Mihadhara ya namna hii ni sahihi...?

Mihadhara ya namna hii ni sahihi...?

Status
Not open for further replies.
wivuuuu mbona dini yetu inazidikukua tena leo mimi nikienda china ni ongoza ibada bila ya wasiwasi ...lol

we utaweza kuongoza ibada china kwa kiswahili..?

Read my post again. I am not here to spoon feed you.
 
I don't know how much intellectual are you, but you can not use the Holy Bible to answer a question related to Koran, inter-alia, you can not use Koran to answer a Biblical question.

Mfano, wewe kama ni mwalimu wa lugha ya Kiswahili, je unaweza tumia Kisukuma kufundisha lugha ya Kiswahili? Itashangaza wengi ukitumia kisukuma kufundisha kiswahili.

Hili ndilo tatizo kubwa sana katika Uislam, mnatumia Biblia kufundisha Koran, na hapo pana onyesha kuwa, Koran haijitoshelezi ndio maana mnakimbilia kwenye Biblia na kusahau hata hadeeth mlizo pewa ili kusaidia Kolani ambayo imeshindwa kujitosheleza.
You know, Quran tells us :2:111"......Say: "Produce your proof if you are truthful."
Kwa hiyo katika Uislam, mtu yoyote anayeleta madai tunamuuliza Ushahidi wake (even Westerners and I am sure in your country, are practising this in your courts).
Sasa nyinyi Wakristo mnadai kuwa mko katika correct path, tukiwauliza proof mnanukuu kutoka katika Biblia (as your witness), sasa sisi tunachofanya, ni ku cross examine your witness(Biblia), na tunachokiona katika Biblia ni kuwa vitu mnavyodai (Yesu ni Mungu, amesulbiwa nk) havimo!
 
YESU - NABII ALIYETOKA NAZARETI MTUMISHI WA MUNGU

Masih hataona uvunjifu kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu.

(Qur'ani) An Nisaa 4.172

Biblia inahakikisha ukweli huu wa Qur'ani. Mara nyingi tunaona Yesu anatafakhari kujitangaza kuwa yeye ametumwa na Mungu, na mara nyingi anaitwa "mtumishi wa Mungu". Katika Injili ya Yohana mathalan tunasoma:

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

Yohana 17.3-4

Kwa unyenyekevu wa safi ya niya Yesu anamkhatibu Mola wake, "Mungu wa pekee wa kweli", siye mungu wa uwongo miongoni wa miungu ya uwongo uwongo iliyokuwa ikiabudiwa na makafiri. Ajuulikane Mwenyezi Mungu na kadhaalika ajuulikane yeye Yesu Kristo, Mtume na mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume kiliomo katika Agano Jipya la Biblia tunasoma:

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.

Matendo 3.26

Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.

Matendo 3.13

Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.

Matendo 4.29-30

Wagonjwa wanaponyeshwa, ishara zinaonyeshwa, na maajabu yanatendeka. Nani afanyae yote haya? Ni kudra na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Jina la Yesu huenda likatumiwa, lakini ni kama chombo tu, wasila, mwombezi, kwani kama atavyokuwa yeye ni "mtumishi mtakatifu wa Mungu." Katika Matendo 3.26 na 3.13 hapo juu Paulo aliwaandikia Mayahudi ambao walimkataa mtumishi wa Mungu, Yesu Kristo, alipowajia na utumishi kutoka kwa Mungu wa babu zao Mayahudi, Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na Yakobo. Mwenyezi Mungu ni yule yule mmoja, Mitume ni mbali mbali, lakini utumishi wao ni mmoja. Mayahudi wakawakubali wote waliotangulia wakamkataa Yesu. Mwenyewe Yesu anawasimanga Mayahudi kama inavyotueleza Injili ya Yohana:

Mimi mnanijua, na huko nitokako mnakujua; wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.

Yohana 7.28-29

Katika Injili ya Marko Yesu anasimuliwa alimchukua mtoto akasema:

Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.

Marko 9.37

Kama hayo aliambiwa Mtume Muhammad s.a.w. na Mwenyezi Mungu katika Qur'ani:

Sema: Ikiwa ninyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakusameheni madhambi yenu, kwani Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

(Qur'ani) Al Imran 3.31

Yesu amesema:

Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.

Yohana 4.34

Haya khasa ndio maana ya neno Uislamu. Uislamu ni kujisalimisha nafsi yako kwenye mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kutenda apendavyo Mola wako Mlezi. Na hicho ndicho chakula chake Yesu, kama asemavyo, yaani kama anavyohitaji kula kila siku ili aishi, kama wanavyohitaji wanaadamu wote, basi hali kadhaalika kuwa daima anajisalimu mbele ya matakwa ya Mwenyezi Mungu aliyemtuma duniani kuwa ni Mtume. Tena Yesu amesema:

Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka. Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu. Yeye anenaye kwa nafsi yake tu hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali anayetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyo ni wa kweli, wala ndani yake hamna udhalimu.

