Dsm ni mji mmoja wa hatari sana,
1. Ni mji unaodhoofisha afya za watu, maana mtu unaamka saa kumi ili uwahi kazini na unarudi usiku sana huku umechoka na hujapumzika vizuri usiku, weekend watu wanatoka kulipiza kisasi cha kukosa muda na bado unacheleweshwa kwa mambo mengi tu
2. Ni mji unaodhoofisha uchumi kwa maana huwezi kufanya mambo mengi kwa siku moja
3. Ni mji ambao umekosa direction kwa maana ya afya watu wanakula vyakula ambavyo si salama
4. Ni mji ambao matapeli yamejaa kila mahali mpaka kwa muuza cd barabarani, ukienda nyumbani ukiangalia unakuta cd inakwaruza.
5. Ni mji ambao unatengeneza stress za kutosha, watu hawana furaha wanajipoza kwa pesa na kutumia kwa sana huku chini "Nyanda za juu kusini"