ilipofika April nilikuwa tayari na kama million tatu na nusu. Mzee baba, nikaichoka kazi, nikawa sitamani kuendelea kufanya kazi za kitumwa tena licha ya kuwa nilikuwa nimepunguziwa majukumu, nikawa najiona de la don ndo mimi, nani atanibabaisha! Niliamua kurudi nyumbani kwetu magharibi, kichwani nikiwa na wazo la kwenda kufungua biashara. Niliondoka mgodini nikarudi zangu home, ila pia niliwajulisha wakuu wangu hapo mgodini, safari ikaiva huyoo magharibi moja!

Mpaka nafika home, plus zawadi, na nini na nini mkononi nilikuwa na kama m mbili na nusu zimebaki. Nikaanza kuwaza wazo la biashara, lakini kisaikolojia sikuwa okay nikijiuliza mbona mapema tu million imekatika. Nikiwa sijapata wazo la biashara, wazo la kubeti lilianza kuitawala akili yangu. Nilianza kutupia mkeka.

Mwanzoni upepo ulikuwa wangu kabla haujabadilika. Nilifanikiwa kuisogeza pesa yote nikawa na milioni tatu, bado sikuridhika nikadhamilia ifike walau na laki tano. Nilikuwa nabeti timu moja tu yenye uwezekano mkubwa wa kushinda ila natumia stake kubwa. Kweli ikafika million tatu na nusu. Sasa nikapanga nibeti kwa mara ya mwisho ifike milioni nne niache kabisa kisha nikafungue biashara, lahaulaa!!

Ilikuwa usiku wa tar 9 mei 2019, ilikuwa ni fainali ya UEFA UROPA league kati ya miamba wa darajani Chelsea na watabe wa bundesliga Utrecht Frankfurt. Ni siku ambayo nilidhamilia nibeti kwa mara ya mwisho. Kwa jinsi Chelsea alivyokuwa anagawa dose nilielewa ni mapema tu Frankfurt atakuwa amechakazwa. Nilitupia mkeka mmoja wenye stake ya milioni tatu, nikimpa ushindi Chelsea.

Dakika za mapema kabisa Chelsea aliongoza kwa goli moja ambalo lilidumu adi kipindi cha kwanza kinaisha. Hapo hamu yangu ilikuwa nishuhudie goli la pili likipachikwa na wababe hao wa ligi ya uingereza. Waliporejea kipindi cha pili dakika ya 49 Frankfurt walisawazisha ikawa moja moja.

Pressure ilianza kunipanda, nikiwaza kuipoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho na damu tena kwenye mazingira yasiyo rafiki. Lakini upande mwingine bado nilijipa matumaini kuwa muda ulikuwa unatosha kwa Chelsea kufanya yake. Dakika zilisogea si kidogo mara dakika ya 80. Nilikuwa kama nasikia shoti zikitokea kwenye mwili wangu.

Dakika ya 89 bado 1:1, kama nataka kuzimia, nilikuwa nikisubiri maajabu ya mtaalamu wa soka wa darajani enzi hizo Eden Hazard lakini wapi. Mara za nyongeza tatu, nilitamani nitoke kwenye kibanda umiza, nilihisi kila aliyekuwepo mule ndani alielewa kuwa sekunde kadhaa mbele naenda kupoteza milioni tatu. Ilikuwa saa sita na dakika nne mpira ulimalizika kwa sare ya 1:1. Nilikuwa nimepoteza shilingi za kitanzania milioni tatu.

Nilijilaani nikajichukia, niliwaza pesa niliyoitafuta kwa zaidi ya miaka miwili leo inakuja kupotea ndani ya usiku mmoja, jinsi ambavyo nimekuwa saa ingine silali nikipambana usiku na mchana kuzitafuta dolali leo nazitoa sadaka kwa wazungu? Astagafuluhilahh!!!! Nilijichukia sana.

