Mikoa mitatu mipya kuanzishwa

Katika hotuba ya Desemba 30 Bungeni Dodoma (nakala ya Kiingereza: SPEECH BY THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, ON INAUGURATING THE FOURTH PHASE PARLIAMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, PARLIAMENT BUILDINGS, DODOMA, 30 DECEMBER 2005),JK hakutangaza kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka.

Toka hapo bajeti ya kila mwaka haikutangazwa kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka!

Sasa haya yametoka wapi?

Kwani yaliyofanyika yote kwa kipindi chote cha miaka minne aliyazungumza alipohutubia Bunge Dec 30?
 
kati ya mambo yote ya ajabu sielewi kwanini Pwani haigawanywi ili kuongeza eneo la mkoa wa Dar!!! it makes absolutely NO SENSE!!!!!
Code:
Pwani ameizungumzia lakini kwa wilaya ya BAGAMOYO AMBAPO alisema Muungwana amekataa kuigawa Bagamoyo kwa sasa.......ila kwa kuugawa mkoamzima wa Pwani hilo halipo kabisa kwenye plan ya SIRIKALI
 
kati ya mambo yote ya ajabu sielewi kwanini Pwani haigawanywi ili kuongeza eneo la mkoa wa Dar!!! it makes absolutely NO SENSE!!!!!

Ingekuwa ni vema kama OM akituambia matokeo ya kuufanya Manyara kuwa mkoa ni yapi. Ni kweli kuwa hatua hiyo imeleta maendeleo zaidi au ni kuwapa watu ulaji na kuangalia manufaa ya chama tu? ni vema kuwe na maelezo ya kutosha na ya msingi kuhusu uamuzi huo, otherwsie ni kuongeza gharama za matumizi ya serikali. It makes no sense at all.
 
ajira ya watu 480 tayari hapo, then kila baada ya miaka mitano hawa wanastaafu na kuweka wapya kabisa, hili litasaidia kuondoa umasikini kwani miaka mitano inatosha kabisa kwa mtu kujivunia kwa kadiri ya uwezo wake akitoka hapo akafungue biashara yake.

tanzania nchi nakupenda kwa moyo wangu wote
 
Hivi huu ukubwa wa mikoa husika umetokea hapa juzi karibuni nini?....Kwani zamani mikoa hiyo ilikuwa midogo?...Kama ni masuala ya ongezeko la watu, basi nadhani Dar ndo ingegawanywa mara tano!...Hawaoni kuwa hitaji la huduma ndio litazidi kwa kuunda mkoa mpya?...Kipi kigumu, kuongeza mikoa na Wilaya au kuboresha huduma zilizokuwepo awali, ambapo nazo zilikuwa za kujikongoja?.....Anyway, idont blame, labda jamaa zangu watapata ajira huko!
 
Rev.Kishoka,
Mkuu kinachonishangaza mimi ni hii migao ya mikoa kusema kweli sielewi kabisa inahusiana vipi na Maendeleo. Kwa mfano mikoa ya Kigoma na Singida ni mikoa iko nyuma sana toka tupate Uhuru. Sasa sielewi maendeleo yao yamekwama kwa sababu ya ukubwa wa nchi au kitu gani. Acha wilaya hata makao makuu ya mikoa hiyo ni duni imeshindwa kabisa kuendelea miaka nenda rudi..

Halafu kinachotumika hapa kuwa kgezo ni kitu gani?..Je ni mtaji unaopewa kila mkoa au inahusiana zaidi na kitu gani kwani kama fedha ndio msingi wa maendeleo ya mikoa hii basi fedha zinagawanywe kulingana na wingi wa wilaya moja na halmashauri zake.. Wenzetu hugawa Mkoa katika majimbo mengi kutokana na hesabu kubwa ya wakazi ktk eneo moja, hivyo maendeleo yanapimwa kutokana na idadi ya wakazi (walengwa) ktk eneo moja na sio ukubwa wa nchi (ardhi)..Navyofahamu mimi maendeleo hulengwa WATU na sii ukubwa wa nchi.

Kinachotakiwa kufanyika ni kuipa mikoa jukumu la kukusanya kodi zao na kupanga maenedeleo yao badala ya serikali kuchukua jukumu lote..Kama kodi ni asilimia 15 basi asilimia 8 iwe ni ya serikali kuu na ile 7 iingie ktk mfuko wa Mkoa. Mikoa inaweza kupunguza kodi zake za ndani toka asilimia 7 kushuka ili kuvutia wawekezaji na kuleta ushindani. Ni rahisi kwa wananchi kufahamu viongozi wazuri toka utawala wenye madaraka mikoani kuliko kutoka serikali kuu kwani kwa kutumia njia hii tulonayo sasa hivi, CCM wameweza kubana maendeleo kwenye mikoa ambayo haikuchagua CCM.

Na hapa ndio wengi tumekuwa tukipigwa bao na CCM kwa sababu tuseme mathalan KIgoma wameichagua Chadema na makusanyo ya kodi asilimia 7 yanapatikana,Chadema ndio watakuwa na mamlaka ya kupanga mikakati ya maendeleo ya Kigoma kutokana na makusanyo ya fedha za kodi ya ndani..Hapa wananchi wanaweza kabisa kukilaumu chama kilichopo na sii kuwalaumu CUF au Chadema kwa maendeleo ya sehemu zao hali anayuwkusanya kodi zooote na kuzigawa ni serikali ya CCM...
 
Kugawa mikoa na wilaya ni hitaji au kipaumbele cha nani? kule kwetu Iselemagazi shinyanga tunahitaji maji, matibabu, waalimu wenye sifa wa watoto wetu, madawa ya mifugo na uhaba wa mvua kwetu ni tishio la maisha. Uhakika wa kesho kwa binamu yangu ni mdogo sana anajua leo imeisha salama, itakuwaje kesho hajui? NANI KAWATUMA KUGAWANYA GAWANYA ?????

Logic ya CCM watakwambia ANGEGAWA mkoloni usingelalamika, kwani ati na wao na raisi wake wana power zote kikatiba. Ni katiba mbaya ndiyo inasabisha yote haya.
 
Haya majina hata hayapendezi, kwa mara ya kwanza tunakuwa na jina/majina ya mikoa abbreviated! walishindwa kukubaliana jina moja zuri (relative term though) lenye maana kama ilivyo manyara? huenda hata majina ya wilaya ni vifupi vya kata zinazounda.

Usishangae ndugu yangu, hizo ni dalili za ukabila waziwazi. Njoluma - yani maana yake Wakinga, Wahehe na Wamanda wote kwa pamoja walitaka jina la Mkoa mpya uwe na initials za wilaya zao ingawa hilo haiwasaidii chochote. Nadhani hapa historia ingeruhusiwa ku-determine majina ya Mikoa na Wilaya, mfano kama jina linabeba historia fulani ambayo bado tunaona ni vema kuitunza.
 
Rev.Kishoka,
Mkuu kinachonishangaza mimi ni hii migao ya mikoa kusema kweli sielewi kabisa inahusiana vipi na Maendeleo. Kwa mfano mikoa ya Kigoma na Singida ni mikoa iko nyuma sana toka tupate Uhuru. Sasa sielewi maendeleo yao yamekwama kwa sababu ya ukubwa wa nchi au kitu gani. Acha wilaya hata makao makuu ya mikoa hiyo ni duni imeshindwa kabisa kuendelea miaka nenda rudi..

Halafu kinachotumika hapa kuwa kgezo ni kitu gani?..Je ni mtaji unaopewa kila mkoa au inahusiana zaidi na kitu gani kwani kama fedha ndio msingi wa maendeleo ya mikoa hii basi fedha zinagawanywe kulingana na wingi wa wilaya moja na halmashauri zake.. Wenzetu hugawa Mkoa katika majimbo mengi kutokana na hesabu kubwa ya wakazi ktk eneo moja, hivyo maendeleo yanapimwa kutokana na idadi ya wakazi (walengwa) ktk eneo moja na sio ukubwa wa nchi (ardhi)..Navyofahamu mimi maendeleo hulengwa WATU na sii ukubwa wa nchi.

Kinachotakiwa kufanyika ni kuipa mikoa jukumu la kukusanya kodi zao na kupanga maenedeleo yao badala ya serikali kuchukua jukumu lote..Kama kodi ni asilimia 15 basi asilimia 8 iwe ni ya serikali kuu na ile 7 iingie ktk mfuko wa Mkoa. Mikoa inaweza kupunguza kodi zake za ndani toka asilimia 7 kushuka ili kuvutia wawekezaji na kuleta ushindani. Ni rahisi kwa wananchi kufahamu viongozi wazuri toka utawala wenye madaraka mikoani kuliko kutoka serikali kuu kwani kwa kutumia njia hii tulonayo sasa hivi, CCM wameweza kubana maendeleo kwenye mikoa ambayo haikuchagua CCM.

Na hapa ndio wengi tumekuwa tukipigwa bao na CCM kwa sababu tuseme mathalan KIgoma wameichagua Chadema na makusanyo ya kodi asilimia 7 yanapatikana,Chadema ndio watakuwa na mamlaka ya kupanga mikakati ya maendeleo ya Kigoma kutokana na makusanyo ya fedha za kodi ya ndani..Hapa wananchi wanaweza kabisa kukilaumu chama kilichopo na sii kuwalaumu CUF au Chadema kwa maendeleo ya sehemu zao hali anayuwkusanya kodi zooote na kuzigawa ni serikali ya CCM...

Ni utaratibu mzuri sana kama CCM wanaweza ukubali, kusimamia na kutekeleza. Kwa namna ni kuunda na KUPELEKA madaraka kwenye serikali za majimbo - China imeendelea haraka sana kwa kutumia utaratibu huo. Lakini CCM hawapo kwa ajili ya maendeleo ya watu, hivyo sahau kua kuna siku watafanya kweli
 
There must be a lunatic on the driving seat!
It turns out that after over 46 years of independence we are as much confused, lost and undecided as ever!
I suspect, more and more of us underrate the strength contained in our votes! We are so lazy to think straight. I have seen the excitement in their eyes as General Election draws near, for they know its time to sell votes! And they sure gonna sell them vote, in exchange with cheap clothing, empty and ridiculous promises, small favours etc, all at the cost of this country's future!
I sometimes wish our society could be rid of such people but I know, after the elections, they will be the very first ones to complain about what the govt is doing and what its not doing!
Ooh, how I feel sad after realizing that we are actively and passionately ruining our lovely country, and a sure thing is, we will handle this country to our sons and daughters in a much worse shape than the state it had when we received it from our ancestors!
At times, I keep wondering. How dare we laugh and scorn our ancestors for signing disadvantegeous contracts with colonialists in exchange with cheap presents and meaningless rewards? At least they had an excuse, they never knew how to read, but now we damn well know how to read and right and weigh and scrutinize, yet we are committing the same grave mistakes, even worse than them! All this because of SELFISHNESS. A recent and deadly EPIDEMIC sweeping across this land with such a great force and menace!

HYPOCRACY everywhere, GOD help us and deliver us from this mess, please start with our mind set, we beg and pray dear Lord, AMEN
 
Rev.Kishoka,
Mkuu kinachonishangaza mimi ni hii migao ya mikoa kusema kweli sielewi kabisa inahusiana vipi na Maendeleo. Kwa mfano mikoa ya Kigoma na Singida ni mikoa iko nyuma sana toka tupate Uhuru. Sasa sielewi maendeleo yao yamekwama kwa sababu ya ukubwa wa nchi au kitu gani. Acha wilaya hata makao makuu ya mikoa hiyo ni duni imeshindwa kabisa kuendelea miaka nenda rudi..

Halafu kinachotumika hapa kuwa kgezo ni kitu gani?..Je ni mtaji unaopewa kila mkoa au inahusiana zaidi na kitu gani kwani kama fedha ndio msingi wa maendeleo ya mikoa hii basi fedha zinagawanywe kulingana na wingi wa wilaya moja na halmashauri zake.. Wenzetu hugawa Mkoa katika majimbo mengi kutokana na hesabu kubwa ya wakazi ktk eneo moja, hivyo maendeleo yanapimwa kutokana na idadi ya wakazi (walengwa) ktk eneo moja na sio ukubwa wa nchi (ardhi)..Navyofahamu mimi maendeleo hulengwa WATU na sii ukubwa wa nchi.

Kinachotakiwa kufanyika ni kuipa mikoa jukumu la kukusanya kodi zao na kupanga maenedeleo yao badala ya serikali kuchukua jukumu lote..Kama kodi ni asilimia 15 basi asilimia 8 iwe ni ya serikali kuu na ile 7 iingie ktk mfuko wa Mkoa. Mikoa inaweza kupunguza kodi zake za ndani toka asilimia 7 kushuka ili kuvutia wawekezaji na kuleta ushindani. Ni rahisi kwa wananchi kufahamu viongozi wazuri toka utawala wenye madaraka mikoani kuliko kutoka serikali kuu kwani kwa kutumia njia hii tulonayo sasa hivi, CCM wameweza kubana maendeleo kwenye mikoa ambayo haikuchagua CCM.