Yohana 7.16-18

Tunaona basi kwa ushahidi wake mwenyewe Yesu kuwa fakhari yake ni kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu wake aliyemuumba na akamtuma kwa Wana wa Israili waliopotea kama kondoo. Kwa uthibitisho wake mwenyewe yeye ni mtumishi wa haki aliyepewa Unabii na kufanywa Mtume. Hataki utukufu wake yeye, bali utukufu wa Mungu wake aliyemtuma na kumpeleka awaongoe watu wafwate njia iliyo nyooka. Katika Injili ya Mathayo anazidi kufafanua nini wadhifa wake na nini cheo chake mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wanaadamu wenziwe. Alipowateua wanafunzi wake kumi na mbili kuwapeleka kuwahubiria Mayahudi alisema:

Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma. Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.

Mathayo 10.40-41

Yeye mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni Nabii. Je, nini mawazo ya wale wafwasi wake waliomuamini na wakamwona na wakaishi naye? Injili zinatwambia:

Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.

Yohana 6.14

Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.

Mathayo 21.46

Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.

Mathayo 21.10-11

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, ni Maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda mbele za Mungu na watu wote.

Luka 24.13-19

Injili kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.
"Hakika huyu ni nabii", anasema Yohana.
"waliwona kuwa nabii", anasema Mathayo.
"Huyu ni yule nabii, Yesu", anasema tena Mathayo.
"Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii", anasema Luka.
Jinsi ya hadhari zake asisingiziwe kuwa anazo au anadai sifa za ungu, Yesu alikataa hata kuitwa "Mwalimu mwema". Sikiliza masimulizi ya Injili ya Marko:

Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akmwuuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.

Marko 10.17-18

Tafsiri kubwa kabisa ya Biblia iitwayo The Interpreter's Bible inasema kuwa kauli hiyo ya Yesu, yaani: "Kwa nini kuniiita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu", imewatatiza wataalamu wa thiolojia (ilimu ya Ungu) ya Kikristo wa baadaye. Wameona taabu kuambatisha maneno haya yalio wazi na imani yao kuwa Yesu ni mungu, na hali hapo dhaahiri yake ni kuwa anakataa ungu. Kwa hivyo basi kujitoa kimasomaso ikaandikwa katika Injili ya Mathayo (ambayo iliandikwa baada ya Marko) kwa njia nyengine. Ilivyoandikwa katika Mathayo ni hivi:

Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja.

Mathayo 19.16-17

Kila imani ilipozidi kugeuka maandiko mapya yaliandikwa na kunasibishiwa Yesu. Kitabu hicho The Interpreter's Bible kinaikataa tafsiri ya kusema kuwa makusudio ya Yesu yalikuwa ni kusema: Kama unanita mwema, basi unakusudia kuwa mimi ni Mungu. Hayo siyo. Aliyokusudia Yesu kusema ni kuwa :Sifai kupewa sifa za Mungu.
Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, ameandika katika kitabu chake The Life of Jesus (Maisha ya Yesu):
"Yesu kwa mara moja alimpa somo zuri kabisa la unyenyekevu, ambalo juu ya mengineyo, ni ushahidi ulio wazi ya kwamba hakupata kabisa kujiona mwenyewe ni sawa na Mungu: Kwa nini kuniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, ndiye Mungu."
Mukhtasari wa yote tuliyokwisha yazungumza, ni kuwa tumepata uthibitisho wa kutosha kutokana na Biblia kuwa Yesu wa Nazareti ni mwanaadamu, Nabii wa Mungu, na Mtume wake.
Jee, Mtume huyo katumwa kwa nani?
progress.gif
 
There is no other religion which fulfills the conditions mentioned above except for religion of Islam, the religion which is accordance to human nature, the religion which has been preached by all prophets since the dawn of man. Other religions found today, such as Christianity and Judaism, are the remnants of the religion brought by the prophets in their time, which was Islam.

Ebu acha uongo. Few (if not one) of the "prophets" and certainly, not since the dawn of man.
 
You know, Quran tells us :2:111"......Say: "Produce your proof if you are truthful."
Kwa hiyo katika Uislam, mtu yoyote anayeleta madai tunamuuliza Ushahidi wake (even Westerners and I am sure in your country, are practising this in your courts).
Sasa nyinyi Wakristo mnadai kuwa mko katika correct path, tukiwauliza proof mnanukuu kutoka katika Biblia (as your witness), sasa sisi tunachofanya, ni ku cross examine your witness(Biblia), na tunachokiona katika Biblia ni kuwa vitu mnavyodai (Yesu ni Mungu, amesulbiwa nk) havimo!
Well said mkuu!
 
Ndugu zangu wachangiaji wa hizi topic mbalimbali zinazokuja hapa Jamii forum. Labda ningeomba muongozo kidogo. labda nilikuwa nimepotea kwa muda nilivyorudi nikakuta home page ya Jamii Forum imebadilika kabisa. zamani ulikuwa ukishalog in kwenye home page unakuta thread zote pale unachagua ni thread gani unaitaka.

Sasa hivi kuna mabadiliko kuna thread kama ya dini haionekani, inabidi mtu uingie kwenye habari mchanganyiko, halafu kwa bahati ndo ukutane na topic yoyote inayohusiana na mambo ya dini, hapo unaweza ku quick reply post yoyote kadri ulivyoichagua kuchangia katikati au mwisho wa page nk.

Sasa hapo ndiko ninakoliona tatizo. Tuseme nimekuta topic mpya, ishachangiwa na watu 10 mathlani, katika watu hao kumi wengine wakatoka nje ya mada japokuwa post zao kwa njia moja au nyingine zinahusiana na dini, lakini haikuwa mada kuu.

Ulivyokuja unakuta pengine post zimefika hata page 10 lakini topics zinapishana kulingana na nani kapenda kumjibu nani kulingana na alivyoguswa na post. Ningependa kuuliza kama ifuatavyo:-

1. Kwa nini topic isiwe moja ichangiwe hadi imalizike?
2. Kwa nini post zisi postiwe mwisho ili iwe rahisi kufollow up debate kuliko ilivyo sasa hivi? manake kuna latest post zinapostiwa lakini zinajibiwa katikati hivyo hazisomwi.

Lets say kesho nakuja nafungua thread ya dini natafuta topic niliyoiacha jana, ninakuta page zimefika 30, that means kuna post nyingi mpya zimeingia, lakini hakuna flow nzuri mtu hawezi kufuatilia dabate vizuri kwa staili iliyopo sasa.

Kama utaratibu ungekuwa mzuri kwamba kila post inayojibiwa iende mwisho chini, basi hata usomaji ungekuwa rahisi, yaani hata kama nikirudi kensho nitapost yangu kishapo nitarudi nyuma niendelee kusoma pale nilikoishia jana yake.

Lakini nikirudi kama niliishia page 10 post ya say 15 kumbe baadae kuna wachangiaji walikuja kuchangia au kujibu post zilizopita nyuma ya pale niliposoma na kuishia, sasa hizo nitazijuaje?

Lakini zikipostiwa mbele kila wakati itakuwa rahisi kwa wasomaji kufualilia flow ya debate. Mfano kulikuwa na topic ya WHY ISLAM na la MIHADHARA. topic hizi hata hazijulikani ziko kwenye thread gani ni mkanganyiko mwingi sana unaweza kufungua habari mchanganyiko na usizione hizo mada. Plz do something

Kingine ninachokiona na repetition ya posts, unakuta page nzima ni post moja inajirudia rudia au kila ukifungua page post hiyo hiyo moja inajirudia mwanzo, sijui hili liko vipi? Hapo sasa mada inakuwa inapoteza flow. Naomba maadministrator JF wanieleweshe kidogo kwa hilo na kwa faida ya wasomaji wengine.
Nanyuki
 
You know, Quran tells us :2:111"......Say: "Produce your proof if you are truthful."
Kwa hiyo katika Uislam, mtu yoyote anayeleta madai tunamuuliza Ushahidi wake (even Westerners and I am sure in your country, are practising this in your courts).
Sasa nyinyi Wakristo mnadai kuwa mko katika correct path, tukiwauliza proof mnanukuu kutoka katika Biblia (as your witness), sasa sisi tunachofanya, ni ku cross examine your witness(Biblia), na tunachokiona katika Biblia ni kuwa vitu mnavyodai (Yesu ni Mungu, amesulbiwa nk) havimo!

Kwahiyo unamaanisha kwamba huwezi kufundisha Kiswahili kwa kutumia Kisukuma, sio?

So, why using Koran to preach Christianity wakati Biblia ya Wakristo Ipo?
 
