Kijana Mzalendo amtuhumu Chongolo kuwa chawa wa DP World

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Kijana Mzalendo Nkindikwa David amemvaa Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo kushabikia Mkataba wa Bandari licha ya kupingwa kila kona ya nchi.

Niwaombe watanzania tuendelee kushikamana kutetea rasilimali zetu na kamwe tusikubali kugawanyishwa na mtu au kikundi cha watu kwa misingi ya dini, itikadi za Siasa, jinsia, makabila wala ubara na uzanzibari bali tusimame imara kupinga vipengele vya mkataba huu ili taifa liweze kunufaika na mali asili zake ilizojaliwa na Mwenyezi Mungu.

Hata ziara zinazofanywa nchi nzima na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Daniel Chongolo na makada wengine wa CCM na baadhi ya Viongozi wa Serikali kupigia upatu mkataba huu unaolaaniwa na kila mtanzania zimeacha maswali mengi sana kwa watanzania.

Leo hii nchi inashuhudia kilio kikubwa cha uhaba wa nishati ya mafuta na kupanda bei ya nishati hiyo ambapo ndani ya kipindi kifupi cha kutoka Juni bei ya nishati ya mafuta imeongezeka kwa zaidi ya shilingi 400 kwa lita na maeneo mengine lita moja inauzwa zaidi ya shilingi 5,000 ambapo imepelekea bidhaa zote kupanda bei, gharama za usafiri na usafishaji kuongezeka na kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania masikini.

Dola za Marekani zimeadimika na kupelekea biashara za kudorora kwa biashara za kimataifa, kushuka kwa thamani ya Tanzania shilingi, bei za bidhaa kuongezeka, Serikali kushindwa kukusanya kodi, Deni la Taifa kuongeka mara dufu na maisha ya watanzania kuwa magumu kupitiliza.

Upande wa huduma ya nishati umeme wananchi wametengezewa mgao feki wa umeme ambao hauna Maelezo yoyote, umeme unakatika kila wakati na kuathiri uzalishaji na kupelekea upungufu wa bidhaa, biashara
kufa, kufilisika na bidhaa kupanda bei.

Matatizo ya Umeme, Dola na nishati ya mafuta yanaendelea kuwatafuna watanzania bila msaada wowote wa Chama cha Mapinduzi, hatujawahi kuona Katibu Mkuu wa CCM akizunguka nchi nzima kupinga masuala
hayo, kukataa dhuluma hizi na kuwawajibisha wahusika ambao wote ni Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

leo hii Katibu Mkuu wa CCM anazunguka nchi nzima na kutumia gharama kubwa kukusanya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini na kukutana sehemu moja kupigia debe mkataba mbovu wa Bandari, Kazi ya kupigia debe mkataba wa Serikali sio kazi ya Chama lakini Katibu Mkuu Chongolo ameamua kuacha majukumu ya Chama ya kuisimamia Serikali na kuwa CHAWA wa Kampuni DP World.

Lakini hata maandiko matakatifu katika Biblia yanasema, Ukisoma Isaya 29:13 inasema Bwana akanena, kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao bali mioyo yao wamefarakana nami, na
kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu walivyofundishwa.

Lakini pia ukisoma Mathayo 15:7-9 inasema Enyi Wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu akisema, watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.
 
Chogolo hawezi kuusoma ule mkataba.
Lugha ya Malkia kwake ni ndoto

 
Kijana Mzalendo Nkindikwa David amemvaa Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo kushabikia Mkataba wa Bandari licha ya kupingwa kila kona ya nchi...
Wamehongwa hao na DPWorld. Inadaiwa wamepewa za kujiandaa uchaguzi mwaka ujao na ahadi kuongezewa dili likikamilika
 
Back
Top Bottom