Mikoa mitatu mipya kuanzishwa

Mikoa mitatu mipya kuanzishwa

Katika hotuba ya Desemba 30 Bungeni Dodoma (nakala ya Kiingereza: SPEECH BY THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, HIS EXCELLENCY JAKAYA MRISHO KIKWETE, ON INAUGURATING THE FOURTH PHASE PARLIAMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, PARLIAMENT BUILDINGS, DODOMA, 30 DECEMBER 2005), JK hakutangaza kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka.

Toka hapo bajeti ya kila mwaka haikutangazwa kuwa Mikoa na Wilaya kuongezeka!

Sasa haya yametoka wapi?



Perhaps, having as many DCs and RCs as possible so as to make sure Chama Cha Map....#1@0* always stays in power.
Kuna mahali nchi yenda kuliwa.
 
hayo ni maandalizi mazuri kwa ulaji wa watoto wao na washikaji zao.....si mnamjua Prezidaa wetu kwa mambo ya uswahiba??haya sasa U-DC,U-RC,U-RPC na vyeo kedekede vya kumwaga

Tena vitagawiwa kwa wale vimbelembele watakaoonekana wakati wa uchaguzi
 
Wacha tu waendelee kuikata nchi vipande vipande na hivyo vipande vipande vinakuwa vua kikabila na hivyo vipande vipande ni kurahisisha kupewa vyeo washikaji wao.
Watu wamekenua meno tu hata wasomi wetu. Unaweza kushangaa kama nchi hii ina wasomi.
 
Ilani ya CCM ya uchaguzi imetaja kuongeza ajira katika kipindi cha miaka mitano inayoishia mwaka huu. Imetangaza ili kupata kura, kura zimepatikana, ajira hazikupatikana, viongozi hawajui ni vipi wanaweza kukuza ajira, sasa huu ndio ubunifu wa CCM kukuza ajira. Hapa statistics zinaonyesha ajira zaidi ya 480 bila kujali tunazalisha au tunaongeza unnecessary burden to tax payers. Haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wasio na ubunifu.
 
Afrika, Afrika, lini tutakuwa liberated kwenye akili zetu? badala ya kufikiria maendeleo ya nchi, viongozi wanafikiria kupeana ulaji, Afrika,
Hizi pesa zikipelekwa kwenye Elimu, Miundombinu, Afya nk hazitoi Ajira? kwa nini viongozi wetu wanajifikiria wao tu? what are we trying to create here? Duh, Waafrika ndivyo tulivyo.
 
Back
Top Bottom