kalooo 25594
JF-Expert Member
- Jun 14, 2016
- 300
- 194
- Thread starter
- #101
95%%%Huu uzi Ni mzuri kuliko ule wa rikiboi una nondo zote ambazo hazifundishwi ofisini muajiriwa mpya anapaswa ajue
Sent using Jamii Forums mobile app
95%%%Huu uzi Ni mzuri kuliko ule wa rikiboi una nondo zote ambazo hazifundishwi ofisini muajiriwa mpya anapaswa ajue
Mh?Nanda crdb processing fee na insurance ni ndogo ukilinganisha na NMB, pia riba ya crdb inapungua kadri deni linavyopungua tofauti na NMB
Mwisho wa bandiko ndio ulikua Target yako,nahisi unapiga kazi nmb
OkNanda crdb processing fee na insurance ni ndogo ukilinganisha na NMB, pia riba ya crdb inapungua kadri deni linavyopungua tofauti na NMB
Wasipoelewa hapa hawatokuja elewa tena.Wacha nikupe Experience yangu as Credit officer
Sheria inasema apply 1/3 katik mshahara wa mtumishi hii imekuja baada ya watumishi mwanzo walikua wanakopa sana kupindukia mpk kufanya washindwe timiza wajibu wao mtu anakop abaki na kitu mpk nauli ya kwenda kazini hana ivyo serikali ikapitisha sheria hii.
525,000/3=175,000
Take home -1/3 Answer
441,000-175,000=266,000
Inamaana mkopo unaoweza kupata bank yoyote inabidi uwe na Makato ya sh 266,000 kushuka chini.
Ukichukua mkopo wa makato ayo inamaana mshahara utakao kua unachukua baada ya makato ya bank ni 175,000 kila mwezi mpk mkopo utakapo isha inategemea na muda wa mkopo labda miezi 6,12,24,36,48,60,72 au 84.
Swali linakuja utaweza ishi kwa iyo pesa 175k kila mwezi kukushi gharama za maisha au tu assume umekubali wakati 260k means 6000 itabaki je unaweza ishi kwa 200k kila mwezi kukidhi maisha yako? Kula, kuvaa, Nauli ya kwenda kituo cha kazi, kodi kulipa na Maji, mzazi akiwa na shida kidogo utaweza msaidia?
USHAURI
1.Kama unataka kukopa nakushauri ufikilio ilo la juu nlilo kuuliza ukipata majibu naomba uchukue mkopo mfupi wa miaka 3-4 alafu makato atleast usizidishe 120k komea apo uone unapata kiasi gani
Muulize afisa mikopo kwa kato la 120k miaka 3 (miezi 36) unapata kiasi gani na miaka 4 (miezi 48) unapata kiasi gani.
2.Taasisi ya kukopa, hapa zipo taasisi nyingi sana zenye riba kubwa na ndogo mfano uliwai jiuliza TPA, TRA kwanini hawakopi kwenye mabank husika ? Jibu ni kua wana SACCOS zao zinazotoza riba Nafuu sana mfano TRA SACCOS wana liba ya 11% kwa mwaka ndio maana hauwezi kuwaona wanaenda kukopa kwenye mabank yenye riba za 15%-20%.
Nakushauri ukitaka kopa fanya reserch ya bank kama tano kulinganisha unafuu wa riba kwakua riba zinatofautiana na kwa maana iyo ina maana kato la 120k kwa muda labda wa miezi 36 mfano NMB na CRDB utapata pesa tofauti sana kwakua
Riba zao ziko tofauti.
Ila hapa naomba nkushauri kama unataka mkopo katika sehemu uliyopo watafute BOA bank kwa sasa ni best of all kwani wao wana riba ya 9% uku Bank nyingine mfano CRDB,Akiba, Access,NMB etc wana 16%, 17%, 18%,20% nk
Usikope katika SACCOS za walimu, Taasisi ndogo ndogo za fedha kama Bayport, Tunakopesha limited, Platinum Credit limited, Fanikiwa,Faidika,Maboto,Banc ABC.
Hizi taasisi zitakupelekea ujute kukopa katika maisha yako wana riba kubwa sana mfano kuna taasisi apo zina riba ya 36%,45%,48% na nyingine 50% sijataka kuzisema kua riba hii ni ya taasisi fulani kuepuka sema nawaharibia biashara na kwa kato ilo la 120k ukienda kwao unaweza ambiwa unapata 2-3M kwa miezi ata 48 uku ukienda Bank kwa kato ilo miezi 48 unaweza pata 6-9M.