Sasa nyinyi Wakristo mnadai kuwa mko katika correct path, tukiwauliza proof mnanukuu kutoka katika Biblia (as your witness), sasa sisi tunachofanya, ni ku cross examine your witness(Biblia), na tunachokiona katika Biblia ni kuwa vitu mnavyodai (Yesu ni Mungu, amesulbiwa nk) havimo!

Surah 5:46 - And We sent after them in their footsteps Isa, son of Marium, verifying what was before him of the Taurat (Jewish Torah) and We gave him the Injeel (Christian Gospels) in which was guidance and light, and verifying what was before it of Taurat and a guidance and an admonition for those who guard (against evil).

Mohammed said. "By Allah, though I am the apostle of Allah, yet I do not know what Allah will do to me." Vol. 5:266

As I exhibited above, Jesus is the only way to God na sio Mtume Muham-mad. Koran yako inakiri hilo kiasi cha Mtume Muham-mad kusema kuwa yeye hajuwi WHAT WILL ALLAH DO TO HIM.

Sasabasi, kwanini nifuate Mtume ambaye hajuwi hata Allah atamfanya nini na wapi anakwenda baada ya kifo?
 
You know, Quran tells us :2:111"......Say: "Produce your proof if you are truthful."
Kwa hiyo katika Uislam, mtu yoyote anayeleta madai tunamuuliza Ushahidi wake (even Westerners and I am sure in your country, are practising this in your courts).
!

Surah 17:90-94 of the Qur'an tells about how, when Muhammad was challenged to perform a miracle and prove he was from the true god, he could not perform any and here he actually says himself: "Am I anything but a man,- a messenger?".

- Surah 29:27 states clearly that, as far as Allah and the Qur'an are concerned, the only true prophets are those related to Isaac (Ishaq) or Jacob (Yaqoub); yet Muhammad, according to Muslim tradition, is related to Ishmael and not Isaac or Jacob.

Accordingly, why should I follow Muham-mad who confess to all that he is just a man per Surah 17: 90-94?

Why should I follow Muham-mad, who is not even in a prophetic bloodline according to Koran Surah 29: 27?
 
surah 17:90-94 of the qur'an tells about how, when muhammad was challenged to perform a miracle and prove he was from the true god, he could not perform any and here he actually says himself: "am i anything but a man,- a messenger?".

- surah 29:27 states clearly that, as far as allah and the qur'an are concerned, the only true prophets are those related to isaac (ishaq) or jacob (yaqoub); yet muhammad, according to muslim tradition, is related to ishmael and not isaac or jacob.

accordingly, why should i follow muham-mad who confess to all that he is just a man per surah 17: 90-94?

why should i follow muham-mad, who is not even in a prophetic bloodline according to koran surah 29: 27?

we ulitaka awe mungu mtu...?
 
Surah 17:90-94 of the Qur'an tells about how, when Muhammad was challenged to perform a miracle and prove he was from the true god, he could not perform any and here he actually says himself: "Am I anything but a man,- a messenger?".

- Surah 29:27 states clearly that, as far as Allah and the Qur'an are concerned, the only true prophets are those related to Isaac (Ishaq) or Jacob (Yaqoub); yet Muhammad, according to Muslim tradition, is related to Ishmael and not Isaac or Jacob.

Accordingly, why should I follow Muham-mad who confess to all that he is just a man per Surah 17: 90-94?

Why should I follow Muham-mad, who is not even in a prophetic bloodline according to Koran Surah 29: 27?

Usitegemee jibu hapa mkuu,
 
Surah 5:46 - And We sent after them in their footsteps Isa, son of Marium, verifying what was before him of the Taurat (Jewish Torah) and We gave him the Injeel (Christian Gospels) in which was guidance and light, and verifying what was before it of Taurat and a guidance and an admonition for those who guard (against evil).

Mohammed said. "By Allah, though I am the apostle of Allah, yet I do not know what Allah will do to me." Vol. 5:266

As I exhibited above, Jesus is the only way to God na sio Mtume Muham-mad. Koran yako inakiri hilo kiasi cha Mtume Muham-mad kusema kuwa yeye hajuwi WHAT WILL ALLAH DO TO HIM.

Sasabasi, kwanini nifuate Mtume ambaye hajuwi hata Allah atamfanya nini na wapi anakwenda baada ya kifo?

Huyu Mwamadi alijuwa alichokuwa anasemaga? Jamaa unaukana utume wake na kujiita just a man, lol,

Waislam wamelamba galasa hapa.
 
Huyu Mwamadi alijuwa alichukuwa anasemaga? Jamaa unaukana utume wake na kujiita jus a man, lol,

Waislam wamelamba galasa hapa.
Tatizo shule hamuwezi kuelewa? nendeni english class pale kwa kakobe
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom