DC Shaka Hamdu Shaka hawezi mikimiki ya Wakulima na Wafugaji wa Kilosa, abadilishiwe kituo

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Wilaya ya Kilosa ni kiini cha migogoro ya Wakulima na Wafugaji. Ma DC wengi na hata wakuu wa mikoa na viongozi wa Polisi mkoa na wilaya watakiri hili.

Uteuzi wa Shaka kwenda pale tena akiwa DC kwa mara ya kwanza utazamwe upya. Hii wilaya yahitaji DC mzoefu au mwenye uwezo mkubwa wa kutatua migogoro.

Sina uhakika Kama Shaka ataimudu wilaya hii. Simdharau ila nasema tu Sina uhakika Kama DC mpya Shaka Hamidu Shaka ataweza mchakamchaka wa Wakulima na Wafugaji wa wilaya ya Kilosa.

Ningependekeza abadilishiwe kituo na kuangalia orodhani kama kuna DC ataimudu wilaya ya Kilosa.

Ni maoni yangu tu.
 
Kuna yule DC wa Arusha (sijui kama kahamishwa). He is very smart.

Angepaweza huko, maeneo yenye mgogoro yanayohitaji mazungumzo kuheshimiana.
 
Sehemu kama hiyo inahitaji mtu atakae zungumza kwa hekima za kiuongozi na anaeweza kutenda kwa mkono wa chuma yani "diktekta" pro max, hao ndugu zetu kwa mazungumzo tuu hawaendi.
 
Kuna yule DC wa Arusha (sijui kama kahamishwa). He is very smart.

Angepaweza huko, maeneo yenye mgogoro yanayohitaji mazungumzo kuheshimiana.
Nadhani yule mama aliyekuweko Handeni anaweza kwa kiasi
 
Pale kuna ocd, dso na das. Watamsaidia sana kama hatapeleka ujuaji.

Hata ukipeleka mwenye manguv ya samson mix busara za suleimani migogoro hutatuliwa kwa kuangalia shamba ni la nani vs mmiliki wa mifugo.

Ikiwezekana, mwenye mamlaka makuu awatake wastaafu na walio na vyeo watoe maeneo yao ili kuwaongezea wafugaji eneo la malisho sambmb na kuwataka wafugaji kuziuza.

Pia waweke mashart magum ya kupeleka mifugo mapolini.

NB. PIA CHUMA KITUMIKE KWA WAKOLA.
 
labda kapelekwa kule kwenda kuchunga maslahi na mashamba ya wakubwa yaliyo kule na wale wapemba wanaolangua mazao ya watu yakiwa mashambani!

LKn Niulize swali; inakuwaje mtu wa ZNZ kwenda kuwa mkuu wa Wilaya Tz Bara? Je haya ni mambo ya muungano?
 
Kupewa wilaya hizo ni busara za Rais, shida yangu nature ya wilaya aliyopewa.
 
Pale kuna ocd, dso na das. Watamsaidia sana kama hatapeleka ujuaji.

Hata ukipeleka mwenye manguv ya samson mix busara za suleimani migogoro hutatuliwa kwa kuangalia shamba ni la nani vs mmiliki wa mifugo...
Kumbuka misimamo na uwezo wa DC pia ni muhimu Sana wilayani.
 
Pale kuna ocd, dso na das. Watamsaidia sana kama hatapeleka ujuaji.

Hata ukipeleka mwenye manguv ya samson mix busara za suleimani migogoro hutatuliwa kwa kuangalia shamba ni la nani vs mmiliki wa mifugo...
Wafugaji ni wagumu mno, Ni wa kukaanao kwa umakini.
 
Wilaya ya Kilosa ni kiini cha migogoro ya Wakulima na Wafugaji. Ma DC wengi na hata wakuu wa mikoa na viongozi wa Polisi mkoa na wilaya watakiri hili...
Ni kweli kabisa,mwanasiasa hafai hapa.Uharibifu mkubwa wa mazingira,rushwa kubwa toka kwa wafugaji ni changamoto kwa viongozi vijana.
 
Sehemu kama hiyo inahitaji mtu atakae zungumza kwa hekima za kiuongozi na anaeweza kutenda kwa mkono wa chuma yani "diktekta" pro max, hao ndugu zetu kwa mazungumzo tuu hawaendi.
Yani ni nguvu kidogo na hekima
 
Naomba wafugaji waheshimiwe Kama anavyo heshimiwa mkulima vinginevyo hatutakubali ss wafugaji kuburuzwa ktk nchi Eti tupunguze mifugo alfu wanasiasa wakamiliki maelfu ya mifugo tusitiane umaskini kila mtu asimame kwenye shughli zAke .Ni ujinga sana kutuambia tupunguze idadi ya mifugo alfu nyinyi ili niniyi wachache mzimiliki hapana siyo haki hata kwenye bibilia wafugaji waliheshimiwa sna na mfuguji alionekana ndio tajiri enzi na enzi

Namnukuu museve " kuwa tajiri Ni pmj na kuwa na mifugo na siyo majengo ya kifahari "

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Naomba wafugaji waheshimiwe Kama anavyo heshimiwa mkulima vinginevyo hatutakubali ss wafugaji kuburuzwa ktk nchi Eti tupunguze mifugo alfu wanasiasa...
Fugeni kisasa, heshimuni mashamba ya Wakulima, heshimuni mapori tengefu na hifadhi za taifa.
 
Back
Top Bottom