Nilienda kulala usingizi haukuja, nilikuwa nimebakiwa na laki tano kwenye account ya mpesa. Nikapata wazo! Yes wazo. Niangalie timu zilizo live nicheze tatu kwa stake ya laki tano, nilijifariji kuwa kama tayari nimeshapoteza milioni tatu iweje laki tano iniume, potelea mbali, lakini pia kama ntakula nitakuwa nimeiokoa milioni tatu yangu na nitaacha kubeti. Laki tano nayo ikaenda kwa hewani kusubiria hukumu, baada ya saa moja majibu yalikuwa yametoka mkeka ulikuwa umechanika, awamu hii sikuona jipya kwani tayari nilikuwa na ganzi nzito ya kibano cha kwanza.

Ikuwa imeshatimu saa Tisa, mpaka na dakika arobaini ndipo usingizi ulinichota, nilikuwa naweweseka na kushituka. Hata ilipofika asubuhi sikuamini nikijitahidi kuhakikisha kama siko usingizini naota, lakini wapi!

Nitarudi kumalizia

Inaendelea...

Katika baraka niliyojaaliwa ambayo muda mwingine huiona ni kama uendawazimu ni uwezo wangu mkubwa wa kulikubali jambo. Milioni tatu na nusu siyo kitoto katika kipindi ambacho nilikuwa nawaza niwe na biashara imara na pengine kufikiria kuoa, lakini leo asubuhi hii naamka nikiwa na laki moja iliyokunjwa mara mbili mfukoni.

Niliwaza kurudi mgodini nikaanze upya kuchimba, lakini bado naikumbuka vyema shuruba ya huko yaani ukishuka manta ni kama unakuwa umeenda dunia nyingine ambayo huna uhakika kama utarudi. Lakini bado nakumbuka nilivyoondoka nimetunisha kifua alihali walikuwa bado wananihitaji, jinsi nilivyojitapa kwa wachimbaji wenzangu kuwa mimi ndo basi tena kuchimba. Yaani kiufupi nilikuwa nachanganyikiwa nisijue nifanye nini.

Baada ya tafakuri ya siku nzima juu ya kile kilichokuwa kimenitokea, niliamua kufikia mwafaka kama ifuatavyo; kwanza, zilizopote ni hela mimi ni buheri wa afya hivyo nafasi ya kusahihisha makosa yangu bado ilikuwepo. Pili, nianze upya kuzikusanya shilingi, nikifanya kazi zozote za halali na nisirudie kosa tena la kutaka utajiri within a single night.

Niliamua kwenda kufanya kazi yangu ya awali ya kubeba mizigo, safari hii nilienda kwenye mashamba ya mpunga huko bende la usangu kwani ndo ilikuwa muda wa mavuno. Nilifanya kazi ya ukuli kuanzia May hadi June msimu ukawa umeisha. Hapo nilikuwa na kama laki tatu tu. Sikuwa na namna ya kufanya nikiwaza kurudi nyumbani.

Katika vipindi vigumu ndipo akili hupata akili ndani yake. Ni katika kipindi ambacho nikiwa nina laki mbili na chenji mkononi sijui nifanyeje, ndipo wazo la kurudi mgodini lilinijia. Niliwaza kuwa, kwani wakati naondoka niliua, niliiba au nilikosana na mtu zaidi tu ya kujiona ninazo?

Nilikata shauri, niliamua nirudi mgodini nikachimbe tena, nilitafuta namba ya simu nikawapiga viongozi kuwajulisha kuwa narudi kuchimba. Walinikaribisha, nilianza safari hatimaye milimani nikatua mgodini. Zilianza kejeli za hapa na pale, lakini nilikuwa nimejipanga kuwajibu, kuwa ggm ni bilionea lakini hajaacha uchimbaji iweje mimi na vichenji maiti vyangu niache kuchimba! Niliwaambia pesa niliyoondoka nayo nimenunulia mazao nitaenda kuyauza bei ikipanda, kumbe siri naijua mwenyewe.

Pale mgodini kitu bangi ni kawaida sana, sasa nikiwa na siku mbili tu tulikuwa manta tunapandisha fero, kuna dogo bangi kama zote, tulipishana kauli akaanza kunichana mazee!! Nawewe braza ni kiwaki tu, uliondoka hapa umepiga hela umefika wapi sasa, zimekuishia umerudi kuchimba komaa k******! Da! Yaani ni kama aligonga nozel fulani kwenye ubongo na kusababisha shoti. Nilimjibu matusi lakini nilikuwa nimekumbushwa kitu ambacho nilikuwa nimeanza kukisahau. Upya nilianza tena kujilaani na kujiona benge la kubwa jinga. Nilipoteza munkari wa kazi nikiziwaza ndoto zangu zilizoyeyuka, iko wapi biashara kubwa niliyoipigania kwa miaka miwili, vipi kuhusu ndoa ya mwanamke niliyepanga kumuoa nikiwa na kipato kizuri nitimize wajibu wangu ipasavyo. I was totally confused! Nilijilaani tena, nikamulaumu Mungu kwa nini ameruhusu pesa niliyoitafuta kwa jasho jingi nikiyaweka maisha yangu rehani ipotee.

Siku zilisonga nikaendelea kufanya kazi pale mgodini nikiwa na laki mbili na ishirini tokea usangu. Siku moja asubuhi nikiwa nachukua dawa ya mswaki kwenye begi nililokuwa natumia kuhifadhia, lilikuwa ni begi chakavu lililokuwa limetelekezwa kwa matumizi lasmi, ila mimi nilikuwa nalitumia kuhifadhia vitu vyangu vya ziada kama tochi, mswaki na dawa na nguo chakavu za kazini.

Sasa siku hiyo nikiwa napekua kuitafuta dawa ya meno ambayo ilikuwa haionekani, nikiwa napekua kwenye kila mfuko wa begi, mara mkono ulienda kushika kitu ambacho roho ilishituka! Nilipokitoa juu kilikuwa ni kitita cha noti za elfu tano tano kimebanwa na raba band. Kidogo akili ilizubaa nisijue nifanye nini. Hiyo pesa niliirudisha humo kwenye begi na kutoka nje ambapo nilikuwa kwenye kigagaziko kikubwa mno, niichukue au niwajulishe viongozi kuwa kwenye hilo begi nimekuta pesa?

Nilirudi tena kuikagua vizuri, ilikuwa ni kubunda ambacho kwa harakaharaka ungekikadiri kwenye laki tano, lakini ni hela ambayo inaonyesha imekuwepo kwenye hilo begi kwa muda mrefu maana kuna namna imejikunja wala hainyooki.

Dadeki, nilidhamilia kuondoka nayo. Niliibeba nikaitia mfukoni nikapotelea zangu porini kwenda kuihesabu.

Inaendelea...

Tunamalizia kiporo, twende sambamba.

Huko porini nilitafuta chaka lililotulia nikakaa hapo huku kibunda changu mkononi. Nilizihesabu noti hizo, jumla ilikuwa laki tatu na sabini. I thanked God though it was illicitly collected. Nilipiga hesabu laki mbili na ishirini niliyobaki nayo baada ya kufika hapo mgodini plus na hizo za rehema sijui ya mungu au ya shetani, nikawa na jumla ya laki tano na tisini. Nilianza kupata faraja upya, nilifurahi mno kuzidi kawaida nikajiaminisha kuwa huenda mwenyezi mungu ana jambo kuhusu mimi.

Mpaka hapo nilikuwa nimeshapata mtaji wa kukopesha kwa riba maana ilikuwa shilingi inazaa shilingi, hivyo kama ningeiingiza yote ningeweza kupata return ya kuanzia laki nane maana huwezi kupata asilimia mia moja, wapo wanaozingua pia anakurudishia mtaji tu.

Ni kama neema ilikuwa imefunguka juu yangu. Kabla sijaenda nyumbani niliteuliwa kuwa kiongozi pale mgodini kusimamia shift, sasa madili ya pesa ni mengi, yaani kila mwenye mchongo na wewe umoo. Nilivyoondoka kuna jamaa alipewa nafasi yangu. Sasa niliporudi nikiwa na siku nne tu pale kazini, jamaa alikamatwa na kashifa ya kuiba mawe ya dhahabu, hivyo ikabidi mwenyewe mcrounmj nipewe hiyo nafasi.

