Mikopo ya Asimilia 10 za Halmashauri zinatolewa kwa ubaguzi wa Kisiasa katika baadhi ya maeneo ya Dar

Mikopo ya Asimilia 10 za Halmashauri zinatolewa kwa ubaguzi wa Kisiasa katika baadhi ya maeneo ya Dar

Joined
Apr 1, 2017
Posts
16
Reaction score
25
Wakati Serikali ikiahidi kutoa kiasi cha Sh 200 Bilioni, kwa mikopo ya vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu, baadhi ya Vijana na wanawake wamelalamika kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa misingi ya itikadi za vyama huku wafuasi na makada wa CCM, wakiwa kipaumbele kwenye mikopo hiyo.



Mwandishi wa habari hizi amekutana na vijana waliomba mikopo mara kadhaa kwenye Halmashauri ya Ubungo, Ilala na Kinondoni huku wakigonga mwamba.



Vijana hao wamemuelezwa kuwa wenzao wa CCM wanapata mikopo hiyo huku wao ambao sio waumini wa siasa wakiachwa solemba.



Khatibu Amrani mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, anasema kuwa yeye na wenzake waliunda kikundi chao kilichokuwa kina sifa za kukopeshwa kwa kuwa kilishajili na Halmashauri ya Ilala lakini hatimaye walikosa mkopo kwa kuweko kwa masharti lukuki.



Amesema kuwa amepata dhana mbaya dhidi ya nia njema ya serikali ya kuwakomboa wananchi kwenye umasikini kwa kuwa kuna kikundi cha hamasa ya cha aliyekuwa mgombea ubunge wa Ilala kimepata mikopo,



“Sisi tunajuana hapa mtaani kwetu sifa za kikundi chao na chetu zinafanana kwanini wao wapate sisi tukose,” amesema.



Peter Simigo, mkazi wa Kimara amesema hatashawishika tena kuomba ameingia kwenye vikundi kadhaa bila mafanikio.

“Kusema kweli nimeliwa sana pesa zangu naambiwa mchango wa kikundi nikiiamini siku moja nitapata mtaji wa kujiimarisha kiuchumi lakini mara zote kikundi chetu kilivyoomba kimekosa na kipo kikundi cha kwa msuguli pale kimepata mara kadhaa kwa nini tuendelee kumaliza pesa zetu si wasema kama wana watu wanalenga”



Desemba 23, 2025, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Reuben Kwagilwa, akiwa katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo alikutana na malalamiko ya danadana za upatikanaji wa miko ya asilimia 10.


Malalamiko hayo yaliibuliwa na mmoja wa wajumbe wa kikundi cha vijana cha maendeleo walichodai kuwa wanapigwa mikopo ya asilimia 10 kwao ni hadithi.



Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Instagram aliyejitambulisha kwa jina ‘mosozeone’ kuwa ni mkazi wa Halmashauri ya Ubungo alisema kuwa vijana wa katika Halmashauri hiyo sio miongoni mwa wanafaika wa mikopo hiyo.

Anasema “Mimi nahisi hapo Ubungo kuna ujanja-ujanja, wanasajilisha vijana kwenye vikundi lakini wanakuwa hawanufaiki na vikundi vinaishia hewani tu.”



Septemba 18, 2025, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, ilifanya mafunzo maalumu kwa vikundi vilivyoomba mikopo ya asilimia 10 ambavyo vinakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo na kufanya makosa wakati wa uombaji.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Rahma Athumani, amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu, Vijana, na Wanawake wanapata mikopo hiyo.


“Kuna baadhi ya changamoto zinazokabili vikundi katika mchakato huu kama vile maandiko ya miradi yasiyo sahihi, kutumia biashara ya mtu mmoja kama msingi wa kikundi, kukosa leseni, kutokuwa na vitambulisho vya wajasiriamali, pamoja na tofauti kati ya mradi waliouombea mkopo na mradi wanaotekeleza, hivyo tumeona ni bora tuwakusanye wote tuwape elimu kwa pamoja,” alisema Rahma.



https://dcc.go.tz/new/vikundi-vya-mikopo-ya-aslimia-10-vyenye-changamoto-vyapatiwa-mafunzo

Hali hiyo inafanana na Visiga, Kibaha mkoani Pwani waliolalamika kuwa hakuna uwazi kwenye utoaji wa mikopo hiyo kwani wao wakiomba wanaambiwa mikopo hiyo imeshatolewa bila kujua ni kikundi gani vilivyopata hiyo mikopo.