Taasisi hizi huwa na tabia ya kuja ofisini kwa mtumishi wanafanya presentation kwa ahadi ya kupata mkopo kwa masaa 24.
3. Mahesabu ya Riba au Rejesho utakalo kua unadaiwa.
Kutaka kujua Rejesho lako kwa taasisi husika tunafanya ivi
Mfano: Nitakatwa 120k kila mwezi kwa muda wa miezi 48 inamaana apo kiwango unachobidi urejeshe ni,
120,000*48= 5,760,000
Unaangalia mkopo ulio chukua mfano 4,900,000
Hivyo 5,760,000-4,900,000=860,000
Hii 860,000 ndio riba ya mkopo wako kwa muda wote.
4. Usikope pesa nyingi kuanzisha biashara tunashauri watu wakope kuendeleza biashara na si kuanza biashara kwa nini?
Kuendeleza biashara ni rahisi kwakua changamoto za biashara yako unazijua vizuri ila kuanza biashara haujui soko lako uhimala wake mfano ukikopa pesa na yote uweke kwenye mzunguko na biashara ikaenda vibaya, mzigo ukiharibika, mzigo ukiibiwa au wanunuzi wakikosekana kulingana na hali iliyopo mfano kipindi hiki cha ugonjwa wa dunia unafikili wangapi wanafikilia kujenga ilihali hawaijui kesho vyakula vikipanda bei au wakitangaza lockdown hakuna kwenda makazini biashara yako itakua mahala pabaya kwakua hakuna wa kununua bidhaa yako ya cement kujenga watu watakua wana spend kwenye kula na kunywa sana.
Hivyo ukikopa mfano 6M weka 3M yaani nusu ya pesa ubaki na balance ya 3M uku ukisoma biashara taratibu sana hii ni kwa biashara inayo anza kuishi maisha ya msoto kwa mshahara nusu wa 200k mpk 250k kila mwezi sio kitu kidogo na hii ni life process itakayokuchukua miaka 3-4
NB Tafuta kuna uzi hunu ndani unaoeleza jinsi watu mikopo ilivyo wafilisi na kuwarudisha nyuma kimaisha usikimbilie mkopo kama hauna elimu ya mkopo na kama hauna uhitaji usifanye jambo kwakua umeambiwa ni fursa chukua muda kudadavua vuzuri utakuja juta kama hauna plan b na ata kituo cha kazi unaweza kukiona kichungu ukakimbia kazi yenyewe kisa Madeni mengi.
Nina cases za walimu wengi walio kopa mikopo mambo yakaenda ndivyo sivyo na Mikopo iko kama Mashetani ukianza kopa hautokuja acha kamwe maishani utakopa mpaka unajikutaumekua mzoefu yani Salary slip unakuta makato taasisi kama 5 ivi bado wale wa Cash unakuta mtu anapokea mpk elfu 80k kwa mwezi kutoka laki 480k uko alafu anamadeni mtaani anabaki na 50K apo anaon bora ajichanganye kuwa boda boda tu.
Mfano kuna jamaa nliwai mkopesha pesa anapokea 75k alafu ni muhasibu wa Mahakama asee mpk nlikua nashangaa uyu jamaa anaishi vipi na apo ana mke na mtoto mchanga afu jamaa alikua anapiga maji sana aya maish ni full stress tu
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hz fursa anazoziona leo wapo watu waliziona miaka 10 nyuma... kiufupi hata baada ya miaka 5 bado kuna fursa zingine zitahitaji kiasi hiki hiki cha pesa...Kwa haraka haraka inaweza kuonekana ni wazo zuri lakini sio rafiki.
Kuna kitu kinaitwa thamani ya pesa lazima ukizingatie. Pia inategemea unataka kufanya jambo gani na huo mkopo. 10M ya leo inaweza kufanya mambo mengi tofauti na 10 M hiyo hiyo miaka mitano au kumi ijayo.
Kwa mantiki hiyo, bora uchukue hiyo pesa uwekeze sasa ikiwa fursa zipo kuliko kusubiria miaka mitano ijayo.
Hz fursa anazoziona leo wapo watu waliziona miaka 10 nyuma... kiufupi hata baada ya miaka 5 bado kuna fursa zingine zitahitaji kiasi hiki hiki cha pesa...