Mikoa 7 kufunga Kampeni za CCM Tanzania

Mikoa 7 kufunga Kampeni za CCM Tanzania

Mkakati wa UKAWA.
Wamepanga kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mgogoro ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka.
Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema,hawatafanikiwa,tunaviomba vyombo ya ulinzi & usalama kuhakikishe ulinzi & usalama wa watu & mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili waweze kupiga simu au kutuma ujumbe wanapobaini vitendo vya kuvuruga uchaguzi.
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa chama, chama kinategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015.
Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi zaidi & dhamana ya uongozi wa dola,tutatimiza wajibu wetu kutunza amani na utulivu.

CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu,chama kinawashukuru viongozi, wanachama na washabiki wake wa makundi mbalimbali ya kijamii kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
 
Propaganda
 
Ukawa ndiyo walete vurugu? Unashangaza! Watakaoleta vurugu ni hao wanaotangaza ushindi wa lazima. Kumbuka mkuu wa Mwanza magesa mulongo alichosema, na kumbuka jinsi ambavyo ccm wanang'ang'ania watu warudi nyumbani baada ya kupiga kura, wanataka kufanya nini?
Ndugu yangu acha uzushi.
 
Hawatafanikiwa. Kama wataahinda sana watapata majimbo 50 tu
 
hiyo mipango wameipanga wapi?? hivi kwani ccm ndio kituo cha police hadi mtoe namba za kuwapigia?
 
Ccm okoeni huduma za afya nchini in hatari kwenu
 
Wakuu,

Leo saa Saba mchana, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Dar es Salaam.

Nitawaletea moja kwa moja kile watakachokuwa wanakizungumza wa ajili ya Watanzania.

================
Hadi sasa wazungumzaji wa Chama hawajafika ukumbini, waliofika hadi muda huu ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

Nimepata taarifa kuwa mkutano huu utarushwa moja kwa moja (live) Azam Two.

attachment.php

Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbvali vya habari wakiwa ukumbuni kusubiri kuanza kwa mkutano huo.

Pindi wahusika watakapofika nitakaanza kuwapa kile walichotuitia.

January Makamba ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni, ameingia ukumbini na sasa anazungumza na waandishi wa habari anasema jambo kubwa ni kuzungumzia jinsi CCM watakavyofunga kampeni zao.

-Amesema watafunga mikutano hiyo katika mikoa 7 nchini. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM kitaifa waliopo madarakani na wastaafu.

Anasema mikoa hiyo na viongozi wakaoongoza mikutano ni pamoja na mkoa wa Mwanza - ambao atakuwepo, Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais

-Mkoa wa Tanga – atakuwepo Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Mkoa wa Mbeya – Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu na -Mtwara – atakuwepo Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu,

-Mkoa wa Kigoma –Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM,Kilimanjaro – Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu, Mara – Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu.

Amesema Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka.

-Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituoa vya redio 67.

-Katika mikutano hii watakaohudhuria wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.

-Ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini.

-Pia tutafanya historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.

-Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015.

-Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.

Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa.

-Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku.

-Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.

-Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.

-Anazungumzia suala la amani kuwa CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu.

-Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu.

-Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
-Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu.

-Makamba anasema kauli za mashabiki baada ya kupiga kura wabaki vituoni kulinda kura ni kauli za watu wasiotaka uchaguzi wa amani, amesema utaratibu hapa nchini, namna pekee ya kulinda kura ni kupitia wakala wako, wao wana nguvu na mamlaka ya kushuhudia zoezi zima la uchaguzi, kuanzia maboksi yanapofunguliwa, kuanzia karatasi zinapofunguliwa, kuanzi kura zinapopigwa, zinapohesabiwa na hadi kutangazwa kwa matokeo.

Kura zinapigwa vituoni, kukiwa na mawakala na wasimamizi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na wa nje. Mawakala wa vyama wanaweka sahihi katika fomu za matokeo yaliyohesabiwa palepale kituoni na matokeo hayo yanabandikwa nje ya kituo cha kura kwa watu wote kuona lakini vilevile kuna kituo kikubwa cha kujumlisha matokeo hapa Dar es Salaam ambapo vyama vinaruhusiwa kupeleka mawakala wake ili matokeo yanayotoka nchi nzima waweze kuthibitisha kama yanafanana na yale ya mawakala wao waliopo vituoni

-Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha vujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura.

-Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwasababu halina nia njema.

-Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa.

-Tunaviomba vyombo ya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

-CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.

Amesema siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani.

-Kuhusu matokeo, CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama.

Sisi tunategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi.

-Amezungumzia pia ajali ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, anaendelea vizuri na pia anaendelea kufanya kampeni zake kaam kawaida.

Amemaliza kuzungumza.
TAARIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA VYOMBO VYA HABARI, ALHAMIS OKTOBA 22, 2015
CCM inapenda kutoa taarifa kuhusu masuala kadhaa kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wake na kwa umma wa Watanzania.
Kufunga Kampeni
CCM itafunga kampeni zake kwa utaratibu mpya na kwa kishindo. Kampeni za CCM zitafungwa kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa mitano. Mikutano hiyo itaongozwa na viongozi wa CCM kitaifa waliopo madarakani na wastaafu. Mikoa hiyo na viongozi wakaoongoza mikutano hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Mwanza – Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Mgombea Urais, na Ndugu Samia Hassan Suluhu, Mgombea Makamu wa Rais
2. Tanga – Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
3. Mbeya – Ndugu Benjamin William Mkapa, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
4. Mtwara – Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa CCM Mstaafu
5. Kigoma – Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
6. Kilimanjaro – Ndugu Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu
7. Mara – Ndugu Joseph Warioba, Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu Mstaafu
Kati ya leo na kesho, maeneo mengine yanaweza kuongezeka. Mikutano hii itaanza saa sita mchana na itarushwa, yote kwa pamoja, kwa matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vitano na vituoa vya redio 67. Vilevile, watakaohudhuria katika mikutano hii wataunganishwa moja kwa moja na mkutano wa Mwanza, alipo Mwenyekiti, Mgombea na Mgombea Mwenza, na wataweza kusikiliza hotuba ya Dkt. Magufuli moja kwa moja kupitia screens zitakazokuwa katika viwanjani vyote hivi saba.
Namna hii ya ufungaji wa kampeni itakuwa ni ya kihistoria, na inadhihirisha nguvu ya CCM inayoiwezesha kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwa siku moja katika maeneo mbalimbali nchini. Lakini pia tutafanya historia katika tasnia ya utangazaji wa televisheni hapa nchini kwa kutangaza na kuunganisha kwa pamoja matukio saba kwa wakati mmoja.
Kwa upande wa Dar es Salaam, tutafanya mkutano mkubwa wa ufungaji wa kampeni za Mkoa wa Dar es Salaam, katika Uwanja wa Jangwani, kesho, Ijumaa, tarehe 23 Oktoba 2015. Siku ya Jumamosi, tarehe 24 Oktoba 2015, Wagombea Ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam watafunga kampeni katika maeneo ya majimbo yao kwa namna mahsusi.
Tathmini ya Kampeni
Kama Chama, tumeridhika na ubora na ukubwa wa kampeni tulizofanya licha ya changamoto za hapa na pale. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wamefanya kazi kubwa, na kwa bidii kubwa, na maarifa makubwa. Wamekuwa barabarani kwa siku 57 wakifanya mikutano kati ya 8 hadi 12 kwa siku. Imani yetu ya ushindi inatokana na kazi kubwa waliyofanya. Pia, CCM inawashukuru viongozi, wapenzi wa washabiki wake – wa makundi mbalimbali ya kijamii - kote nchini kwa kazi kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.
Kutokana na kazi kubwa na nzuri iliyofanyika, na kutokana na mwenendo wa tafiti huru na tafiti zetu za ndani, CCM inategemea ushindi wa asilimia zisizopungua 69.
Uchaguzi wa Amani
CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu. Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi wengi zaidi, na chenye dhamana ya uongozi wa dola, tutatimiza wajibu wetu wa kuhimiza utulivu kwa wapenzi, washabiki na wanachama wetu. Tunawataka na wenzetu wafanye hivyo.
Kauli za wenzetu kwamba kura zitaibiwa ni kauli za kutojiamini na kujiandaa kufanya vurugu. Kauli za kwamba washabiki wa UKAWA wakishapiga kura wabaki vituoni kulinda kura si kauli za wanaotaka uchaguzi wa amani.
Kwa utaratibu wetu wa uchaguzi, utaratibu wa pekee kwa Chama kulinda kura zake ni kwa kupitia wakala wa vyama waliopo kwenye kila kituo cha kupiga kura na wenye nguvu na mamlaka ya kisheria ya kushuhudia zoezi zima, kuanzia kupiga kura, kuhesabu kura hadi kutangaza matokeo. Kura zinapigwa na kuhesabiwa vituoni mbele ya wasimamizi wa uchaguzi, mawakala wa vyama na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Mawakala wa vyama na wasimamizi wa uchaguzi wanaweka sahihi kwenye fomu za matokeo, na matokeo hayo yanatangazwa na kubandikwa kwenye kituo. Kwenye kituo kikuu cha Tume cha kujumlisha matokeo, mawakala wa vyama pia huwepo na Tume hujumlisha matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo za vituo vya nchi nzima zilizosainiwa na mawakala wa vyama kwenye kila kituo. Kwa viongozi wa UKAWA kuwaambia watu waingie barabarani au kuvizunguka vituo vya kupigia kura eti ili kulinda kura hakuna maana yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuhalalisha vujo, vurugu na uporaji na kuwazuia watu wengine, hasa wanawake, kupiga kura. Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwasababu halina nia njema.
Mkakati wa UKAWA ni kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mazingira ya mgogoro wa kisiasa ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka. Mkakati huo hautafanikiwa. Tunaviomba vyombo ya ulinzi na usalama vihakikishe ulinzi na usalama wa watu wote na mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
Siku ya Jumamosi, CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili siku kabla ya uchaguzi, siku ya uchaguzi na mara baada ya uchaguzi, waweze kupiga simu au kutuma ujumbe pale watakapokuwa wanabaini au kushuhudia vitendo vya kuvuruga amani na kuvuruga utaratibu mzima wa uchaguzi.
Kupokea Matokeo
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa Chama. CCM inategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015.
Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
22 Oktoba 2015
 