Hoja hiyo iliibuliwa kwenye mkutano wa Hadhara wa Meya wa Manspaa ya Kibaha, Dk, Nicas Mawazo ambaye alisema kuwa kinachokwamisha mikopo hiyo ni kudorora kwa urejeshaji mikopo hiyo.



https://www.mwananchi.co.tz/mw/haba...hauri-yataja-changamoto-ya-urejeshaji-5314870



Januari 27, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alikabidhi Hundi ya thamani ya Sh 7.5 bilioni ikiwa ni fedha ya mikopo inayotokana na 10% ya Mapato ya ndani ya Manispaa inayokwenda kutolewa kwa kundi la Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu.


Pesa hiyo iligaiwa kwa mgawanyo wa asilimia 4 ya wanawake, 4 ya vijana na 2 watu wenye ulemavu, Vikundi 122 vya Wanawake vimepata Tshs 3,006,858,658, Vikundi 95 vya Vijana navyo vikipatiwa Tsh 3006,858,658 na Vikundi 20 vya walemavu vimepata Tsh 1,503,429,329.



https://dsm.go.tz/new/rc-chalamila-akabidhi-hundi-bilioni-75-temeke

Mgawo huu ulimuibua Sauda Amiri Mkazi wa Buza, Tanesco, akisema kuwa yeye na kikundi chake kiliomba na kuona ishara za kibaguzi waziwazi “tukiwa katika harua za mwanzo za kujisajili walitufuata watu wa CCM mtaani kwetu na kutuambia madam uchaguzi mkuu 2025 hakuwa upande wao hiyo mikopo tutaisikia tu.



“Kweli mikopo hatujapewa juzi mkuu wa mkoa umeona amekabidhi hudi ya fedha chungu mzima lakini mimi na vikundu vya wenzetu hatumo tuliambiwa kwamba mchakato huu kama hujuupigania kwa kuvaa sare za kijani ukaingia mtaani ukanadi sera na ukafahamika huwezi kupata sasa yametimia,”alisema Sauda.



Naye Salma Mbwana wa Tandika, alimwambia Mwandishi wa habari hizi kuwa kwa kuwa yeye ni kijana aliyekuwa akikinadi chama cha ACT-Wazalendo anadai kuwa hiyo ndio sababu ya yeye na wenzake kuweka kando.



“Huu mchakato unaanzia ngazi za chini huku tunapojuana itakadi zetu ndio maana unaona sisi ambazo sio CCM tumekosa wale wenzetu wa Kilimahewa wamepata kwa sababu wale wotye ni vijana wa hamasa wa chama tawala itoshe kusema kuwa hatuwezi kupata mikopo hiyo kwa sababu sisi tulikuwa hamasa wa dhambarau,” alisema Salma.



Naye, Njopeka Matimbwa mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally alisema yeye aliambiwa waziwazi kuwa yeye ni kijana wa Chama cha Wananchi (CUF), hivyo mikopo hiyo haimuhusu.



Peter Dismas Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Manzese amesema kuwa mikopo hiyo haijawahi na haitatolewa kwa itikadi za kivyama.

"Hizi Proganda tu sio kweli kwamba mikopo hiyo inatolewa kwa upendeleo nenda kwenye Halmashauri yoyote ambayo ishaanza kutolewa mikopo hiyo kama utaona kuna wanachama wa CCM pekee wanaokopeshwa," amesema Dismas.

Amesisitiza kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi huwaandaa wanachama wao kwa kuwaambia wachangamkie fursa za mikopo.



Hata hivyo Serikali tarehe 29 Januari 2026 imetoa masharti mapya ya mikopo ya asilimia 10 ikiwemo ulazima wa wakopaji kuwa na kitambulisho cha taifa (NIDA), mjadala huo umeibuka bungeni wakati Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba akijibu maswali ya wabunge ya papo kwa papo ambapo Mbunge wa Segerea (CHAUMMA), Agnesta Kaiza, aliuliza kuhusu namna serikali inaweza kulegeza masharti ya mikopo hiyo.




Amesema hivi karibuni alikutana na wafanyabiashara ndogondogo, machinga na mama lishe, ambao moja ya mambo waliyozungumzia ni mikopo ya asilimia 10 na masharti yake.



Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, ni lazima mikopo hiyo iende kwenye uhalisia, kwani machinga hawezi kuwa na hati ya nyumba wala kuwa na udhamini wa mtumishi wa Serikali.



“Maelekezo ya Serikali ni kulegeza masharti ya hati ya nyumba, barua za udhamini na vigezo vingine. Wenzetu wa benki walikuwepo, na niliwaambia utaratibu uwe ni kuwapambanua ili wanufaika wawe Watanzania kweli na wawe na Kitambulisho cha Taifa (Nida). Kwa ambaye hatakuwa na kitambulisho hicho, anatakiwa kuchunguzwa na kuombwa vielelezo zaidi,” aliesema.



Baada ya majibu hayo ya Dk Mwigulu, Spika wa Bunge, Mussa Zungu, aliweka msisitizo kwa wakurugenzi wa halmashauri kusimamia maelekezo ya Waziri Mkuu, akisema zipo biashara ambazo hazihitaji kuwepo kwa ofisi wala vitu vingine zaidi ya uaminifu, akitoa mfano wa biashara za mitandaoni.




Septemba 28, 2025 akizungumza kwa njia ya mtandao, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole alikosoa ahadi iliyotolewa na Rais Samia kuwa akichaguliwa tena ndani ya siku 100 atatoa Sh. 200 bilioni kwa ajili ya uwezeshaji wa uchumi kwa wajasiriamali na wale wenye biashara changa.



“Ahadi hiyo ni hadaa kwa wananchi, CCM kimeshindwa kuzitumia Sh.577.4 bilioni za miaka mitano mfululizo zilizotengwa kuwainua Watanzania kiuchumi na badala yake fedha hizo zimeliwa. Sasa leo hii wanakuja na hadithi nyingine,” alisema



Mwanadiplomasia huyo alisema kuwa kama CCM kingekuwa kina nia njema kingeeleza utaratibu, malengo, matokeo na namna ya kutekeleza uwezeshaji huo.



“Chama na viongozi wake wamesema watatoa Sh. 200 bilioni ndani ya siku 100 kuwawezesha wananchi kiuchumi, hoja sio hela hoja ni muundo, mfumo, utaratibu, malengo, matokeo na namna ya kutekeleza jambo hilo la kuwawezesha wananchi kiuchumi, hayo niliyoyasema yote hayajafanyiwa kazi,”alisema Polepole.



Alisema kuwa serikali kutoka mwaka 2021 mpaka 2025 ingekuwa na kiasi cha 577.4 cha makusanyo ya asilimia 10 za halmashauri zote nchini.



“Tuliwahi kuona hizi sh.577.4, zimewekewa malengo mahususi , matokeo, shabaha kisha ziwekewe utaratibu wa namna ya kuzitoa kwa wajasiriamali na hawa wajasiriamali sio wa kuokoteza wale wanaofahamika wenye biashara ndogo na za kati na tunawatazama vijana, wanawake na walemavu nawahakikishia hii tungekula maziwa na asali,”





“Unaposema unakuja kutoa bilioni 200 katika msingi upi mbona hawafafanuzi msihadaike sasa nitakupeni mfano , nchi hii hela sio tatizo hela ipo tatizo wanakula, nitawaonesheni hela walizokula ndani ya kipindi hiki Rais Samia ameongoza , na namna ambavyo hazisaidii watu masikini.



Ukienda ukurasa 197 wa hotoba aliyoitoa Waziri wa Fedha , Mwigulu Nchemba bajeti kuu ya serikali yam waka wa fedha 2025/2026.



“Wameeeleza kwa wastani makusanyo ya ndani yay a halmashauri (OSR), kwa miaka mitano kibajeti kwa mujibu wa sheria makusanyo ya halmashauri ya ndani asilimia 10 yanatakiwa yakatwe itolewe mikopo kwa vijana wanawake na kwa watu wenye ulemavu nitakupa takwimu ili uelewe Bilioni 200 ni danganya toto.



