Wanao kanusha habari za uchawi Sumbawanga acha wakanudhe, maana lipo linalowahusu. Juzi tu nadhani kati ya mwezi wa tatu ama wa nne, afisa mtendaji alilazwa nje ya nyumba yake, yeye na familia yake yote, mbaya zaidi wote wako uchi wa mnyama, wameamka asbuhi wako nje uchi Baba, mama na watoto wa kike na kiume, halafu mnakanusha vitu ambavyo vipo. Hii nilisikia mwenyewe jamaa akiripoti kupitia radio free. Miaka nyuma nilisoma habari gazeti la mfanyakazi wakati huo, huko Sumbawanga kijana mmoja aliekua anamfukuza ng'ombe aliekua anakula mazao yaliyopandwa karibu na nyumba yao. Kitendo cha kumchapa fimbo yule ng'ombe, ile fimbo iliwaka moto pale pale. Na yeye akanza kuota mvi siku ile ile, na akawa mzee siku ile ile, mpaka akazeeka kiasi cha kuwa babu hasa siku ile ile. Na hatimae kuumwa na kufari siku ile ile. Na kisa kingine nitakiweka baadae jioni, ni visa vya kweli ambavyo huwezi vipata kwingine Tanzania ispokua Sumbawanga.