Inawezekana unamchukia yule mama kwa sababu yoyote ile, hiyo ni personal issue baina yako na yeye (inawezekana alikukatalia). Asha-Rose ameshetembea na wanaume wangapi , ana uamainifu gani katika ndoa yake, ana uhusiano gani na JK siyo mambo yanayotuhusu katika mada hii. Hayajibu swali la msingi iwapo kweli Prof Migiro alimsidia mama yule kupata digrii zake zote za sheria (LLB, LLB na Ph.D.) Kudai umeleta "changamoto" bila facts ni umbea mtupu unaotokana na hisia zako binafsi.Halafu tena, tambua kuwa matukio ya UDSM miaka ya leo hayana uhusiano kabisa na matukio ya UDSM miaka 35 iliyopita! Inawezekana leo UDSM wanafanya upuuzi sana, lakini huwezi ku-extrapolate upuuzi huo kwenda miaka 35 iliyopita bila ushahidi wowote. Kuna factors nyingi sana zinazosababisha kuwepo tofauti: social dynamics katika jumuia ya watu 900 wakati huo ni tofauti ya jumuia ya watu zaidi ya 18,000 leo; vile vile mfumo wa maisha kwa jumla siku hizi ni tofauti sana na miaka 35 iliyopita.Kunitafutia majina ya ajabu kutokana na mjadala huu ni kuonyesha ufinyu wa akili yako; ndiyo matokeo mazuri ya ya cross-examination.