mzee wa nguna
Senior Member
- Dec 5, 2012
- 132
- 113
Nimefuatilia matokeo ya walioomba mikopo ya kugharamia masomo ya elimu ya juu tangu walipotoa awamu ya kwanza hadi ya mwisho juzi tarehe 4/11/2021.
Kwanza idadi kubwa ya waombaji wa mikopo hiyo hawakupata. Pili, moja ya kundi kubwa la waombaji ambao hawakupangiwa mikopo kwa sababu mbalimbali ni watoto wenye mmojawapo wa wazazi ambaye ni mtumishi wa umma (mwajiriwa serikalini).
Ukitafakari kwa kina, halafu ufanye rejea ya hali za watumishi wa umma walio wengi katika hii nchi, vipato vyao havikidhi vema maisha yao na pia wana mikopo lukuki kwenye benki mbalimbali.
Sote tutakubaliana kwamba, watumishi wa umma kama ilivyo watanzania wengi, watoto na wategemezi walionao si mmoja au wawili pekee, huenda ni idadi kubwa. Kwa uelewa wangu, hakuna ruzuku yoyote ya ziada ambayo serikali inampa mtumishi wa umma kwa madhumuni ya kusomesha watoto. Aidha kinachotolewa na HELSB ni mkopo wa kuwezesha wasio na uwezo kumudu kusoma elimu ya juu. Inashangaza sana kigezo hiki cha Loan Board kuwaweka kando watumishi wa umma.
Najiuliza watanzania wenzangu, hivi vigezo viliwekwa kumsaidia nani? Na kwanini nchi yetu isiamue kuongeza bajeti ya elimu ili kila muombaji wa mkopo apate?
Chondechonde kama kuna uwezekano wahusika wapitie upya vigezo vyao, tusijikute tumesababisha watoto wa watumishi wa umma wabaki kuishi kwa kuunga-unga huko vyuoni kisa tu mzazi yupo kwenye payroll ya serikali.