Mikoa mitatu mipya kuanzishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikoa mitatu mipya kuanzishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Jun 18, 2010.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ame-hint Pinda leo wakati akihitimisha bajeti yake. Mmoja utaitwa Njoluma, utahusisha wilaya za Njombe, Ludewa na Makete. Mwingine ni Simiu utakaogawanywa kutoka Shinyanga na mkoa wa Geita.

  Pia kuna mipango ya kuanzisha wilaya mpya kama 20 hivi.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kati ya mambo yote ya ajabu sielewi kwanini Pwani haigawanywi ili kuongeza eneo la mkoa wa Dar!!! it makes absolutely NO SENSE!!!!!
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  Haya majina hata hayapendezi, kwa mara ya kwanza tunakuwa na jina/majina ya mikoa abbreviated! walishindwa kukubaliana jina moja zuri (relative term though) lenye maana kama ilivyo manyara? huenda hata majina ya wilaya ni vifupi vya kata zinazounda.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, hata Moro unastahili kugawanywa, ni mkubwa ajabu na administration ayke ni ngumu sana. Just imagine, kwa kaskazini unapakana na mikoa inayopakana na nchi jirani na kwa kusini unapakana na mikoa inayopakana na nchi jirani pia.
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  mkuu naomba hint namna alivyojibu hoja za Dr. Slaa.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  amepiga politiki tu... zile hoja ngumu kujibika kwa mtu mkweli kama Pinda
   
 7. Sun Tzu

  Sun Tzu Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mimi naamini it makes no sense kuongeza ukubwa wa Mkoa wa Dar Es Salaam. ikiwezekana Dar Es Salaam ilipaswa kugawanywa kuwa kama mikoa ya kipolisi. yaani mikoa mitatu. Hata hivyo kuongeza idadi ya mikoa pamoja ya kuwa tunasogeza huduma kwa jamii, kinachotokea ni kuongezeka ukubwa na mzigo kwa serikali. Ukubwa wa mkoa au jimbo siyo kitu muhimu sana kwani nchi kama Marekani kuna majimbo makubwa sana ambayo ni scarcely populated na kuna mengine madogo sana lakini densely populated.

  Kitu muhimu ni allocation of resources na kuzitumia zilizopo effeciently. Labda zoezi hili la kuongeza idadi ya mikoa linatoa msukumo wa kuweka miundombinu muhimu karibu na wananchi.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ili kuharakisha maendeleo ya watu (watakaopewa vyeo) tunatakiwa kuwagawa watanzania katika magroup ya watu laki tano tano katika kila mkoa na kuwapatia mkuu wao wa mkoa na kila laki moja mkuu wao wa wilaya yaani kwa watu Millioni 40 tunakuwa na mikoa 80 na wilaya 400.

  Ajira ya watu 480 tayari hapo, then kila baada ya miaka mitano hawa wanastaafu na kuweka wapya kabisa, hili litasaidia kuondoa umasikini kwani miaka mitano inatosha kabisa kwa mtu kujivunia kwa kadiri ya uwezo wake akitoka hapo akafungue biashara yake.

  HILI NDILO LILILOBAKI, MAANA MIMI SIONI UMUHIMU WA KUGAWANYA GAWANYA VIJISEHEMU NA KUPEANA KISHIKAJI WAKATI KAZI WANAZOFANYA KWA WANANCHI HAZIONEKANI ZAIDI YA KUWA WAHAKIKI WA WATAKAOPIGIA KURA CCM NA KUPANGA MIKAKATI YA WIZI WA KURA.
   
 9. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Absoluliyuit! unajua nilipoona mikoa inagawanywa nikajua moro upo...loooh!
  ila haya majina hapana .....hata kama lingekuwa jina mchumba wangu ......noma hata kulitamka kwa mashosti...
  mix with yours
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama mtazamo wa kugawanya ndiyo huu basi na nchi pia igawanywe tuwe na marais watano, wa zanzibar, wa kanda ya ziwa, wa kanda ya magharibi, wa kanda ya kati na wa kanda ya kaskazini na pwani. Maana li nchi likubwa kweli hata kuliongoza inakuwa ngumu kwa rais mmoja.

  Hapa suala si ukubwa wa eneo ni suala la effective and efficiency governing ambayo huwa hailetwi kwa kupeana kama zawadi bali ni kuwa na watu capable kwa Tanzania hilo hatuna
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  The whole move is just not cost effective and by no means it will improve efficiency.... ni kama kuongeza mke baada ya matatizo ya mke wa kwanza

  i would rather see tumeongeza barabara kuliko kuongeza wakuu wa mikoa
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Faida ya kuwa na mikoa mingi ni nini? Najua Australia kuna majimbo saba tu ukiondoa lile la makao makuu, ambalo ni mji mdogo tu, lakini wana maendeleo ya juu sana kuliko sisi. Je wingi wa mikoa unatuisadia nini zaidi ya kuongeza ukubwa wa serikali na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji na probability ya wizi wa raslimali za umma?

