Mikakati ya kumaliza migogoro ya Wakulima na wafugaji Kilosa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
"Tumejipanga na tunakuja na mkakati kabambe kumaliza Migogoro ya wakulima na wafugaji, nataka tuandike pamoja historia ya kumaliza kabisa changamoto ya migogoro hii Kilosa.

Namimi nikiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hii nitaanza na watendaji ndani ya serikali ambao ni sehemu ya ustawi au wanufaika wa migogoro hiyo, hivyo niwahahakishie kama kuna mtu yeyote miongoni mwetu, anafaidika na migogoro hii ama anahusika kwa namna moja ama nyingine kuistawisha atakutana na mkono mkali wa sheria kwenye hili hatutangaliana usoni"

Kauli ya DC Shaka Hamdu Shaka wakati akiweka msisitizo asubuhi Alkhamis 16 Februari 2023 alipokuwa akiongea na Madiwani katika kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya Kilosa ambapo wakati wa. Jioni alipata fursa kufika eneo la Magomeni ambako wananchi walifikisha malalamiko yao ofisini kwake jana.

#Kilosa2Fursa2
#Maendeleo endelevu

IMG-20230217-WA0004.jpg
 
Aise.....ngoja tuone

Huu moto alianza nao

Ila kwa sisi tunaoijua kindakindaki wilaya ya kilosa na sakata la matatizo ya wakulima na wafugaji huko,naona kama maneno tu ya wanasiasa haya.

Ova
 
Back
Top Bottom