Miezi mitatu baada Oktoba 29, waliofiwa bado wasaka wapendwa wao

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,601
AA1V8Eif.jpg

Manenos Selanyika alipata mazishi ya mfano tu. Familia yake haikuwahi kuupata mwili wake baada ya machafuko makubwa ya uchaguzi wa Tanzania yaliyotokea miezi mitatu iliyopita.

Mwandishi huyo wa habari mwenye umri wa miaka 40 aliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama tarehe 30 Oktoba, majirani waliiambia familia yake.
Alikuwa ametoka kwenda kununua chakula katikati ya maandamano yaliyokuwa yamelikumba taifa wakati wa uchaguzi siku iliyotangulia.

Majirani waliieleza familia kuwa alipigwa risasi katika Barabara ya Mbezi Africana pembezoni mwa jiji kubwa zaidi nchini, Dar es Salaam, lakini polisi hawakuruhusu mtu yeyote kuuchukua mwili wake.

“Sipendi kupindisha maneno. Ilikuwa ni polisi (waliompiga risasi),” mmoja wa ndugu zake alisema. Jina lake limefichwa ili kumlinda dhidi ya kulipiziwa kisasi.

Familia ilitembelea katika hospitali mbalimbali, ikikagua miili mingi ya marehemu katika siku zilizofuata, lakini haikupata chochote.

Baada ya zaidi ya wiki moja bila mafanikio, waliamua kukata tamaa na kufanya mazishi ya mfano katika kijiji cha Lambo, karibu na Mlima Kilimanjaro.

“Tulikuwa na alama tu kuonesha kuwa hapa ndipo kaburi lake lingekuwa,” ndugu huyo alisema.

Buguruni- Dar es Salaam

Miili iliyopotea

Inaaminika kuwa mamia ya familia ziko katika hali kama hiyo. Mamlaka zinatuhumiwa kutupa miili ya marehemu katika makaburi ya halaiki.
Maandamano yalichochewa na madai ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, huku pia kukiwa na matukio ya watu kutekwa na kuuawa.

Rais Samia alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 97.6 ya kura, katika uchaguzi uliokuwa na utata kutokana na maandamano yaliyosababisha uharibifu wa mali, mauaji na watu kujeruhiwa, huku intaneti ikizimwa kwa siku tano.

Serikali hadi sasa haijatoa idadi rasmi ya waliouawa, lakini inakadiriwa kuwa mammia ya watu wameuawa.

Sheila Gyumi (si jina lake halisi) alipoteza mume wake siku ya uchaguzi baada ya kutoka nyumbani kwenda kazini kama kawaida, akifanya kazi ya kusafirisha abiria na mizigo kwa pikipiki.

“Wakati huo hali haikuonekana kuwa mbaya, kila kitu kilionekana tulivu,” alisema. “Baadaye niliona hali imebadilika, nikaanza kumpigia simu lakini hakupokea.”

Familia ilitembelea vituo vingi vya polisi na hospitali kubwa zote, lakini walihisi kila mahali walizuiwa kupata msaada.

“Ninajisikia vibaya sana. Mume wangu alikuwa mtu aliyeijali sana familia yake,” alisema.
“Sijui alipo. Kuna maumivu makubwa, na kuna maswali ambayo mtoto ataendelea kuuliza,” aliongeza, akisema sasa anahangaika kulipa kodi ya nyumba na ada ya shule.

Daktari mmoja katika hospitali kubwa ya Dar es Salaam aliyenukuliwa kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kuwa mamia ya miili ilichukuliwa kutoka mochwari na vikosi vya usalama na kupelekwa maeneo ya siri wakati wa kilele cha machafuko.

“Tunaamini huenda (Selanyika) yupo miongoni mwa waliotupwa katika kaburi la halaiki, kama vyombo vya habari vilivyoripoti, ingawa serikali ilikanusha,” alisema ndugu wa mwandishi huyo.

“Imepita miezi mitatu. Hatuna matumaini ya kuupata mwili wake,” aliongeza.

‘Hofu’

Mashirika ya kutetea haki za binadamu na mashuhuda wanasema wengi wa waliouawa walikuwa raia wasio na hatia, huku wengi wakiogopa kuzungumza kwa hofu ya kulipiziwa kisasi.

“Kumekuwa na hofu kubwa juu ya usalama wetu, ikiwemo hatari ya kukamatwa na vyombo vya usalama,” alisema ndugu mwingine wa Selanyika.

Serikali imeahidi kufanya uchunguzi lakini kwa kiasi kikubwa imepunguza uzito wa machafuko hayo, huku rais akisema nguvu iliyotumika ilistahili kwa waandamanaji waliotaka kuipindua Serikali.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Novemba 25, Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba alikwepa kujibu swali la idadi ya watu waliouawa wakati wa maandamano hayo.

“Tunaongelea maisha ya watu, tunaongelea watu kupoteza wapendwa wao, haya si majengo, nchi ya aina gani ya ku-celebrate maisha ya watu? Inabidi tuweke miiko, mtu amepotelewa na mpendwa wako wewe unapost?

“Kwa nini tunataka kushereka watu kupotea, nilidhani tukubali jambo kutokea, lakini tuko bize tunataka tuanze kuhesabu kama watoto wamezaliwa, mnataka tuanze kuhesabu kama mafanikio, mnataka tuhesabu kama magari, maisha ya watu?” alihoji.
AA1V8Qqe.jpg

Waandishi wa habari walivyobanwa

Haikuwa rahisi kwa waandishi wa habari kupata vibali vya kuriipoti uchaguzi huo, huku waandishi wa ndani nao wakikumbwa na vitisho, huku kukatishwa kwa intaneti kukikwamisha kazi za uandishi na kulazimisha baadhi ya vyombo vya habari kufungwa kwa siku tano.

Miongoni mwa waandishi waliopata misukosuko ni Godfrey Thomas wa Millard Ayo TV, aliyekamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uhaini kwa kuripoti kuhusu maandamano hayo. Hata hivyo, baadaye aliachiliwa huru.

“Kilikuwa kipindi kigumu sana,” alisema mwandishi mkongwe wa habari, ambaye naye jina lake limefichwa.
Alisema picha zilizooneshwa kwenye televisheni ya Taifa (TBC), “zilikuwa hazilingani kabisa na hali halisi iliyokuwa inaendelea mitaani. Hata matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa—sijui yalitoka wapi,” alisema.
 
View attachment 3539525

View attachment 3539529

View attachment 3539531

Duh!!! hao ndo wata tambuliwa kama mashuja wakweli, walipigania Tanganyika yao.
 
Back
Top Bottom