Safari hii nilikuwa na wakati mzuri mno licha ya kwamba mgodi ulikuwa umepunguza sampo ya madini. Uaminifu niliokuwa nimeujenga ulitoa mwanya wa kuaminiwa kuachiwa kusimamia mizigo yenye madini, hivyo lilikuwa ni swala la mimi kujiongeza. Safari hii sikuutaka usamalia wema na sifa za kijinga, nafasi ilipopatikana nilipiga tena hasa.

November 2019 niliweka mikakati kuwa nifanye kazi za machimbo hadi March 2020. Hapo nitakuwa na mtaji mkubwa tu ambao utanisaidia kufungua biashara. Mambo yalianza kubadilika, hela zikawa zinanipa moyo siku hadi siku. Niliiheshimu chapaa, niliikusanya kutoka kwenye mgao wangu wa shift, madili ya hapa na pale nikitumia mgongo wa cheo changu na kutoka kwenye biashara ya kukopesha. Sikutaka kujihusisha na pombe, japo bidada walitumika mara mojamoja sana.

Mapema April 2020 nilikuwa nimericover, pesa yangu ilikuwa inasoma zaidi ya milioni tatu. March ilifika, nilikuwa bado nimenogewa kupiga job, nilifanya kazi mpaka May, siku ambayo nilipanga ndo naacha kazi ilikuwa ni siku nimeandaa mchongo wa mawe ya dhahabu yenye thamani ya kama milioni. Yaani sijui ni nani alinichomea ila nilishangaa boss anakuja moja kwa moja kwangu kunikagua. Hapa ndugu msomaji wangu naomba uelewe wizi wa madini migodini ni jambo la kawaida. Huwezi kuwa mchimbaji uliyeiva kama hujui mbinu za kuiba. Hiyo ndiyo sifa ya mchimbaji. Basi walichukua mawe mimi wakaniacha, lakini kwa heshima niliyokuwa nayo siku hiyo niliaibika, lakini ndio uchimbaji kwaiyo ilikuwa kishikaji sana.

Baada ya hapo sikuwa na mudi ya kazi tena, nilitamani niondoke nikaanze maisha yangu, na nilikuwa na pesa kesh milioni tano na upuuzi. Safari hii sikutaka kurudia makosa, wala sikutaka kwenda home. Nilidhamilia jambo. Yes jambo!! Niliondoka kimyakimya nikaenda zangu town kufatilia vibali vya kununulia dhahabu, yaani nianze biashara ya dhahabu. Nilifanikiwa kupata leseni. Nikarudi porini kwangu. Safari hii sikurudi kama mchimbaji bali nilirudi kama digara au blocker.

Nilifungua ofisi. Yapo mengi yalijili ikiwemo kuletewa songombingo kutoka kwa boss wangu pale mgodini, madigara wakongwe. Lakini nilisimama. Nilifanya kazi kwa nguvu kubwa ya kuitangaza ofisi na kutafuta wateja. Haikuwa kazi ngumu kwani nimekuwa nikifahamiana na wachimbaji tangu nachimba. Nikiri tu kuwa nimekutana na changamoto lukuki lakini mafanikio yamekuwa makubwa zaidi ndani ya miezi hii minne ya biashara.

Labda nitahadhalishe tu kuwa sijaweka hapa bandiko hili kwa lengo la ufahari, big NO!! Nimeweka bandiko hili la safari ya kuhangaika kwangu kuukumbusha ulimwengu wa vijana kuwa changamoto wanazozipata katika harakati za utafutaji wazichukulie ni ngazi ambazo wanatakiwa wazikanyage kuelekea kufanikiwa. Mimi mwenyewe ndoto yangu ni kubwa mno bado sijafika japo napata amani nikiangalia salio linasoma kwenye early eight digits in tz shillings, Oh salale! Vijana tufunge mikanda, yajayo yanafurahisha.
 
Familia yangu ya hapa jf hi for everybody!!!

Baada ya kumaliza chuo na kujikusanya vijisenti vya bumu, niliamua kuchangamkia fulsa ya kilimo cha WhatsApp kilichokuwa kinavuma kwa kipindi hicho. Nilijiunga kwenye group moja la WhatsApp la jamaa mmoja aliyekuwa anavuma huko insta kama bikira wa kisukuma ( r.i.p). Ama kweli utajiri ulikuwa kama wote kwa jinsi nondo zilivyokuwa zinashushwa. Niliingiza pesa nyingi sana kwenye kilimo na yote ilifia huko yaani zaidi ya milion nane yaani ukumbuke wakati nikiwa chuo nilikuwa nakopesha hivyo niliweza kutengeneza capital nzuri tu ya kuja kuanzia maisha uraiani.

