Mikutano ya teuzi za CHADEMA kwa ajili ya uchaguzi 2020 kutokuwa live kwenye mainstream media: je, chama kiliomba na kukataliwa au hakikuomba kabisa?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Unajua siye wengine hapa ni CCM.
Lakini tangu misingi ya chama ianze kukiukwa baada ya Mwalimu JKN kuondoka (RIP mzee), sisi wana CCM asilia tumejikuta njia panda na imefikia mahala tumejikuta tunatamani chama chetu kiwekwe benchi na upinzani ili kiamke usingizini.

Ndiyo maana mnatusoma mara kadhaa humu jukwaani tuki sympathize na kambi ya upinzani, hususani chini ya awamu hii ya 5 ambapo tumeshuhudia katiba ikisiginwa wazi wazi na haki za binadamu zikikandamizwa.

Lakini nimejiuliza kuhusu mikutano 2 mikubwa ya Chadema (Baraza Kuu na Mkutano Mkuu) ikifanyika bila live media coverage. Wakati huo huo naona kesho mkutano wa ACT utakuwa na live coverage ya TV (ITV).

Ndiposa najikuta najiuliza mwenyewe.... Chadema wamekwama wapi kufanikisha hili ambalo wenzao ACT wameweza kufanikisha? Chadema waliomba wakakataliwa au hawakuomba kabisa? Kama walikataliwa ni kwa nini?
Na kama hawakuomba ni kwa nini?

These pertinent questions ni kwa nia njema kabisa ya kuondoa mzizi wa tatizo tunapoelekea October kwani hata sisi CCM baadhi yetu tunataka kuona upinzani unashika dola sasa, huku Tundu Lissu akiwa our new head of state.

CHADEMA Chadema Diaspora
 
Huwa vinalipiwa, siyo bure. Tena bei zake ni kubwa kwa saa! CCM iliweza kulipa media zaidi ya tano 24 hours for 4 days. ACT wamemudu kulipia media moja (ITV) kwa saa moja.
Chadema wameshindwa kabisa kwa kwa sababu ya ukapa!
 
Huwa vinalipiwa, siyo bure. Tena bei zake ni kubwa kwa saa! CCM iliweza kulipa media zaidi ya tano 24 hours for 4 days. ACT wamemudu kulipia media moja (ITV) kwa saa moja.
Chadema wameshindwa kabisa kwa kwa sababu ya ukapa!
haya ndiyo majibu ninayohitaji kuyasikia kutoka kwa wadau wa Chadema humu ndani.

CHADEMA Chadema Diaspora
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huwa vinalipiwa, siyo bure. Tena bei zake ni kubwa kwa saa! CCM iliweza kulipa media zaidi ya tano 24 hours for 4 days. ACT wamemudu kulipia media moja (ITV) kwa saa moja.
Chadema wameshindwa kabisa kwa kwa sababu ya ukapa!
Unataka kusema kuwa CHADEMA haina pesa za kulipa Media.
Watu wamekodi ukumbi pale mlimani city how comes washindwe kulipia Media?
Kuna kitu hapo sio bure tusidanganyane.
 
Jibu ndo hilo ACT ni programu ya Chama tawala kupunguza nguvu ya Chadema so wao kuoneshwa live na channel zenu uchwara ni moja ya mipango mikakati ya CCM kuua nguvu ya Chadema
Mbona hatujaona kiongozi yeyote wa CHADEMA kujitokeza kuzungumzia hilo Kama ni kweli walikwenda kwenye Media zote wakakataliwa? CHADEMA wafanyiwe hivo alafu wakae kimya!? mmh subutu labda si CHADEMA hii ninayo ijua mimi.
 
Unataka kusema kuwa CHADEMA haina pesa za kulipa Media.
Watu wamekodi ukumbi pale mlimani city how comes washindwe kulipia Media?
Kuna kitu hapo sio bure tusidanganyane.
Pesa walizokuwa wanakatwa wabunge wao zimeishia kulipia huo ukumbi na kutunisha mifuko ya wakubwa. CCM ina kumbi inazozimiliki yenyewe.
 
Swali muhimu hili Mkuu. Je, kama hawakuomba ni kwa sababu wamepoteza imani na vyombo vya habari husika? Na kama waliomba kwanini walikataliwa?

Chadema waliomba coverage au hawakuomba?
 
Kama ni rahisi means majibu unayo, sasa kwanini unauliza, unataka majibu gani zaidi ya uliyo nayo?
taratibu ndugu, hii game weka mbali na hasira...

swali langu #1:
(a) waliomba?
(b) kwa nini walinyimwa?

swali langu #2:
(a) hawakuomba?
(b) kama hawakuomba, kwa nini?
 
Huu uzi una maswali muhimu yanayohitaji majawabu.

Tafadhali tuwaachie wenye uwezo wa kutoa majawabu ya maswali yaliyoulizwa.
Ili kupata jibu la swali lako ni budi kujiuliza:
√ Kuna vyombo vya habari nchini vinavyomilikiwa na watu binafsi?
√ Je, kuna ushahidi kwamba vyama vya upinzani vilitaka mikutano yao kurushwa mubhashara, vikawa tayari kulipia, vikamyimwa nafasi?
 
Back
Top Bottom