Na hapa ndio wengi tumekuwa tukipigwa bao na CCM kwa sababu tuseme mathalan KIgoma wameichagua Chadema na makusanyo ya kodi asilimia 7 yanapatikana,Chadema ndio watakuwa na mamlaka ya kupanga mikakati ya maendeleo ya Kigoma kutokana na makusanyo ya fedha za kodi ya ndani..Hapa wananchi wanaweza kabisa kukilaumu chama kilichopo na sii kuwalaumu CUF au Chadema kwa maendeleo ya sehemu zao hali anayuwkusanya kodi zooote na kuzigawa ni serikali ya CCM...
Ndugu mkandara, nakumbuka tuliyazungumza haya kwa kirefu sana wakatu ule wa mjadala wa majimbo.Tulitabiri kwamba baada ya miaka kumi ijayo tutakuwa na mikoa karibia hamsini na wilaya zaidi ya miatatu kwa kigezo cha kusogeza maendeleo kwa wananchi. Itafikia wakati ambapo wataweka kwenye ilani yao na kuahidi kugawa mikoa au wilaya mpya kama kigezo cha maendeleo.

Ukweli unabaki kuwa mfumo wa sasa wa kiutawala haukidhi mahitaji ya kimanedeleo hasa kwenye eno la kuvutia, kubuni, kusimamia na kugawanya rasilimali. Ni mfumo uliodumaza wananchi wengi kufikia hatua hata wanapotengeneza baraza la mawaziri wanajaribu kulazimisha watu watokee mikoa mbalimbali ili kuzuia manun'guniko,inakuwa hivyo kwa maana watu wanaoanisha moja kwa moja uwaziri na mgawanyo. Jimbo linapokuwa na waziri linataraji kufaidika zaidi, hata ziara za viongozi wa kitaifa zinatazamwa kama neema kwenye maeneo husika hizi ni ishara tosha kuwa mfumo wa utawala uliopo hauwezi kutatatua changamoto tunazozikabili.

Wakati mabapo tunangalia maeneo ya kudhibiti gharama za utawala, hawa jamaa wanaendelea kuziongeza na kuthibitisha ile dhana kwamba utawala ndio sekta kubwa katika nchi zinazoendelea. Vyanzo vya mapato vimebaki kuwa vile vile, kodi kwenye bia,sigara na soda, tumeshindwa kuwa wabunifu kwenye mapato lakini bado tunaibua maeneo mapya ya kiutawala!Sulushisho ni usismamizi wa rasilimali na kukuza mapato ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi na sio maeneo mapya ya kiutawala. Sera ya majimbo ya CHADEMA inabakia kuwa sera mbadala itakayoweza kutatua changamoto hizi.
 
Inasikitisha sana. Nchi masikini kwa kila kitu lakini tunaendesha mambo kianasa sana. Tuna Serikali kubwa sana. Baraza la Mawaziri ni kubwa sana. Bunge letu kubwa sana na linazidi kupanuliwa kwa majengo na idadi ya Wabunge. Mahakama kuu na Mahakama ya Rufani nazo zinaongezwa Majaji bila mpangilio. Sasa tunaongeza Mikoa na Wilaya! Baadhi yetu tulitarajia haya kufanyika ili kupunguza gharama:
1.Baraza la Mawaziri lingepunguzwa KIKATIBA kwa kutaja idadi ya WIZARA kwenye Katiba. Wenzetu Kenya watalifanya hili Katiba yao mpya ikipita.
2. Tulitarajia Bunge lipunguzwe KIKATIBA pia. Itamkwe ndani ya Katiba kwamba kila Halmashauri/mji/manispaa iwakilishwe na Mbunge mmoja tu.
3.Mikoa ingepunguzwa hadi kuwa 20 tu Bara na miwili Zanzibar.
4.Wilaya zisingezidi 100 kwa Bara na tano kwa Zanzibar.
Tungeelekeza mapesa ambayo yangeokolewa kwa upunguzaji huu kwenye kujenga na kuimarisha HUDUMA za jamii kama mashule, zahanati, barabara, mahakama, vituo vya polisi, maktaba, maabara,....
 
Wana JF mwaonaje,

Ni Bora Kuongezwa Mikoa au Kuundwa Majimbo, Kipi kati ya hivi viwili vinaweza kutuharakishia maendeleo katika jamii yetu ya watanzani,

Maana hii kila kukicha hawa viongozi wanajifanya kuwa wao ni Creative kwa vitu vyepesi vyepesi sana hawatakia kabisa kupoteza muda wao kwa ajiri ya maendeleo ya Taifa hili kwa vizazi vijavyo no one kataka serikali hii wanafikilia hicho, Ni mshauri gani aliye mshauri Rais Mikoa iongezeke kwa vigezo vipi?

Sasa hii si kudhiirisha Umma kuwa serikali ya CCM haijui kutawala nchi kama tu wameshindwa kuamisha makao makuu ya serikali kuwa DODOMA nashaanga wao wanaweza kupata fungu la kuweza ongeza mikoa mingine mitatatu basi nchi hii inapesa ila jinsi ya kuzifanyia kazi yake ipaswavyo haukuna watu wenye upeo huo huo wa kuona mbali.

Me nadhani viongozi wetu ni wafinyu sana kwa kupanga mikakati ya kimaendeleo au ni kufanya kusudi au kuan mkono wa mtu ndio una remote hii nchi basi. na hii inaashiria wazi wazi kuwa viongozi wetu wenye dhamana ndani ya nchii hawataki kata kat maendeleo ya wanchi wao walio wachangua
 
Hivi huu ukubwa wa mikoa husika umetokea hapa juzi karibuni nini?....Kwani zamani mikoa hiyo ilikuwa midogo?...Kama ni masuala ya ongezeko la watu, basi nadhani Dar ndo ingegawanywa mara tano!...Hawaoni kuwa hitaji la huduma ndio litazidi kwa kuunda mkoa mpya?...Kipi kigumu, kuongeza mikoa na Wilaya au kuboresha huduma zilizokuwepo awali, ambapo nazo zilikuwa za kujikongoja?.....Anyway, idont blame, labda jamaa zangu watapata ajira huko!

Moja ya lengo la kuongeza wilaya/mikoa mipyakusogeza huduma(za jamii na utawala)/maendeleo kwa wananchi kulingana na jiografia ya eneo husika na idadi ya watu. Kuna sababu isiyo rasmi(binafsi naiona ni ya kibaguzi) kuwa wanagawa kulingana na maslahi ya kisiasa na mchango wa eneo husika kiuchumi, kwamba kama eneo husika halina manufaa kiuchumi basi na maendeleo hayapelekwi. Ndio maana maeneo mengi nchi hii yako nyuma kiuchumi!
 
hayo ni maandalizi mazuri kwa ulaji wa watoto wao na washikaji zao.....si mnamjua Prezidaa wetu kwa mambo ya uswahiba??haya sasa U-DC,U-RC,U-RPC na vyeo kedekede vya kumwaga
 
Nafikiri ili kuharakisha maendeleo ya watu (watakaopewa vyeo) tunatakiwa kuwagawa watanzania katika magroup ya watu laki tano tano katika kila mkoa na kuwapatia mkuu wao wa mkoa na kila laki moja mkuu wao wa wilaya yaani kwa watu Millioni 40 tunakuwa na mikoa 80 na wilaya 400.

Ajira ya watu 480 tayari hapo, then kila baada ya miaka mitano hawa wanastaafu na kuweka wapya kabisa, hili litasaidia kuondoa umasikini kwani miaka mitano inatosha kabisa kwa mtu kujivunia kwa kadiri ya uwezo wake akitoka hapo akafungue biashara yake.

HILI NDILO LILILOBAKI, MAANA MIMI SIONI UMUHIMU WA KUGAWANYA GAWANYA VIJISEHEMU NA KUPEANA KISHIKAJI WAKATI KAZI WANAZOFANYA KWA WANANCHI HAZIONEKANI ZAIDI YA KUWA WAHAKIKI WA WATAKAOPIGIA KURA CCM NA KUPANGA MIKAKATI YA WIZI WA KURA.
nyerere aliliona hilo na kulifanyia kazi lakini likamshinda
 
inawezekana pakawa na mikoa kumi ila cha msingi ni VIPAUMBELE. nchi hii inahitaji zaaidi miundombinu (physical and social). tunahitaji barabara za lami, madaraja, njia za reli (phisical), mahospitali si zahanati, mashule, masoko, maji, umeme (social). haya hata yakiwekwa sehemu zusuzo na watu, watu watazifuata hizi huduma. wakati mwingine viongozi si lazima wawe hawa wa kisiasa, hata wa kijadi wanaweza kutawala maeneo yao, cha msingi tu serikali iweke hiyo miundombinu na mengine yatakuja automatikale
 
Back
Top Bottom