“Mwaka 2021/2022 mwaka wa bajeti ya kiserikali makusanyo ya Halmashauri asilimia 10 yake ilikuwa Sh. 88.9 bilioni mwaka 2022/2023 makusanyo hayo ya jumla yalikuwa sh. 102.1 bilioni Mwaka 2023/2024 makusanyo hayo yalikuwa sh. 114.7 bilioni,”



“Mwaka 2024/2025 makusanyo hayo ya asilimia 10 yalikuwa Sh135.6 bilioni na mwaka huu tumepanga kukusanya hii ndio ipo kwenye bajeti ni Sh 136.06 hii ni miaka mitano ya mama Samia ukijumlisha hizo hela zote utapata sh.577.4 bilioni kwa miaka mitano”



Polepole alisemwa kuwa kiasi cha Sh 577.4 bilioni, zingewekewa malengo mahususi , matokeo, shabaha kisha ziwekewe utaratibu wa namna ya kuzitoa kwa wajasiriamali wenye biashara ndogo na za kati na tunawatazama vijana, wanawake na walemavu “nawahakikishia hii tungekula maziwa na asali”.




Akizungumza katika ziara yake mkoani Songwe, Waziri wa Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka, alisema ziara hiyo imelenga kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi, hususan vijana wa mkoa huo.

Daudi Simwinga aliibuka Waziri kuongeza mgao wa mikopo ya Halmashauri kwa vijana akisema: “Vijana tumeguswa kwa asilimia nne, lakini asilimia hiyo haiendani na idadi ya vijana wasio na ajira. Tunapendekeza kutoka asilimia kumi za mapato ya Halmashauri, basi vijana tuongezewe mpaka asilimia 10 au 15.”

Kwa upande wake, Waziri Nanauka ameeleza kuwa ongezeko la fedha zinazotolewa na Serikali kupitia mikopo na mitaji litasaidia kufidia maeneo ambayo vijana wamekuwa wakikosa mitaji.

“Inawezekana kutokana na wingi wa mahitaji fedha zilizopo bado hazitoshi. Ndiyo maana Mh. Rais ameahidi kuachilia Bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake,” alisema Nanauka huku akiwataka viongozi wa Halmashauri kote nchini kuwasaidia vijana ambao hawajakidhi vigezo ili waweze kupata mikopo hiyo kwa ufanisi.

Katika hatua nyingine, Wizara imekusudia kuanzisha mfumo maalum wa kiteknolojia utakaowawezesha vijana wote nchini kuwasilisha maoni na changamoto zao moja kwa moja, ambapo watumishi wa Wizara pamoja na Waziri watazipitia taarifa hizo na kutoa majibu au ufumbuzi stahiki.
 
Pole nje ya mada.

Hivi kwa nini hii mikopo waseme ni kwa ajiri ya VIJANA, WANAWAKE NA WALEMAVU?

Ni kama vile kuna kundi limetengwa ila pia kuna kundi limependelewa mara mbili.

Ukisema VIJANA, automatically ni wa kike kwa kiume.

Kama jibu ni ndio, maana yake hili kundi la WANAWAKE ni kina mama wenye umri mkubwa.

Kama ni ndio, kwa nini kundi la WANAUME hatukupewa nafasi katika mikopo hii?

Au kumaanisha kundi la WANAUME woote wamejipata? Wao hawahitaji mkopo?

Huu ni zaidi ya ubaguzi, huu ni unyanyasaji wa kijinsia, kwa sababu, kama ni majukumu mie naona wanaume ndio wana majukumu makubwa.

Hao unaosema vijana, na wanawake, bado pia wanahitaji pesa ya baba(matumizi)kuendesha maisha ya kila siku, baba anapata wapi pesa wakati hata humuwezeshi, unaenda kuwawezesha watu ambao wanamtegemea.

Wanaume kwa pamoja tushtuke mapema, huko mbeleni tunakoenda sio poa kwa kisingizio cha kumuwezesha mwanamke.

Hii mibunge nayo ikienda bungeni ni kupiga meza na kusifia wakati wanaume wenzenu wanabanwa mbavu.

Ukiwa kijana wanakuweka kwenye list ili usiwe violent ukawasumbua kwa kisingizio cha kukosa ajira, lakini ukishaufikia ubaba unakutana na spana kama kawaida, vijana msiwe wajinga.
 
Back
Top Bottom