  Badala ya kuongeza mikoa na wilaya, serikali inatakiwa kuboresha usafiri kutoka vijijini hadi makao makuu ya mikoa na wilaya, na kuongeza ufanisi maosifisbni kusiwe na kupteza muda wqa umma.

  Niliwahi kwenda ofisi fulani wizara ya elimu ya juu (wakati huo) hapo Dar majira ya saa nne asubuhi nikamkuta afisa (mama mmoja) anaonega kwenye simu na rafiki yake kuhusu kitchen party hadi majira ya saa sita. Nilipomweleza shida zangu akasema alikuwa na njaa hivyo kuniambia nirudi baada ya lunch. Sikwenda popote nikaendeklea kumsubuiri hadi saa nane, na kupata huduma yangu karibu saa tisa yaani zaidi ya saa tano kupata sahihi kwenye makaratasi yangu. Upuuzi wa namna hiyo ndio unaotakiwa kushughuliwa na serikali mara moja kjuliko kuongeza ukiritimba
   
 13. M

  Malunde JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kugawa mikoa na wilaya ni hitaji au kipaumbele cha nani? kule kwetu Iselemagazi shinyanga tunahitaji maji, matibabu, waalimu wenye sifa wa watoto wetu, madawa ya mifugo na uhaba wa mvua kwetu ni tishio la maisha. Uhakika wa kesho kwa binamu yangu ni mdogo sana anajua leo imeisha salama, itakuwaje kesho hajui? NANI KAWATUMA KUGAWANYA GAWANYA ?????
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ooooppppss! i forgot ile tactic ya wakoloni ya DIVIDE AND RULE!!!!
   
 15. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Hii nchi kila kitu ni siasa tu.....tuna siasa ni kilimo (azimio), sijui siasa ni kazi na naona mikoa na wilaya hadi tarafa ni siasa tu
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu hapo ndipo panaponitatiza mimi... we have politicized even our graveyards!!!
   
 17. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtazamo wangu ni kama wa MKJJ, wangetanua dsm...wapunguze pwani, waachane na hiyo mingine. Kuongeza mikoa mipya ni kuongeza ukubwa wa serikali bila ulazima wowote... kuna kujenga makao makuu, wakuu wa mikoa wapya na ofisi zao nzimanzima, duh ulaji huo..
   
 18. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakubaliana na wewe 100%
  Hata China pamoja na ukubwa wake ina majimbo 25 tu na ni nchi inayoendelea kwa kasi ajabu. Mi nadhani serikali yetu imekosa mfumo wa kiutawala maana tuna kila aina ya viongozi katika ngazi za mikoa na wilaya!! mfano kwa Majiji tuna Mkuu wa Mkoa, Meya wa Jiji, Mkurugenzi wa jiji, Mkuu wa Wilaya, Meya wa Manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa ambapo ukiangalia vizuri utakuta kuna watu hapo ofisi zao ni redurndant kabisa. Hawana kazi za kufanya na wakati mwingine wanaishia kugombania kazi na ofisi zingine!

  Cha muhimu kwangu mimi ni kwanza serikali itambue uongozi wa mkoa unatakiwa uweje ili uwe cost effective na ufanisi pia uongezeke. Wakishalitambua hilo waende step ya pili kuadopt na kuhakikisha katika mikoa iliyopo kila kitu kinaenda sawa. Hakuna haja ya kuwa na mikoa 29 wakati kanchi kenyewe hakana uwezo wa kussuport such administration!

  Kwa upande mwingine mi naona hapa kuna ulaji unatengenezwa kwa ajili ya watu flani flani.......
   
 19. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,741
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Mtazamo wangu ni tofauti kidogo.. Sioni kwa nini wanaamua kuanzisha mikoa wakati mikoa iliyopo tumeshindwa kuiletea maendeleo
  Kwani ukubwa au udogo wa eneo ndio kutokupatikana kwa maendeleo? Maendeleo yanaletwa na watendaji na si size ya eneo. Mbona wenzetu Marekani na Canada nchi kuuuuubwa na mikoa yao mikuuuubwa wanayo maendeleo iweje sisi tushindwe. Hizi zawadi za kupeana kwa vifurushi zina mambo sana. Huku ni kuongezeana mizigo kwa sisi walipa kodi kwani wilaya itabidi ziongezeke, wakuu wa mikoa, wilaya, kata, tarafa, vijiji etc etc itabidi kuwe na bajeti yao sasa si kubebeshana mizigo hapa wajameni. Hizo wilaya zina maendeleo kiasi gani ya kupewa umkoa labda kama mimi sielewi vigezo wanavyotumia kuipa sehemu mkoa au wilaya. Sehemu hazina barabara, maji, umeme mnataka eti ziitwe mikoa tutafika kweli????
   
 20. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #20
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nilifikiri kuwa itapunguzwa na kuwa minane tu, kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni wa Mwingereza!

  Nilitumaini ni wakati wa kufinya matumizi ya pesa za umma; kumbe ni kinyume! Ni yale yale ya kutumia mabilioni ya pesa kwa faida ya dakika 90 za kusaidia "usafirishaji" au kuleta timu ya Brazil huko Afrika Kusini!
   
Loading...