SoC02 Mifumo ya CCTV kamera ni jicho pekee litakalotazama jiji la Dar es Salaam

Stories of Change - 2022 Competition

muhin

Member
Jul 16, 2021
7
6
Tupo kwenye kwenye karne ya 21 kwenye zama za sayansi na teknologia ambayo hujaribu kutatua na kuleta mbadala wa huduma na kazi zinazofanywa na mwanadamu kwenye kuhakikisha maisha ya wanadamu yanaenda na kuendelea kwa hali iliyo nzuri na ya kuridhisha .

Kwa kufanikisha hilo wanasayansi kwenye nyanja tofauti hutumia njia za kisayansi kwenye kutatua matatizo kadhaa ya wanadamu au kuleta njia mbadala ya mambo kadhaa kwenye kuhakikisha ubora wa maisha ya mwanadamu.

Kuna mifano kadhaa kwa upande wa teknologia ambayo imeleta utatuzi au mbadala wa kazi ambazo zilikua zikifanywa na mwanadamu ila kwa sasa zinafanywa na teknologia na zimeleta ufanisi mkubwa ambao mimi na wewe tunaushuhudia, kabla ya kwenda mbali sana kimifano upo mfano wa uhalisia kabisa ambao ni huu ujumbe unaousoma kutoka kwangu ni matunda ya teknologia kwenye kutatua matatizo ya kurahisha njia za mawasiliano ambayo hapo awali ilikua ngumu mimi niliyekuepo mbagala Dar es salaam nijadiliane na wewe uliyekuepo mkuhungu Dodoma tena ana kwa ana au kwa vipindi husika kulingana na haja ya wanaofanya mazungumzo.

Na ndipo hapo dunia ilipooamua kujikita kwenye sayansi na teknologia kwenye kutatua matatizo ya sehemu zao husika sababu ufanisi wake ni wakuridhisha ukilinganisha na ule wa kibinadamu.

Teknologia ni kubwa na sayansi ni pana hivyo wanasayansi hutoa kidogo tu kwenye hiyo sayansi na teknologia kutupatia sisi ambao hatutaki kuchanganua akili zetu na yaliyobaki huachiwa mimi na wewe kwenye kuendeleza pale walipoishia

Ukiacha mataifa ambayo yenyewe tayari yameendelea yapo mataifa ambayo yana fanana na taifa letu hili lakini mataifa hayo yaliamua kutumia ujuzi au huduma zilizotokana na sayansi na teknologia kwa matumizi au kuziendeleza na zimeleta ufanisi kwenye mataifa husika.

Mfano wa kihalisia matumizi ya CCTV kamera kwa nchi ya Rwanda yameleta mapinduzi na maendeleo makubwa kwenye taifa lao huku sisi watanzania tukibaki tukiwaangalia , si vibaya kuiga mazuri ya jirani na pale alipokosea kumnasihi kwa lugha nzuri yenye busara .

CCTV kamera imepunguza uhalifu kwenye miji ya kigali katika mitaa ya nyarugenge,gosobo,kicukiro na miji jirani toka iliivyoanzishwa mifumo hii ukilinganishanisha na zamani.

CCTV kamera imepunguza ugaidi au kuondoa kabisa kwenye mji wa kigali na miji jirani baada tu ya kuanza kutumiwa kwa mifumo hii.

CCTV kamera imesaidia ulinzi na usalama wa barabarani kwenye barabara kuu zile za Rwanda kwa kuwasaidia maofisa wa polisi kuangalia baadhi ya barabara kwa wepesi ikilinganishwa na awali hayo ni kwa mujibu wa idara ya polisi ya Rwanda (RNP)

CCTV kamera imepunguza kwa kiasi fulani tatizo sugu la Afrika nalo ni rushwa za barabarani na maeneo ya umma sababu ikisemwa watu huisi wanaonekana pindi watakapotoa au kupokea rushwa hivyo mazoea hujenga tabia na kiwango cha rushwa kimepungua kwenye mji wa kigali na Rwanda kwa ujumla.

Uhalisia wa umuhimu huu wa CCTV kamera tayari unaonekana swali la kujiiliza kwenye mji ambao una watu wa aina mbalimbali za kitabia nao ni Dar es salaam tutaitumiaje teknogia hii ili ilete ufanisi maana kama uhalifu , ujambazi , ugaidi , ulinzi na usalama wa barabarani pamoja na rushwa vyote kwenye jiji hili vipo .

Kwa hali ilivyo nimeona nifanye jitihada juu ya kueleza namna ipi nzuri ya kulifanya hili , hivyo kwa maono yangu nimeonelea tulifanye hili kwa awamu tatu maana mbuyu huanza kama mchicha.

Awamu ya kwanza (1) sehemu muhimu na zile zenye mikusanyiko mingi ya watu mfano sehemu muhimu za serikali na zinazohitaji usalama mkubwa kama uwanja wa ndende , bandarini , mahakama kuu, magerezani , kwenye ofisi muhimu za serikali na maeneo ya umma yanayohusisha wengi wa watu kama uwanja wa mpira wa benjamini wiliam mkapa, viwanja vya sababa, fukwe maarufu na sehemu zile pendwa ambazo wengi hupenda kuhudhuria.

Baadhi ya sehemu tayari mifumo hii ipo mfano uwanja wa ndege na bandarini na kwenye baadhi ya ofisi muhimu za serikali ila changamoto iliyokuwepo katika sehemu ambako bado hakuna matumizi ya mifumo hii na je kwa sehemu ambazo zipo je kuna muunganiko wa sehemu izo maanekane je kuna makao makuu ya kuunganisha mifumo hiyo ambayo ipo kwenye sehemu izo ? kama jibu ndio basi itakua vema na kama hapana ni muda wa kufanya ilo.

Awamu ya pili (2) itahusisha barabara,reli kuu zote za jiji la Dar es salaam pamoja na vituo vya mabasi na vile vya gari moshi (treni)

Kwa uwamu hii nafikiri umuhimu wa mifumo hii ya CCTV ndipo utakapoanza kuonekana kwa sababu utaisaidia polisi kwenye masuala ya usalama na ulinzi wa barabarani na ulinzi wa raia na mali zao kwa ujumla uhalisia uliopo kwenye jiji letu baadhi ya barabara zetu tayari mifumo hii ipo kwa mfano makutano ya ubungo na yale ya tazara lakini bado haitoshi inatakiwa mifumo hii kwa awamu hii ifungwe kwenye barabara kuu zote za jiji . Kuhusu changamoto sijui kama kwa sehemu ambako mifumo hii ipo inafanya kazi na kama inafanya kazi je imeunganishwa na makao makuu ya taifa ya kuongoza mifumo hii .

Awamu ya tatu (3) kwa awamu hii itagawanyika kwenye hatua tatu ambazo ni

(a) kufunga mifumo ya kamera mitaani kwa kutumia viegesho au mistimu ya tanesco kwenye mitaa mbali mbali ya jiji sababu itakua rahisi kufanya kazi kwa kuhitaji umeme na sehemu mahusi ya kuchukua picha na video kwa ajili ya matumizi.

(b) kufunga mifumo ya kamera kwenye baadhi ya mitaa ,maeneo ya umma na majumba mengine kwenye zile sehemu hatarishi na zisizo hatarishi.

(c) kama tujuavyo kuna watu binafsi na makampuni ambayo tayari kwenye sehemu zao zina hii mifumo kwa hatua hii ni kuunganisha mifumo ya kamera binafsi ili iwe imeuungana kwenye makao makuu ya mifumo hii.

Ni muda wa serikali kwa sekta zinazohusika kama TCRA na idara zingine kama polisi ziangalie wamefikia wapi kwenye hili au waanzie wapi kwenye kulifanikisha hili.

Hivyo bajeti , sera , sheria zipangwe na maoni yachukuliwe kutoka kwa wadau mbalimbali ili tulifanye jiji letu liwe ni miongoni mwa miji salama Afrika na ulimwenguni.
 
Back
Top Bottom