Kesi dhidi ya JamiiForums (namba 458): Maxence Melo na Mike Mushi wajitetea. Inasubiriwa hukumu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,981
Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media na Mwanahisa wake) imesikilizwa leo, 20 Agosti 2020 majira ya saa tano asubuhi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar

Mara ya mwisho, kesi hii ilisikilizwa Julai 30, 2020

Leo washitakiwa wamejitetea katika kuelekea hitimisho la kesi hii.

Mawakili wa Utetezi Walikuwa ni Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya huku Upande wa Jamhuri akiwa ni Wakili Faraji Nguka

Kibatala ndiye aliyeanza kumuuliza Maswali Maxence Melo mara baada ya kujitambulisha na kula kiapo...

Kibatala: Mwambie Hakimu kama unakumbuka mashitaka

Maxence: Ndio nayakumbuka Mashtaka

Kibatala: Shitaka la kwanza linasema wewe na Mwenzako mlioperate JamiiForums ambayo haijasajiliwa hapa Nchini, Mwambie hakimu kuhusiana na hili

Maxence: Sisi tulikuwa tumesajilia Nchini na tulikuwa tunaitumia

Kibatala: Ni kweli mlikuwa wakurugenzi wawili?

Maxence: Si kweli kwamba tulikuwa wakurugenzi wawili

Kibatala: Wewe ulikuwa na uhusiano gani wa Jamii Media Company Limited?

Maxence: Nilikuwa kama Secretary na Director

Kibatala: Wenzetu walileta ushahidi wa BRELA (P1) barua hiyo inaonesha kwamba ulikuwa Secretary na Director

Maxence: Ni kweli, nilikuwa Secretary na Director wakati tunasajili kampuni.

Kibatala: Je, ni kweli mlisajili?

Maxence: Ni kweli tulisajili tarehe 20 Juni 2008

Kibatala: Wao wanasema hadi kipindi cha mashitaka (2016) ulikuwa Mkurugenzi (Director).

Maxence: Tulifanya mabadiliko, niliandika barua BRELA ya kufanya Mabadiliko ya kujiondoa kuwa Secretary na mabadiliko kwenye ukurugenzi. Siwezi jua nini kipo BRELA kwani nilinyimwa faili niweze kuangalia kama bado wananitambua kama Mkurugenzi au la! Walisema shauri lipo mahakamani hawezi kunipa faili.

Kibatala: Hii Jamii Media kwamba ilioperate bila kusajiliwa na kikoa cha do.tz, kwanza hii Do.tz ni nini?

Maxence: Hakuna kitu kama hicho inatakiwa kuwa (dot tz). Yaani jamiiforums.co.tz au jamiiforums.or.tz. au jamiiforums.ac.tz

Kibatala: Kuna shahidi alikuja kubadilisha kuhusiana hiyo do.tz?

Maxence: Shahidi wa kwanza wa Jamhuri pia alisema walicholeta kwenye hati ya mashitaka sio sahihi. Shahidi huyo alisema tumeshasajili na alisema tulikuwa na domain mbili. Alitoa vielelezo kuthibitisha majina yalikuwa yamesajiliwa. Alikuwa anaongoza in-chief na yeye ndo alikuwa Msajili wa vikoa.

Kibatala: Vipi kuhusu kutumia kikoa?

Maxence: Tulisajili domain mbili alikuja nazo shahidi. D1 iliyoingizwa kama kielelezo na kinaonesha tulisajili domain mbili, www.jamiiforums.co.tz na www.jf.co.tz

Kibatala: Wanasema hamtumii ni kweli?

Maxence: Tunatumia domain zote mbili na zimesajiliwa. Ikiwezekana mtu yeyote azitembelee aone kama zinafunguka

Kibatala: Unaposema tutembelea unamaanisha nini?

Maxence: Ukitembelea Domain hizo zinafanya kazi. Mtu yoyote anaweza kutumia simu au kifaa chochote cha kidijitali chenye mfumo wa intaneti kuangalia kama zinafanya kazi.

Kibatala: PW1 wakati anaulizwa maswali na wakili Tundu Lissu baadae mimi, alisemaje?

Maxence: PW1 alikiri mwaka 2009 alishirikiana na mimi kuhamasisha watanzania kusajili kikoa cha .tz. Shahidi huyo alisema haikuwa lazima kutumia bali ilikuwa ni kuhamasisha uzalendo

Kibatala: Wewe na mwenzako hamkutoa ushirikiano kwa Polisi. Unasemaje kuhusiana na kuzuia upelelezi?

Maxence: Mimi sijazuia upelelezi

Kibatala: Wenzetu walitoa vielelezo vya barua kwamba barua hii ndo msingi wa wao kwa Polisi kutoa Ushirikiano. Mwambie Hakimu kuhusu hii barua ya Januari 26, 2016 imekuwa addressed kwa nani na ilitoka wapi?

Maxence: Ilitoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Cyber Crimes Unit. Ilielekezwa kwa Mwanasheria wa Jamii Forums Media.