Baada ya kilimo kunifanya hamna, niliishiwa hadi mia mbovu. Ikanibidi nianze upya kuzichanga sarafu ndogondogo, nilifanya kazi zote za halali, nilijifunza ukuli nikawa napakia na kupakua mizigo kwenye magari, nilibeba sana mizigo sokoni pale mgandini tanga. Baada ya kama mwaka mzima nikiwa nafanya hizo kazi bila kubadilisha upepo wa maisha, niliamua kujiingiza kwenye uchimbaji madini. Huko kwenye madini nilijitoa mhanga, hata familia yangu sikuwajulisha kuwa nachimba, it is very risk! Unashuka zaidi ya mita mia na hamsini chini ya ardhi, hata iwe mchana huko ni giza totoro. Nilifanya kazi hiyo ngumu na ya risk kwa malengo mnoo. Ilipofika January 2019 nilibadilisha upepo, kulingana na juhudi niliyokuwa nayo katika kazi nikapewa usimamizi pale mgodini, pia nikawa nakopesha kwa riba kwa wachimbaji ambao walikuwa wanakatwa kwenye mgao siku ya mwisho. Nilitengeneza pesa, afya yangu ya enzi namaliza chuo ikaanza kurejea!!

Ng'ombe wa maskini hazai!! Ni kauli ya kipuuzi kwelikweli lakini ni kama ina ukweli fulani. Ilipofika April nilikuwa tayari na kama million tatu na nusu. Mzee baba, nikaichoka kazi, nikawa sitamani kuendelea kufanya kazi za kitumwa tena licha ya kuwa nilikuwa nimepunguziwa majukumu, nikawa najiona de la don ndo mimi, nani atanibabaisha! Niliamua kurudi nyumbani kwetu magharibi, kichwani nikiwa na wazo la kwenda kufungua biashara. Niliondoka mgodini nikarudi zangu home, ila pia niliwajulisha wakuu wangu hapo mgodini, safari ikaiva huyoo magharibi moja!

Mpaka nafika home, plus zawadi, na nini na nini mkononi nilikuwa na kama m mbili na nusu zimebaki. Nikaanza kuwaza wazo la biashara, lakini kisaikolojia sikuwa okay nikijiuliza mbona mapema tu million imekatika. Nikiwa sijapata wazo la biashara, wazo la kubeti lilianza kuitawala akili yangu. Nilianza kutupia mkeka. Mwanzoni upepo ulikuwa wangu kabla haujabadilika. Nilifanikiwa kuisogeza pesa yote nikawa na milioni tatu, bado sikuridhika nikadhamilia ifike walau na laki tano. Nilikuwa nabeti timu moja tu yenye uwezekano mkubwa wa kushinda ila natumia stake kubwa. Kweli ikafika million tatu na nusu. Sasa nikapanga nibeti kwa mara ya mwisho ifike milioni nne niache kabisa kisha nikafungue biashara, lahaulaa!!

Ilikuwa usiku wa tar 9 mei 2019, ilikuwa ni fainali ya UEFA UROPA league kati ya miamba wa darajani Chelsea na watabe wa bundesliga Utrecht Frankfurt. Ni siku ambayo nilidhamilia nibeti kwa mara ya mwisho. Kwa jinsi Chelsea alivyokuwa anagawa dose nilielewa ni mapema tu Frankfurt atakuwa amechakazwa. Nilitupia mkeka mmoja wenye stake ya milioni tatu, nikimpa ushindi Chelsea.

Dakika za mapema kabisa Chelsea aliongoza kwa goli moja ambalo lilidumu adi kipindi cha kwanza kinaisha. Hapo hamu yangu ilikuwa nishuhudie goli la pili likipachikwa na wababe hao wa ligi ya uingereza. Waliporejea kipindi cha pili dakika ya 49 Frankfurt walisawazisha ikawa moja moja.