Kupokea Matokeo.

Kuna mtu alizungumzia mambo watakayofanya ccm hizi siku za mwisho hasa tar 23 na 24 na moja kati ya aliyoyazungumzia ni pamoja na kumtumia mama Maria Nyerere limetokea kuhusu kuvitumia vyombo vyote vya habari ndio hilo la kesho na kuhusu kuwepo kwa umeme siku ya kesho kwa maeneo karibia nchi nzima. Nahisi kuna tuhuma zitatolewa kesho halafu keshokutwa umeme hautakuwepo
 
Hahahahaha nyinyiemu bana ina maana shinyanga simiyu na bukoba maji mingi haiwezi kuyaoga.si mnasema jamaa msukuma khaaaaaaa
 
Mgombea ubunge Wa jumbo la bumbuli amesema eti vyama vya upinzani vimepanga kuleta Fuji siku ya uchaguzi.Taarifa ya January makamba huo in uongo mkubwa acha kuwadanganya wananchi.CCM mmekuwa Na kampeni za matusi zikiongozwa Na Kiongozi mkubwa sana Mstaafu Rais Mkapa pale alipowatukana Watanzania kuwa ni MALOFA Na WAPUMBAVU.
 
Msumari ulipoingia ndipo utapokea
mtu anayejinyea mbele za watu hana kumbukumbu na kuongea anashindwa lakini anawanyima usingizi?
Lowasa ndo raisi mtarajiwa hakuna mwenye uwezo wa kuzuia mpango wa Mungu mwaka huu.

Labda usingizi unaukosa wewe, hivi uliona lile zezeta linatusumbuwa? Tumelipiga chini ndani ya CCM itakuwa nje? Fikiri.
 
Mkakati wa UKAWA.
Wamepanga kufanya vurugu baada ya kushindwa na kutengeneza mgogoro ili Jumuiya ya Kimataifa iingilie kati na kupendekeza kugawana madaraka.
Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama vizuie hili jambo kwa sababu halina nia njema,hawatafanikiwa,tunaviomba vyombo ya ulinzi & usalama kuhakikishe ulinzi & usalama wa watu & mali zao siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
CCM haitakubali hata kidogo ushindi wake kuhojiwa au kutiliwa shaka kwasababu tu ya vurugu zilizoanzishwa na watu wengine.
CCM itatangaza namba maalum za simu kwa Watanzania wote ili waweze kupiga simu au kutuma ujumbe wanapobaini vitendo vya kuvuruga uchaguzi.
CCM imeweka utaratibu wa kupokea matokeo kwa kutumia mawakala wake moja kwa moja vituoni na kupitia mtandao wa chama, chama kinategemea kuwa na matokeo ya uchaguzi nchi nzima ifikapo saa nne usiku, siku ya uchaguzi, tarehe 25 Oktoba 2015.
Sisi kama chama kikubwa cha siasa nchini, chenye wafuasi zaidi & dhamana ya uongozi wa dola,tutatimiza wajibu wetu kutunza amani na utulivu.

CCM haitachoka kuendelea kusisitiza uchaguzi wa amani na utulivu,chama kinawashukuru viongozi, wanachama na washabiki wake wa makundi mbalimbali ya kijamii kote nchini kwa kazi kubwa ya kampeni waliyoifanya.

Mkuu wa kaya, kwa hofu kuu aliyonayo ya vichinjio, alishatangaza state of emergency. Jeshi liko stand-by, tayari kuua wananchi walioichoka magamba na wameamua kuchagua MABADILIKO.

Sio mbaya, kwani Mungu aliumba na majeshi/policcm watatwaa roho za wananchi, jina lake lihimidiwe.
 
Back
Top Bottom