Mikoa wa Katavi na Rukwa ni kiboko

Haya mambo ni dhahania tupu!!,Hakuna ukweli wowote,mimi nimeolea huko na huwa ninakwenda kila mwaka,wala sijawahi kutana na mambo unayoyasimulia;Kuhusu magonjwa ya ajabu ndugu yangu ni kwamba "Kabla hujafa,hujaumbika",Duniani uwanja wa Shida,kuna magonjwa ya kutisha kuliko hata hayo ambayo wewe unastaajabia na kuona kwamba kweli yanahusiana kwa karibu na ushirikina,sivyo,hamna kitu km hicho.AFRIKA LINI TUTAACHANA NA UPUUZI HUU WA KUUPA HESHIMA YA JUU USHIRIKINA KULIKO MUUMBA WETU???.

Kwani ni nani aliyeupa heshima ishirikina na ni kitabu gani cha dini hakitambui uwepo wa ushirikina?Kama unaamini Mungu kwa nini usiamini uwepo wa ushirikina?Na ni Mungu yupi unayemwamini wewe asiyeitambua ushirikina?Anza torati mpaka ufunuo kisha nipe andiko linalokanusha uwepo wa ushirikina.
 
198bc73a1048677d76cd8e2c180ac259.jpg

Kikao cha mababu, mabibi na machief huko Sumba-wanga....ni hatari tupu
 
Kule Nkasi Sumbawanga kata ya Kipili hii kata ipo karibu na ziwa Tanganyika kuna Mzee mmoja aliuza kiwanja kwa Kijana fulani baadae yule Kijana akataka aanze ujenzi kwa kununua tofali. Kijana akamfuata mwenyeji wake yule Mzee kumuuliza kuhusu usafirshaji wa hizo tofali Mzee akamwambia Kijana tukubalie bei halafu wewe nenda zako utakuta Tofali zako zote hapa kiwanjani kwako wakati wanakubaliana hayo ilikuwa in saa12 jioni. Kesho yake asubuhi saa1 Kijana akarudi kwa Mzee kumpa hela ya usafirishaji kwenda anashangaa kukuta Tofali zote zipo pale kiwanjani. Kubwa zaidi lililomshtua ni kusikia wanakijiji wakilalamika kuwa usiku hawakulala na wote wameamka na Vumbi la Mchanga wa tofali kuanzia wanaume mpaka wakina mama kwa maana hiyo Mzee alibebesha kijiji kizima Tofali.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
hata bure siendi huko nitaendelea kuishia tunduma tu.........
 
Hahahahaaa kipili noma.. Nimecheka sana..nikakumbuka watafiti wa UDSM walipoenda kufanya research ya maji Nkasi ile wamefika kupiga kambi usiku wake wakalala fresh..ile kuamkia sana Chale mpk kwenye vichwa vya mbo0 ikabidi wafungashe virago watimke!
ni shidaaaaaaaaaa mpaka kiumeni
 
Bahati mbaya maeneo hayo watu hawawangi bali ni kuroga mwanzo mwisho.
 
Nimezaliwa hospital ya masista chala st joseph (ile ya zamani karibu na uwanja wa shule sio mpya) Nimeshoma shule ya msingi chalantai na secondary ya chala , nimewai kuishi Namanyere , kipiri, kala, kaengesa, karema, mwese, mpanda, kambanga, kibo, sumbawanga mjini Nk,
Kiufupi naifahamu Rukwa na Katavi nje ndani ( bara na ziwani)
Kuna sehemu nyingi ambazo zinavutia sana kutembelea kama hifadhi ya katavi, kalambo force kuna vyakula vizuri sana samaki na dagaa wazuri na wenye radha nzuri kuliko wote tz, watu wanalima sana mahindi, maharage, mpunga nk, na ardhi ina rutuba ya kutosha kiufupi suala la njaa kule ndoto,
Kuhusu uchawi na magonjwa ya ajabu kama mleta uzi anavyodai sipingi wala sikubali maana kila jamii ina imani zake
Suala la uchawi n suala la imani ni kweli kuna maeneo yana wanaoitwa wachawi na waganga ila vingi ni story tu kama ulikuwepo ilikuwa zaman sana ila walichokifanya wazee waliopo sasa wamebaki wanatumia ule uzee wao na history kuwatisha watu tu, jamii ya wachawi walikufa na uchawi wao na waganga walikufa na dawa zao maana hawakutaka kuwarithisha wajukuu na watoto wao waliorithi n wachache sana ndio maana hata habar za uganga Sumbawanga cku hzi utaibiwa tu, watu wamekufa na utaalamu wao eg kina Mzee Maua,
Ukienda Sumbawanga utasikia story tu ila hakuna hao mapaka wala nn watu wanaishi kwa history tu, ila sehemu inayobaki kuwa hatari ni pwani ya ziwa Tanganyika huko cheza salama
 
Back
Top Bottom