Fahamu Viwanja bora katika kila bara!

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,089
Teknolojia imeleta maendeleo makubwa katika utendaji kazi; kazi za uzalishaji mali miaka ya 1923 ni tofauti na mwaka 2023, hii ni miaka mia moja ambayo tumepata kushuhudia matumizi makubwa ya akili ya mwanadamu. Leo natamani tuangazie kwa uchache namna ambayo kila bara limepata kuwekeza katika michezo hususani ni upande wa viwanja. Ni suala la wazi na lisilo na ubishi kuwa bara la Ulaya pamoja na Amerika ya kaskazini katika uwekezaji wake katika kuwa na viwanja vingi vyenye kiwango. Duniani kuna viwanja maelfu ila kuna viwanja ukivisikia basi unaona jeuri na pesa na namna watu walivyo serious kwenye michezo.

images.jpg
Viwanja

images%20(1).jpg

Kwa Ulaya uwanja wa Barcelona na una uwezo wa kuingiza mashabiki 99,354 na umepata kujengwa mwaka 1957, uwanja huu ndipo ilipopigwa michuano ya UEFA Euro ya mwaka 1964, Michuano ya kombe la dunia la mwaka 1982.

images%20(2).jpg

Nambari mbili ni Wembley ndani ya London Uingereza uwanja ambao unaingiza mashabiki 90,000 huku ukipata nafasi ya kuchezwa kwa fainali za UEFA Champions league kwa mwaka 2011 na 2013 pamoja na fainali ya mwaka 2024.

images%20(3).jpg

Uwanja wa tatu, Santiago Bernabeu wa Uhispania. Kuna viwanja zaidi ya 32 ambavyo vinaingiza mashabiki zaidi ya 60,000, huku viwanja zaidi ya 32 vikiingiza mashabiki 50,000.

Panoramic_santiago_bernabeu.jpg

Kwa upande wa bara la Asia viwanja vingi vinatumika kwenye michezo ya mpira wa miguu, cricket, riadha pamoja na baseball ila mara kadhaa imekuwa ikitofautiana kuendana na uwezo ambao unakubaliwa na mamlaka husika ya eneo ambalo uwanja upo. Uwanja ambao unaongoza kwa ukubwa upo Kusini mwa Asia katika taifa la India ndani ya Jiji la Ahmedabad na uwanja huo umepewa jina la Narendra Modi International Stadium huku ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 132,000 kwa wakati mmoja.

images%20(4).jpg

Uwanja wa pili kwa ukubwa ni uwanja wa Rungrado 1st of May Stadium ambao huu unapatikana Mashariki mwa Asia katika Jiji la Pyongyang, Korea ya Kaskazini ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 114,000.

images%20(5).jpg

Uwanja wa tatu upo Kusini Mashariki mwa Asia ambao ni Bukit Jalil National Stadium ambapo upo katika Jiji la Kuala Lumpur ndani ya nchi ya Malaysia, uwanja huu unaweza kuingia mashabiki 87,411.

images%20(6).jpg
Kwa bara la Asia kuna viwanja zaidi ya 40 ambavyo hivi vina uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000, viwanja kama vile Takhti Stadium cha Iran, pia kuna Dongdaemun Stadium cha Korea Kusini, Paljor Stadium cha Indonesia, Dasarath Rangasala Stadium cha Nepal, Chiba Sports Center Stadium cha Japani, Yangsan Stadium cha Korea Kusini, Guru Nanak Stadium cha Indonesia, Al-Wihda Stadium cha Yemen, pamoja na Wunna Theikdi Stadium cha Myanmar.

images%20(7).jpg

Yaani kuna viwanja zaidi ya 82 ndani ya bara la Asia ambavyo vina uwezo wa kuingia mashabiki 30,000 na hii inatosha kuweka takwimu kuwa Asia ina viwanja zaidi ya 320, ingawa kwa taifa kama Korea ya Kusini wao wana jumla ya viwanja zaidi ya 130 ikiwemo kiwanja kikubwa cha Seoul Olympic Stadium ambacho kinaingiza mashabiki 69,950 pamoja na Seoul World Cup Stadium ambacho hiki kinaingiza mashabiki takribani 66,806, viwanja vyote hivi viwili vipo ndani ya Jiji la Seoul.

images%20(8).jpg

Upande wa Amerika ya Kusini kuna kiwanja cha Mas Monumental uliopo Buerno Aires Arjentina ambao unatumiwa na timu ya River Plate na chenye uwezo wa kuingiza mashabiki 86,049.

images%20(9).jpg

Monumental cha Peru ni nambari mbili kiwanja ambacho kinatumiwa na timu ya Universitaro na chenye uwezo wa kuingiza mashabiki 80,093.

EstadioUniversitario.jpg

Namba tatu ni Maracana cha Brazil ambacho kinaweza kuingiza mashabiki 78,838 na kinatumiwa na timu za Flamengo na Fluminense.

images%20(10).jpg

Ajabu ni kwamba katika orodha ya viwanja 10 Barani Amerika ya Kusini viwanja 6 vipo Brazil. Wafunga dimba ni Douradao na Mario Heleriro vya Brazil pamoja na Estadio La Ceiba cha Venezuela ambapo viwanja hivi vinaingiza mashabiki 30,000.

Kwa upande wa nyumbani Afrika, uwanja wa Soccer City uliopo kwenye jiji la Johannesburg ndo uwanja mkubwa barani Afrika kwani uliongezewa uwezo wa kuingia mashabiki mpaka kufikia mashabiki 94,700 kwa sababu ya Michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2010, ujenzi ambao uligharimu dola milioni 600 ulitosha kufanya kuwa ndo uwanja ghali zaidi barani Afrika.

download.jpg

Borg El Arab uliopo pale Misri katika Jiji la Alexandria unaingiza mashabiki 86,000 na unatumika na timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Misri, huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuna uwanja unaitwa Stade des Martyrs ambao unaingiza mashabiki 80,000 na unapatikana ndani ya jiji la Kinshasa na pia umekuwa ukitumiwa na timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

images%20(11).jpg

Cairo Internartional Stadium uwanja ambao upo pia Misri ambao huu unaingiza mashabiki 74,100 uwanja huu umekuwa ukitumiwa na Taifa ya Mpira wa Miguu ya Misri, vilabu vya soka vya Al Ahly pamoja na Zamalek.

images%20(12).jpg

Kiwanja chetu cha Taifa maarufu kama Lupaso kinachoingiza mashabiki 60,000 kipo nafasi moja sambamba na viwanja kama vile, Stade Leopold Senghor cha Senegal, Tigray Stadium pamoja na Bahir Dar Stadium vyote vya Ethiopia, pia kiwanja cha Stade Municipal de Kintele cha Congo Brazzaville, Stade Olympique Hammadi Agrebi cha Tunisia pamoja na Paul Biya Stadium cha Cameroon, kitaalamu kuna viwanja takribani 12 ambavyo uwanja wa Mkapa vimelingana uwezo wa kuingiza mashabiki.

images%20(13).jpg

Viwanja vya Ahmed Kaid Stadium Stade Tahar, na August 20 19955 Stadium vya Algeria, Jalingo City Stadium cha Nigeria, Stade Amahoro cha Kigali Rwanda, Nyayo National Stadium cha Nairobi Kenya, Stade de Kegue cha Togo, Independence Stadium cha Gambia, Rand Stadium cha Afrika Kusini, Stade Municipal cha Burkina Faso, Beni Ebeid Stadium na Al Salam Stadium vya Misri.

Nakivubo Stadium cha Kampala Uganda, Abebe Bikila Stadium cha Ethiopia pamoja na Stade Larbi Zaouli cha Moroco vinatengeneza hesabu vya viwanja 21 ambavyo vina uwezo wa kuingia mashabiki 30,000 katika kila kiwanja, Kiwanja cha CCM Kirumba cha Mwanza kina uwezo wa kuingiza mashabiki 35,000 kipo juu kwa nafasi 38 zaidi ya kwenye orodha ya viwanja ambavyo vinaingiza mashabiki wengi zaidi ya 30,000. Uwanja wa Khartoum Stadium uliopo pale Sudani. ulipata nafasi ya kipekee ya kuhodhi michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 1957 pamoja na mwaka 1970, ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 23,000 pekee.

images%20(14).jpg

Uwanja wa Alexandria Stadium uliopo Misri wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 19,676 tu, uliwahi kuchezwa michuano ya mataifa ya Afrika ya mwaka 1974, mwaka 1986, mwaka 2006 pamoja na mwaka 2019 (yaani michuano ya mataifa ya Afrika mara nne). Uwanja wa Nuevo Estadio de Malabo uliopo Equatorial Guinea wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,250 uliwahi kuhodhi michuano ya mataifa ya Afrika mara mbili, mwaka 2012 pamoja na 2015. Hapa hakuna kiwanja ambacho kinaizidi CCM Kirumba kwa kuingiza mashabiki vyote vinaingiza mashabiki kwa uchache sana! Ama 35,000 ni ndogo kwa 15,250 au 19,676?

Mbao_FC_-_Kagera_Sugar_2016-2017.jpg

Tukutane sehemu ya pili............
 
Nadhani itakuwa viwanja vinavyoingiza mashabiki wengi zaidi duniani, maana ubora unavitu vingi vya kuangalia...au ukubwa ndo ubora?
 
Unajua nilivyoona kichwa cha habari tu nilitegemea nikutane na kitambaa cheupe,sport bar korogwe na zingine zingine huko kwenye miji ya watu kumbe sio nilichofikiria yani sisi walevi bhana
 
Back
Top Bottom