Pressure ilianza kunipanda, nikiwaza kuipoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho na damu tena kwenye mazingira yasiyo rafiki. Lakini upande mwingine bado nilijipa matumaini kuwa muda ulikuwa unatosha kwa Chelsea kufanya yake. Dakika zilisogea si kidogo mara dakika ya 80. Nilikuwa kama nasikia shoti zikitokea kwenye mwili wangu. Dakika ya 89 bado 1:1, kama nataka kuzimia, nilikuwa nikisubiri maajabu ya mtaalamu wa soka wa darajani enzi hizo Eden Hazard lakini wapi. Mara za nyongeza tatu, nilitamani nitoke kwenye kibanda umiza, nilihisi kila aliyekuwepo mule ndani alielewa kuwa sekunde kadhaa mbele naenda kupoteza milioni tatu. Ilikuwa saa sita na dakika nne mpira ulimalizika kwa sare ya 1:1. Nilikuwa nimepoteza shilingi za kitanzania milioni tatu. Nilijilaani nikajichukia, niliwaza pesa niliyoitafuta kwa zaidi ya miaka miwili leo inakuja kupotea ndani ya usiku mmoja, jinsi ambavyo nimekuwa saa ingine silali nikipambana usiku na mchana kuzitafuta dolali leo nazitoa sadaka kwa wazungu? Astagafuluhilahh!!!! Nilijichukia sana.

Nilienda kulala usingizi haukuja, nilikuwa nimebakiwa na laki tano kwenye account ya mpesa. Nikapata wazo! Yes wazo. Niangalie timu zilizo live nicheze tatu kwa stake ya laki tano, nilijifariji kuwa kama tayari nimeshapoteza milioni tatu iweje laki tano iniume, potelea mbali, lakini pia kama ntakula nitakuwa nimeiokoa milioni tatu yangu na nitaacha kubeti. Laki tano nayo ikaenda kwa hewani kusubiria hukumu, baada ya saa moja majibu yalikuwa yametoka mkeka ulikuwa umechanika, awamu hii sikuona jipya kwani tayari nilikuwa na ganzi nzito ya kibano cha kwanza.

Ikuwa imeshatimu saa Tisa, mpaka na dakika arobaini ndipo usingizi ulinichota, nilikuwa naweweseka na kushituka. Hata ilipofika asubuhi sikuamini nikijitahidi kuhakikisha kama siko usingizini naota, lakini wapi!

Nitarudi kumalizia
Kwenye kutafuta kuna mengi sana wwngine wanapotea wao wenyewe (kufa). Na wengine wanapoteza pesa kama ww
 
Pole sana
 
Familia yangu ya hapa jf hi for everybody!!!

Baada ya kumaliza chuo na kujikusanya vijisenti vya bumu, niliamua kuchangamkia fulsa ya kilimo cha WhatsApp kilichokuwa kinavuma kwa kipindi hicho. Nilijiunga kwenye group moja la WhatsApp la jamaa mmoja aliyekuwa anavuma huko insta kama bikira wa kisukuma ( r.i.p). Ama kweli utajiri ulikuwa kama wote kwa jinsi nondo zilivyokuwa zinashushwa. Niliingiza pesa nyingi sana kwenye kilimo na yote ilifia huko yaani zaidi ya milion nane yaani ukumbuke wakati nikiwa chuo nilikuwa nakopesha hivyo niliweza kutengeneza capital nzuri tu ya kuja kuanzia maisha uraiani.

Baada ya kilimo kunifanya hamna, niliishiwa hadi mia mbovu. Ikanibidi nianze upya kuzichanga sarafu ndogondogo, nilifanya kazi zote za halali, nilijifunza ukuli nikawa napakia na kupakua mizigo kwenye magari, nilibeba sana mizigo sokoni pale mgandini tanga. Baada ya kama mwaka mzima nikiwa nafanya hizo kazi bila kubadilisha upepo wa maisha, niliamua kujiingiza kwenye uchimbaji madini.

Huko kwenye madini nilijitoa mhanga, hata familia yangu sikuwajulisha kuwa nachimba, it is very risk! Unashuka zaidi ya mita mia na hamsini chini ya ardhi, hata iwe mchana huko ni giza totoro. Nilifanya kazi hiyo ngumu na ya risk kwa malengo mnoo. Ilipofika January 2019 nilibadilisha upepo, kulingana na juhudi niliyokuwa nayo katika kazi nikapewa usimamizi pale mgodini, pia nikawa nakopesha kwa riba kwa wachimbaji ambao walikuwa wanakatwa kwenye mgao siku ya mwisho. Nilitengeneza pesa, afya yangu ya enzi namaliza chuo ikaanza kurejea!!

Ng'ombe wa maskini hazai!! Ni kauli ya kipuuzi kwelikweli lakini ni kama ina ukweli fulani. Ilipofika April nilikuwa tayari na kama million tatu na nusu. Mzee baba, nikaichoka kazi, nikawa sitamani kuendelea kufanya kazi za kitumwa tena licha ya kuwa nilikuwa nimepunguziwa majukumu, nikawa najiona de la don ndo mimi, nani atanibabaisha! Niliamua kurudi nyumbani kwetu magharibi, kichwani nikiwa na wazo la kwenda kufungua biashara. Niliondoka mgodini nikarudi zangu home, ila pia niliwajulisha wakuu wangu hapo mgodini, safari ikaiva huyoo magharibi moja!

Mpaka nafika home, plus zawadi, na nini na nini mkononi nilikuwa na kama m mbili na nusu zimebaki. Nikaanza kuwaza wazo la biashara, lakini kisaikolojia sikuwa okay nikijiuliza mbona mapema tu million imekatika. Nikiwa sijapata wazo la biashara, wazo la kubeti lilianza kuitawala akili yangu. Nilianza kutupia mkeka.

Mwanzoni upepo ulikuwa wangu kabla haujabadilika. Nilifanikiwa kuisogeza pesa yote nikawa na milioni tatu, bado sikuridhika nikadhamilia ifike walau na laki tano. Nilikuwa nabeti timu moja tu yenye uwezekano mkubwa wa kushinda ila natumia stake kubwa. Kweli ikafika million tatu na nusu. Sasa nikapanga nibeti kwa mara ya mwisho ifike milioni nne niache kabisa kisha nikafungue biashara, lahaulaa!!

Ilikuwa usiku wa tar 9 mei 2019, ilikuwa ni fainali ya UEFA UROPA league kati ya miamba wa darajani Chelsea na watabe wa bundesliga Utrecht Frankfurt. Ni siku ambayo nilidhamilia nibeti kwa mara ya mwisho. Kwa jinsi Chelsea alivyokuwa anagawa dose nilielewa ni mapema tu Frankfurt atakuwa amechakazwa. Nilitupia mkeka mmoja wenye stake ya milioni tatu, nikimpa ushindi Chelsea.

Dakika za mapema kabisa Chelsea aliongoza kwa goli moja ambalo lilidumu adi kipindi cha kwanza kinaisha. Hapo hamu yangu ilikuwa nishuhudie goli la pili likipachikwa na wababe hao wa ligi ya uingereza. Waliporejea kipindi cha pili dakika ya 49 Frankfurt walisawazisha ikawa moja moja.

Pressure ilianza kunipanda, nikiwaza kuipoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho na damu tena kwenye mazingira yasiyo rafiki. Lakini upande mwingine bado nilijipa matumaini kuwa muda ulikuwa unatosha kwa Chelsea kufanya yake. Dakika zilisogea si kidogo mara dakika ya 80. Nilikuwa kama nasikia shoti zikitokea kwenye mwili wangu.

Dakika ya 89 bado 1:1, kama nataka kuzimia, nilikuwa nikisubiri maajabu ya mtaalamu wa soka wa darajani enzi hizo Eden Hazard lakini wapi. Mara za nyongeza tatu, nilitamani nitoke kwenye kibanda umiza, nilihisi kila aliyekuwepo mule ndani alielewa kuwa sekunde kadhaa mbele naenda kupoteza milioni tatu. Ilikuwa saa sita na dakika nne mpira ulimalizika kwa sare ya 1:1. Nilikuwa nimepoteza shilingi za kitanzania milioni tatu.

Nilijilaani nikajichukia, niliwaza pesa niliyoitafuta kwa zaidi ya miaka miwili leo inakuja kupotea ndani ya usiku mmoja, jinsi ambavyo nimekuwa saa ingine silali nikipambana usiku na mchana kuzitafuta dolali leo nazitoa sadaka kwa wazungu? Astagafuluhilahh!!!! Nilijichukia sana.

Nilienda kulala usingizi haukuja, nilikuwa nimebakiwa na laki tano kwenye account ya mpesa. Nikapata wazo! Yes wazo. Niangalie timu zilizo live nicheze tatu kwa stake ya laki tano, nilijifariji kuwa kama tayari nimeshapoteza milioni tatu iweje laki tano iniume, potelea mbali, lakini pia kama ntakula nitakuwa nimeiokoa milioni tatu yangu na nitaacha kubeti. Laki tano nayo ikaenda kwa hewani kusubiria hukumu, baada ya saa moja majibu yalikuwa yametoka mkeka ulikuwa umechanika, awamu hii sikuona jipya kwani tayari nilikuwa na ganzi nzito ya kibano cha kwanza.

Ikuwa imeshatimu saa Tisa, mpaka na dakika arobaini ndipo usingizi ulinichota, nilikuwa naweweseka na kushituka. Hata ilipofika asubuhi sikuamini nikijitahidi kuhakikisha kama siko usingizini naota, lakini wapi!

Nitarudi kumalizia
Hahaaa stori za watu wa kubet huwa zinafanana.

Yaani ukipigwa hela unaona kama umeonewa hivyo unatafuta namna ya kuirudisha. Mimi nimepigwa kama 350k ndani ya miezi hii miwili. Sijui nairudishaje. Hapa nipo napanga majeshi
 
Aisee unabet hadi million 3??, hii addiction siyo 🙄🙄

Pole sana mkuu
Kuna watu wana pesa za mchezo aisee... Hiyo si unapandisha kabisa nyumba kwenye kale kaeneo kako? Matofali 2000 hapo na ujenzi juu unaanza.😂😂

Ila dhahabu ili ipendeze haina budi kupita kwenye moto mkali. Kwenye utafutaji tunapitia mengi sana.
 
Pope sana mkuu, katika siku pia watu hawatoisahau ni siku ile sio msimu huu ulioisha... Hapana ule mwingine Man city yuko form lalipigwaga tena na Lyon hatua ya makundi. Kuna mtu alipoteza zaidi ya milion.
 
Kuna watu wana pesa za mchezo aisee... Hiyo si unapandisha kabisa nyumba kwenye kale kaeneo kako? Matofali 2000 hapo na ujenzi juu unaanza.😂😂

Ila dhahabu ili ipendeze haina budi kupita kwenye moto mkali. Kwenye utafutaji tunapitia mengi sana.
Kwakweli 😀 na si kwa ubahili huu, kuliko kumpa mhindi ningekua nishafungua lile banda langu la chips. Ila si mbaya atakua makini sasa💪
 
Mimi niliwahi kuwa ninabet basket nikawa ninakula sana halafu mimi nilikuwa sibet chini ya 20k mpaka 200000 kwa mechimoja au mbili nikawa ninakula sana yani halfu nilikuwa nabet quater to quater yani mpaka mechi inaishanimeshakula sana.

Nikaamua kutenga pesa kabisa ikawa nimeweka milion kwenye betpawa,kila nikila natoaianabaki milioni.

Kuna siku bwana nikatupia mkeka wa laki nani ukaliwa first quater, ikawa imebak kama lak mbili na ushee, nikataka irudisha hiyo ela yangu nikahamisha ela toka akaunti nikaongeza nikatupia mwingine ukachanika.

Nikaongeza tena ukachanika ilikuwa mwaka jana mwezi wa 11 nadhani.

Toka siku hiyo niliapa sitobet tena na sijawahi kubet mpaka sasa. Asante Mungu nimeondokana na kubet kwakweli. Ile ela iliniuma sana sana nikawaza bora hata ningeenda mnunulia maza flani anaishi mtaani earing aid.

Halafu ukiliwa pesa nyingi ukataka kurudisha lazima upigwe tena.
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom