Mike Mushi, mmoja wa wenye hisa Jamii Media ahojiwa na Polisi

Wakiwamaliza the owners, sasa watatugeukia sisi members tunaochangia kwa mada ambazo sio furahishi kwa watawala.

Tanzania tulichagua viongozi ili watuongoze, baada ya kuwapa kura za kutosha na kuwapa mamlaka, sasa kuongoza ni basi bali kutawala! .

Nchi ikiishakosa mifumo, dira na mwelekeo, kila mtu anajikuta hajiamini, hivyo kuzua zua vikesi kwa lengo la kumfurahisha mfalume, huku wakijiamini ndio wanamsaidia, lakini kiukweli hawamsaidii na sana sana wanamharibia!.

Yana mwisho haya!.

Paskali.
ndo tujiandae kuhojiwa maana hawa jamaa wanashangaza sana wanashindwa kufanya mambo ya msingi ya matatizo ya balaa la njaa ninawashangaa sana
 
Hii nchi huwa hatupendi wazawa wafanikiwe, kitu kikionyesha kupendwa na watu kukiunga mkono au kwa maana nyingine kitu kikiwa kimbilio la wanyonge tunaanza kuangalia mmilki wake ni nani na yupo wapi wakati kuna watu wameleta damage kubwa kwa Taifa wamilki wake ni siri kubwa kama yule mwarabu aliekuwa anamilki mitambo flani ya umeme.

Ila facebook au whatapps wao ni poa tu hata kama wamesajiriwa nje, hizo dosari kama zipo si ni za kurekebisha tu, humu michango yote ni ya Member wenyewe wala wahusika aka wamilki hawahusiki kinachoandikwa kama ilivyo facebook na mitandao mingine (angalau hata humu kuna mods wanafuatilia mabandiko yanayokinzina na matakwa ya jamii
 
Watalii wakija waambiwe na haya maajabu mengine mapya ya Tanzania...

Hivi haya nayo ni mambo ya kutushughulisha kama nchi?
Tanzania ni nchi ya kimasikini kuanzia mwili mpaka roho.
Kwa ujinga huu ndiyo tutegemee wawekezaji waje labda wawekezaji wa shisha
 
Hivi hamjui kwanini haya yanatokea Leo?

Hoja kubwa,kumkamata Mike kutaondoa watu katika mjadala wa Njaa

Masheikh na maaskofu wamesema kuna tatizo na waumini wao wasali ' njaa'

Rais kaambiwa hadharani kuna tatizo

Haya yote ni kuondoa watu katika mjadala wa Njaa, kwa kujua kumkamata kutabadili upepo wa maongezi.

Na maongezi yatabadilika kwa kutibua mijadala ya JF. Kutibua ni kutia misuko suko uongozi
 
Ni shida utawala huu.Eti wakiwa na taarifa yao mkurgenzi wa mawasiliao ikulu wanaileta jf wakati huohuo wanawaandama wamiliki wake. Shame on you.
 
Back
Top Bottom