Kibatala: Mwambie mheshimiwa Hakimu kama wewe ni Mwanasheria

Maxence: Mimi sio Mwanasheria

Kibatala: Kuna Shahidi alisema wewe ni Mwanasheria?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Jamii Forums Media ni kitu gani?

Maxence: Sijui

Kibatala: Taasisi zilizozungumziwa na mashahidi wote ni zipi?

Maxence: Mashahidi walikuwa wanazungumzia Jamii Media Company Limited na wengine Jamii Forum

Kibatala:
Hii barua imesainiwa na nani?

Maxence: Imesainiwa na Joshua Mwangasa – ASP

Kibatala: Joshua Mwangasa alishawahi kutoa ushahidi?

Maxence: Hajawahi kuja mahakamani kutoa ushahidi wa barua hii ingawa yeye ndo kasaini

Kibatala: Wapi ilielekezwa kwako, muoneshe Hakimu kama kuna sehemu inaonyesha barua hii ilielekezwa kwako

Maxence: Sioni sehemu yoyote kuwa barua iliekezwa kwangu

Kibatala: Kuna shahidi alisema ilipokelewa na wewe binafsi kuhusu mashitaka haya?

Maxence: Hakuna aliyefanya hivyo

(Kibatala narudisha kwa hakimu ushahidi P3)

Kibatala: Wenzetu walikuja na kielelezo P4, msomee Hakimu

Maxence: Ni barua ya Januari 26, 2016 kutoka kwa Victory Attorneys ilisainiwa na Benedict Alex

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Hakimu kama Benedict Alex aliwahi kuitwa kutoa Ushahidi mahakamani

Maxence: Hajawahi

Kibatala: Kuna shahidi aliyesema juu ya huyu shahidi kushindwa kuja mahakamani baada ya kuitwa kutoa Ushahidi?

Maxence: Hakuna aliyekuja kusema hivyo

Kibatala: Ni shahidi yupi alileta uthibitisho kuwa wewe ndiye ulimtuma Benedict ajibu hizi barua?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Na ni shahidi yupi alisema wewe umepata nakala yake?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Kielelezo P6 walileta ushahidi ni barua gani kutoka wapi?

Maxence: Ni barua ya Februari 4, 2016

Kibatala: Aliyeandikiwa hiyo barua ni nani?

Maxence: Aliandikwa Mwanasheria wa Jamii Forums Media. Mimi si mwanasheria wa Jamii Forums Media.

Kibatala: Wapi Hakimu ataona ulipokea kielelelezo au Mwanasheria wa Jamii Forums Media ameshitakiwa?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Imesainiwa na Kagae. Je, alishaitwa kutoa Ushahidi?

Maxence: Sijawahi kumuona

Kibatala: Kielelezo walileta pia in dispatch ya hiyo barua inaonesha barua imeelekezwa kwa nani?

Maxence: Alipokea Advocate Benedict

Kibatala: Aliwahi kuitwa mahakamani kusema amepokea hiyo barua?

Maxence: Sijawahi kumuona

Kibatala: Kuna sahihi (signature) inaonekana kuwa ni ya Benedict kuonesha kama ndiye alipokea barua. Kuna ushahidi uliwahi kuletwa kama uthibitisho kuwa ni sahihi yake?

Maxence: Haijawahi kuletwa

Kibatala: Wewe ndo unashitakiwa. Kwenye hivi vielelezo kuna sehemu wamekuonesha kwenye hizi barua?

Maxence: Hakuna sehemu yoyote

Kibatala: Kielelezo namba P7, Mwambie Hakimu unaona nini

Maxence: Hii ni barua imetoka Victory Attorneys na ni ya Februari 12, 2016. Inaelekezwa kwa Kamishna wa Cyber Crimes Unit na imesainiwa na Benedict Alex.

Kibatala: Kuna shahidi alithibitisha kuwa mliwahi kupata nakala?

Maxence: Hakuna

Kibatala: Nina maswali matatu, manne matano

1. Mwambie Hakimu kama shahidi wa mwisho toka CRDB alikutaja popote kwenye ushahidi wake

Maxence: Hakunitaja

2. Kuna shahidi alisema una manufaa hadi uzuie uchunguzi?

Maxence: Hakuna

3. Ulikuwa unanufaika na nini hadi uzuie uchunguzi?

Maxence: Sikuwa na interest yoyote, sikuwa na sababu ya kuzuia upelelezi

Kibatala anasema amemaliza

======

Wakili wa Jamhuri anafanya cross-examination:

Wakili Nguka: Unaijua kampuni ya Jamii Forum?

Maxence: Hapana

Nguka: Jamii Media Company Limited?

Maxence: Naifahamu

Jamhuri: Ilisajiliwa lini?

Maxence: Sikumbuki tarehe kamili lakini ilikuwa Juni mwaka 2008

Jamhuri: Nani anasomeka kuwa Mkurugenzi?

Maxence: Nilikuwemo mimi na wenzangu wawili. Tulikuwa wakurugenzi watatu (anataja wengine wawili)

Nguka: Ni lini uligota kuwa Mkurugenzi?

Maxence: Nilipeleka nyaraka BRELA 2012 kujiondoa kuwa Secretary

Nguka: Ulipata nyaraka zozote kukubaliwa?

Maxence: Ndio nyaraka hizo zipo

Nguka: Ulitoa nyaraka mahakamani?

Maxence: Hapana

Nguka: Ni nani anaweza kusajili makampuni?

Maxence: Msajili wa Makampuni

Nguka: Kielelezo P4 naomba unisomee fomu namba 14 A. Nisome Directors hao

Maxence: Inaonesha mimi ni Secretary na Director wa Jamii Media Company Limited mwaka 2008

Nguka: Kusajili na kutumia ni kitu kimoja au viwili?

Maxence: Ni vitu viwili tofauti

Nguka: Shahidi wa kwanza alisema wamesajili na hawatumii

Maxence: Charge sheet ilisema hatukusajili

Nguka: Unakumbuka barua ya tarehe 26 Januari 2016? Je, Barua uliiona?

Maxence: Ndio niliiona hapa mahakamani, kabla ya mahakamani sikuiona popote

Nguka: Kuna barua ilijibiwa?

Maxence: Sijui kwa sababu kuna barua walikuwa wanajibizana. Nliziona mahakamani

Nguka: Umeona nakala za barua?

Maxence: Ndio, nakala ya Jamii Media. Lakini Sijawahi kuipata barua hiyo, niliionea hapa mahakamani

Wakili Nguka: Naishia hapo

Wakili Kibatala anasema hana maswali ya re-examination kwa Maxence. Anaruhusiwa kupisha mshtakiwa wa pili

===

Sasa anaulizwa Maswali Mshitakiwa namba mbili.

(Anaapa)

Kibatala: Katika hati inasomeka Micke William, je ndo jina lako?

Mike: Hapana, mimi naitwa Mike William Mushi. Imeandikwa kwenye cheti cha kuzaliwa hati ya kusafiria, leseni ya Udereva nk (Ametoa kielelezo cha leseni ya udereva kama ushahidi)

Kibatala: Unamkumbuka shahidi Beatrice alisema nini?

Mike: Alisema mimi sihusiki na kesi hii

Kibatala: Beatrice alikuwa anafanya kazi gani?

Mike: Mpelelezi

Kibatala: Ni shahidi gani alikutaja sehemu yoyote au mahali popote?

Mike: Hakuna

Kibatala: Uliwahi kuhusiana na ku-operate au kutumia hiyo website ya JamiiForums.com?

Mike: Sijawahi kusajili wala kutumia domain ya JamiiForums.com

Kibatala: Wewe umewahi kuwa Director wa Jamii Media Company Limited?

Mike: Sijawahi

Wakili Kibatala amemaliza…

Wakili wa Jamhuri anamuuliza Maswali Mike Mushi:

Nguka: Shahidi tusaidie, kabla ya shauri kusikiliza tulisema tunakuja kufanya PH?

Mike: Sina kumbukumbu nzuri

Nguka: Siku ya kwanza ulisomewa hati ya mashitaka Mahakama ilikutamka vizuri?

Mike: Sina kumbukumbu sahihi

Nguka: Mwanzoni hukuona umuhimu wa kuelezea majina yako hapa Mahakamani?

Mike: Kama ambavyo sijui kwanini mimi nipo hapa

Wakili Nguka amemaliza…

(Kibatala anaingia kufanya re-examination)

Kibatala: Wewe umeanza kujitetea lini tangu kesi hii ianze?

Mike: Sasa hivi, ndo siku ya kwanza kuongea hapa Mahakamani

Wakili Kibatala anasema hana maswali zaidi

Hakimu: Mtahitaji kuleta Submissions?

Wote: Ndio

Hakimu: Basi tarehe 21 Septemba 2020 ndo siku ya mwisho kufanya submissions na mention kwa ajili ya hukumu itakuwa siku hiyo hiyo.

Dhamana inaendelea hadi tarehe 21 Septemba 2020.

Kesi namba 458 inayomkabili Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Melo kutajwa leo
 
Kwa maelezo ya Maxence Melo na Mike utagundua kuwa:

1. Kampuni inayoshitakiwa siyo ya kwao, na pia wao sio wenye vyeo tajwa.

2. Micke anayeshitakiwa (kwa mujibu wa hati ya mashitaka) siyo Mike aliyefikishwa mahakamani.

3. Kwenye hati ya mashtaka kuna makosa badala ya dot tz imeandikwa do.tz

4. JF imesajiliwa kwa kikoa cha dot tz

5. Si lazima kusajili kwa kikoa cha dot tz ila ni 'uzalendo' tu kufanya hivyo.

6. Hakuna namna imethibitishwa kuwa Benedict (mwanasheria) alikuwa akimuwakilisha Melo au Mike

7. Barua zote za Victory Attorneys hazioneshi kuelekezwa kwa Melo.
 
Serikali inapoteza fedha kwenye mambo ya kijinga sasa. Chanzo cha haya yote ni kampuni fulani kuumbuliwa jinsi wanavyo kwepa kodi ya mafuta bandarini.

Polisi na DPP wanatumika kwa maslahi binafsi ya mafisadi na wakandamizaji.
 
Back
Top Bottom