SoC01 Mifumo yetu ya malipo, Benki, utumaji pesa na ulipaji Kodi kuendana na Kasi ya Teknolojia (kutumia Blockchain technology)

Stories of Change - 2021 Competition

Allist

Member
Jun 17, 2019
7
23
Mifumo yetu ya malipo, Benki, utumaji pesa na ulipaji Kodi iendane na spidi ya Teknolojia (kutumia Blockchain technology).

Blockchain technology ni teknolojia mpya iliyogunduliwa mwaka 2008 na kushika kasi kuanzia 2014, ni mfumo madhubuti ambao ni ngumu Ku hack na kuiba data au pesa. kwa kutumia teknolojia hii watu wameweza kutengeneza Mifumo ya malipo na pesa za kidijitali (cryptocurrency)

Kwa sasa teknolojia hii inatumika zaidi kutengeneza pesa za kidijitali (cryptocurrency) mfano bitcoin, Etherum, Ripple, Stellar, Tron, Binance na Cardano,

Pesa hizi za kidijitali zinaweza kutumika kufanya malipo ya bidhaa mbali mbali, kulipa kodi na kutuma kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine popote Duniani tena kwa gharama nafuu kwa baadhi ya pesa hizi. na tena kwa muda mfupi ukilinganisha na Mifumo ya sasa ya benki pesa kutoka nchi moja kwenda nyengine inaweza kuchukua muda mrefu.

Mfano wa pesa hizi za kidijitali ni Stellar coin, ambapo mtu anaweza kutuma pesa kwenda nchi yoyote kiasi chochote hata kama ni Tsh billion 1, kwa gharama nafuu isiofika hata shilling 1. tena ndani ya dakika 10 inakuwa imeshamfikia mtu popote alipo duniani.

Kama tutahamia katika mfumo huu wa Blockchain, benk zetu, serikali yetu na sisi wenyewe tukiwa tunatumia, miamala mingi na pesa zetu zitakuwa salama zaidi, na tutakuwa tunafanya miamala kwa bei nafuu na kwa haraka zaidi hata tukiwa tunatuma pesa nje ya nchi,

pia itaipunguzia serikali gharama za kutengeneza pesa, maana kwa mfumo huu hakutokuwa na uhitaji wa kutengeneza pesa nyingi.

UMUHIMU WA TEKNOLOJIA YA BLOCKCHAIN

1. NI SALAMA ZAIDI


kuhifadhi pesa kwenye Mifumo hii ni salama zaidi hakuna mtu anaeweza Ku hack au kuiba pesa ndani ya mfumo, hivyo benki zitu zitakuwa salama zaidi na hata pesa za watu binafsi zitakuwa salama kutokana na wizi wa mitandaoni, kwani hakuna atakaeweza kuufikia muamala wowote utakaofanyika kwenye sytem hii na kuiba labda muhusika mwenyewe atume pesa kwenda sehemu husika. hivyo mtu au kampuni inaweza kufanya miamala mikubwa hata ya mabillion ya pesa bila ya wasi wasi.

2. HUWEZI KUPOTEZA PESA KWA AJALI, Mfano Moto

Pia mfumo huu ni salama zaidi kwa kuhifadhi pesa kwa sababu huwezi kupotesa pesa kwa ajila kama vile moto, pesa zinakuwa kwenye Mifumo maalumu ambapo hata benk kama itashika moto na kuungua yote, bado utaweza kupata pesa zote zilizo hifadhiwa kwenye mfumo, kwani data huwa hazihifaziwi kwenye computer moja, computer nyingi hutumika kuhifadhi data ambazo zipo maeneo tufauti katika dunia hivyo hata computer moja ama nyingi zilizopo eneo moja zitaharibika, bado upo uwezekano wa kuzipata pesa zote bila kupoteza hata shilling.


3. NI NAFUU NA HARAKA KIMATAIFA

kwa kutimia mfumo huu mtu anaweza kutuma hadi Billion 20 kwa ada ya shilling 0.005, ndani ya dakika 10, kwenda popote duniani kwa kutumia mfano Steller coin (pesa ya digitali kwenye Mifumo wa blockchain). hakuna gharama kubwa kutuma pesa hasa kwa makampuni makubwa yanayohitaji kutuma pesa nyingi kwa wakati mmoja, gharama in nafuu sana.

4. MTU YOYOTE ANAWEZA KUTUMIA

Teknolojia hii mtu yeyete mwenye simu janja (smartphone), laptop au computer anaweza kutumia popote na wakati wowote, kufanya malipo, kutuma pesa kulipa kodi n.k. haihitaji ujuzi mkubwa ili kuweza kutumia

5. ITAPUNGUZA GHARAMA ZA KUTENGENEZA PESA

Kwa kutumia Mfumo huu watu wataweza kufanya malipo kulipa kodi na kutuma pesa mahali popote bila ya uhitaji ya pesa za kushikika (cash) tena kwa gharama nafuu, hivyo selikali inaweza kutengeneza pesa chache tu, na gharama nyingi zilizowekwa kutengeneza pesa zikatumika katika maendeleo.

6.NI RAHISI KUSAFIRI NAZO

Kwa kutumia mfumo huu mtu hatohitaji kubeba pesa, popote ulipo ukiwa na simu ama computer yenye internet tu, unaweza kuingia kwenye account yako na kufanya miamala hata ukiwa nje ya nchi.

Kwa sasa nchi nyingi zimeanza kujaribu kutumia teknolojia hii kwa kuitungia sheria na nyengne ikiwa tayari zimesharuhusiwa kisheria kama vile Ujerumani, Marekani Japan na Australia, Ingawa watu wa nchi nyingi ikiwemo Tanzania tayari wanatumia japo haijapitishwa kisheria, ni vyema tukaiangalia teknolojia hii kwa jicho la pili ili kuboresha Mifumo yetu ya pesa.

Na kwa kutumia teknolojia hii kuna fursa nyingi za kupata pesa hasa kwa vijana, kwa kuuza na kununua hizi pesa za dijitali.

Kulingana na hali ya sasa ya uhaba wa ajira kwa vijana, vijana wengi haswa vyuoni wameanza kujifuza huhusiana na teknolojia hii, na jinsi wanavyoweza kujiajiri katika teknolojia hii

Ninao mfano mzuri wa kijana mmoja anaitwa Sir jeffdenis ni muhamasishaji wa teknolojia hii hasa Twitter, na vijana wengi wanamfatilia kwa ukaribu sana.

Ni bure kabisa tutashauriana kama vijana, ili tuweze kutengeneza pesa na tuepukane na utegemezi
 
Unge elezea faida na hasara kwa wale ambao ni wenyeji kwa sababu block chain technology in kitu ambacho kina mambo mengi
 
Unge elezea faida na hasara kwa wale ambao ni wenyeji kwa sababu block chain technology in kitu ambacho kina mambo mengi
Kwa upande wa harasa sio kubwa saana, ukilinganisha na faida, mfano moja ya changomoto ninayoiona ni kubwa ni kwamba miamala yake ukishatuma ndo unetuma, huwez kuurudisha (irreversible)
 
Back
Top Bottom