Mikoa Mipya kuanza hivi karibuni

Mikoa Mipya kuanza hivi karibuni

Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.
<br />
<br />
Tunahitaji kuunganisha mikoa iwe kikanda ili kurahisisha uendeshaji badala ya kuendelea kuigawa. Historia inaonyesha kuwa zile nchi zilizounganishwa katika mfumo wa majimbo zina maendeleo makubwa. Nawasilisha
 
Nafikiri kipindi cha Serikali ya awamu ya nne ndicho kipindi pekee ambacho tumeshuhudia Serikali ikijiongezea mzigo mkubwa katika gharama za uendeshaji; Baraza la Mawaziri limekuwa kubwa, Idadi ya Wabunge wa kuteuliwa na viti maalum, majaji wameongezwa zaidi ya mara tatu, idadi ya mikoa na wilaya na mambo mengineyo mengi ambayo kimsingi hayana tija kwa mustakabali wa nchi na wananchi wake kwa ujumla.

Jambo hili halijawahi kufanywa na Marais wa awamu tatu za nyuma na kubwa linaloonekana hapa ni kuwa Rais wa awamu ya nne anafanya hivyo kwa ajili ya kupata nafasi za kuwaweka marafiki zake na sio kwa maendeleo ya nchi
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.

Wanatapatapa tu, na mie nimesikia leo yule waziri mkuu 'jina' kasema hayohayo; Swali kwangu nawauliza - kama wameshindwa kuwateua wakuu wa mikoa flanflan wawe watendaji kamili badala ya 'acting RC' wataweza mipya? Ni sawa na pangu pakavu tu...
 
Watu wanatengenezewa vitengo hapo.kuna maswahiba waliokosa kazi nao walishaahidiwa vyeo.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.
MIKOA MIPYA HATUHITAJI NA HAINA TIJA KWETU BORA HIZO PESA WAZINUNULIE MADAWATI NA KUJENGA MADARA.SIKU TUKIWA NA CHAMA CHENYE KULETA MAENDELEO KWELI TUNAONDOA NAFASI ZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA HAWANA WANACHOFANYA
Igunga(1).jpg
 
haikuwepo kwenye bajeti na huu ni mzigo kwa walipa kodi...ya nini? mikoa kibao na wilaya zake hakuna wakuu na maisha yanaenda
 
Sijalewa. Mikoa mipya inaanzishwa kisha ndiyo iangaliwe kama ina hitajika????????????
Ni kweli mdau,katika hali ya kawaida unaweza usielewe kipi ni kipi katika swali ulilouliza. Kimsingi,uanziswhaji wa maeneo mpya za kiutawala una hatua zake kabla ya kuanza rasmi. Moja ya hatua muhimu ndio hii tunayoiona hapa. Kwanza kabisa wananchi wa huwa ndio wanaotoa mapendekezo kwa mamlaka zinazohusika(Rais) kupitia kwa wawakilishi wao(wabunge na madiwani) juu ya haja ya kuanzishwa kwa maeneo mapya ya kiutawala (tarafa,wilaya,na Mikoa).Lengo kubwa likiwa ni kurahisisha na kusogeza huduma kwa katika maeneo yao. Maombi hayo yakimfikia Rais huyatafakari kisha kutoa uamuzi wa ama kuunga mkono au kutokuunga mkono. Endapo Rais ataunga mkono uanzishwaji wa maeneo hayo ya kiutawala (kama alivyofanya sasa) atalazimika kwa kwa mujibu wa sheria kutoa tangazo rasmi la serikali (government notice) ili kutoa fursa kwa wananchi wa mikoa husika kujadili mapendekezo yaliyomo kwenye tangazo hilo hususani makao makuu ya maeneo hayo mapya kiutawala. Lakini pia anaweza asiunge mkono mapendekezo hayo kama ilivyotokea kwa baadhi ya maeneo kutokana na sababu fulani fulani.Sasa nadhani tatizo kubwa liko kwenye sentensi"kama wanakubali maeneo yaanzishwe au la " . Maneo hayo yanaweza kuchanganya hasa tukizingatia kuwa mchakato wa uwepo wa maeneo hayo ulitoka kwa wananchi wenyewe. Sasa nini huwa kinaaminshwa hapa? Ni kwamba,inawezekana kabisa maoni ya wananchi wengi wa maeneo husika wasikubaliane na suala la mipaka na miji iliyoteuliwa kuwa makao makuu ya maeneo hayo.Ikitokea hivyo, basi mwisho wa siku wananchi wanaweza kuamua kwamba hatutaki tena uwepo wa maeneo hayo mapya angalau kwa sasa, mpaka hapo tutakapokubaliana katika mambo ya msingi.
 
sasa sijui ataitangaza nani, ....Mzee Luhanjo!!??? Watanzania hawana imani naye tena
 
Kwa mujibu wa taarifa ya TBC Taifa, Rais Kikwete alisaini hati maalumu ya kuanza kwa mikoa na wilaya mpya tarahe 5/9/2011 na tangazo rasmi litaandikwa kwenye gazeti la serikali tarehe 10/9/2011. Wananchi watapaswa kutoa maoni yao kwa siku 30 kama wanaihitaji au la.Naomba kuwasilisha.
<br />
<br />
itasaidia kuongeza ajira na kupunguza tatizo la ajira ukizingatia ma DC na Rc watakaoajiriwa ni watz..mi nashauri mikoa mipya ingekuwa laki moja na wilaya mpya milioni moja, umeona hiyo, zaidi ya wa-tz 1m wangepata ajira kama wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya..more good news ni kwamba kila mmoja angemiliki Vx na Vogue..
 
Oh, Mungu iponye Tanzania na Viongozi wabovu walio na choyo pasipo kujali wengine. Bali kuanzisha vitu ambavyo vilivyopo wanashindwa hata kuviendeleza kwa sababu ya kuficha uovu wao.
 
Back
Top Bottom