Mikoa Mipya kuanza hivi karibuni

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
1,195
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.
 
Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
0
Ni mizigo zaidi hiyo kwa mlipakodi aliyekamulika hadi damu kwa ufisadi reja reja kila mahali.

Uzoefu umeonyesha, kutokaana na mikoa ambayo haina wakuu wa mikoa hadi hivi sasa, kwamba wakuu wa mikoa na wilaya hawana tija yoyote kwa mlipakodi zaidi ya CCM kuzalisha ajira zaidi kwa maswahiba walioaachwa kwenye baridi baada ya uchakachuaji 2010.

Mheshimiwa rais, haatuhitaji mizigo zaidi kwa makali haaya ya maisha.
 
Dopas

JF-Expert Member
Aug 14, 2010
1,151
1,195
Kwa ufanisi ni sawa. Lakini itakuwaje wakati hii iliyopo inashindikana kuhudumiwa vizuri? Kwa sasa kugawa mikoa sio kipaumbele.
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
0
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.

Kama wanahitaji au la!

Kwa hiyo kuna kimoja kilifanyika kabla kingine au hadaa za uchaguzi kama kawaida ya watawala wetu!?
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
32,961
2,000
Huu ni mojawapo ya mambo ambayo hayaingii akilini.. hivi ni lini ardhi ya Tanzania iliongezeka? wanachofanya ni kuigawa ardhi ile ile ndogo kwenye mikoa kuficha kushindwa kwao kuendeleeza mikoa iliyopo as if kwa kuongeza mikoa zaidi ndivyo watabadilisha mikoa iliyopo! It makes absolutely no sense.
 
IPECACUANHA

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
2,984

I belive from practical experience that Regional Commisioners are celebrative Redundunt figures. See what has happened from election in October last year, where more that eight regions are running without sitting regional commisioners. To add more regions I found that absolutely absurd.
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
22,604
2,000
Ujinga tu..
Wanaacha kuhangaika na mambo ya maana wanataka kugawa ardhi na kuongeza mikoa ambayo itawacost wananchi zaidi ya kuwasaidia!
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,932
2,000
Huu ni mojawapo ya mambo ambayo hayaingii akilini.. hivi ni lini ardhi ya Tanzania iliongezeka? wanachofanya ni kuigawa ardhi ile ile ndogo kwenye mikoa kuficha kushindwa kwao kuendeleeza mikoa iliyopo as if kwa kuongeza mikoa zaidi ndivyo watabadilisha mikoa iliyopo! It makes absolutely no sense.
Maana ya mikoa/wilaya adhima yake nikuwasogezea wananchi huduma karibu na wala si kuteua mkuu wa mkoa nk. Enzi zile kwanini mtu anayetaka passport aliyoko mpakani mwa ngara aende DSM arudi ndo aende rwanda?

Ama mwalimu kule kwa gegemkeni kwanini asafiri km 700 kwenda mkoani kuonana na mkurungezi wake wa elimu? tatizo watu wanaupotosha ukweli na hali halisi.
Harafu unapofanya mikoa mingi ama wilaya mingi ndo maendeleo yanasambaa kote kwa uwiano, kwanini uwe na magorofa yaliyoenda juu pale dsm wakati ukikatiza dakika 15 tu unakutana na nyumba za msonge za kufa mtu? kwangu mimi kuwa na wilaya mingi naa mikoa mingi ndo njia sahihi ya ku decentralize maendeleo.

Harafu mkitoka hapo mtakuja kuhoji kwanini watu wanakimbilia mjini
 
Nailyne

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
350

sasa badala ya kutumia fedha kuanzisha ofisi mpya za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na kuajiri utitiririr wa watumishi, hizo pesa kwa nini zisiende kujenga shule,hospitals, barabara kwenye hayo maeneo ambayo hajafikiwa na hizo huduma??? watendaji wa serikali na wanaomshauri rais ifike wakati waangalie maamuzi yenye manufaa kwa taifa , haya mambo ya kuangalia ulaji kuna siku tutaambiwa rais atia saini kigoma kuwa nchi inayojitegemea!
 
SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,769
2,000
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.
Hivi wangapi wana access ni hili gazeti? Kwanza hata kwenye tovuti ya Utumishi halionekani
 
bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
195
08 Septemba, 2011
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MIKOA MIPYA KUTANGAZWA KESHO - PINDA
WAZIRIMKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itatoa tangazo rasmi la Serikali(Government Notice) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya na wilaya mpya ambalolinatarajiwa kuchapishwa kesho (Ijumaa, Septemba 9, 2011).

Ametoakauli hiyo jana jioni (Jumatano, Septemba 7, 2011) wakati akizungumza naviongozi wa mkoa wa Rukwa na wa wilaya ya Mpanda mara baada ya kuwasili katikakiwanja kidogo cha ndege cha Sitalike katika Hifadhi ya Wanyama ya Katavi nakupokea taarifa ya Mkoa na Wilaya.

“MheshimiwaRais Jakaya Kikwete alisaini tangazo lile tarehe 5 Septemba, na litatolewarasmi Ijumaa wiki hii ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuonyesha nia ya MheshimiwaRais kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya,” alisema.

“Tangazohili likishatoka litakuwa likionyesha makao makuu ya mikoa mipya na makao makuuya wilaya yawe wapi. Hivyo wananchi watapata fursa ya kutoa maoni yao kwa mudawa siku 30... wanaruhusiwa kusema kama wanataka mikoa na wilaya vianzishwe aula!”

Alisemawananchi wanapaswa kuzingatia kwamba taarifa zao ni lazima ziwasilishwe makaomakuu ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika mudawa siku 30 kuanzia siku ambayo Rais Kikwete alisaini tamko hilo.

WaziriMkuu alisema hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa zoezi la kuweka mipaka mipyakutoka kwenye wilaya na mikoa ya zamani na kisha kuchora ramani za kuoneshamikoa mipya na wilaya mpya.

WaziriMkuu Pinda amewasili wilayani hapa kwa ajili ya ziara rasmi ambapo anatarajiwakuzindua matawi mawili ya Chuo Kikuu Huria na tawi la Benki ya CRDB. Kesho(Ijumaa, Septemba 9, 2011) anatarajiwa kuzindua tawi la Chuo Kikuu Huria laSumbawanga huko mjini Sumbawanga.

Keshokutwa, (Jumamosi, Septemba 10, 2011) Waziri Mkuu atakwenda wilayani Mpandaambako pia atazindua tawi la Chuo Kikuu Huria Mpanda. Mchana huo huo, atazinduatawi la Benki ya CRDB Mpanda. Anatarajiwakurejea jijini Dar es Salaam Jumapili ijayo, (Septemba 11, 2011)

.(mwisho)

IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,ALHAMISI, SEPT. 08, 2011.
 
juu kwa juu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
260
170
kwa maendeleo ya sasa bila wakuu wa wilaya na mikoa hakuna maendeleo, kwa vile mpaka sasa ndio figures pekee zinazoweza kuwakemea wakurugenzi na wakuu wengine wa idara wasifanyae wanachotaka. kama hoja ni kufuta veo hivyo basi wafutwe hata viongozi wa vyama vya siasa wa wilaya na mkoa kwa vile walio taifani wanatosha. kuna mihimli ya dola,mahakama na bunge. katika ngazi za wialya DC ndio mhimili wa dola na Rc the same. kwa hiyo nafasi hizo napendekeza ziboreshwe kwa kupewa madaraka zaidi ili kuharakisha maendeleo.
 
Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,605
1,225
mikoa ya NJORUMA, KATAVI, GEITA, SIMEU etc kweli viongozi wa Bongo kwa kutaka umaarufu wa kisiasa duh!
 
Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,433
2,000
sasa badala ya kutumia fedha kuanzisha ofisi mpya za wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na kuajiri utitiririr wa watumishi, hizo pesa kwa nini zisiende kujenga shule,hospitals, barabara kwenye hayo maeneo ambayo hajafikiwa na hizo huduma??? watendaji wa serikali na wanaomshauri rais ifike wakati waangalie maamuzi yenye manufaa kwa taifa , haya mambo ya kuangalia ulaji kuna siku tutaambiwa rais atia saini kigoma kuwa nchi inayojitegemea!
Ningeshangilia kama ingetokea hapo kwenye red pakawa hivyo maana nimechoka kuishi katika li-nchi ambalo kila siku mabalaa yanaibuka...mara mafuta, oooh, ...sukari,...oooh, kagoda..., ohhh mgao wa umeme na taktk nyingi.....ikitokea nitahamia Jamhuri ya Kigoma haraka mno...
 
Bambo

JF-Expert Member
May 18, 2009
238
195
sina tatizo sana na mikoa mipya..bali napinga kwa nguvu zote jinsi ya kupata viongozi wa mikoa/wilaya hizo.kama mtindo ni kuteuliwa hapo siungi mkono na ni ufujaji wa mali ya umma kwani ni ulaji usio na maswali..ningependa viongozi hao nao wachaguliwe kwa kura na wananchi wa mikoa hiyo husika along side the presidential vote, ili wawajibike kwa wananchi na ikibidi wawe wazawa wa mikoa/wilaya hiyohiyo!!!kwa mfumo wa sasa mh..tutaendelea kuwapata akina monica mbega huko Ruvuma(zamani) wakati ni wabunge wa sehemu nyingine na wanatumia perks za mkoa mwingine kufuatilia maendeleo ya majimbo yao..
pili hivi hilo gazeti la serikali linaonekana wapi??dunia ya leo si yawatu wachache kujifungia na kagazeti kao halafu kanatoa maamuzi ya kitaifa!!
 
tunalazimika

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,100
1,195
akili za mwanakijiji huwa hazina macho kwa mazur yanayofanywa na serikali na mabaya yanayofanywa na chadema_ni kwa mising hiyo mijadala mbalimbali ambayo hutumia muda mwing kuiandaa huwa haina mashiko kwsbb pamoja na ukweli uliomo katika mada hizo kinachomharibia ni kwamba yeye kama muelimishaji hatakiwi kuonyesha muelekeo wake hadharani _na hik ndicho kifo cha jf, kwsbb mambo yote ni udini tu na chadema
 
afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,147
2,000
mikoa yote mipya imefaidika au kujiendeleza kiasi gani?
Je kuanzisha hii mikoa kuna faida gani kwa mwananchi wa kimo cha chini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom