Hukumu ya kesi namba 456 ya 2016 inayowakabili Wakurugenzi wa Jamii Media kusomwa leo (Aprili 2, 2020)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,091
2,000
Kesi namba 456 ya mwaka 2016 inawakabili Mkurugenzi wa Jamii Media Ndg. Maxence Melo na mwana hisa mwenzake Mike Mushi itasomwa leo Aprili 02, 2020 mbele ya Hakimu Thomas Simba kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Hukumu hii awali ilipangwa kutolewa Novemba 26, 2019 lakini iliahirishwa mara nne (4) kwa kigezo kwamba Hakimu alikuwa hajamaliza kuandika hukumu hiyo. Tarehe nyingine ilizoahirishwa ni Desemba 06, 2019, Januari 22, 2020, Februari 19, 2020 na Machi 19, 2020.

Historia ya kesi hii

Kampuni ya Oilcom iliandikwa katika mtandao wa Jamii Forums ikidaiwa kukwepa kulipa kodi na kuchakachua mafuta kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Baada ya taarifa hizo kuandikwa kwenye mtandao wa Jamii Forums, Polisi waliandika barua kwenda kwa “Mkurugenzi wa Jamii Forum” kuomba taarifa za mtu aliyeandika ujumbe kuhusu Oilcom. Polisi wanadai hawakufanikiwa kupata taarifa hizo ndipo walipoamua kumkamata na kumuhoji Ndg. Maxence Melo na kumfungulia shitaka la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi alipotakiwa kutoa taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums kinyume na kifungu namba 22(1) cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni ya Mwaka 2015.

Ndg. Maxence Melo alikamatwa mnamo Desemba 13, 2016 na alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Desemba 16, 2016 na kufunguliwa kesi tatu (3) tofauti zenye shitaka moja la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi juu ya taarifa za walioandika kwenye mtandao wa Jamii Forums. Hata hivyo, alijikuta analazimika kupelekwa gereza la Keko kwa siku 3 baada ya kuchelewa kupewa dhamana.

Mapema mwaka 2017 upande wa Jamhuri ulimuongeza Micke William (Mike Mushi) kwenye kesi hizo kama mmoja wa wanahisa wa kampuni ya Jamii Media.

Kuhusu kesi zilizofunguliwa mahakamani

Kesi 3 zilizofunguliwa ni zifuatazo:

Mosi, Kesi namba 456 ya mwaka 2016 ambapo Ndg. Maxence Melo alishtakiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa polisi juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu Oilcom kwenye mtandao wa Jamii Forums. Katika nyakati tofauti za usikilizwaji wa kesi hii namba 456 upande wa Jamhuri umewahi kukiri kwamba Micke William aliingizwa kimakosa kwenye kesi hiyo. Aidha, upande huo wa mashtaka mashahidi wote walikiri watuhumiwa walijibu barua zote za polisi wakisema wapo tayari kutoa ushirikiano endapo jinai ya mwanachama wao itabainishwa na jeshi la Polisi.

Pili, Kesi namba 457 ya mwaka 2016 ambapo washitakiwa walituhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa ushirikiano juu ya taarifa za aliyeandika kuhusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kulipa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania.

Uamuzi wa shauri hilo (shauri namba 457) ulitolewa Juni 01, 2018 ambapo Hakimu Godfrey Mwambapa aliamua kwamba Washitakiwa hawakuwa na kesi ya kujibu na hivyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru.

Katika kesi hiyo pia, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada KWAYU na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu. JamiiForums haikutoa taarifa binafsi za wanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

Tatu, Kesi namba 458 ya mwaka 2016 ambapo washtakiwa wanatuhumiwa kwa kosa la kuzuia upelelezi kwa kutokutoa ushirikiano kwa Polisi kuhusu Benki ya CRDB ambapo Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa “Jamii Forum” kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums walioandika kuhusu Benki ya CRDB.

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala iliyosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Benki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Taarifa za Wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Kesi hii bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Huruma Shaidi na haijawa na shahidi tangu Novemba 2018.

Tutawaletea updates za hukumu hii kadiri muda utakavyoruhusu

UPDATE:

Kesi imepigwa tena kalenda hadi Aprili 8, 2020 baada ya Hakimu Thomas Simba kuomba muda zaidi aipitie hukumu hiyo na kulinganisha na submissions zilizofanywa. Soma hapa > Hukumu ya kesi namba 456 ya 2016 inayowakabili Maxence Melo na Mike Mushi iliyokuwa itolewe leo, imeahirishwa kwa mara ya 5 - JamiiForums
BE34B3F3-BDAC-4444-9591-4B1D670E393E.jpeg
 

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
6,383
2,000
Police nao hawana ustaarabu, hawajui kuwa wahusika kamili wa mambo sio waandishi hapa JF.

Walitakiwa kufanya uchunguzi wao na wenyewe kukamata makosa, sio kupenda mteremko.
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
5,379
2,000
If JF will lose on this case, then this will be a last nail to the coffin of the only and remaining strong platform for free speech in Tanzania.

Tanzanians for 4 years now have been denied and highly intimidated by state organs against their constitution right of freedom of expression, their only hope remained to be JF where people would disguise their IDs to present their opinions and feelings.

It goes without say that without JF, this country will turn out to be another form of North Korea. God Forbid
 

Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
15,036
2,000
Kama kawaida, mahakama itatenda haki. Kwa kuwa Mheshimiwa rais na Waziri mkuu walikuja kugundua kuwa kulikuwa na wizi bandarini na kila mahali;

ingekuwa busara kuipongeza JF kwa kudhubutu kuyasemea maovu yaliyokuwa yanaendelea.

Kwa maoni yangu haya yote yalifanyika kwa nia njema kabisa ya kufichua maovu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom