Mikutano ya Chongolo kutetea mkataba wa bandari kiini macho

saidoo25

JF-Expert Member
Jul 4, 2022
602
1,407
Mikutano ya Katibu Mkuu wa Ccm anayoifanya kikanda ni kiini macho kumdanganya Rais aone kwamba mikutano ya CCM inapata watu wengi na kwamba wana ccm wote wanaunga mkono mkataba wa bandari jambo ambalo ni kiini macho.

Mikutano ya Chongolo mfano uliofanyika Singida unachukua viongozi wa CCM ngazi ya Kata kutoka Kata zote za mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Tabora wote wanakutana sehemu moja Singida na wanachama hao wanasafirishwa kutoka kwenye kila kata za mikoa mitatu ndiyo maana sisi tulioko nje ya nchi tunaona ni mikutano mikubwa.

Lakini viongozi hao kuna tetesi kuwa wanalipwa posho ya sh kati ya 30,000 na 50,000 kwa ajili ya chakula na malazi ili kufanikisha kampeni ya Chongolo ya kujaza mikutano kwa lengo la kumfurahisha Rais aone kumbe jambo hilo linaungwa mkono na watu wengi.

Viongozi hao Kata wahoji siku zote hawana mishahara wala posho wanajiuliza fedha anazotumia chongolo kusafirisha watu kutoka kila kata za mikoa mitatu anazitoa wapi? Kama CCM ina fedha ya kuwasafirisha wanachama kutoka kila kata je kwanini hawana fedha za kuwalipa mishahara?

Sasa kwa utaratibu huu wa Chongolo mikutano itaacha kujaa kama wanakuja watu kutoka kila kata kwa mikoa mitatu hadi minne kutegemeana na kanda husika.

Mfano Kanda ya Ziwa ina mikoa sita Mara, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita na Kagera wakija viongozi wa CCM kutoka kila kata wakutane Mwanza Furahisha ni lazima mkutano huo ujae.

Naomba fuatilieni kwa kina tujue anayefadhili mikutano hii Chongolo aseme fedha ametoa wapi?
 
Mikutano ya Katibu Mkuu wa Ccm anayoifanya kikanda ni kiini macho kumdanganya Rais aone kwamba mikutano ya CCM inapata watu wengi na kwamba wana ccm wote wanaunga mkono mkataba wa bandari jambo ambalo ni kiini macho...
Mbona hilo ni la kawaida sana kwa mikutano mingi ya CCM, wanatumia mda huo kuwapa viongozi wa chama maelekezo zaidi na nini la kufanya.
 
Ule Mkataba hauna shida acha waarabu wapewe nao wale Nchi wewe hushangai ziwa Victoria lipo mwanza na bado kuna mgao wa maji? Misri ipo jangwani lakini hakuna mgao wanao kataa mkataba hawaoni mbali
 
5.0. Maoni na Ushauri

Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneomachache yafuatayo:-19a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (EarlyProject Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwaMkataba.

Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bungekuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwamabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa nikufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingirana kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence),kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.

Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli zaMradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini nakwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifajuu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRALArbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 chaSheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali naMaliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources[Permanent Sovereignty] Act, 2017).

Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana namatumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katikamahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vyasheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwaSerikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba(denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha(terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja namazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material20breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba(fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wakidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabauzozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.

Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 231) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli zamradi huu zitakapokuwa zimekamilika.

Serikali iombwe kutoa ufafanuzikuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huuutaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingiaau kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifawakati wa utekelezaji wa Mkataba.

Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujawekamuda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingiamakubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendeshabandari zake.f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakikawa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuziwa Serikali.

Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo.Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulinganana wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti yaMkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka yakusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusainiMkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai.Tunaomba kuwasilisha.

Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge
 
Hii hatari sana sasa hivi hawezi kusafiri kwenda ng’ambo kiti hicho kinatafutwa walati wowote lazima atume balozi ng’ambo. Mtaelewa tu
 
Kwanini kila kiongozi anataka kumhadaa Mh. Rais kuna siri gani hapa, kama ni kweli watu wanasombwa kutoka kila kata za mikoa 3 kuja kwenye mkutano wa Chongolo ili apate picha za watu wengi amtumie Mh Rais kwamba wananchi wameelewa na wanakubali uwekezaji wa DP World. Huu unafiki na uongo siku sio nyingi Mh. Rais atajua watu alionao ni wa aina gani
 
Mikutano ya Katibu Mkuu wa Ccm anayoifanya kikanda ni kiini macho kumdanganya Rais aone kwamba mikutano ya CCM inapata watu wengi na kwamba wana ccm wote wanaunga mkono mkataba wa bandari jambo ambalo ni kiini macho.

Mikutano ya Chongolo mfano uliofanyika Singida unachukua viongozi wa CCM ngazi ya Kata kutoka Kata zote za mikoa mitatu ya Dodoma, Singida na Tabora wote wanakutana sehemu moja Singida na wanachama hao wanasafirishwa kutoka kwenye kila kata za mikoa mitatu ndiyo maana sisi tulioko nje ya nchi tunaona ni mikutano mikubwa.

Lakini viongozi hao kuna tetesi kuwa wanalipwa posho ya sh kati ya 30,000 na 50,000 kwa ajili ya chakula na malazi ili kufanikisha kampeni ya Chongolo ya kujaza mikutano kwa lengo la kumfurahisha Rais aone kumbe jambo hilo linaungwa mkono na watu wengi.

Viongozi hao Kata wahoji siku zote hawana mishahara wala posho wanajiuliza fedha anazotumia chongolo kusafirisha watu kutoka kila kata za mikoa mitatu anazitoa wapi? Kama CCM ina fedha ya kuwasafirisha wanachama kutoka kila kata je kwanini hawana fedha za kuwalipa mishahara?

Sasa kwa utaratibu huu wa Chongolo mikutano itaacha kujaa kama wanakuja watu kutoka kila kata kwa mikoa mitatu hadi minne kutegemeana na kanda husika.

Mfano Kanda ya Ziwa ina mikoa sita Mara, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita na Kagera wakija viongozi wa CCM kutoka kila kata wakutane Mwanza Furahisha ni lazima mkutano huo ujae.

Naomba fuatilieni kwa kina tujue anayefadhili mikutano hii Chongolo aseme fedha ametoa wapi?
 
Attachments

  • CD94F016-6B49-44B0-AAD8-81E53C004B85.jpeg
    CD94F016-6B49-44B0-AAD8-81E53C004B85.jpeg
    47.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom